PAZIA 3
JF-Expert Member
- Jan 30, 2018
- 1,074
- 1,857
Kutoka maeneo mbalimbali kwenye viunga vya mji wa Dodoma, Tundu Lissu leo anachukua Fomu ya Urais.
===
Tundu Lissu leo kwa Mara ya kwanza anarejea katika mji wa Dodoma akienda kwa ajili ya kuchukua fomu ya kugombea Urais. Ikumbukwe Tundu Lissu mara ya mwisho kuondoka katika mkoa huu ni baada ya kupigwa risasi.
Fuatilia baadhi ya matukio na picha mbalimbali za tukio hilo.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA Tundu Lissu akiwa amewasili katika Ofisi za CHADEMA Kanda ya Kati zilizopo jijini Dodoma na kupokelewa na viongozi mbalinbali wa Chama, wanachama, wapenzi na mashabiki wa CHADEMA, kabla ya kuelekea Ofisi za Tume ya Uchaguzi kuchukua fomu, leo Jumamosi 08/08/2020.
====
TUNDU LISSU AFIKA OFISI ZA NEC KUCHUKUA FOMU YA UTEUZI
Mgombea Urais Tanzania kupitia Chama cha CHADEMA, Tundu Lissu amefika katika Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuchukua fomu ya Uteuzi ya kugombea Urais
Lissu amefika katika Ofisi hizo na Mgombea Mwenza Salum Mwalim huku wakiwa wamesindikizwa na Wanachama wengine. Wamekabidhiwa fomu hizo na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji wa Rufaa (Mst), Semistocles Kaijage
Uchukuaji fomu za kugombea kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa 2020 umeanza Agosti 5 hadi 25,2020.
Lissu amechukua fomu, wamezihakiki na kujiridhisha kisha wameondoka katika Ofis za NEC ili kuendelea na taratibu nyingine za kichama.
#JamiiForums #Siasa #JFSiasa #Uchaguzi2020