Theb
JF-Expert Member
- Jan 25, 2019
- 3,929
- 7,272
Andiko hili litakua katika sehemu tatu. Sehemu ya kwanza itakua utangulizi hapa nitaelezea maana ya mfumo wa malipo ya mishahara ya waajiriwa, Sehemu ya pili hapa nitatoa changamoto au madhaifu ya mfumo wa malipo ya waajiriwa wapya, Sehemu ya tatu na mwisho nitatoa mapendekezo au mtazamo wangu wa namna ya kuuboresha mfumo na faida zake.
MFUMO WA MALIPO YA MISHAHARA.
Ni mchakato wa kulipa wafanyakazi wa kampuni au serikali unaojumuisha kukusanya orodha ya wafanyakazi wanaopaswa kulipwa, kuhesabu malipo ya wafanyakazi, kusambaza malipo kwa wakati, kurekodi gharama za malipo, pia kukokotoa makato mangine kama vile kodi na bima. (Maana kutoka blog ya zoho)
WAAJIRIWA
Ni wafanyakazi waliothibitishwa na kusajiliwa kwa kuzingatia elimu au ujuzi wenye kuhusiana na kazi wanayofanya.
Kwenye andiko hili nimeangazia zaidi waajiriwa wa kada ya Elimu na Afya. Nimewatumia kama kielelezo cha wengi maana wao ndio huajiriwa kwa idadi kubwa kila mwaka.
MFUMO WA MALIPO YA MISHAHARA YA WAAJIRIWA WAPYA UNAKUMBWA NA MAPUNGUFU YAFUATAYO:-
1. HAUENDANI SAWA NA KASI YA UKUAJI WA SAYANSI NA TEKNOLOJIA.
Mfumo wa malipo ya wafanyakazi au waajiriwa wapya kila mwaka unaenda taratibu vile vile. Waajiriwa wanaripoti vituoni wanakaa zaidi ya mwezl mmoja au miezi miwili au zaidi bila kulipwa mishahara yao. Hili jambo limejirudia kwa miaka sasa. Serikali iwajibike kwa kuboresha kasoro hii. Tupo dunia ya sayansi na teknolojia mambo mengi yanafanyika kwa njia ya internet (mitandao) lakini bado hali imekua yakujirudia. Maboresho katika hili yafanyike.
2. MFUMO WA SASA UNASABABISHA MALIMBIKIZO YA MADENI YA WAAJIRIWA.
Mfumo wa sasa kutokana na utendaji usio endana na wakati tuliopo husababisha kulimbikizwa kwa madeni ya mishahara ya mwanzoni ya waajiriwa wapya. Jambo huiongezea serikali mzigo wa madeni na migororo baina ya wafanyakazi na serikali. Hili linadhibitishwa na kauli ya katibu mkuu wa tamisemi Profesa Shemdoe aliposema "wakurugenzi hakikisheni ndani ya muda huo waajiriwa wote wapya mnawaingiza kwenye orodha ya malipo ya mishahara ili wapate mishahara yao. Kuchelewa kuwaingiza kwenye mfumo wa malipo ya mishahara kutasababisha kwanza kuweka madeni ya watumishi ambalo sio lengo la serikali na pia kuwapa shida watumishi na kujikimu kimaisha" (Profesa Shemdoe 2021, Habari leo).
3. MFUMO ULIOPO WA MALIPO YA WAAJIRIWA HUSABABISHA USUMBUFU AU HUWAONGEZEA WAAJIRIWA UGUMU WA KUJIKIMU.
Mfumo wa malipo ya waajiwa uliopo kutokana na kuchelewa kuwalipa waajiriwa wapya hupelekea usumbufu kwa waajiriwa wapya pia huwaongezea ugumu wa kujikimu kwenye vituo viyao vya kazi walivyopangiwa. Kutokana na hali hiyo ni jambo jema kuuboresha mfumo wa malipo uweze kuwalipa waajiriwa wapya kwa wakati ili wajikimu kimaisha kwenye vituo vyao vya kazi. Hili linasibitishwa na kauli ya Profesa Shemdoe aliposema "kuchelewa kuwaingiza kwenye mfumo wa malipo ya mishahara kutasababisha kuweka madeni ya watumishi ambalo sio lengo la serikali na pia kuwapa shida watumishi na kujikimu kimaisha" (Profesa Shemdoe 2021 Habari leo).
4. MFUMO WA MALIPO YA WAAJIRIWA WAPYA HUSABABISHA WAAJIRIWA KUINGIA KWENYE MADENI ILI WAWEZE KUJIKIMU.
Mfumo wa malipo ya waajiriwa wapya jinsi unavyochelewa kuwalipa waajiriwa wapya hupelekea waajiriwa kuingia kwenye kukopa pesa kutoka kwa watu wanao wazunguka ili waweze kujikimu jambo ambalo sio sahihi kwa maana mishahara hiyo ikisha chelewa inakua malimbikizo ya madeni ambayo hulipwa baadae sana.
MAPENDEKEZO NA USHAURI KUHUSIANA NA UDHAIFU WA MFUMO WA MALIPO YA WAAJIRIWA WAPYA.
1. MFUMO UFANYIWE MABORESHO MAKUBWA YATAKAYO ENDANA NA SAYANSI NA TEKNOLOJIA.
Mfumo uliopo lazima ufanyiwe maboresho makubwa zaidi ili uweze kufanya kazi kwa haraka na kwa wakati na kuweza kuwalipa waajiriwa wapya katika halimashauri zote nchini kwa wakati ili kuondoa usumbufu na kupunguza au kuondoa malimbikizo ya madeni ya waajiriwa serikalini.
2. SERIKALI IONGEZE NGUVU KAZI KATIKA MFUMO WA MALIPO YA WAAJIRIWA WAPYA ULIOPO KWA SASA
Serikali inapaswa kuongeza nguvu kwa kununua vifaa au vitendea kazi bora zaidi pia kuwezesha upatikanaji wa internet kwenye kila halimashauri tena kwa kiwango chenye ubora ili kurahisisha. Pia serikali iwezeshe kuongeza wataalamu wenye ubora zaidi katika mfumo uliopo wa malipo ya waajiriwa wapya. Naimani haya yakifanyika yatasaidia kwa ukubwa na kwa ufanisi zaidi
3. MAANDALIZI YA KUWAPOKEA WAAJIRIWA WAPYA KILA MWAKA YAWEPO TAYARI KWA WAKATI KWA WILAYA ZOTE.
Serikali kupitia halimashauri zote nchini wanapaswa kujiandaa kwa ukamilifu kuanzia kuwapokea waajiriwa wapya, usajili wao na mpaka malipo yao ya kujikimu kwa wakati huo huo. Kwasasa waajiriwa wanaripoti alafu wanasubiria muda wasioujua ndipo walipwe hela ya kujikimu. Mfano tumeshuhudia kwa miaka kadhaa wajiriwa wapya wanaripoti vituoni kwa wakati ila malipo ya hela za kujikimu yanachukua muda mrefu yaweza kuwa wiki mbili, tatu au hata mwezi mmoja. Jambo hili linapaswa kutazamwa kwa umakini maana linawapa usumbufu na ugumu wa maisha kwa waajiriwa wapya.
MFUMO UKIFANYIWA MABORESHO UTAKUWA NA FAIDA ZIFUATAZO.
1. UTAPUNGUZA MALIMBIKIZO YA MADENI YA WAJIRIWA SERIKALINI.
Mfumo huu ukiboreshwa itasaidia kuondoa na kupunguza malimbikizo ya waajiwa serikalini. Kwa sasa kila mwaka serikali ina bakia na malimbikizo ya mishahara ya waajiriwa kutokana na udhaifu katika mfumo au kuchelewa kuwaingiza waajiriwa katika mfumo wa malipo ya mishahara (payroll).
2. KUBORESHWA KWA MFUMO WA MALIPO YA WAAJIRIWA KUTAONDOA USUMBUFU WANAOUPATA WAAJIRIWA WAPYA KILA MWAKA.
Kwa sasa kila mwaka waajiriwa wapya wanapata usumbufu mno miezi ya mwanzo kutokana na kuchelewa kwa malipo ya mishahara yao na hela zao za kujikimu. Mfano kwa mwaka huu wa 2022/2023 waajiriwa wapya walioajiriwa mwezi wa sita na mwezi wa saba hawaja lipwa hela za kujikimu ikiwa pia pesa za mishahara yao ya mwezi wa saba hawajalipwa. Je wataishije kwenye vituo vyao vya kazi.