KERO Serikali ibadilishe mfumo wa ulipaji wa kodi ya majengo, washushe mzigo kwa Wapangaji uende kwa Wamiliki

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Naiomba serikali iweke chaguo katika ulipaji wa kodi ya majengo.

Serikali iandae mfumo wa kuomba Control number kupitia namba za mita ili mwenye jengo aweze kufanya malipo kwa muda anaoutaka na ikiwa hajalipia kwa muda fulani mfano miezi 6 au mwaka mzima basi deni hilo lihamishiwe moja kwa moja kwenye luku yake ya umeme na akatwe pindi atakaponunua umeme wa kwanza baada ya deni hilo kuamishwa. Kupitia hili itaondoa adha na kuwaondolea mzigo wapangaji ambao si walengwa wa kodi hii na mara nyingi wao huwakodi ya jengo pindi wanapohitaji kutumia umeme.

TRA iandae mfumo ambao utamwezesha mwenyenyumba kuchagua muda wa kulipia kodi iwe mwezi mmoja, miezi miwili au zaidi au mwaka mzima.

Kiuhalisia kodi hii ya pango, mzigo hubebeshwa wapangaji badala ya wamiliki.

Kwa kutumia njia hii Mpangaji hatakubali kulipia kiasi kikubwa kwa mfano Tsh. 18,000 na badala yake atapeleka mrejesho kwa mmiliki.

Na hii huenda ikiwa ndiyo mwarobaini wa kilio cha wapangaji.
 
Back
Top Bottom