Mshahara wa Mwezi wa tisa na mwezi wa 10 haujaingia kwa baadhi ya Waajiriwa wapya, huko Karatu-Arusha

Monosex

JF-Expert Member
Jun 10, 2017
892
1,618
Kwako waziri husika, sanasana hapo Tamisemi.

Kwanza nitoe shukrani kwa Rais wa Tanzania, kwa kuweza kutoa ajira, hatimaye nikaitwa kufanya usaili na mwisho wa siku nikapata ajira na kupangwa halmashauri ya karatu.

Kwakweli huu mchakato wa kuingia kazini kwa baadhi ya waajiri wapya umekuwa mchungu sana.

Mimi nilifanikiwa kupata barua ya kupata kazi mwisho wa mwezi wa nane, hiyo barua niliipeleka halmashauri kuripoti kazini, ilikuwa mwanzoni mwa mwezi wa 9, nilijaza kilakitu pamoja na kuandika barua ya kuomba baadhi ya posho ambazo anastahiki kuzipata mwajiriwa mpya.

Baada ya kumaliza hizo hatua, nilipewa likizo ya wiki mbili, wakitoa sababu ya kushughulikia hizo stahiki ili iwe rahisi kwa mimi kuanza kazi. Wiki mbili zilipita bila ya kufanyika chochote, mwisho wa wiki ya tatu mkuu wangu wa idara akanipigia simu kuwa sionekani kituo cha kazi, nikamjibu sina namna ya kuishi huko,sababu sina hela, yeye akasema kuna watu huko hauwezi kufa njaa, nikasema mimi siwezi kuja huko bila hela.

Nikiwa nasubiria stahiki zangu kuingia, bahati nzuri Waziri wa tamisemi akatoa waraka wa kutaka waajiriwa wapya wapewe hela za kujikimu kabla ya Oktoba 30, nikiwa zangu mtaani huko napambana na maisha nikapokea simu tena, hii simu ilikuwa inatoka kituo changu cha kazi ikinitaka kwenda kujaza (Vendor form), nikasema huu mbona ni usumbufu, kwanini hii fomu hawakunipa kipindi nimefika kuripoti awali na niliandika barua ya kuomba hela za kujikimu(Siasa)

Nilikopa hela na kwenda kujaza hiyo fomu na wasaa huo nikachukua barua hapo halmashauri(HQ), na kwenda kuripoti kituo cha kazi, hiyo ilikuwa ni wiki ya mwisho ya mwezi wa 9, hapo ukizingatia mwezi wa tisa umepita hakuna hela yoyote iliyoingia kwenye akaunti.

Mwezi wa kumi mwishoni nikitegemea hata hela ya mshahara na kujukimu kuingia, lakini haikuwa hivyo, lile agizo la Waziri wa Tamisemi likatekelezwa, hela ya kujikimu iliingia na ilikuwa laki 5 na 60, lakini mshahara hakuna wa mwezi wa tisa na mwezi wa kumi, hadi leo.

Sasa hiyo hela tajwa hapo juu ndiyo isafirishe mizigo, nauli, hela ya kupanga nyumba(ukizingatia huko kijijini hakuna nyumba za watumishi), hiyo hela ndiyo uende nayo field ukahudumie wananchi na ruti moja inakutaka utumie mafuta lita nne kwenye pikipiki, na huko kijijini lita ya mafuta ni shilingi elfu 4x4=16000.

Ukienda kuulizia mshahara kwa HR( HQ), anatoa jibu rahisi tu, eti utaidai serikali sijui masuala ya areazi(sijui ni nini hii)

Sasa Waziri husika wa hili naomba ulitatue, la hela ya kujikimu walitekeleza, vipi mishahara ya miezi miwili, mpaka sasa hakuna, mimi nilikuwa nadhani watumishi wanaokimbia vituo vya kazi wanafanya makusudi, kumbe wana mengi moyoni Dkt. Gwajima D naomba unisaidie Kumpatia huu ujumbe Mh. Mchengerwa.
 
Back
Top Bottom