Charles Mandela
JF-Expert Member
- Dec 9, 2011
- 2,472
- 2,165
Mimi sio muongo, wala mimi sio mtu wa kupenda sifa kwa sababu mimi ningelikuwa mpenda sifa, TANZANIA nzima ingelinifahamu lakini kwa sababu sipendi sifa, hata kitongoji ninachoishi kwa sasa hawanitambui.Huyu jamaa ni mwongo na ni mpenda Sifa
NECTA siku zote huwaga wanatoa Grade tu sio maksi na kama mtu wakawanza ameongoza mathalani ana one point 7 hii haizuhi mwanafunzi mwingine kuwa na one point 7 ila hapa utpfauti unabakia kuwa wakwanza alikuwa na alama zipi kwa wastani wake ukilinganisha na huyu mwingine ambaye hata kumi Bora hajaingia lakini ki grade wanalingana na yule aliyekuwa wakwanza
Pia swala la matokeo yaliyo tajwa kutofautiana na na yale yaliyoko kwenye cheti au mfumo sio kweli hakuna udanganyifu wa hivyo leo hii mtu anatajwa kwenye matokeo ukiangalia net utakuta hivyo hivyo na hata kwenye cheti huwa hivyo hivyo
Kwa maelezo yake huyu jamaa Mandela, ni upotoshaji na pia anapandikiza chuki kwa watanzania kuhusu watu wa MARA
Hii nchi inamisingi yake ambayo imetukuka toka enzi na enzi na pia hilo Baraza la mitiani NECTA limepata heshima kubwa ndani na nje ya Tanzania kwa waledi na ufanisi ulio tukuka
Inabidi na wewe, ifike mahala useme ukweli, kwa sababu hata Rais Magufuli mwenyewe anasema - Msema kweli ni mpenzi wa Mungu! Sasa mimi ni nani hata niseme uongo!?
Kwanza mimi nikisema uongo huwa naota ndoto mbaya usiku! Huwa silali kabisa! Kwa hiyo huwa najitahidi kusema ukweli ili niepuke ndoto zisizo na ulazima wa kuziota.
Sasa nisizungumzie wengine! Nipate hii fursa ya kujitetea na tuhuma za kuniita mimi ni muongo. Wakati mimi siku zote nimekuwa nikiishi kwa kusema ukweli.
Haya angalia matokeo ya wanafunzi bora waliofanya vizuri kitaifa kidato cha nne - mwaka 2007. Halafu uangalie na matokeo ya wanafunzi wa shule ya UHURU iliyopo mkoa wa Shinyanga. Angalia hata kwenye website ya NECTA tu! Halafu uniambie ukweli wako kuhusu mimi ni upi?
Mimi ni kijana mwenye heshima! Siwezi kuingia kwenye mitandao ya kijamii na kuanza kusema uongo! Napata faida gani! Na ili iwe nini?
Pengine wewe unaweza kuwa unanifahamu lakini mimi sikufahamu, kwa sababu unatumia utambulisho usio rasmi!
Mimi ningelikuwa ni kijana muongo, nisingelifika huku nilipo leo! Na nilitaka kupiga hatua kimataifa zaidi, lakini vyeti ndio vikaleta shida!
Mimi sio mtu muongo muongo! Hata mafanikio yangu nikiwa Chuo Kikuu Cha Dodoma yanajieleza wazi.
Hauwezi kupata nyadhifa zote hizi kama wewe ni mtu muongo muongo tu. Kuwa Deputy Speaker Of The Parliament, Speaker Of The Parliament na mwaka huo huo kuwa Council Secretary Of The Federation, haikuishia hapo tu nilikuwa President Of College Of Humanities & Social Sciences, mwaka 2012/13. Hii ikiwa ni mara ya kwanza kabisa kwa College Of Humanities & Social Sciences kuwa na Rais kutoka College Of Earth Sciences - School of Mines & Petroleum Engineering.
Kwa hiyo unapojadili kitu fulani na mimi, fahamu kuwa unajadili kitu hicho na kijana mwenye haiba ya URAIS!
Na nadhani kuna kitu natakiwa kufanya kwa College Of Humanities & Social Sciences kama shukrani, kwa sababu kitendo cha kuwa Rais wa awamu 5 kutoka College nyingine haikuwa kazi rahisi. Waliokuwepo watasimulia, haikuwa kazi ndogo hakika!
Sasa natakiwa kuandaa mradi ambao utakuwa ni mradi endelevu wa maendeleo ya kitaaluma, sio jambo jema kuzungumza mapema! Muda ndio hakimu mzuri, ukifika utaamua!