Abdusmigo
Member
- Feb 2, 2024
- 9
- 3
Kwa majina naitwa Abdul Komando Mtimbe (19) ninaishi Dar es salaam Tanzania.Nimezaliwa tarehe 07.12.2004
Nimepata elimu yangu ya msingi katika shule ya msingi Mchangani wilaya ya Kinondoni jijini DAR ES SALAAM ambapo nilianza mwaka 2010 na kumaliza 2016 na nilifanikiwa kujiunga na elimu ya sekondari mnamo mwaka 2017 kidato cha kwanza mpaka mwaka 2019 kidato cha tatu(sikufanikiwa kumaliza shule kwa sababu nilifukuzwa kwa makosa ya utoro) katika shule ya Makumbusho iliyopo wilaya ya Kinondoni mkoa wa DAR ES SALAAM.
Ilipita muda kadhaa baada ya jitihada za kujaribu kurudi shuleni kugonga mwamba
Kipindi chote hicho nilikuwa nipo tu mtaani huku nikiwa sina shughuli ya kufanya.Ndipo mnamo mwaka 2021 nilpoamua kwenda kumtembelea kaka yangu mkoani Lindi.Yeye (kaka yangu) alijaribu kunitafutia shule lakini ilishindikana ndipo mwaka uliofata (2022) ndipo lilipo kuja wazo la kwenda kusoma QT (Qualifying Test) katika kituo cha Lindi Secondary school centre ili niweze kupata credits za kufanya mtihani wa kumaliza kidato cha nne.Namshukuru mungu mwaka ule niliweza kujisajili ili niweze kufanya huo mtihani.Nilifanikiwa kufanya mtihani na kufaulu(pass) mimi pekee ambapo kiujumla tulikuwa wawili tu (mwenzangu alikuwa ni binti ambaye nilimjua kwa majina Mwajuma Mbwesso) kituoni hapo tunaofanya mtihani wa QT.Hivyo basi kwa namna moja au nyingine niliweza kupata credits ambazo ziliniifanya niwe na sifa ya kufanya mtihani wa mwisho wa elimu ya sekondari.
Baada ya hapo mwaka uliofuata (2023) nilirudi tena kituoni hapo ili niweze kujisajili kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya sekondari namba yangu ya mtihani ni P.0324/0007.Nilifanikiwa kujisajili masomo yapatayo kumi (History,Geography,Kiswahili,English, Civics, Mathematics, Physics, Biology, Chemistry pamoja na Literature) na niliweza kulipa gharama zote na gharama za ziada (pesa ya vifaa kwa ajili ya mitihani ya vitendo yaani practical masomo ya Biology, Chemistry pamoja na physics). Basi siku zilipita huku na mimi mwenyewe nikijitahidi kwa juhudi zangu binafsi katika kusoma mpaka ilipofika kipindi cha mitihani na nilifanikiwa kufanya mitihani yote hapo kwenye kituo na kumaliza salama kabisa.
Mnamo mwaka huu(2024) majibu yalirudi huku nikipata ufaulu huo ambapo ulikuwa kama ifuatavyo;
Civ.D, Kisw.D, Hist:A, Geo:C, Eng L.:C, Lit:C, Phy:C, Chem:C, Bios:C, B.Math.D.
Baada ya kusema hayo hivi sasa nina tamani nifikie ndoto zangu za kuwa mtumishi katika sekta ya afya hapa nchini kwani bado nahitaji kusoma niongoze elimu lakini nikiitazama hali ya uchumi nyumbani kwetu ni shida mno (nimelelewa na mzazi mmoja tu mpaka nakuwa ambaye ni mama yangu) na hapa nilipo nipo njia panda kwanza sijui kuwa kama nitachaguliwa kuendelea na elimu ya juu yaani Advance au kwenda chuo(college).
Hivyo basi kwa yeyote ambaye ameguswa na hili na atakae tokea kunisaidia iwe kwa ushauri,maoni au hata kunisaidia ili niweze kupata fedha za ada ili niweze kujiunga na chuo nipo tayari.
Mawasiliano yangu ni
0685747569
0626691587
ASANTENI