Mfahamu T.O Kihombo 2006 aliyepata Degree yake ya Kwanza baada ya Miaka 11

Evans Richard Arsenal

JF-Expert Member
Jul 11, 2018
365
750
Imepita miaka takribani 12 sasa, tangia Tanzania ilipapata kumshuhudia mwanafunzi aliyeshindikana katika maswala ya Elimu hapa namzungumzia,Tanzania One (2006) Elias Kihombo katika matokeo ya Kidato cha Sita mwaka 2006 akitokea shule ya sekondari Tosamaganga wengi wanapenda kuiita Tosa Boy's

Mwaka 2006, Necta ilimtangaza mwanafunzi Elias Kihombo kutoka Tosamaganga Secondary School kuwa ndo kipanga wa mwaka huo akiwapita wanafunzi wenye akili zaidi waliovuma toka shule kongwe na special schools kama kibaha, ilboru, mzumbe, kilakala, Tabora boys etc ukweli ni kwamba Elias Kihombo hakuwa maarufu kwa kipindi hiko na wengi walisikia tu story zake haswa kwa wanafunzi wa Mzumbe Boys ambao Mara nyingi walipata kumuona katika mazingira yao.

Kumbuka kwamba Elias Kihombo hakupewa Priority kubwa sana ya kuwa T.O wa Advance Level kutokana pia na matokeo yake ya Kidato cha Nne (4) kuonekana kuwa ya kawaida sana, Kihombo alifanikiwa kupata Division One (1.14) akiwa na Physics-A Chemisrty-A Biology-B na Mathematics-B, Mwaka huo 2003 alipata kuchaguliwa Tanga Technical school iliyopo mkoa wa Tanga (tetesi) kuendelea na masomo ya kidato Cha tano, lakini baadae aliamua kurudi tena katika shule yake ya zamani yaani Tosamaganga secondary school kuendelea na masomo yake ya Advance level.

Mwaka 2006 alifanikiwa kumaliza kidato Cha sita katika shule ya secondary Tosamaganga secondary akiwa ndiye mwanafunzi bora kitaifa, Alifanikiwa kupata maksi za juu sana na kupata Division One of point Three (1.3)
Physics-A
Chemistry-A
Advanced Mathematics-A

October 2006 Alichaguliwa kujiunga na University of Dar Es Salaam (UDSM) akiwa kama T.O kusoma Bachelor of Science In Telecommunication Engineering (4years) na tetesi zinasema alifanikiwa kupata ufadhili wa masomo yake chini ya kampuni ya Airtel.

Siku zilienda na alikuwa karibu kumaliza Elimu yake ya chuo kikuu, huku akipata madili mengi ya kufundisha Tuition maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dar Es Salaam na shule nyingi za sekondari ndani ya Tanzania hasa shule za Advance.

Lakini baada ya Miaka 4 kupita ikiwa miezi michache tu imebaki ya kumaliza chuo Tanzania One Kihombo ali-disco chuo na hivyo kumfanya asifanikiwe kupata degree yake ya kwanza mwaka huo 2010, lakini wengi wanasema hakupaswa kudisco chuo lakini ndivyo ambavyo Hatima yake ilipoishia hapo. (tetesi ).

Moja kati ya maneno ambayo wengi wanamnukuu aliyopata kuyasema ndani ya Miaka hiyo, alisema "Duniani walionipita kwa akili ni watu wawili tuu wa kwanza Mola, wa pili ni Mzungu" hapa ndipo hatima yake inavyosemekana ikafungwa na wakuu wake lakini wengine wanasema vingine.

Elias hakutaka kwenda chuo chochote kile na ndani ya Miaka hiyo mitatu baada ya kudisco chuo, yaani 2011,2012 na 2013 alikuwa anazunguka shule mbalimbali za sekondari Tanzania kupiga mapindi ya Physics na Chemistry na kwelii huyu jamaa alikuwa ni Invisible katika masomo hayo mawili, Japo Pure Mathematics alikuwa hafundishi kabisa kwasababu alikuwa anasema "Siwezi kufundisha Somo rahisi duniani kama Pure Mathematics, Mimi nafundisha Physics na Chemistry tu"

Ndipo baada ya Miaka mitatu kupita (3) T.O Elias Kihombo aliyetukuka zaidi katika vinywa vingi vya wanafunzi wa Tanzania, kutokana na ufundishaji wake na kuwaita wanafunzi wake nyumbu na kuwa na jeuri ya kuwa na akili zaidi ya watu wengine, alifanikiwa kurudi tena ndani ya University of Dar Es Salaam safari hii akiwa ameamua na amedhamiria kuchagua kozi nyingine Mpya kabisa iliyoanzishwa mwaka huo 2013 hapohapo Udsm iliyoitwa (Bachelor of Science In Petroleum Engineering). Hii kozi ilikuwa inachukua wanafunzi 20 pekee Tanzania nzima tena wale waliosoma PCM tu (Physics, Chemistry na Advanced Mathematics) na waliopata Marks za juu kabisaa. Na safari hii alikutana na Mbabe mwenzake Tanzania One wa mwaka huo 2013 aliyeitwa ERASMUS INYASE kutoka Shule ya sekondari ILBORU Mkoani Arusha kwenye kozi moja ndani ya University Of Dar Es Salaam (UDSM).

Inawezekana mwaka 2013 ndio mwaka pekee katika historia ya Tanzania kuchukua Ma-T.O wawili kwenye Kozi moja (Petroleum engineening). Kumbuka kwamba ELIAS KIHOMBO alipata Division 1.3 (AAA) kwa mwaka 2006 na huku Tanzania one wa mwaka 2013 ERASMUS INYASE alipata Division 1.5 (CAA). Na hivyo kumfanya ELIAS KIHOMBO kuongoza kwa Cut off points 15 na akifatiwa na ERASMUS INYASE mwenye Cut off points 13.

Baada ya Miaka 4 kupita, ndipo July 2017, T.O Elias Kihombo alifanikiwa kumaliza Degree yake ya kwanza (Bachelor of Science In Petroleum Engineering) na mnamo November 2017 Elias Kihombo alifanikiwa kutunukiwa Degree yake ya kwanza akiwa ndani ya University of Dar Es salaam baada ya Miaka 11 kupita.

Hapa imepita Miaka mingi tangia, 2006 Engineer Elias Kihombo alivyotangazwa kuwa Tanzania One lakini ilimchukua Miaka mingine 11 mpaka kutunukiwa Degree yake ya kwanza. Huyu ndiye The Best Of The Best, Eng Elias Kihombo Mwanafunzi aliyepata kutokea Tanzania na kuwaonesha wengine uwezo wake katika nyanja nzima ya Elimu.

Wapo wengi wanaojiuliza Eng Elias Kihombo yupo wapi kwa sasa, Lakini mpaka sasa Kihombo yupo chini ya Himaya ya Mkoa wa Geita Nyumbani kwa Mheshimiwa Rais John Joseph Pombe Magufuri, huku akiendeleza harakati zake na akiwa na vitabu vyake vingi alivyoviandika kuwasaidia vijana wa Tanzania ikiwa pamoja na Physics Books na Chemistry Books.


Written by Eng EVANS RICHARD.

We Always Live To Fight Another Day




IMG_20180725_093224.jpg
IMG_20180725_094553.jpg
IMG_20180725_093123.jpg
 
Last edited:
Yani mtu aliyepata bachelor degree baada ya miaka 11 ndo unamsifia hivi!!?

Nlivoanza kusoma uzi nlifikiri ntakutana na mtaalamu aliyevumbua kitu fulani kumbe ni mwalimu wa tuition.
Kila mtu ana passion fulani ndani yake. So kama passion yako ww ni kupata pesa nuingi, mwingine passion yake ni kufundisha, mwingine kuvumbua.. na n.k

Nilivyo muelewa mtoa post ni kwamba jamaa ni genius but aliamua kufuata passion yake regardless alichokisomea. Most of genius huwa wanaona regular job ni boring so huwa wanafuata passion zao.
 
Back
Top Bottom