Mfahamu Ferruccio Lamborghini, mwanzilishi wa kampuni ya LAMBORGHINI, mapito yake binafsi ya kimaisha na kampuni yake mpaka sasa

I am Groot

JF-Expert Member
Jul 20, 2018
3,731
10,033
KARIBU SANA MWANA JAMIIFORUM TUJIFUNZE na ruksa kukosoa chapisho.

images (6).jpeg

FERRUCCIO LAMBORGHINI


Zamani nilinunua magari mashuhuli sana ya gran Turismo na katika kila hizi gari nililinunua niliona zina mapungufu. Yana joto sana, au hayakupi ile starehe, au hayana kasi ya kuridhisha au hayajamaliziwa kikamilifu. Sasa, nataka kutengeneza gari za G.T. zisizo na mapungufu. Na wala sio mabomu ya kimakenikia tu. Ya kawaida sana, rasmi sana, ila gari lililo bora"– Ferruccio Lamborghini (1963)

Mwaka 1958, mtengeneza matrekta Ferruccio Lamborghini hatimaye alipata pesa za kutosha kununua gari yake mwenyewe aina ya Ferrari 250GT. Kwa mafadhaiko ya Lamborghini na shida ya krachi (clutch) aliyokuwa akikutana nayo, ilimlazimu kuipeleka gari yake mara kwa mara gereji kwa matatizo yale yale ya clutch. Alikuwa na waajiriwa wake mwenyewe ambao walikuwa wakiishughulikia Ferrari, mara kadhaa walikutana na vifaa kama vile vile alivyokuwa akitumia kutengezea trakta zake. Lamborghini aliapa kama kutakuwa na watu atakuwa wananunua magari ya michezo (sports cars) kutoka Italia, basi watastaajabishwa sana na mwenendo wa hilo gari, uundwaji wake, na hata urembo wake wa hali ya juu ambayo ipo siku atatengeneza. Mwaka mmoja baadae, Lamborghini alianzisha kampuni yake ya utengenezwaji wa magari wa aina hiyo (sports cars) lakini pia (luxurious car kwa pamoja 2 in 1). Hivi ndivyo kampuni AUTOMOBILI FERRUCCIO LAMBORGHINI S.P.A ilizaliwa.
images (12).jpeg


Tumeanzia mbali kidogo, basi hebu ngoja nikurudishe kwanza nyuma zaidi kabla ya yote hayo. Karibu tuendelee...

Ferruccio Lamborghini, alikuwa ni mtoto mkubwa zaidi katika familia yao ya watoto watano, na alizaliwa katika eneo linaloitwa Renazzo, huko nchini Italia mnamo mwaka 1916. Alikuwa katika familia ya kikulima na waliishi na familia yake huko kwenye shamba la familia katika kigango cha ferrara, alipata mchocheo wa maisha kwenye karakana moja ya farmstead akijifunza na kutengeneza tengeneza mashine mbalimbali. Aliacha shule ya msingi na kwenda kujiunga chuo cha ufundi cha Fatelli Taddia karibu na mji wa Bologna na kupokea leseni yake ya ufundi mwaka 1934, aliajiriwa kwenye kiwanda cha Cavalier Righi kilichopewa tenda ya kuzalisha vyombo vya kivita.

Wakati vita vya dunia vya pili (WWII) vilipoingia Italia, jeshi la anga la italia ITALIAN ROYAL AIRFORCE ilimchagua pia Lamborghini, mkanikia mzoefu na kumtuma huko Rhodes nchini Greece. Aliandikishwa kwenye kitengo cha kumi na tano cha mafundi wa mota wa kampi mbalimbali chini ya sera moja. Kundi hili liliwajibika na matengenezo na ukarabati wa vifaa vya jeshi la Italia kwenye kisiwa hicho, ikiwemo matrekta na malori ya diseli yaliyotumika kuvuta ndege. Lamborghini mapema sana alichaguliwa kama kiongozi mkuu wa karakana.

Mwaka 1943, baada ya vita huko Rhodes, alibaki kwenye kisiwa kilichotwaliwa na Ujerumani na kufungua duka lake la kwanza la spea za makenika. Katika kipindi hiki, alikutana na mke wake wa kwanza, Clelia. Mwaka 1946, alirudi Italia na kuchukulia fulsa ya programu ya maboresho ya kiuchumi, alifungua duka la spea za maboresho na vifaa vya kuundia vyombo vya moto katika kijiji cha Cento.

Wakati akiwa Cento, Lamborghini aligundua wakulima wa eneo hilo wakihangaika kulima mashamba yao bila matrekta, kitu ambacho kiuhalisia wasingeweza kumudu hata hivyo. Hapo ndipo alipopata wazo la kutengeneza matrekta yasiyo na gharama kimanunuzi na utunzaji, na ambayo yatakuwa rahisi kuyatengeneza yakipata itilafu.

Wazo hilo lilimpelekea Lamborghini kukopa pesa kwa baba yake ambazo zingewasaidia familia katika kipindi kigumu hasa cha kilimo. Kutokana na wazo la Ferruccio la kuanzisha kampuni ya trekta kuonekana gumu kutekelezeka; ilimchukua baba moyo mzito sana kuitoa sadaka familia yake kisa mtu mmoja. Lakini alifanikiwa kutokana na ujasiri na kutokuogopa changamoto.

Mwaka 1948, kipindi cha mavuno, Lamborghini alitambulisha trekta lake na kufanikiwa kuuza trekta 11 kwa mara moja. Kama nilivyoeleza kabla; kwa ruhusa ya baba yake, aliweka shamba la baba yake kama dhamana benki ili kununua injini 1,000 na kuanzisha uzalishaji mkubwa wa matrekta.
images (7).jpeg


Lamborghini ya kwanza (gari; sports car), model 350 GTV ilibuniwa na Franco Scaglione. Gari ya majaribio (prototype) ilitengenezwa kwa miezi minne, na iliwekwa katika jumba la maonyesho ya magari mapya ya Turin Motor Show mwaka 1963.
1965_Lamborghini_350_GT.jpg

~350 GTV model

Uzalishaji wao wa kwanza wa magari ulikuwa ni wa aina ya 350 GT, ukifuatwa baadae na aina ya 400 GT. Shauku na umakini wa Lamborghini uliwaongoza mafundi wake kuongeza ubunifu wa ukisasa katika magari ya sports cars kama aina ya Miura, Islero, Espada, na Jarama, na ulimwengu wa kipekee wa kila toleo la kila modeli mpya iliyotoka..
download.jpeg


Miaka ya 1970, kipindi cha mtikisiko wa kuyumba kwa soko la mafuta; uliyumbisha na kubadilisha sana soko la magari ya kifahari ya kiwango cha juu. Mwaka 1987 Ferruccio aliiuza kampuni ya Lamborghini kwa Chrysler. Na mwaka 1994, Chrysler aliuza brand kwa MegaTech, na mwaka 1998, the Volkswagen Group walinunua brand.
images (14).jpeg


Linapokuja swala la luxury, utendaji bora, na urembo, majina kidogo ya manjonjo inaipa sana heshima Lamborghini. Kampuni ya Lamborghini huzalisha wastani wa magari chini ya magari 8,500 kwa mwaka, Lamborghini ina matamasha machache sana. Ujasiriamali moyoni, safari ya Lamborghini ilianza kwenye karakana katika shamba la familia; ilimbeba na kumpelekea kuunda matrekta yaliyotokana na spea pati za vyombo vya moto vya jeshi, mpaka kuwa mmoja wa waanzilishi wa magari ya luxury sports bora sana ya duniani. Nini kinamtofautisha Lamborghini na wengine? ni kile alichotuachia (legacy): Diablo, Miura, Countach, na Murciélago.
images (9).jpeg


Leo hii tunajivunia kuona ndoto ya Lamborghini ikiendelea kuenziwa vilivyi kwa kuletewa sokoni modeli bora kabisa katika ushindani wa magari ya sports cars kama LAMBORGHINI; Huracan EVO na
Huracán.
images (13).jpeg

~Lamborghini Huracán. 9.5. (2024)
 
Back
Top Bottom