Mfahamu muigizaji Hrithik Roshan (KRRISH)

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Sep 7, 2016
17,431
21,120
Jina lake kamili anaitwa Hrithik Rakesh Roshan ni mtoto wa pili kuzaliwa na mtayarishaji,muongozaji na muandishi wa filamu Rakesh Roshan (baba) na Pinky Roshan (mama).

Hrithik Roshan ni mtoto wa pili kuzaliwa (mziwanda) wa kwanza ni dada yake anaitwa Sunaina Roshan.

Hrithik Roshan alizaliwa 10 January 1974 huko Mumbai (Bombay) katika Jimbo la Maharashtra magharibi mwa India.

Mumbai ilibadilishwa jina na kuitwa Bombay mwaka 1995.
Hrithik Roshan, amesoma shule ya Bombay scoottish,na baadaye kujiunga na chuo kinachoitwa Sydenham college,ambako alipata bachelor degree in commerce, baadaye alienda kusomea Sanaa za Maonyesho katika taasisi ya Gordonstoun nchini Scotland.

Hrithik Roshan alipata ugonjwa wa uti wa mgongo ujulikanao kama Scoliosis akiwa na miaka 21 na madakatari wakasema hatoweza tena kuigiza wala kucheza muziki lakini Hrithik Roshan hakukata tamaa hivyo ikamlazimu kufanyiwa upasuaji na bahati nzuri upasuaji ulienda vizuri akaweza kuvuka changamoto hiyo.

Hrithik roshan ni muigizaji maarufu na mwenye mafanikio katika industry ya Bollywood,pia amewahi kupata tunzo 6 za Filmfare awards,Hrithik ametajwa na media mbalimbali za India mara kadhaa kuwa ndio muigizaji mwenye mvuto zaidi .

Kabla ya kuwa muigizaji,Hrithik Roshan alikuwa anamsaidia baba yake Mzee Rakesh Roshan kwenye uongozaji wa filamu (muongozaji msaidizi) pia alikuwa anafanya kazi ya kuhudumia chakula na kufanya usafi sehemu ambazo zilitakiwa kufanyiwa filamu.

Miongoni mwa filamu maarufu ambazo Hrithik Roshan alikuwa muongozaji msaidizi ni Karan Arjun na filamu ya Koyla zote alicheza Shah Rukh Khan(SRK).

Hrithik Roshan alianza kuigiza mwaka 2000 na filamu yake ya kwanza ilikuwa inaitwa Kahona Pyaar Hai ambayo alicheza na Amesha Patel na wote hao hiyo ndio ilikuwa filamu yao ya kwanza ,na iliwaletea mafanikio makubwa mno.

Filamu zingine alizowahi kucheza Hrithik Roshan ni pamoja na ;
  1. Kabhi Khushi Kabhie Gham (2001)
  2. Koi... Mil Gaya (2003)
  3. Dhoom 2 (2006)
  4. Jodhaa Akbar (2008)
  5. Zindagi Na Milegi Dobara (2011)
  6. Agneepath (2012)
  7. Krrish Series: Krrish (2006), Krrish 3 (2013)
  8. Super 30 (2019)
  9. War (2019) pamoja na filamu ya 10)Kites iliyotoka mwaka 2010 alicheza pamoja na Kangana Ranaut.
Hrithik amepitia mahusiano ya kimapenzi na waigizaji: Kareena Kapoor, Kangana Ranaut na Barbara Mori(Huyu ndiye mchepuko aliyesababisha Hrithik kutengana na mkewe(Suzan Khan)).

Pia kumewahi kuwepo fununu ya Hrithik kuwa na mahusiano na Shweta Bachchan (Binti wa Amitabh Bachchan) na muigizaji Saba Azad.

20 Desemba 2000 alifunga ndoa na Sussane Khan ambaye walitalakiana mwaka 2014. Hadi Sasa ana watoto wawili wa kiume, Hrehaan Roshan na Hridhaan Roshan.

Ikumbukwe Hrithik ni muhindu na Suzan Khan alikuwa muislamu japo dini haikuwa kikwazo Cha wao kutalikiana.

Baada ya filamu ya Main Prem Ki Deewani Hoon (2003) kutoka, aliyekuwa mke wake alimkataza kufanya filamu nyingine na Kareena Kapoor baada ya kuona ukaribu wao wakati wa ufanyaji wa filamu hiyo

Jamaa anapenda sana mazoezi ya viungo na kujali sana afya yake na mlo. Aliwahi kuwa na uraibu wa sigara, alipofanikiwa kuacha uvutaji amekuwa akiipiga vita na kuwasisitiza watu kutovuta.

Wakati filamu Zindagi Na Milegi Dobara (2011) inafanyika aliamua kufanya mwenyewe matukio hatarishi yote: Kukimbizana na fahali(ng'ombe dume), Kuruka kutoka angani(Skydiving) na kuzama chini ya maji(Underwater Diving).

Mwaka 2009 wakati akifanya filamu ya Kites (2010), alifanikiwa kukutana na mtu aliyefanya apende kucheza muziki, Michael Jackson.

Licha ya utajiri wake Lakini ana shida ya kushindwa kusimamia pesa zake: Mama yake ndiye anayezisimamia, na mke wake alikuwa anasaidia.

Wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa huko Afrika ya Kusini, picha yake ilitumika kupiga kampeni za kukipa kura chama pinzani, Democratic Alliance (DA), jambo ambalo lilipelekea filamu zake kufungiwa kuoneshwa Afrika ya Kusini.

Tiger Shroff ndiyo shabiki yake mkuu na anamuhesabu Hrithik kama msukumo wake katika filamu.

565849040.jpg

Nje ya kazi ya kuigiza,Roshan pia ni stage performer na playback singer,pia ameendorse bidhaa mbalimbali ,ikiwa ni pamoja na kuhost reality show inayoitwa Just dance, na pia amelaunch nguo zake/brand yake.
 
Ikumbukwe Mtanzania mwenzetu mwanadada Irene Uwoya aliamua kumpa mwanaye jina la Krish baada ya kuvutiwa na uigizaji wa Hrithik Roshan katika filamu ya Krrish filamu ambayo Hrithik Roshan akitumia jina la Krish (kifupi) au Krishna (kirefu chake) .

Sababu kuu aliyoamua kujikatisha jina kutoka Krishna mpaka Krish ili watu wasiweze kumtambulisha kuwa ni yeye ndiye aliyekuwa akifanya maajabu na ili kuficha utambulisho wake akaamua kabisa kutafuta na mask kuficha sura yake.
 
Baadhi ya matukio katika filamu ya Koi Mil Gaya , humu jamaa alionesha uwezo wa hali ya juu wa body transformations
 
Jina lake kamili anaitwa Hrithik Rakesh Roshan ni mtoto wa pili kuzaliwa na mtayarishaji,muongozaji na muandishi wa filamu Rakesh Roshan (baba) na Pinky Roshan (mama).

Hrithik Roshan ni mtoto wa pili kuzaliwa (mziwanda) wa kwanza ni dada yake anaitwa Sunaina Roshan.

Hrithik Roshan alizaliwa 10 January 1974 huko Mumbai (Bombay) katika Jimbo la Maharashtra magharibi mwa India.

Mumbai ilibadilishwa jina na kuitwa Bombay mwaka 1995.
Hrithik Roshan, amesoma shule ya Bombay scoottish,na baadaye kujiunga na chuo kinachoitwa Sydenham college,ambako alipata bachelor degree in commerce, baadaye alienda kusomea Sanaa za Maonyesho katika taasisi ya Gordonstoun nchini Scotland.

Hrithik Roshan alipata ugonjwa wa uti wa mgongo ujulikanao kama Scoliosis akiwa na miaka 21 na madakatari wakasema hatoweza tena kuigiza wala kucheza muziki lakini Hrithik Roshan hakukata tamaa hivyo ikamlazimu kufanyiwa upasuaji na bahati nzuri upasuaji ulienda vizuri akaweza kuvuka changamoto hiyo.

Hrithik roshan ni muigizaji maarufu na mwenye mafanikio katika industry ya Bollywood,pia amewahi kupata tunzo 6 za Filmfare awards,Hrithik ametajwa na media mbalimbali za India mara kadhaa kuwa ndio muigizaji mwenye mvuto zaidi .

Kabla ya kuwa muigizaji,Hrithik Roshan alikuwa anamsaidia baba yake Mzee Rakesh Roshan kwenye uongozaji wa filamu (muongozaji msaidizi) pia alikuwa anafanya kazi ya kuhudumia chakula na kufanya usafi sehemu ambazo zilitakiwa kufanyiwa filamu.

Miongoni mwa filamu maarufu ambazo Hrithik Roshan alikuwa muongozaji msaidizi ni Karan Arjun na filamu ya Koyla zote alicheza Shah Rukh Khan(SRK).

Hrithik Roshan alianza kuigiza mwaka 2000 na filamu yake ya kwanza ilikuwa inaitwa Kahona Pyaar Hai ambayo alicheza na Amesha Patel na wote hao hiyo ndio ilikuwa filamu yao ya kwanza ,na iliwaletea mafanikio makubwa mno.

Filamu zingine alizowahi kucheza Hrithik Roshan ni pamoja na ;
  1. Kabhi Khushi Kabhie Gham (2001)
  2. Koi... Mil Gaya (2003)
  3. Dhoom 2 (2006)
  4. Jodhaa Akbar (2008)
  5. Zindagi Na Milegi Dobara (2011)
  6. Agneepath (2012)
  7. Krrish Series: Krrish (2006), Krrish 3 (2013)
  8. Super 30 (2019)
  9. War (2019) pamoja na filamu ya 10)Kites iliyotoka mwaka 2010 alicheza pamoja na Kangana Ranaut.
Hrithik amepitia mahusiano ya kimapenzi na waigizaji: Kareena Kapoor, Kangana Ranaut na Barbara Mori(Huyu ndiye mchepuko aliyesababisha Hrithik kutengana na mkewe(Suzan Khan)).

Pia kumewahi kuwepo fununu ya Hrithik kuwa na mahusiano na Shweta Bachchan (Binti wa Amitabh Bachchan) na muigizaji Saba Azad.

20 Desemba 2000 alifunga ndoa na Sussane Khan ambaye walitalakiana mwaka 2014. Hadi Sasa ana watoto wawili wa kiume, Hrehaan Roshan na Hridhaan Roshan.

Ikumbukwe Hrithik ni muhindu na Suzan Khan alikuwa muislamu japo dini haikuwa kikwazo Cha wao kutalikiana.

Baada ya filamu ya Main Prem Ki Deewani Hoon (2003) kutoka, aliyekuwa mke wake alimkataza kufanya filamu nyingine na Kareena Kapoor baada ya kuona ukaribu wao wakati wa ufanyaji wa filamu hiyo

Jamaa anapenda sana mazoezi ya viungo na kujali sana afya yake na mlo. Aliwahi kuwa na uraibu wa sigara, alipofanikiwa kuacha uvutaji amekuwa akiipiga vita na kuwasisitiza watu kutovuta.

Wakati filamu Zindagi Na Milegi Dobara (2011) inafanyika aliamua kufanya mwenyewe matukio hatarishi yote: Kukimbizana na fahali(ng'ombe dume), Kuruka kutoka angani(Skydiving) na kuzama chini ya maji(Underwater Diving).

Mwaka 2009 wakati akifanya filamu ya Kites (2010), alifanikiwa kukutana na mtu aliyefanya apende kucheza muziki, Michael Jackson.

Licha ya utajiri wake Lakini ana shida ya kushindwa kusimamia pesa zake: Mama yake ndiye anayezisimamia, na mke wake alikuwa anasaidia.

Wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa huko Afrika ya Kusini, picha yake ilitumika kupiga kampeni za kukipa kura chama pinzani, Democratic Alliance (DA), jambo ambalo lilipelekea filamu zake kufungiwa kuoneshwa Afrika ya Kusini.

Tiger Shroff ndiyo shabiki yake mkuu na anamuhesabu Hrithik kama msukumo wake katika filamu.

View attachment 2836833
Nje ya kazi ya kuigiza,Roshan pia ni stage performer na playback singer,pia ameendorse bidhaa mbalimbali ,ikiwa ni pamoja na kuhost reality show inayoitwa Just dance, na pia amelaunch nguo zake/brand yake.
Umesahau movie yake moja bang bang
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom