Meremeta & TANGOLD Revealed!

Meremeta & TANGOLD Revealed!

waziri mkuu asisistiza kuwa hawezi kusema kwani meremeta ,deepgreen finance,Nedbank,Trinex na Tangold zote zilikuwa zinahusika na jambo moja .

amesema kuwa hawezi kusema ni ulinzi gani wa nchi ...no way thank you Pinda
Wee..... PINDA usitufanye sisi wajinga..... hujui kulala na njaa wewe watoto wako wanasoma nje, wewe na kizazi chako mnatibiwa nje ya nchi kwa hizo hizo fedha zetu, hujui ni nani huwa anashusha magunia ya vyakula kila mwezi pale kwako oysterbay, hujui mafuta kwenye gari unayopanda yamewekwa saangapi, achilia mbali ni lita ngapi, hujui nini maana halisi ya kukosa umeme na maji, hujui hata direction ya masoko.... acha kucheza na njaa yetu wewe.....
 
Hawa ni wezi na nitamwaga vitu hapa kuwa hii Trinnex ni mali ya nani kule Africa ya Kusini wasifikiri watu wanatoa hoja bila kuzifanyia kazi hapa .

we will say it whatever the consequences...........

mwaga data mzee tuanze.................
 
Jamani hawa watu wameshajua kuwa tutapiga kelele tu mwisho tutanyamaza na kudakia mengine.....
 
Jamani hawa watu wameshajua kuwa tutapiga kelele tu mwisho tutanyamaza na kudakia mengine.....

The already know that; you are very right! JF hakyna threat yoyote itakayotokea. They know we 'll talk and talk and cry but at the end we will forget!! They need action; you know which action??
 
Mkuu,

Chochote kile Zitto (Mh.) atakachokisema Jumatatu, chochote kile, ameshatuambia tayari kwamba itakuwa ni kuwa call out wanao mdanganya Pinda. Tatizo sio Pinda, Mbunge anasema. Wengine tunamkosoa kwa kusema tatizo sio Pinda. Hilo halihitaji kusubiri maelezo. Kesha lisema. Wakati wengine - na wewe ukiwemo - tumedhani Pinda kaharibu.

Mwanakijiji hilo umesha likubali, na umeenda kwenye rekodi kwa mara ya kwanza leo kusema Pinda ana mushkeli kwa kutoleta ukweli. Hapa, Zitto (Mh.) kasema tatizo sio Pinda. Kwa hiyo wewe, logically, lazima utafautiane na Zitto (Mh.).

Aidha hivyo, au useme umekurupuka kumshutumu Pinda. Mwombe msamaha Pinda kwa kumfungulia thread ya kumkosoa kwa mara ya kwanza toka achaguliwe. Hii si maoni yangu. Ni masharti ya logic. Aidha Zitto kakosea kumtetea Pinda au wewe umekosea kumkosoa Pinda. Simple mathematics. Chagua sumu yako mtu wangu!

na yeye pinda sio mzigo wa kuni au cement...wakumlaumu hapa wa kwanza ni pinda ssb anatetea mafisadi hali akijua afanyalo, ingekuwa ni busara kama angeachia ngazi kwa kukataa kuburutwa/kulazimishwa kuwatetea ili kutunza heshima yake....ama sivyo.... sijapata kuona mtu BOGUS kama PINDA
 
.... Hapa Tanzania, Kuna haja kubwa ya migomo makazini kuanza kutumika kama mashinikizo kwa serikali yetu... Bunge na kanuni zake naona hazitoshi na hazitoshelezi!!

....Migomo makazini kwa nchi nzima is an unexplored option ambayo ni "salama" na huleta matumaini kwa wanyonge pale ambapo haki hazitendeki au zinakiukwa makusudi!!

....Kama migomo inakubalika, Watanzania tukubali kusafa kwa hata wiki moja alimradi tu hatuanzishi uasi baina yetu ili kuonesha kutoridhishwa kwetu... at the end of the day, tunasafa tayari na kupotea kwa hela hizi ambazo nyingi zinaendelea kupotea bila hata wanaohusika kuona adha inayowapata walalahoi.

Hii ni bonge ya point.....

Unajua hawa wanasiasa wetu....hawana uchungu kabisa na rasilimali za taifa letu.

Cha kwanza hawalipi kodi katika asilimia 90 ya matumizi na mapato yao. Hivyo sisi wafanyakazi ambao kila tunachokifanya tunakatwa kodi lazima tusikie uchungu tunapoona kodi zetu zinachezewa.

Wao wananunuliwa magari, tena 4WDs, wanayatumia kutoka kwenye nyumba za kupewa bure oysterbay na Masaki, mafuta wanajariwa kila siku, kila kikao wanalipwa (hata huko bungeni.....safari, malazi pamoja na chakula na chenchi kubaki juu).

Sisi walalahoi, gari ukinunua ndo utalipia kodi mpaka ulie, mshahara unakatwa, ukipewa bonus inakatwa, ukinunua mafuta kuna mikodi kibao, chakula ghali coz ya mikodi kibao,,,, etc etc.

Wao wamekalia tu kutumia, hawajui kuchangia kuongeza kipato cha nchi...ndo maana walipoona EPA wakafikiria jinsi ya kuitumia, Meremeta nayo hivyo hivyo,,,na mengine mengi.

Hawa mafisi-hadi washatuona sisi wananchi ni wapumbavu sana, kwanza nashangaa kwa nini tuwaite waheshimiwa....tumewachagua sisi ni sawa na kuwapa kazi watutumikie sisi, watuheshimu sisi, wawe answerable kwetu, na ndo maana tunawalipa, lakini wao washaona ni haki yao kuwa viongozi na sisi vibaraka wao.

Sasa ni wakati tuamue tusizalishe......tuone watakula wapi, watapata wapi kodi....by the way nimekuwa nikifikiria hakuna njia ya mtu kukataa kukatwa kodi???? kama hawa watu hawako wazi na tayari kuonyesha matumizi ya jasho langu, je nalazimishwa kulitoa???
 
ttz la migomo kuna unafki mwingi sana unaofanywa na maboss kuwatenga watu, watz sidhani kama tumeshakuwa na umoja kuwa hata kama tukiambiwa anaetaka kazi asign ndo aingie kazini, umaskini huwa unatufanya siku zote kukose umoja, na serikali kushinda
 
Mzee Mwanakijiji,

Mkuu najua sana uliyosema isipokuwa kumbuka hapa tuna deal na serikali ya Tanzania (Mafisadi) ambao wanaweza tumia kila hila kuepusha balaa hili.. hivyo kidogo swala la Uranium linaweza kutumika.
Kwa Mdanganyika ukimwambia Meremeta ni kampuni ya Jeshi ambayo ina deal na uchimbaji na security ya Uranium kutofika mikononi mwa magaidi (terrorist) wengi watakubali kirahisi bila hata kufikiria.. ndio maana nimetanguliza hekima ya uzee wangu ktk kutazama ni kigezo gani haswa Pinda anajaribu kutumia hapa as Usalama wa Taifa.

Ninafahamu vizuri kwamba uchimbaji wa Uranium sio siri na haswa inatakiwa Bunge lifahamu kwa sababu ni hilo bunge linalopitisha bajeti ya jeshi letu kikatiba. Nakumba wakati wa Nyerere miaka ya 70 hadi 80 mwanzoni ilikuwa siri ya serikali ktk matumizi ya wizara mbili Jeshi na ELIMU ya juu..lakini hii siri ilikuwa ndani ya nchi haikutoka nje ktk vyombo vya habari ama taasisi zinazokusanya data hizo.
Report nyingi za nje wakati ule hazikuwa na report hiyo kabisa, lakini bunge letu walifahamu kilichokuwa kinaendelea hata chuo Kikuu tu pekee wazungu walishindwa kuelewa serikali ya Tanzania inatumia kiasi gani kwa mwaka isipokuwa walikisia.. Na ni hivi majuzi tu ndio hizo takwimu zimekuwa released ama bado wametumia kukisia hilo sina hakika.

Kwa Pinda kupindisha ukweli na kuliacha nje bunge letu kama vile ni kitengo fulani cha serikali kuu, hakika kinatisha sana! Huu usalama wa Taifa kama kweli unahusiana na baadhi viongozi tu wa nchi tena kundi dogo sana ndani ya chama CCM ina maana nchi imetekwa!... Nashangaa hata baadhi Wabunge wa CCM wameshindwa kujiuliza hilo.. Hii ni sawa na kile alichokitetea Adam malima kuhusiana na kashfa ya Karamagi na Buzwagi! unakumbuka alisema na kumwomba Karamagi kama kuna deal kama hilo kwa ajili ya wilaya/mkoa wake anaomba anamkaribisha!... yaani bungeni mtu kama Adam leo hii waziri, analiambia bunge kuwa madeal ni ruksa maadam waliopewa wadhfa wamelikubali!..
Hii hatari kubwa sana na namuomba Zitto asikubali kabisa na hasa kuwatumia hao hao wabunge wa CCM kuwafahamisha kiza walichoingia kutetea Ufisadi.
 
Huyu mkulu naye si inasemekana alikuwa na dili la kuuza mafuta ya jeshi Morogoro na yule muarabu(jina limenitoka)...Alivyostaafu akapewa kuongoza Meremeta, baada ya muda mfupi "ikafilisika"...kuna kazi hapa!!!

Hapa imebidi inichukue 5 min kuvunjika mbavu. Ooh God!! I love JF


Mkuu I, maneno yako ni mazito sana kwa sababu sio kwamba wezi wa Meremeta hatuwafahamu, hapana hata pinda in a private anasema wazi kuwa anawajua, ila anaogopa tu wazito, ila with time wote tutawasema tu wewe subiri uone tena hapa hapa JF!
 
Hawa Ni Wale Walemanyangau..mlishaona Usalama Wa Taifa Anamtoa Nishai Uslama Mwenzake Kalaga Bao Hakuna Cha Epa Wala Richmonde!!!!!!!
 
Mi Nashauri Tutafute Email Za Wahusika Na Kuwatumia Mojakwamoja Na Hasa Wakubwa Zao Itakuwa Bora Zaidi!!!!!huku Wataendelea Tu Kutuchora
 
Mkuu ukweli ni kwamba bado tuko kwenye siasa za mazingara magumu sana, ni kweli kuwa tuna mtihani mkubwa sana mbele ya safari,

lakini pole pole kuna dalili za mwanga maana kina Rostam wanapowatafuta baadhi ya wabunge wa kundi la Mwakyembe in private na kuwaomba wawasikilize their side of story, ina maana wanajua kuwa tunasogea japo kidogo sana, lakini ogopa maandishi maaana huwa hayafutiki, muulize Mahalu!
 
Suala la Meremeta linahitaji majibu

Tahariri
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, jana amehitimisha mjadala wa hotuba ya bajeti ya wizara yake, kwa kujibu hoja nyingi za wabunge, likiwamo suala la zabuni tata ya Richmond, kampuni ya Marekani ya kufua umeme wa dharura, wizi wa sh bilioni 133 kutoka kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) na hatua iliyofikiwa na Serikali katika kuwashughulikia watuhumiwa wa kashfa hizo. Hata hivyo, Pinda alikataa kulizungumzia suala la kampuni iliyoibua mjadala nchini ya Meremeta, kwa maelezo kuwa shughuli za kampuni hiyo zinahusiana na masuala ulinzi na usalama wa taifa.

Hoja ya Meremeta ililetwa bungeni na Katibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Waziri Kivuli wa Tamisemi, Mbunge wa Karatu, Dk. Wilibrod Slaa (CHADEMA). Katika hotuba yake, ambayo kwa sehemu kubwa ilijikita katika masuala kuhusiana na ufisadi, Dk. Slaa aliitaka serikali kutoa maelezo ya kina kuhusu shughuli za kampuni ya Meremeta, moja ya kampuni zinazodaiwa kulipwa mabilioni ya sfedha za serikali katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu uliopita.

Akijibu hoja hiyo jana na nyingine kadhaa za baadhi ya wabunge waliochangia hotuba ya bajeti yake, Pinda alisema suala la Meremeta linajikita ndani ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Alisema uamuzi wa kutolizungumzia suala hilo bungeni unalenga kulinda maslahi ya nchi, kwani si mradi wa kiraia unaoweza kusemwa kwa namna yoyote ile.

Hoja hiyo ya Pinda ilikolezwa na Naibu Spika wa Bunge, Anna Makinda, ambaye baada ya Pinda kukamilisha kujibu hoja za wabunge, aliwakumbusha wabunge sheria inayokataza masuala ya usalama wa taifa kujadiliwa bungeni.

Makinda alisema kwa mujibu wa sheria hiyo, masuala hayo yanaweza kujadiliwa bungeni iwapo tu yatapata ridhaa ya Rais kwa maandishi, na kuwataka wabunge kwenda kuisoma sheria hiyo.

‘Tanzania Daima’ tunakubaliana na hoja zote mbili kuanzia ile ya Waziri Mkuu Pinda na hata ya Makinda, kwani tunaamini maslahi ya taifa lazima yawekwe mbele na kila mtu bila kujali itikadi.

Hata hivyo, kwa vile suala la Meremeta limekuwa likiibuka kila wakati wa mikutano ya Bunge kutokana na utata wake, tunafikiri kwamba kuna haja sasa ya sheria inayotoa nafasi ya kampuni hiyo kujadiliwa bungeni itumike ili kuondoa wingu la mashaka lililotanda juu yake.

Tunasema hivi tukizingatia ukweli kuwa Meremeta ni moja ya kampuni ambazo shughuli zake hazijawahi kuwekwa bayana wakati wowote, lakini imewahi kutajwa kama moja ya kampuni ambazo zilipokea malipo ya mabilioni ya shilingi kutoka serikalini bila kuelezwa zilitumika kwa kazi gani.

Tunasema hivi tukiwa na hofu kuwa wakati mwingine masuala ya ulinzi na usalama wa taifa, yanaweza kutumika kama kichaka cha kuficha maovu ya aina hiyo.

Tukirejea kilichotokea wakati wa suala la fedha za EPA, aliyekuwa Waziri wa Fedha, Zakia Meghji, aliwahi kuandika barua kuelezea mabilioni ya shilingi yaliyotolewa BoT katika akaunti ya EPA, kwenda kwa moja ya kampuni zinazotuhumiwa na ziko kwenye uchunguzi sasa, kwamba zilitolewa kwa sababu maalumu ya masuala ya usalama wakati haikuwa sahihi.

Ili kuondoa hofu ya masuala ya ulinzi na usalama kutumika kama kichaka cha kuficha maovu, tunalitaka Bunge kuhakikisha kuwa suala la Meremeta linapata ridhaa ya Rais Jakaya Kikwete, ili sasa liletwe bungeni na kujadiliwa kwa ukweli na uwazi.
 
Kuna similarities nyingi sana kati ya ZANU PF na CCM. Wakati JK anajifanya kumkemea Mugabe na chama chake, CCM na JK wanayafanya yale yale ambayo yameifikisha pabaya Zimbabwe. Kweli nyani haoni......
 
Nadhani kwa sasa serikali haioni sababu ya Kamati, EPA kama anahyusika atatajwa tu... Hawa wanasukuma ajenda wana sababu tu. Kama kuna ushahidi zaidi ya tulio nao mtu anaweza kuuleta tukautazama.

Mimi wananichanganya hawa. Ukileta ushahidi wanaoutaka wanakwambia una nyaraka za siri za serikali......................!!!!!!!!!!!?????????? sasa ushahidi upi wanaouzungumzia kuutaka jamani??
Nisaidieni.
 
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, ameliambia Bunge kwamba, suala la Meremeta ni wizi na halina uhusiano na mambo ya ulinzi na usalam. Anaendelea kunguruma. Amesema USALAMA wa TAIFA HAINA MENO
 
MEREMETA: The inside story


-Plus the questions that just won't go away


THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

THE involvement of the Tanzania People's Defence Forces (TPDF) in the controversial Meremeta Limited formally ceased in 2005/06 after the joint venture company between the government and South African investors was officially dissolved, impeccable sources have revealed to THISDAY.

Insiders familiar with the whole saga say that, contrary to Prime Minister Mizengo Pinda's claims in the National Assembly last week that the now-defunct company was a classified military project, the army was never involved in subsequent deals involving TANGOLD and Deep Green Finance.

According to these sources, Meremeta Ltd was initially registered in the Isle of Man, United Kingdom in April 1997, and received certificate of registration number 3424504.

Going by official government records, Meremeta was registered as a 50-50 joint venture project between the Tanzanian government and Triennex (PTY) Limited of South Africa.

However, other strong evidence indicates the presence in Meremeta�s affairs from the outset of at least two British legal firms, London Law Services Ltd and London Law Secretarial Ltd, both described as 'nominal shareholders.'

In October 1997, the company was given certificate of compliance number 32755 by the Business Registration Licensing Authority (BRELA), allowing it to formally operate in Tanzania.

Working in collaboration with the TPDF at the Buhemba open pit gold mine in Mara Region, Meremeta officially began gold mining operations in February 2003, with its operations being heavily financed by Tanzanian taxpayers through the Bank of Tanzania (BoT).

In 2005, the Meremeta company announced it had produced 2,075 kilogrammes of gold at a cash cost of $384 per troy ounce of gold.

Apart from the Buhemba gold mine, Meremeta also held the Kilamongo and Mwizi deposits, both located south of Buhemba, and the Nyasanero deposit.

But then in 2006 - only a year after officially beginning gold production the company declared bankruptcy, and was formally dissolved.

''With the dissolution of Meremeta, both the TPDF and the South African company (Triennex) formally pulled out of gold mining activities at Buhemba,'' said one of our well-informed sources, adding: ''So officially, any military involvement in the Meremeta project ended in 2006 when the company was declared bankrupt.''

Insiders further say the initial involvement of the TPDF in the Buhemba gold mining operations was aimed at raising funds to finance its cash-strapped vehicle manufacturing division - Tanzania Automotive Technology Centre, better known as the Nyumbu project.

It is understood that Meremeta was also set up to assist in developing the country's informal gold mining sector.

Official government records show that as Meremeta Ltd was winding up its operations, the BoT paid more than $118m (approx. 150bn/-) to Nedcor Trade Services Limited after having guaranteed a loan from the South African firm to Meremeta.

The BoT raised the funds to pay off the loan to Meremeta through a controversial 155bn/- Treasury bond, in a transaction that raised serious queries from auditors.

Following the liquidation of Meremeta Ltd, the Ministry of Energy and Minerals announced in Parliament that a wholly-owned government company, TANGOLD Limited, had been formed and assumed all Meremeta company assets, including the Buhemba gold mine.

Investigations by THISDAY have already established that the BoT paid another $13.34m (approx. 17bn/-) to TANGOLD through an account at the National Bank of Commerce Limited's Corporate Branch in Dar es Salaam.

TANGOLD was initially registered as an offshore company in Mauritius in April 2005, with its address listed as Suite 520, Barkly Whart, Le Caudan Waterfront, Port Louis.

In February 2006, the company was registered in Tanzania, with its local shareholders including former BoT governor Daudi Ballali (now deceased); the then Minister for Infrastructure Development, Andrew Chenge; and the Permanent Secretary in the Ministry of Finance, Gray Mgonja.

Other TANGOLD shareholders are the current PS in the Ministry of Water and Irrigation, Patrick Rutabanzibwa; and the then permanent secretary in the Ministry of Livestock Development, Vincent Mrisho.

Although the Ministry of Energy and Minerals claimed that TANGOLD was 100% owned by the government, it has failed to explain why the company was registered in Mauritius and not Tanzania, and why its articles of association give the listed shareholders permission to transfer all or part of their shares to their next of kin.

TANGOLD is also not listed at the Treasury Registry among companies partly or wholly-owned by the government, and has thus not been subjected to statutory auditing by the Controller and Auditor General (CAG).

When addressing the National Assembly in Dodoma last Friday, premier Pinda appeared evasive to the point of fumbling in his attempts to answer queries from opposition members of parliament regarding Meremeta, TANGOLD and Deep Green Finance Limited.

His reference to the controversial Meremeta question as a ''military affair and therefore one of national security'' in particular only served to raise more questions rather than provide any answers to the mystery.
 
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, ameliambia Bunge kwamba, suala la Meremeta ni wizi na halina uhusiano na mambo ya ulinzi na usalam. Anaendelea kunguruma. Amesema USALAMA wa TAIFA HAINA MENO

Kitaeleweka tuu..... hawawezi kutudanganya siku zote hawa, Mungu hakubali mambo haya...
 
Back
Top Bottom