Meremeta & TANGOLD Revealed!

Meremeta & TANGOLD Revealed!

Bunge limechemka ,waziri mkuu kasema hawezi kuendelea kusema ,kwani hana majibu ya zaidi .

Swali ni kuwa kampuni hizi zilikuwa zinapeana fedha august 2005 mpaka disemab 2005.hivi hapa ndio palikuwa na ulinzi ?
 
WIZI FEDHA ZA UMMA:

:: Ni ile iliyohusishwa na ufisadi BoT :: Msimamo wa CAG wamkaanga Balali
:: Asema hakuwahi kukagua hesabu zake :: Mbunge ahoji ni ya umma au binafsi

Na Godfrey Dilunga, wa Mtanzania

WAKATI Bunge likianza Mkutano wake ujao, keshokutwa, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, amekana kuitambua wala kukagua hesabu za kampuni tata ya Meremeta, inayohusishwa na ufisadi wa mabilioni Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Taarifa iliyowahi kutolewa na Serikali ilieleza kuwa, kampuni hiyo ilikuwa ikimilikiwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kwa ajili ya mradi wake wa Nyumbu, Kibaha, Mkoa wa Pwani.

Hata hivyo, Utouh anasisitiza kuwa, haimo katika orodha ya kampuni 158 za umma, zilizomo katika orodha ya ukaguzi.

CAG aliikana Meremeta Ltd jana jijini Dar es Salaam, katika semina kati ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mashirika ya Umma (POC), na wenyeviti na watendaji wa mashirika ya umma.

Alifikia hatua hiyo baada ya Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono, kutaka Msajili wa Mashirika ya Umma kueleza kampuni hiyo ni ya binafsi au umma. Kama ni ya umma, alitaka CAG aeleze kama aliwahi kukagua hesabu zake.

Kwa mujibu wa Mkono, waliowahi kuwa wafanyakazi wa kampuni hiyo wamekuwa katika hali ngumu ya kufuatilia mafao yao na wamekuwa wakitaka kujua hatima yao kutoka kwake, kama mbunge.

"Ndugu mwenyekiti (wa Kamati ya Bunge, Kabwe Zitto) siijui Meremeta na si kati ya mashirika na taasisi za umma 158 ambazo nimekagua hesabu zake," alisema CAG.

Kampuni ya Meremeta inadaiwa kuwahi kuendesha shughuli za uchimbaji dhahabu, Musoma Vijijini.Hata hivyo, baadaye kampuni hiyo inadaiwa kuchotewa mabilioni ya fedha kutoka BoT katika mazingira yenye utata.

Ni miongoni mwa kampuni zilizowahi kutamkwa bungeni mwaka jana, zikihusishwa na ufisadi wa mabilioni katika Benki Kuu.

Inadaiwa kwamba, aliyewahi kuwa Gavana wa Benki Kuu, Dk. Daudi Balali aliidhinisha au kuruhusu au kunyamazia malipo ya dola za Marekani 118,396,460.36 zinazodaiwa kupelekwa katika akaunti isiyojulikana ya Benki ya Nedbank Ltd. ya Afrika Kusini.

Fedha hizo zinadaiwa kupelekwa huko kama malipo ya madeni ya kampuni muflisi ya Meremeta Ltd, iliyokuwa inachimba dhahabu katika eneo la Buhemba Wilaya ya Musoma, mkoani Mara.

Tangu kuanzwa kutajwa kwa kampuni ya Meremeta bungeni, Serikali imekuwa ikitoa taarifa mbalimbali.

Taarifa hizo ni pamoja na inayodai kuwa Meremeta Ltd, ilikuwa kampuni ya Kitanzania iliyokuwa ikimilikiwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kwa ajili ya mradi wake wa Nyumbu, Kibaha, Mkoa wa Pwani.Hata hivyo, habari zilizowahi kuandikwa na vyombo vya habari nchini, zilidai kuwa nakala ya usajili iliyotolewa na Msajili wa kampuni Uingereza na Wales, inaonyesha kampuni hiyo iliandikishwa nchini Uingereza.

Iliandikishwa Uingereza, Agosti 19, mwaka 1997 na ilifilisiwa huko huko Uingereza, Januari 10, 2006.

Hapa nchini, inadaiwa kuwa taarifa ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) ya Mei 31, mwaka 2005 inaonyesha Meremeta Ltd ni tawi la kampuni ya kigeni iliyosajiliwa Tanzania kama tawi, Oktoba 3, 1997.

Vile vile taarifa hiyo inaonyesha kwamba hisa 50 za Meremeta Ltd.

zilikuwa zinamilikiwa na Kampuni ya Triennex (Pty) Ltd. ya Afrika Kusini na hisa 50 zilizobaki zilikuwa zinamilikiwa na Serikali ya Tanzania kwa kupitia kwa Msajili wa Hazina katika Wizara ya Fedha.

Inadaiwa kuwa, Gavana Balali aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Meremeta Ltd. kati ya mwaka 2004 na 2005.

Hata hivyo, kuna utata mkubwa juu ya nani ni mmiliki hasa wa Meremeta Ltd. kwa kuwa taarifa ya BRELA inaonyesha pia kwamba kampuni mbili za Kiingereza – London Law Services Ltd. na London Law Secretarial Ltd. zinamiliki hisa moja moja za Meremeta Ltd.Kampuni hizo zinadaiwa kutumia anwani moja iliyoko 84 Temple Chambers, Temple Avenue, jijini London.

Baadhi ya hoja zinazogonga vichwa vya wafuatiliaji wa masuala ya kitaifa, ni kwamba, hajulikani ni kwa nini Gavana Balali aliruhusu fedha za umma kutumika kulipia madeni yote ya kampuni ambayo Serikali ilikuwa inamiliki hisa 50 tu, wakati kampuni nyingine za kigeni zilikuwa zikimiliki hisa 52.
 
Bunge limechemka ,waziri mkuu kasema hawezi kuendelea kusema ,kwani hana majibu ya zaidi .

Swali ni kuwa kampuni hizi zilikuwa zinapeana fedha august 2005 mpaka disemab 2005.hivi hapa ndio palikuwa na ulinzi ?

Inajulikana kabisa kuwa huu ulinzi - ulikuwa ni kusaidia ushindi wa kishindo wa JK Kikwete.
 
Pinda: Inapofikia mahali unashindwa hapa tuseme nini, Hakuna cha Meremeta moja au mbili, kuna TRINEX kuna Deep Green kuna task force: Cheyo anataka kutuambia tusema hawa wote walikua wana deal na nini, nasema NO!!!

Bull........
 
Wametunga UONGO na kulihusisha jeshi ili kutufunga mdomo!
Hii nchi yetu si ya jeshi!
Ni ya utawala wa kisheria zilizotungwa na zenye kusimamiwa na wawakilishi wetu tuliowachagua ili kusimamia haki na maslhai ya TAIFA.
Haya mambo ya siri ya jeshi ni ya zamani enzi za UJAMAA!
Karne hii mpya kila mtu ama mwananchi ni MDAU WA NCHI MWENYE KUSTAHILI TAARIFA ZOTE ZINAZOHUSIANA NA MASLAHI YETU,YA WATOTO WETU PAMOJA NA VIZAZI VIJAVYO.
Kama hizo pesa na migodi ni ya wananchi na wanahitaji taarifa zake na si kusema ni mali ya jeshi!
MBONA WANAWACHONGANISHA WANANCHI NA JESHI?
AMA NI WAPI TUNAKOENDA?
 
Mhe. Dr. Slaa (Mb), nakuomba sana uandae hoja binafsi, wananchi hatujaridhika na majibu ya Mhe. Pinda. Tunahitaji majibu zaidi, yenye kueleweka vinginevyo bunge liunde kamati teule. Ninategemea kwamba wabunge wengi watakuunga mkono na wale wasiounga mkono tutawatambua na kuwahubiri ili wasirudi tena katika jumba hilo tukufu. Asante Mhe natumaini ujumbe huu utaupata.
 
Wametunga UONGO na kulihusisha jeshi ili kutufunga mdomo!
Hii nchi yetu si ya jeshi!
Kama hizo pesa na migodi ni ya wananchi na wanahitaji taarifa zake na si kusema ni mali ya jeshi!
MBONA WANAWACHONGANISHA WANANCHI NA JESHI?
AMA NI WAPI TUNAKOENDA?

Kwa sababu Jeshi ndiyo taasisi pekee ambayo watu bado wanaiamini? Na wanajua ukisema ni kitu cha jeshi basi watu hawawi wakali sana. Binafsi ningependa kumsikia Mwamunyange aelezee suala hili la Meremeta. Kuna mtu ana contacts zake please.
 
Mheshimiwa Mkono anawaju Wamiliki wa Meremeta.na hii ndiyo siraha yake kwa serikali,Chama kimekuwa cha ovyo sababu kila mtu anajua ubou wa mwenzake na wanalindana.Mwamunyange naye si alipandishwa vyeo harakaharaka..

Yaani ni kama kupeana Vijiti.I have an idea....
 
Kama Huo Upuuzi Ukikubalika Na Wabunge...then Wakitoka Huko Wananchi Wawapige Mawe Na Warudi Huko Vijijini Na Hatuwataki Tena Kwani Wengine Ni Wa Mirembe Na Wengine Belongs Segerea Na Si Bungeni Ama Serikalini Na Ikulu!
 
Hawa ni wezi na nitamwaga vitu hapa kuwa hii Trinnex ni mali ya nani kule Africa ya Kusini wasifikiri watu wanatoa hoja bila kuzifanyia kazi hapa .

we will say it whatever the consequences...........
 
Hivi Kama Kweli Meremeta, Tangold, Deep Green Zingikuwa Ni Za Jeshi, Kugekuwa Na Kurithishwa Wake, Wajukuu Wa Akina Balali, Chenge, Et Al?

Hii Ndiyo Silaha Ya Chenge, Hawawezi Kumfanya Lolote Sasa, Maana Anajua Kila Kitu Kuhusu Meremeta.

Hatuna Serikali
 
Mpaka kieleweke,
Weka mambo hadharani mwanawane......Pinda kachemsha hata picha haijaanza duh! noma kishenzi
 
kwa Sababu Jeshi Ndiyo Taasisi Pekee Ambayo Watu Bado Wanaiamini? Na Wanajua Ukisema Ni Kitu Cha Jeshi Basi Watu Hawawi Wakali Sana. Binafsi Ningependa Kumsikia Mwamunyange Aelezee Suala Hili La Meremeta. Kuna Mtu Ana Contacts Zake Please.

Hapo Ndio Ukweli Ulipo!
Na Huu Ujumbe Ni Kwenu Nyie Wabunge WOTE!
Kabla Hamjatoka Huko Bungeni Tunataka Kujua Msimamo Wa Kila Mbunge Bila Kujali Chama!
Kama Msipofata Ushauri Huu...then Mnajuwa YAliyompata Killango Hapa!
Jf Iliufutilia Mbali Upambe Wake Wa Maneno Matamu Matamu!
Wao Wanafikiri Kwasababu Wananchi Wengi Ni Less Educated Na Un Infromed..basi Wengine Tutakaa Pembeni!
Wamekosea!
Tutapambana Kwa Niaba Ya Wananchi Wote.
God Willing...we Will Be Victorious!
Wabunge Wafanye Mambo Kwa Maslahi Ya Taifa Na Si Baadhi ya Wanajeshi Na Wananmtandao.
Nimeshagundua Hii Ni Plan B Baada A Killango!
Tatizo wameenda kutoka A hadi P PINDA HAKI!
Wamevuka herufi takriban 16 hivi!
HAWAFAI KUTUONGOZA TENA!
Ubishi Wao Hautawafikisha Wao Popote Na Ni Hatari Kwa Taifa!
 
Hawa ni wezi na nitamwaga vitu hapa kuwa hii Trinnex ni mali ya nani kule Africa ya Kusini wasifikiri watu wanatoa hoja bila kuzifanyia kazi hapa .

we will say it whatever the consequences...........

Mkuu nafahamu bado uko dodoma,Naomba unipe khali ya wabunge wanasemja baada ya kauli ya Pinda,Ningependa kusikia Maoni ya Spika sitts na Zitto Kabwe.

Who own Trinnex?asije akwa yule jamaa mwenye kipara na ana mwili mkubwa ambaye ni rafiki mkubwa wa nchi yetu..
 
Bunge is still going on, na waziri mkuuanasema kuwa mahakama ya kadhi sio issue kwa sasa kwani hawapo tayari kuliweka kwenye katiba ya nchi.

Pili anavyosema hivyo ni kuwa CCM ilipoweka kwenye ilani walikuwa wanatongoza kura za waislamu.....naibu spika kakataa asijibiwe
 
Mkuu nafahamu bado uko dodoma,Naomba unipe khali ya wabunge wanasemja baada ya kauli ya Pinda,Ningependa kusikia Maoni ya Spika sitts na Zitto Kabwe.

Who own Trinnex?asije akwa yule jamaa mwenye kipara na ana mwili mkubwa ambaye ni rafiki mkubwa wa nchi yetu..

Maoni ya kila mtu yawekwe hapa!
Mambo ya ZIMBABWE TUSHAWAACHIA WAZIMBABWE!
NA SASA NI TANZANIA!
WALE WANAOJIDAI KUWA NA UCHUNGU NA ZIMBABWE KULIKO TZ NI UAFRIKA BORA HAWAELEWI MAMBO WALA THE REAL MEANING TO PATRIOTISM!

SASA HII ISSUE A SIRI YA JESHI IMEKAA KINYERERE NYERERE KWANI ENZI HIZO ZA UJAMAA NDIO ILIKUWA KAULI MBINU!
SASA SIJUI MKAPA AMBAYE NI FAMILIA YA NYERERE ALIKUMBUSHIWA GIA HIYO NA NANI!
MAANA HATA WALE VIMBELE MBELE KAMA KINA BUTIKU NA WARIOBA WALIOKUWA WAKISEMA WAKAMATWE SASA NI KIMYA!
TUTAJUA KILA KITU NA WATAKAOCHAGUA UPANDE WA MAFISADI NI WA KUCHOMELEWA MBALI!
 
Bunge is still going on, na waziri mkuuanasema kuwa mahakama ya kadhi sio issue kwa sasa kwani hawapo tayari kuliweka kwenye katiba ya nchi.

Pili anavyosema hivyo ni kuwa CCM ilipoweka kwenye ilani walikuwa wanatongoza kura za waislamu.....naibu spika kakataa asijibiwe

Assuming that CCM assumed that Waislamu wana vote dini, kwa nini aliona Uislamu wake hautoshi mpaka aongezee kuwatongoza kwa ishu ya Kadhi?

Halafu ni kwa nini hawakuogopa kwamba huku kutongoza Waislamu nje nje hivi kunge wa alienate wapiga kura Wakristo? Hususan kama candidate ni Muislamu?

Walikuwa wanafikiria nini haswa?
 
We need the Government to say who is involved in Trinnex mining........

He is someone very big in the RSA..........
 
Back
Top Bottom