Meremeta & TANGOLD Revealed!

Meremeta & TANGOLD Revealed!

Mwenzio akinyolewa wee tia maji. Naamini sasa tunaelekea kule Harare. Mambo ya kuelekeza Meremeta jeshini ili wananchi washindwe kuhoji ni ujinga. Kama jeshi liko chini ya serikali iliyowekwa na watanzania, basi hawana budi kujibu haya maswali. Ni mradi gani unaweza kuwa siri kwa watanzania kama ni wa kujiendeleza? Watu hawawezi kuendekeza UFISADI kwa mgongo wa Usalama wa Taifa. Huu ni utumbo kama Waziri Mkuu anakuwa na jibu kama hili kwa watanzania. Jamani watanzania tulidhani kama huyu jamaa ni mkweli, muadilifu n.k kumbe na yeye naye ni ka-bomu fulani ambako kameanza kuchemka. Kadri siku zinapokwenda kuna hatari ya haka ka-bomu kuzidi kutoa mionzi yenye athari kubwa kwa watanzania. Mafisadi tayari walishamnywesha mchuzi, na sasa muda mfupi tu tayari ameshasahau kutambua kuwa anawatumikia Watanzania wote na si kikundi kidogo cha watu wenye nia ya kuifilisi Tanzania. Sasa baada ya miaka 2 atakuwaje??

..Mkuu kuna mtu ameshawahi kucomplain aina ya font ulizochagua kuwa zinaumiza macho?? at least zingekuwa ktk size kubwa kidogo...
...Nakubalina na hoja yako ktk post niliyoiquote ila baada ya dk kumi ya kuisoma
 
dugu mushi
mimi sikutetei wewe au zito or who ever, kitu kikubwa hapa ni kutumia busara, na kwenda mbele.
na hapa usifikiri kama vitu vyote anavyo sema zito nakubaliana nae au vipi, au utakacho ongea wewe na uki-deal na kitu concetrate na kimoja, usiwe kama amerika unapigana irak , afaghanistan nna vyote vimemshinda huku ana zungumzia iran.jifunze kuisha na watu wa kila aina bila kuharibu integrity yako.
nafikiri kwa haya maelezo yangu mafupi imenielewa.
 
Warioba hayuko meremeta yuko mwnanchi Gold.

Mkuu na huku pia yupo na viongozi wengine wamo humu kwa kuitumia ccm kama chambo, ndio maana mkwara ni mkubwa sana aliopigwa pinda, kupindisha ukweli! hizo kampuni zote ni hao hao tu mkuu ila walibadili majina tu!

And by the way, wewe ulijueaje kuwa Warioba hayumo humu, au kuna something unakijua kuhusu hii dela nzima?
 
mnahukumu watu mapema sana.... ningekuwa mimi nyinyi ningesubiri nimsikie Zitto atakapotoa mchango wake Bungeni, theni ningejajudge kile. Alichosema hapa ni kuzungumza na washkaji zake n.k lakini tunataka kujifanya kama tuko kwenye Bunge letu wenyewe ambapo ni baraza la wenye haki, wasiokosea. Tunajigeuza kuwa self rightious to the point kwamba we have to be right. No room for mistakes or erros.

I have been wondering a lot... and I continue to wonder. Hekima inatulazimisha kutofanya haraka kuhukumu ili tutakapotoa hukumu basi iwe ni hukumu inayokaribiana na haki kweli.

Si ndiyo maana nikasema nasubiri atoke huko kigoma aende Dodoma na mimi ninamsikilizia!

Na nikasema akini prove wrong i will apologize!
Siasa ni mchezo mchafu!

Imani tuliyokuwa nayo kwa watu machachari ambao wangeweza kuuzuia hii umafia kama wange stand strong for the people..The likes of firebrand politicians like Msumbukaji LAMWAI and OFCOURSE KABURU WALIDI LA KIGOMA!

Sitaki nasema sitaki!

IDDI SIMBA NI FISADI LA EPA!
LIKAPEWA MAJUKUMU YA MUSTAKABALI WA MADINI YETU!
ZITTO NAYE AKAWEKWA HUMO!

SI MBAYA KAMA AKIWAGEUKA!

KWANI HUWEZI KUSEMA LUGHA YOYOTE JUHUSU EPA NA ccm KAMA USIPOTAJA JINA LA IDDI SIMBA ALIYEKUWA MWENYEKITI WA ccm WAZAZI ambaye alitumia cheo chake hicho cha ccm mtandao akishirikiana na MALEGESI NA LUKAZA!

Na mimi pia najua everything kwani nimeshapitia ripoti zote.
Na hivyo basi...TUSUBIRI KAULI KWANI SASA SI MAJINA TENA HUKO BUNGENI!

NI KAULI!
NDIZO ZITAKAZOTUKONGA NYOYO ZETU KWANI TUNAJUWA EXCACTLY KILE WANACHOTAKIWA KUSEMA NA KUFANYA!

ASANTE.
 
CCM sio chama cha magaidi mimi sio gaidi na mwanachama wa CCM, lakini magaidi wachache ndani ya CCM tunawajua na tuko njiani kuwafanyia kazi ingawa sio rahisi, tizama hii topic utaona vizuri wanajua vizuri kuhusu Meremeta lakini wanajaribu kutudanganya hapa,

siku zenu zinakaribia kufika mwisho, kumshinikiza pinda aseme uongo haina maana mnatudanganya wote sisi wananchi kuna tulioamka na tunaujua ukweli!

Mkuu,

Natoa ombi la lazima. Waafrika tulikuwa na njia mbili tu za kumpata kiongozi shupavu. Ama alitia fora kwenye mapambano (mostly vita) au alirithi full stop. Ukiacha Mwalimu, hatuna kiongozi mwingine yeyote aliyefuatia ambaye kwa namna yoyote angestahili kushika hizo nafasi walizoweza kuwa nazo. Huu mtindo wa ku''pick'' bwege from nowhere halafu kuanza kumtafutia sifa ambazo kwa hakika kabisa hana, ndio mwongozo namba moja wa CCM.

Mtu yeyote vile ambaye mpaka dakika hii bado ana ndoto na imani na CCM kama ilivyo hivi sasa kwamba itaweza kufanya tofauti ama anajidanganya au ni moja wao. Wakuu, you cant eat your cake and have it. Kama hukubaliani na watendayo CCM (inspite of mikutano yao hiyo yote ya kisanii, mara Butiama, Bungeni n.k) get out now. Stand up and be counted and I can bet my .s. , you will have a following, me included. Hebu fkiria mtu mzima anapewa mandate na zaidi ya asilimia 80% ya wananchi (ambao obviously wengi wao si wanachama wa CCM) anashindwa kupambana na wanaomkwamisha, inaingia akilini kweli ama ni moja wao. Na hao ambao bado wana imani naye tuwaiteje.

Hizi data ambazo wengine humu tunakuwa kama tunazihodhi tunazipataje kama hatushirikiani nao kwa namna moja ama nyingine. Kwa sababu tunajua wazi kwamba katika prevailing atmosphere these guys (CCM) are acting with impunity. With or without dataz nothing will happen so to hoodwink us even more they will continue to bombard us piecemeal with the so called dataz. Wabunge wengine hivi sasa wanatumiwa kukurupuka na scathing attacks ku preempt malalamiko ya wananchi, beware, kwani hata humu JF wamo.

Idi Amin kila alipotaka kuwashughulikia wapinzani wake ali"invent'' mambo ku"distract" wananchi kama vile kuvamiwa na nchi jirani n.k. Can you imagine hata REDEP inaweza kutumiwa kuisifu ofisi ya raisi na wakati huo huo kuiponda serikali iliyoundwa na raisi huyo huyo. Kuna wengine humu wanatuzuga kwa sababu zao ambazo hata hivyo are bound to fail because you cant do it to all the people all the time. Tanzania ninayoilia haitapatikana ndani ya CCM kama ilivyo. Siku njema wana JF.
 
mnahukumu watu mapema sana.... ningekuwa mimi nyinyi ningesubiri nimsikie Zitto atakapotoa mchango wake Bungeni, theni ningejajudge kile.

... Tunajigeuza kuwa self rightious to the point kwamba we have to be right. No room for mistakes or erros.

Mkuu,

Chochote kile Zitto (Mh.) atakachokisema Jumatatu, chochote kile, ameshatuambia tayari kwamba itakuwa ni kuwa call out wanao mdanganya Pinda. Tatizo sio Pinda, Mbunge anasema. Wengine tunamkosoa kwa kusema tatizo sio Pinda. Hilo halihitaji kusubiri maelezo. Kesha lisema. Wakati wengine - na wewe ukiwemo - tumedhani Pinda kaharibu.

Mwanakijiji hilo umesha likubali, na umeenda kwenye rekodi kwa mara ya kwanza leo kusema Pinda ana mushkeli kwa kutoleta ukweli. Hapa, Zitto (Mh.) kasema tatizo sio Pinda. Kwa hiyo wewe, logically, lazima utafautiane na Zitto (Mh.).

Aidha hivyo, au useme umekurupuka kumshutumu Pinda. Mwombe msamaha Pinda kwa kumfungulia thread ya kumkosoa kwa mara ya kwanza toka achaguliwe. Hii si maoni yangu. Ni masharti ya logic. Aidha Zitto kakosea kumtetea Pinda au wewe umekosea kumkosoa Pinda. Simple mathematics. Chagua sumu yako mtu wangu!
 
Hahaha,

Unataka kunifanya Augustino Ramadhani siyo?

OK, wacha niwe Jaji Mkuu.

Probably the diplomatic type, muheshimiwa Zitto ukimfuatilia hapa anaonyesha kuwa mpinzani fulani mwenye core beliefs katika respect for authority.At a time when one may expect prominent opposition leaders to rightfully unleash salacious and even malicious tirades against the president, muheshimiwa Zitto distinguished himself arguably reasonably amicably by cautioning people here to "Respect the presidency if not the president himself". Those were some notable words, especially coming from his side of the power divide. My austere "see good in everybody" default philosophy wants to believe this, and unless a trend is established I will have to defer to this and give muheshimiwa the benefit of the doubt.

Having said that, muheshimiwa Zitto is not outside the domain of all politicians, a lot that is characteristically driven by ambition. Ambition can allow some azzkissin to the extent of excusing an obvious "error" under the guise of "PM kadanganywa"

Nimekupata vizuri. Nashaurika....... Nakosoleka....... JF inasomwa na wengi.... coded, can it be Pundit?
 
dugu mushi
mimi sikutetei wewe au zito or who ever, kitu kikubwa hapa ni kutumia busara, na kwenda mbele.
na hapa usifikiri kama vitu vyote anavyo sema zito nakubaliana nae au vipi, au utakacho ongea wewe na uki-deal na kitu concetrate na kimoja, usiwe kama amerika unapigana irak , afaghanistan nna vyote vimemshinda huku ana zungumzia iran.jifunze kuisha na watu wa kila aina bila kuharibu integrity yako.
nafikiri kwa haya maelezo yangu mafupi imenielewa.

Naanza na Tanzania...baada ya kupata uhuru..Then Zimbawe..THEN THE REST OF AFRICA.
Its just the strategic PLAN for the freedom of AFRIKA!
AFRIKA NI THE TAJIRIEST OF ALL THE CONTINENTS!
 
Mkuu,

Chochote kile Zitto (Mh.) atakachokisema Jumatatu, chochote kile, ameshatuambia tayari kwamba itakuwa ni kuwa call out wanao mdanganya Pinda. Tatizo sio Pinda, Mbunge anasema. Wengine tunamkosoa kwa kusema tatizo sio Pinda. Hilo halihitaji kusubiri maelezo. Kesha lisema. Wakati wengine - na wewe ukiwemo - tumedhani Pinda kaharibu.

Mwanakijiji hilo umesha likubali, na umeenda kwenye rekodi kwa mara ya kwanza leo kusema Pinda ana mushkeli kwa kutoleta ukweli. Hapa, Zitto (Mh.) kasema tatizo sio Pinda. Kwa hiyo wewe, logically, lazima utafautiane na Zitto (Mh.).

Aidha hivyo, au useme umekurupuka kumshutumu Pinda. Mwombe msamaha Pinda kwa kumfungulia thread ya kumkosoa kwa mara ya kwanza toka achaguliwe. Hii si maoni yangu. Ni masharti ya logic. Aidha Zitto kakosea kumtetea Pinda au wewe umekosea kumkosoa Pinda. Simple mathematics. Chagua sumu yako mtu wangu!

Great analysis Kuhani........

ha ha ha..
 
Hizi data ambazo wengine humu tunakuwa kama tunazihodhi tunazipataje kama hatushirikiani nao kwa namna moja ama nyingine. Kwa sababu tunajua wazi kwamba katika prevailing atmosphere these guys (CCM) are acting with impunity. With or without dataz nothing will happen so to hoodwink us even more they will continue to bombard us piecemeal with the so called dataz. Wabunge wengine hivi sasa wanatumiwa kukurupuka na scathing attacks ku preempt malalamiko ya wananchi, beware, kwani hata humu JF wamo.

Can you imagine hata REDEP inaweza kutumiwa kuisifu ofisi ya raisi na wakati huo huo kuiponda serikali iliyoundwa na raisi huyo huyo. Kuna wengine humu wanatuzuga kwa sababu zao ambazo hata hivyo are bound to fail because you cant do it to all the people all the time. Tanzania ninayoilia haitapatikana ndani ya CCM kama ilivyo. Siku njema wana JF.

Mkuu usijaribu kuuharibu huu mjadala, kama kawaida yako, umepewa nafasi kubwa sana toka jana kuuweka ufisadi wangu na wa ndugu zangu kama unao uuweke hapa, umeshindwa sasa here you are, huweki ukweli lakini unajaribu kupandikiza mbegu za chuki na ninajua kuwa the next thing, sasa untaka mjadala ufungwe maana pale nilipounga mkono maneno ya Nyangumi, najua kuwa nimekugusa pabaya tayari, ngoja niyaweke tena maneno ya Nyangumi ili wananchi wayaone tena na wajue kuwa tunao hapa hapa JF, yaani mafisadi wanaohuiska na Meremeta!
 
Mkuu,

Chochote kile Zitto (Mh.) atakachokisema Jumatatu, chochote kile, ameshatuambia tayari kwamba itakuwa ni kuwa call out wanao mdanganya Pinda. Tatizo sio Pinda, Mbunge anasema. Wengine tunamkosoa kwa kusema tatizo sio Pinda. Hilo halihitaji kusubiri maelezo. Kesha lisema. Wakati wengine - na wewe ukiwemo - tumedhani Pinda kaharibu.

Mwanakijiji hilo umesha likubali, na umeenda kwenye rekodi kwa mara ya kwanza leo kusema Pinda ana mushkeli kwa kutoleta ukweli. Hapa, Zitto (Mh.) kasema tatizo sio Pinda. Kwa hiyo wewe, logically, lazima utafautiane na Zitto (Mh.).

Aidha hivyo, au useme umekurupuka kumshutumu Pinda. Mwombe msamaha Pinda kwa kumfungulia thread ya kumkosoa kwa mara ya kwanza toka achaguliwe. Hii si maoni yangu. Ni masharti ya logic. Aidha Zitto kakosea kumtetea Pinda au wewe umekosea kumkosoa Pinda. Simple mathematics. Chagua sumu yako mtu wangu!

Nimekuelewa
 
Wakuu wote hapa JF muwe macho, jamaa amechukizwa na haya maneno ambayo nimeyaunga mkono ni maneno ya Nyangumi, sasa naomba watu wenye akili nyingi wajiulize ni kwa nini?

Quote:- Nyangumi

1. Wakati wa uongozi wa jenerali Mbona kuliwahitokea kutunishiana misuli kati ya Mkapa na Mboma katika kipindi ambacho Mboma alikaribia kustaafu.

2. Nyepesi nyepesi zilisema ilikuwa ni mambo ya pesa(labda ndo hiyo Meremeta) ili kumpooza Mboma, vibali vya kuingiza sukari toka nje bila ushuru vilitolewa.

3. Baada ya magazeti kuandika kuhusu utolewaji huo wa vibali na waziri wa fedha(Yona)bila kufuata taratibu wakaona watumie kofia ya jeshi, lakini ukweli ni kuwa matani ya sukari iliyoingizwa yalimnufaisha Mboma, kuanzia ushuru.
 
Mkuu,

Chochote kile Zitto (Mh.) atakachokisema Jumatatu, chochote kile, ameshatuambia tayari kwamba itakuwa ni kuwa call out wanao mdanganya Pinda. Tatizo sio Pinda, Mbunge anasema. Wengine tunamkosoa kwa kusema tatizo sio Pinda. Hilo halihitaji kusubiri maelezo. Kesha lisema. Wakati wengine - na wewe ukiwemo - tumedhani Pinda kaharibu.

Mwanakijiji hilo umesha likubali, na umeenda kwenye rekodi kwa mara ya kwanza leo kusema Pinda ana mushkeli kwa kutoleta ukweli. Hapa, Zitto (Mh.) kasema tatizo sio Pinda. Kwa hiyo wewe, logically, lazima utafautiane na Zitto (Mh.).

Aidha hivyo, au useme umekurupuka kumshutumu Pinda. Mwombe msamaha Pinda kwa kumfungulia thread ya kumkosoa kwa mara ya kwanza toka achaguliwe. Hii si maoni yangu. Ni masharti ya logic. Aidha Zitto kakosea kumtetea Pinda au wewe umekosea kumkosoa Pinda. Simple mathematics. Chagua sumu yako mtu wangu!

Kuhani, je kama Mh. Zitto katika muda wake toka habari hii ifike hapa amefanikiwa kuongea na Mh. Pinda lakini contents za maongezi hataki kuzitoa hapa, ila ameamua kusema tu kuwa 'tatizo siyo pinda,' ila wanaomdanganya.... je hapo Mh. Zitto ana haki ya kusema hivyo?
 
Na hapo ndio nabaki nikijiuliza kama BALLALI ALILETWA KWA MAKUSUDI YALE YALE YA KUWACHAFUA VIONGOZI ILI KUWAFANYA MA PUPPET!

MAANA SINCE BALLALI ALIKUWA USA...KIKWETE HAKUWA NA HAJA YA KUUZA UHURU KWA MCHINA BALI MMAREKANI.

MCHINA NAYE AKACHUKIA AKAICHUKUA ZAMBIA..NA SASA ZIMBABWE!

SO THE SCRAMBLE FOR AFRIKA STRATEGY NI KUMWEKA PALE KAMA AU CHAIRMAN NA KUMSHIKIA BANGO LA UFISADI ILI NA YEYE APELEKE MAJESHI ZIMBABWE KWANI HUKO G8 SUMMIT KILISHAPANGWA IRAQ ZIMBABWE STRATEGY AS IN SADDAM AND MUGABE!

WAZALENDO NI KURESIST!

KWANI SIELEWI NI KIVIPI BUSH ANA NIA NZURI NA AFRIKA MPAKA ASIKILIZWE HIVYO NA KIKWETE NA BENDERA ZAO KUPANDISHWA KILA KONA!
 
humu ndani wote wana hekima, lakini "hekima" za wengine ni za kupuuza!! Kwa mwelevu upenda kusoma zaidi ya ku-type keyboard!!

Ndugu yangu hapa umesema sahihi. Mama anasema "baeleze bayuwe. Kutomboka bila kitu mukichwa hakumpi mtu upredeje.

Kuna watu hapa wakurupukaji ile mbaya na wanapenda kuwavaa baadhi ya watu ili sijui waonekane vipi!!!
 
Pundit, i beg your pardon. Sio joker...... kuna kitu zaidi ya hapo. Kadanganywa vibaya sana. Bunge, lisiambiwe ni usalama wa Taifa. Kamati ya Rais ya Madini inaambiwa.... usalama gani wa Taifa kwa watu ambao hata hawajala kiapo cha kuficha siri? Usalama gani wa Taifa mbele ya wafanyabiashara wasio wabunge na wengine hawajawahi kuwa katika utumishi wa Umma. Kuna distortions from the government side and from the opposition side. Now the whole truth has to be said. HAKUNA USALAMA WA TAIFA. Nipo Kigoma, narudi huko. Mungu aniweke tu.... Nasema hapa ilki iwe wazi na sina cha kuficha ili niibuke tu Bungeni.

Its not about Pinda, its the nation. Our country!

Mkuu Zitto,
Nakubaliana na wewe kabisa kuwa hakuna kitu kama usalama wa Taifa. Ila, ingawa Pinda ni mshikaji wako, itakuwa vizuri pia ukamfahamisha kuwa kama kazi haiwezi, ikiwa ni kutokana na yeye kuja bungeni na majibu yaliyokomboka, basi aseme ili JK atafute mwingine atakayeweza kazi, au bunge lipige kura ya kutokuwa na imani naye.

Kwa maana nyingine ni kuwa Pinda anajua anachokifanya na hakudanganywa. Pesa za Meremeta + Tangold n.k., zinagusa sehemu nyeti za uwepo wa JK madarakani hivi leo na huo ndio usalama wenyewe wa taifa.
 
Mimi nilivyomwelewa Mwanakijiji ni kwamba uko hapa unajua ukweli(Pinda kama waziri mkuu anatakiwa kujua ukweli wa jambo hili), halafu unaenda mbele ya wananchi(wabunge) unasema uongo, hili ni jambo ambalo linarudi moja kwa moja kwa aliyetoa kauli wakati anajua ukweli.

Tatizo lote hapa haliko lilipokuwa hila kwa pinda aliyewadanganya wananchi wa Tanzania.
 
Kuhani, je kama Mh. Zitto katika muda wake toka habari hii ifike hapa amefanikiwa kuongea na Mh. Pinda lakini contents za maongezi hataki kuzitoa hapa, ila ameamua kusema tu kuwa 'tatizo siyo pinda,' ila wanaomdanganya.... je hapo Mh. Zitto ana haki ya kusema hivyo?

Uwaziri Mkuu hapewi kila mtu. Ni madaraka ambayo ili upewe shurti uwe mtu makini sana kwenye kutetea hoja kisahihi. Pinda kama waziri mkuu, hata kama akiambiwa na washauri wake kwamba moja jumlisha tatu ni sabini, inampasa awe makini kwa lolote atakaloliongea kwa raia. Alichotueleza ndugu Pinda ni upindishaji kauli ambao alitegemea kuutumia kutupumbaza bila ya yeye kuwa accountable na maneno yake. Huu ni mda muafaka kumfundisha kwamba Wadanganyika hatukubaliani naye kabisa kwenye kauli zenye kupindisha ukweli wa mambo.
 
Ni Kivipi Mashirika Ya Fedha Duniani Walikuwa Wakimpa Sifa Mkapa Kuwa Uchumi Unakuwa Na Huku Watu Wakifa Kwa Magonjwa,njaa Nk?
Wakati Wakimpa Misifa Kuwa Anapandisha Uchumi Wetu Kumbe Ni Wakati Anauza Nchi!
Na Mitego Ikeandele Kwa Kuwatega Wengine Kama Epa Etc Etc!
Sasa West Propaganda Si Applcable Kweli?
Badala Ya Kuripoti Ujambazi Wa Resouces Zetu..wao Wakampamba Mkapa(mtupu)
Kumbe Ni Propaganda Za Hizo Corporations Kwani Nchi Weshakabidhiwa..bisha?
 
Haya mambo ya kusingizia kila kitu Usalama wa Taifa inabidi yafike mwisho sasa...Huwezi kuamini kuna mtu nilimuuliza aina ya silaha wanazobeba walinzi wa rais akaniambia ni siri...

**Mkjj angalia PM yako and let me know
 
Back
Top Bottom