Mengi Vs Masha tuhuma, vitisho na matokeo!

Mengi Vs Masha tuhuma, vitisho na matokeo!

Status
Not open for further replies.
Nina predict kwamba hii issue itaishia kimya kimya. Kesho hakutakuwa na action yeyote ile ya Serikali dhidi ya Mengi. Na Masha hata step down wala kuhamishiwa wizara nyingine. Badala yake kutakuwa na mkutano wa kupooza mambo na Waziri Mkuu ndio atakayekuwa mediator, baada ya hapo kutakuwa na photo op..kuuonyesha umma kwamba things are OK. Kutakuwa hakuna comments kutoka either camp na sisi speculators tutaachwa wihtout any information ili tu form opinions zetu.
 
Capitol Hill,

Kuna watu wengine zaidi ya Mengi "wameishainunua kesi" na wanasema wana ushahidi, according to JF sources.

Inaonekana kuwa hata ndani ya CCM people are not too crazy about Masha, and now they wanna watch him fully self destruct.
 
Good point Pundit. Naona kwa vile everybody is on Mzee Mengi's side, kitakachofanyika ni damage control. Based on quote yako hapo juu yenye bold letters..nafikiri CCM will try to stop the bleeding. Masha ataachwa lakini nafikiri atakuwa amejifunza kitu kutokana na this saga.
 
Watu wa USA msianze yale mambo ya watu wa London miaka miwili iliyopita, ya kuleta ugomvi wenu wa mitaani hapa JF. Hivi hamjiulizi wale wakali wote wa London wameishia wapi?

Mkianza kuleta ya mitaani huko kwenu mtafukuza watu wengi sana. Huo ni ushauri tu.

Mada hii ni Masha vs Mengi, hawa wawili ndio tunatakiwa kuwajadili.

Ushauri mzuri sana Mtanzania,

Kwa upande wangu sijaona wide spread ugomvi kwa watanzania wa USA. Hapa watu wametapakaa sana na US ni kubwa kwa hiyo ni vigumu sana kwa mafisadi kusambaratisha watu.

Kama watu wa NY wakigombana, sisi wengine San Francisco, ATL, Chicago na kwingineko bado tutakuwa hapa kuwapa mafisadi a big run for their ufisadi..

Hata hivyo, ushauri wako ni mzuri sana na natumaini wakali wa London wengi wao wataendelea kuwa hapa (au kwingineko kokote) wakiendeleza vita hii dhidi ya wezi, majambazi, wauaji, na wakoloni wazawa wanaoangamiza nchi yetu.
 
Nina predict kwamba hii issue itaishia kimya kimya. Kesho hakutakuwa na action yeyote ile ya Serikali dhidi ya Mengi. Na Masha hata step down wala kuhamishiwa wizara nyingine. Badala yake kutakuwa na mkutano wa kupooza mambo na Waziri Mkuu ndio atakayekuwa mediator, baada ya hapo kutakuwa na photo op..kuuonyesha umma kwamba things are OK. Kutakuwa hakuna comments kutoka either camp na sisi speculators tutaachwa wihtout any information ili tu form opinions zetu.

nasikia hivi sasa mhe. masha yupo nje ya nchi ameongozana na waziri mkuu kwenye mkutano mmoja wa shirika la umoja wa mataifa (naamini safari hii ilikuwa kwenye ratiba kabla ya songombingo hili). labda mheshimiwa wazri mkuu anaweza tumia muda huu kumpa busara za ziada zinazohusu mahusiano ya kiongozi na wananchi wake.
 
Hiyo 'labda' ilitakiwa iwe kwa herufi kubwa 'LABDA'.

Maana hapa ni assuming kuwa Masha anamheshimu na kumsikiliza Waziri Mkuu wa sasa, PKMP. Sisemi kuwa hafanyi hivyo, lakini nina shaka kama kweli hilo lipo kutokana na uhusiano uliopo wa Masha na ENL.

Nyingine ya 'kutokea' inayozungumziwa ni kuwa Masha hakusema 'siku saba' kutokea lini, ingawa hii inapwaya kwani hata barua haijapokelewa (kama imeandikwa). Pia wanajaribu kusema kuwa taarifa alizotoa Mengi pale O'bay Polisi inatosheleza matakwa ya Waziri Masha, na kuwa Mengi hana haja ya kutoa taarifa zaidi. Utajaza .....

Capitol Hill yuko kwenye right path kuhusu damage control rather than fact-finding. Yetu macho na masikio.
 
Naona hali imetulia kidogo na sasa tunaweza kurudi kwenye mada bila makelele yasiyo na lazima.

Hapa kuna kitu kikubwa ambacho wengi tunashindwa kulitilia maanani. Ikiwa viongozi wa serikali iliyowekwa madarakani na wananchi wanaweza wakaitisha kikao cha siri na kupanga namna ya kumhujumu mwananchi - hii maana yake nini.

Ikithibitika kuwa kweli walifanya hivyo bila kujali hizo siri zilivyovuja, sisi kama wananchi tuna jukumu ya kuwawajibisha.

Kwanza kabisa tumpongeze kwa dhati huyo shujaa aliyeweza kuanika hiyo mipango ya kishetani.

Pili tulaani kwa nguvu zetu zote mtu ama watu ambao wamethubutu kupanga huo uovu - tukemee tabia hii kwa nguvu zetu zote.

Tatu tumwogope anayejaribu kutetea kitendo kama hiki cha aibu na kichafu kama ukoma.

Nne, tusiishie hapa tu bali tuwakaange kwa mafuta yao wenyewe - hawa watu ni wahaini.

Tano, waliohusika wote wavuliwe nyadhifa zao na wafikishwe mahakamani haraka sana.
 
Nimesoma kwamba kuna msomi mmoja pale Mlimani kasema kwamba Mengi kapeleka ujumbe mzito kwa JK , mara akasema ni hatari kwa siri za vikao vikubwa kujulikana na ni kosa kwa Mengi kuyajua haya .Mie nasema uliyetoka na tape kwaba sauti zipo on record nakupa ongezi .Lazima tufike mahali tuwe na vikao vya kujenga na kuihifdhi Nchi .Hiki cha kummaliza Mengi si kikao cha kujenga ni uharamia .Tape ioko nje sasa Masha endelea kubisha watu wana kungojea wamwage upu upu maana everyone is on record .
 
Naona hali imetulia kidogo na sasa tunaweza kurudi kwenye mada bila makelele yasiyo na lazima.

Hapa kuna kitu kikubwa ambacho wengi tunashindwa kulitilia maanani. Ikiwa viongozi wa serikali iliyowekwa madarakani na wananchi wanaweza wakaitisha kikao cha siri na kupanga namna ya kumhujumu mwananchi - hii maana yake nini.

Ikithibitika kuwa kweli walifanya hivyo bila kujali hizo siri zilivyovuja, sisi kama wananchi tuna jukumu ya kuwawajibisha.

Kwanza kabisa tumpongeze kwa dhati huyo shujaa aliyeweza kuanika hiyo mipango ya kishetani.

Pili tulaani kwa nguvu zetu zote mtu ama watu ambao wamethubutu kupanga huo uovu - tukemee tabia hii kwa nguvu zetu zote.

Tatu tumwogope anayejaribu kutetea kitendo kama hiki cha aibu na kichafu kama ukoma.

Nne, tusiishie hapa tu bali tuwakaange kwa mafuta yao wenyewe - hawa watu ni wahaini.

Tano, waliohusika wote wavuliwe nyadhifa zao na wafikishwe mahakamani haraka sana.

Mkuu Mag3... JK angekuwa mchukia ufisadi wa kweli kweli.. huyu Masha asingedhubutu kutoa wazo kama hilo. My suspicious mind tends to believe that kinara wa hii mikakati ya kuwanyamazisha watu wanaopigia kelele ufisadi ni JK mwenyewe. Huyu jamaa ni msanii hana lolote .. washirika wake wote ni mafisadi na ndio waliomwingiza madarakani......
 
Wana JF,
Kumbe hata CCM yenyewe kuna watu wana WIVU? Kibaya zaidi ni kwamba hata Mawaziri wenyewe wa CCM, wanawivu saaana. Wanamuonea WIVU Masha na huo wivu ni wa waziwazi. Wanashindwa kuamini kuwa mwenzao, kasoma USA, akaja UDSM akaitwa Mmarekani mweusi. Akarudi USA na kufanya Master. Akawa aajiriwe World Bank ila akaghaili. Kaja kafanya kazi mbili tatu na mara huyoooo, kawa waziri akiwa na miaka 38 tu. Mawaziri wa CCM donge hilooo. Wakaamuwa kumrekodi kwenye kikao na kumpa tape Mengi. Shame on you Mawaziri mliomrekodi mwenzenu na tape kumpa Mengi. Mnaona WIVU kuwa mwenzenu kafanikiwa akiwa kijana namna hiyo, ana kampuni ya Uwakili, mbunge na katembea sana tu dunia hii. Nyie mmesoma kwa mbinde, km 10 kwenda shule (kupiga umande) na jioni kumi kurudi nyumbani. Mkaenda Secondary, JKT (kuruta nyie) na baadaye ndiyo Chuo kikuu. Mkimuona Masha DONGE hiloo hadi mnashindwa kuhema. Muone AIBU. Watu wazima kumfanyia mwenzenu huo mchezo. WIVUUU Mbaya!!!!

NB: Sina mapenzi naona, INGAWA MACHO SINAA!!!
 
Maneno mazito kama haya si ya kupita bila kuungwa mkono kwa kweli .Umepiga hadi Ikulu kaka .
 
The folly of this post is that it utterly and sheerly disregard the despicable contents of the alleged tape.
 
Wana JF,
Kumbe hata CCM yenyewe kuna watu wana WIVU? Kibaya zaidi ni kwamba hata Mawaziri wenyewe wa CCM, wanawivu saaana. Wanamuonea WIVU Masha na huo wivu ni wa waziwazi. Wanashindwa kuamini kuwa mwenzao, kasoma USA, akaja UDSM akaitwa Mmarekani mweusi. Akarudi USA na kufanya Master. Akawa aajiriwe World Bank ila akaghaili. Kaja kafanya kazi mbili tatu na mara huyoooo, kawa waziri akiwa na miaka 38 tu. Mawaziri wa CCM donge hilooo. Wakaamuwa kumrekodi kwenye kikao na kumpa tape Mengi. Shame on you Mawaziri mliomrekodi mwenzenu na tape kumpa Mengi. Mnaona WIVU kuwa mwenzenu kafanikiwa akiwa kijana namna hiyo, ana kampuni ya Uwakili, mbunge na katembea sana tu dunia hii. Nyie mmesoma kwa mbinde, km 10 kwenda shule (kupiga umande) na jioni kumi kurudi nyumbani. Mkaenda Secondary, JKT (kuruta nyie) na baadaye ndiyo Chuo kikuu. Mkimuona Masha DONGE hiloo hadi mnashindwa kuhema. Muone AIBU. Watu wazima kumfanyia mwenzenu huo mchezo. WIVUUU Mbaya!!!

Kwahiyo unang'ang'ania na kumaanisha kwamba Mawaziri wenzake wameona wivu na hivyo kutoa siri kuhusu ujambazi wa Waziri Masha kama ni kweli alifanya hivyo? Kweli wewe mkuu mvivu wa kufikiri na una wivu wa mawazo pia..!
 
Wana JF,
Kumbe hata CCM yenyewe kuna watu wana WIVU? Kibaya zaidi ni kwamba hata Mawaziri wenyewe wa CCM, wanawivu saaana. Wanamuonea WIVU Masha na huo wivu ni wa waziwazi. Wanashindwa kuamini kuwa mwenzao, kasoma USA, akaja UDSM akaitwa Mmarekani mweusi. Akarudi USA na kufanya Master. Akawa aajiriwe World Bank ila akaghaili. Kaja kafanya kazi mbili tatu na mara huyoooo, kawa waziri akiwa na miaka 38 tu. Mawaziri wa CCM donge hilooo. Wakaamuwa kumrekodi kwenye kikao na kumpa tape Mengi. Shame on you Mawaziri mliomrekodi mwenzenu na tape kumpa Mengi. Mnaona WIVU kuwa mwenzenu kafanikiwa akiwa kijana namna hiyo, ana kampuni ya Uwakili, mbunge na katembea sana tu dunia hii. Nyie mmesoma kwa mbinde, km 10 kwenda shule (kupiga umande) na jioni kumi kurudi nyumbani. Mkaenda Secondary, JKT (kuruta nyie) na baadaye ndiyo Chuo kikuu. Mkimuona Masha DONGE hiloo hadi mnashindwa kuhema. Muone AIBU. Watu wazima kumfanyia mwenzenu huo mchezo. WIVUUU Mbaya!!!!

NB: Sina mapenzi naona, INGAWA MACHO SINAA!!!

I think this is meant to be sarcastic!.....
 
wandugu,

..naona tuko too obssesed na huyu dogo Masha. hebu twende hatua moja mbele. Waziri Masha alikuwa anauza idea ya kumhujumu Mengi kwa nani?

..Je, alifanya hivyo ktk mazingira ya vikao rasmi vya serikali, na vilivyoitishwa na kuwa chini ya uongozi wa nani?

..kama ilikuwa ni kwenye vikao vya serikali ni nani wengine waliokuwepo ktk kikao hicho? je, hili wazo la Masha kumhujumu Reginald Mengi lilipokelewa vipi na wajumbe wenzake? na zaidi ni nini ilikuwa maazimio ya kikao hicho kama kilikuwepo?

NB:

..naona kama vile watu hawako as open as i would have wanted them to be.

..Reginald Mengi mwenyewe pia hayuko open, na zaidi anadai kwamba amemsamehe huyo waziri kijana. sasa kama amemsamehe kulikuwa na haja gani kulileta suala hili mbele ya jamii?
 
Wana JF,
Kumbe hata CCM yenyewe kuna watu wana WIVU? Kibaya zaidi ni kwamba hata Mawaziri wenyewe wa CCM, wanawivu saaana. Wanamuonea WIVU Masha na huo wivu ni wa waziwazi. Wanashindwa kuamini kuwa mwenzao, kasoma USA, akaja UDSM akaitwa Mmarekani mweusi. Akarudi USA na kufanya Master. Akawa aajiriwe World Bank ila akaghaili. Kaja kafanya kazi mbili tatu na mara huyoooo, kawa waziri akiwa na miaka 38 tu. Mawaziri wa CCM donge hilooo. Wakaamuwa kumrekodi kwenye kikao na kumpa tape Mengi. Shame on you Mawaziri mliomrekodi mwenzenu na tape kumpa Mengi. Mnaona WIVU kuwa mwenzenu kafanikiwa akiwa kijana namna hiyo, ana kampuni ya Uwakili, mbunge na katembea sana tu dunia hii. Nyie mmesoma kwa mbinde, km 10 kwenda shule (kupiga umande) na jioni kumi kurudi nyumbani. Mkaenda Secondary, JKT (kuruta nyie) na baadaye ndiyo Chuo kikuu. Mkimuona Masha DONGE hiloo hadi mnashindwa kuhema. Muone AIBU. Watu wazima kumfanyia mwenzenu huo mchezo. WIVUUU Mbaya!!!!

NB: Sina mapenzi naona, INGAWA MACHO SINAA!!!

Okay, lets assume kwamba waliompatia hiyo tape bwana Mengi ni Mawaziri wanaomwonea wivu Lau. Mawaziri hao walikuwepo kwenye hicho kikao. Implication haitakuja kwa Masha peke yake bali wote waliokuwa kwenye hicho kikao wakipanga mikakati. Kwa hiyo hata hao wanaomwonea wivu nao watakuwa ndani ya saga. Meaning that hao mawaziri wa CCM wana wivu hadi wanajifanyia wivu! Mtego wa panya hunasa na waliomo na wasiokuwemo.
 
Hii kitu bado inatokota tu? Safi sana. Huyu Waziri suspect aliye-leakisha wa wizara nyeti anaweza kuwa nani
Vigogo wawindana serikalini

• Mzozo wa Mengi, Masha

na Charles Mullinda

KUVUJA kwa mikakati ya siri serikalini kumetajwa kuwa chanzo kikuu cha mzozo unaoendelea hivi sasa kati ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha na mfanyabiashara maarufu, Reginald Mengi, Tanzania Daima Jumatano imedokezwa.

Habari ambazo Tanzania Daima imezipata kutoka vyanzo vya kuaminika zinaeleza kwamba, kauli aliyoitoa Mengi wiki iliyopita imesababisha baadhi ya maofisa wa juu serikalini kuanza kuchukua hatua za kuwasaka viongozi, wakiwamo mawaziri ambao wamekuwa wakivujisha taarifa mbalimbali ya kimaamuzi ndani ya serikali.

Chanzo kimoja cha habari kimeieleza Tanzania Daima Jumatano kwamba, hatua ya Waziri Masha kumpa Mengi siku saba zinazoisha kesho, akimtaka athibitishe madai yake kwamba kuna waziri kijana anayeongoza wizara nyeti, anayeshawishi serikali kumhujumu kibiashara, inalenga kumlazimisha mfanyabiashara huyo amtaje mtu aliyemweleza taarifa hizo ambazo kimsingi zilijadiliwa katika vikao viwili vikubwa vya ngazi ya kitaifa.

Hatua ya Masha kumuandikia Mengi barua ya kumtaka awasilishe ushahidi wa madai yake hayo, inaonekana kuwashtua baadhi ya wanasiasa ambao wameitafsiri hatua hiyo kuwa inayoweza kuwa na madhara makubwa kisiasa katika siku za usoni.

Uchunguzi wa Tanzania Daima Jumatano unaonyesha kwamba, mshtuko huo ndio ambao katika siku za hivi karibuni umesababisha kuibuka kwa wanasiasa kadhaa wazito ambao ama wamejitokeza kumpinga Masha hadharani huku wengine wakitahadharisha na kutaka kusitishwa kwa malumbano haya.

Wanasiasa kadhaa wa CCM na wale wa upinzani waliozungumza na gazeti hili wanasema, lengo moja la mzozo huu wa sasa ni hatua ya baadhi ya viongozi serikalini kujaribu kumdhibiti Mengi ambaye katika miaka ya hivi karibuni vyombo vyake vya habari vimeonekana kuwa mstari wa mbele katika kuhujumu kile wanachokielezea kuwa masilahi yao na ya taifa.

‘‘Wakubwa kadhaa serikalini kwa kauli moja wamefikia hatua ya kuanza kumuona Mengi kuwa ni tatizo. Huyu jamaa haeleweki ana malengo gani kisiasa, kwani amekuwa nyuma ya kila jambo kubwa hapa nchini. Ameshiriki kutukifisha mahali pagumu sana, hata kusababisha serikali ishindwe kufanya kazi yake sawasawa, kwa kweli ni lazima ashughulikiwe ipasavyo,” alisema mbunge mmoja wa CCM anayeunga mkono hatua ya Masha kumpa Mengi siku saba.

Ofisa mmoja wa juu serikalini aliyezungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa jina gazetini alisema, pendekezo la kutaka serikali ichukue hatua ya kumbana Mengi lilitolewa kwanza katika kikao kimoja cha juu cha kiserikali kinachoshughulikia masuala ya usalama nchini kabla ya jambo hilo hilo kujadiliwa tena katika Baraza la Kazi linalojumuisha mawaziri kadhaa.

‘‘Kilichoishtua serikali ni kumsikia Mengi akizungumza kuhusu mambo yaliyojadiliwa katika kikao kimoja nyeti cha kitaifa kinachohusisha watu wazito. Sasa jamaa walichofanya wanataka kumlazimisha Mengi amtaje mtu aliyempa taarifa hizo ili hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi yake,” kilisema chanzo kimoja cha habari.

Chanzo kingine cha habari kilichozungumza na Tanzania Daima Jumatano kinaeleza kwamba, tayari maofisa wa serikali wanaofuatilia nyendo za baadhi ya mawaziri wameshaanza kumtaja waziri mmoja anayeongoza wizara nyeti kuwa mtu ambaye alimpelekea Mengi taarifa za kuwapo kwa mjadala huo, ambao hata hivyo bado haujachukuliwa kuwa msimamo rasmi wa serikali.

Hata hivyo, katika hatua ambayo inaweza kumnusuru waziri huyo, habari hizo zinaeleza kwamba, siku na wakati vikao hivyo vikikaa, waziri huyo ‘anayetafutwa’ hakuwa miongoni mwa wajumbe waliohudhuria kikao kimojawapo ambacho baadhi ya washiriki wake ni wakuu wa taasisi nyeti za dola.

Hata hivyo katika hatua nyingine, kuibuka kwa mzozo huo kumesababisha kuibuka kwa nadharia mbalimbali kuhusu utendaji na uwajibikaji wa viongozi serikalini.

Kundi moja la wadadisi wa mambo, wanakielezea kitendo cha waziri kupendekeza mfanyabiashara kuhujumiwa kuwa ni hatua ya kihalifu ambayo haipaswi kuungwa mkono kwa namna yoyote na serikali ambayo imeruhusu kisheria ushindani wa kibiashara katika misingi ya haki.

Miongoni mwa watu wenye mtazamo wa namna hii ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, ambaye anasema, ni jambo la fedheha kwa kiongozi wa dola kufikia hatua ya kufikiria kumhujumu mfanyabiashara mzalendo kwa kutumia njia za kihalifu.

Hata hivyo kundi jingine la wadadisi wa mambo, pasipo kuangalia uhalali au uharamu wa hatua hii ya kumdhibiti Mengi, wanaeleza kushangazwa na hatua ya maamuzi na mijadala nyeti serikalini kuvuja.

Mmoja wa wahadhiri waandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam aliyezungumza na gazeti hili, alisema kuwa, kufanikiwa kwa Mengi kunasa siri za kikao nyeti serikalini, kunaashiria kuwapo kwa mgawanyiko mkubwa kati ya viongozi waandamizi.

“Mengi si mjumbe wa vikao nyeti serikalini, hivyo kuibuka kwake na kueleza kuwa amenasa taarifa kutoka ndani ya vikao vya juu vya viongozi waandamizi, kuna maana kwamba, yupo kiongozi ambaye ni mjumbe wa kikao hicho aliyemfikishia kile kilichojadiliwa ndani ya kikao hicho au mjumbe huyo alikifikisha kwa rafiki wa karibu na Mengi, hivyo kuwa rahisi kumfikia.

“Na hii maana yake ni kwamba, serikali haiko salama, maana nyingine ni kumfikishia ujumbe Rais Kikwete kuwa anaoshirikiana nao kuongoza wanamzunguka au wanazungukana. Lakini ujumbe muhimu kwa rais ambao mimi naona Mengi ameamua kumtumia ni kwamba baadhi ya wasaidizi wake hawafai kuwa viongozi, hawajui nini maana ya siri za serikali,” alisema msomi huyo.

Mwingine mwenye mtazamo huo, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe, alieleza kuwa Waziri Masha hapaswi kumtisha Mengi kwa kumpa siku saba ili kutoa ushahidi wa madai yake, kwa sababu hata yeye (Zitto) amepata kuzisikia taarifa hizo.

Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, alikaririwa hivi karibuni akieleza kuwa ana taarifa kuwa waziri mmoja ndiye aliyepeleka hoja ya kutaka serikali itumie vyombo vyake kumhujumu Mengi kwa kumbambikia kodi kubwa katika biashara zake.

Habari za hivi karibuni zilizoifikia Tanzania Daima Jumatano na kuthibitishwa na baadhi ya wanasiasa walio karibu na Zitto zinaeleza kuwa, Waziri Masha alishtushwa na kauli hiyo ya Zitto hata akafikia hatua ya kumtumia ujumbe mfupi kupitia simu yake ya kiganjani akimtaka kutojiingiza katika sakata hilo.

Taarifa ambazo zimethibitishwa na Zitto mwenyewe zinaeleza kwamba, Masha alimweleza bayana kwamba, jitihada zake za kujaribu ‘kununua’ kesi yake na Mengi haziwezi kumfanya ‘amuuzie’ yeye.

Mengi katika mazungumzo yake na waandishi wa habari, mbali ya kumzungumzia waziri huyo, alisema kuwa alitumiwa ujumbe wa vitisho vya kuuawa kwa sumu.

Sehemu ya maandishi yaliyo katika ujumbe wa maandishi wa simu uliotumwa kutoka simu namba 0768-373967, ulisomeka hivi: ‘‘Ni afadhali kunyofoa roho yako upotee kuliko kukuachia uchafue amani na utulivu kwa tamaa zako za kutaka kuwa rais... unachafua sana amani ya nchi kwa uchochezi wako. Tunajua unawahonga wahariri wote na kukusujudia kama Mungu mtu. Unapenyeza sumu kali ya uzandiki watu waichukue serikali. Hivi yakitokea machafuko wewe utasalimika? Wewe ni mnafiki mkubwa, unajifanya upo karibu na ‘Government’ kumbe ni mnafiki wa kutisha. Jihadhari lazima tukuue!”

Siku chache baada ya Mengi kutoa madai hayo, Waziri Masha alitoa kauli ya kumtaka athibitishe madai ya kuwapo kwa waziri kijana anayefanya njama za kutaka kummaliza kibiashara.
 
Ok,
Naona hamkunielewa. Nimemalizia na sentensi :-
NB: Sina mapenzi naona, INGAWA MACHO SINAA!!!

Hivi ndiyo tumehubiriwa kila tukisema Masha kachemka. Kila anayemshambulia Masha basi ana wivu. Kama ulikuwa ni mkutano wa Mawaziri na wakamrekodi, ina maana pia wao hawakubaliani naye na kila asiyekubaliana naye, hapa anaambiwa kuwa ANAWIVU.
Ni katika kusema "If A=B, and B=C, then A=c". Simple mathematics, can't you see??
NB:- Mwenye Mapenzi haoni, ingawa macho anayo!!!!!
 
Kwahiyo unang'ang'ania na kumaanisha kwamba Mawaziri wenzake wameona wivu na hivyo kutoa siri kuhusu ujambazi wa Waziri Masha kama ni kweli alifanya hivyo? Kweli wewe mkuu mvivu wa kufikiri na una wivu wa mawazo pia..!

Akilimtindi,
Angalia usije ukawa wewe ndiyo MVIVU wa kufikiri.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom