Mengi Vs Masha tuhuma, vitisho na matokeo!

Mengi Vs Masha tuhuma, vitisho na matokeo!

Status
Not open for further replies.
Wana JF,
Kumbe hata CCM yenyewe kuna watu wana WIVU? Kibaya zaidi ni kwamba hata Mawaziri wenyewe wa CCM, wanawivu saaana. Wanamuonea WIVU Masha na huo wivu ni wa waziwazi. Wanashindwa kuamini kuwa mwenzao, kasoma USA, akaja UDSM akaitwa Mmarekani mweusi. Akarudi USA na kufanya Master. Akawa aajiriwe World Bank ila akaghaili. Kaja kafanya kazi mbili tatu na mara huyoooo, kawa waziri akiwa na miaka 38 tu. Mawaziri wa CCM donge hilooo. Wakaamuwa kumrekodi kwenye kikao na kumpa tape Mengi. Shame on you Mawaziri mliomrekodi mwenzenu na tape kumpa Mengi. Mnaona WIVU kuwa mwenzenu kafanikiwa akiwa kijana namna hiyo, ana kampuni ya Uwakili, mbunge na katembea sana tu dunia hii. Nyie mmesoma kwa mbinde, km 10 kwenda shule (kupiga umande) na jioni kumi kurudi nyumbani. Mkaenda Secondary, JKT (kuruta nyie) na baadaye ndiyo Chuo kikuu. Mkimuona Masha DONGE hiloo hadi mnashindwa kuhema. Muone AIBU. Watu wazima kumfanyia mwenzenu huo mchezo. WIVUUU Mbaya!!!!

NB: Sina mapenzi naona, INGAWA MACHO SINAA!!!

Wewe, hujatukana mawaziri wa CCM tu, umetutukna watu wote tuliosoma kwa kupiga umande. Mimi naona umetuvunjia heshima watu wote tulio kwenda JKT na kusota mwaka mzima, ili wale wote waliokacha kwa sababu baba zao wana sauti serikalini waendelee kupeta.

Unachokionyesha hapa ni Utamaduni wa kifisadi ambao nadhani ndiyo ulio kulea.Walikuwepo maelfu ya watoto Mahillsiders waliokacha kwenda JKT siyo kwa sababu ya ujanja ila ni kwa sababu za kifisadi. Leo hii unatuonyesha kwamba kuto kwenda JKT ulikuwa ujanja?
Utetezi ulioutoa juu ya Masha hauna msingi na zaidi umejaa dharau na zaidi hoja yako inaunga mkono umoja na mshikamano wa uovu ndani ya CCM.

Kuhusu hilo la Mafisadi kugeuziana vibao wenyewe kwa wenyewe hilo siingilii kwa sababu ni sehemu ya utamaduni wao kulana mikia ndani ya CCM.
Kama anayeliwa mkia sasa hivi ni Masha kisha atafuata Nchimbi hilo ni tatizo ndani ya CCM.
 
DEEP GREEN + MASHA KUMLILIA LOWASSA + MASHA KUWATEMBELEA MAFISADI GEREZANI + MASHA KUMFILISI MENGI = ?

Ndugu zangu kwa kweli ni wazi sasa kuwa sitakua nimefanya dhambi kusema kuwa mbio za sakafuni huiishi ukingoni.

Mimi ni mmoja wa vijana waliokuwa wakiangalia uteuzi wa Masha kama mwanzo mzuri wa utekelezaji wa mapinduzi ya CHIMWAGA yaliyotoa ushindi kwa kizazi kipya cha uongozi wa CCM nchini. Kwa mara chache nilizopata kumuona Masha na michango yake katika mijadala niliamini kuwa akiacha ubrazameni basi ana mchango mkubwa katika kuleta mabadiliko ya utamaduni wa kisisiasa nchini. Ingawa nilikuwa na maswali mengi kuhusu mwenendo wake kijamii lakini niliamini kuwa Masha akiwa kijana aliyepata bahati ya kuujua ulimwangu wa kidemokrasia, kuwa na upeo mzuri wa mambo ya kisiasa na kisheria na kutokana na historia yake kuwa katika siasa za upinzani kabla kurudi nyumbani CCM, basi angeweza kuwa kiungo muhimu katika juhudi za kubadili utando wa uongozi mbovu na usiojali demokrasia wala utawala bora miongoni mwa viongozi wetu wanaoshindwa kuona mbali zaidi juu ya hatima ya Tanzania na ile ya CCM.

Likaanza suala la kutoa siri za serikali akiwa maskani pale rosegarden, likaja la kumlilia Lowasa, likaja la nyumba ndogo hadharani, likaja la DEEP GREEN (nililisikia kabla lakini nikampa benefit of doubt), Likaja la kuandaliwa na kina ROSTAM na LOWASSA kushindana na JK 2010 (nikadhani ni yaleyale), Likaja la kuwatembelea MAFISADI gerezani, Mara sasa hili la mkakati wa kufilisi wanaothubutu kutoa sauti dhidi ya mfumo fisadi nchini mwetu....

Kwanza nilifikiri kuwa ni moja ya yale matamshi yake akishapata vinyaji vyake lakini kumbe ni kwenye kikao nyeti kabisa? Hii ni kali tena kutoka kwa mwanasheria aliyekulia katika mazingira kama ya MASHA. Kwa kweli hii sio tu ni kuvunjika moyo na vijana wenzangu lakini pia ni aibu kubwa sana.

Tukumbuke wako wengi ambao bado wanafikira ya kutokuamini kuwapa majukumu makubwa vijana. Kupewa nafasi kuwa waziri tena wa wizara nyeti kwa ndugu Masha kulikuwa ni muhimu katika kuwafanya wazee wetu waliogubikwa na fikira za kihafidhina kuamka na kuthamini mchango wa uthubutu wa vijana katika maswala ya uongozi. Makosa ya Lawrence Masha si tu yanatia aibu lakini pia ni pigo kubwa kwa wote wenye kuamini umuhimu wa kuwaamini vijana kupewa nyeti za uongozi. Kwa kifupi Masha amem......JK na ajenda yake ya kizazi kipya. Masha amewaangusha vijana wa Tanzania....

Tanzanianjema
 
Wewe, hujatukana mawaziri wa CCM tu, umetutukna watu wote tuliosoma kwa kupiga umande. Mimi naona umetuvunjia heshima watu wote tulio kwenda JKT na kusota mwaka mzima, ili wale wote waliokacha kwa sababu baba zao wana sauti serikalini waendelee kupeta.

Unachokionyesha hapa ni Utamaduni wa kifisadi ambao nadhani ndiyo ulio kulea.Walikuwepo maelfu ya watoto Mahillsiders waliokacha kwenda JKT siyo kwa sababu ya ujanja ila ni kwa sababu za kifisadi. Leo hii unatuonyesha kwamba kuto kwenda JKT ulikuwa ujanja?
Utetezi ulioutoa juu ya Masha hauna msingi na zaidi umejaa dharau na zaidi hoja yako inaunga mkono umoja na mshikamano wa uovu ndani ya CCM.

Kuhusu hilo la Mafisadi kugeuziana vibao wenyewe kwa wenyewe hilo siingilii kwa sababu ni sehemu ya utamaduni wao kulana mikia ndani ya CCM.
Kama anayeliwa mkia sasa hivi ni Masha kisha atafuata Nchimbi hilo ni tatizo ndani ya CCM.

Naona Madela wa Madilu et al. hamjaielewa post ya Sikonge ilikuwa na maana gani! If you took time to think about it, you would have understood what he/she meant!
 
Wewe, hujatukana mawaziri wa CCM tu, umetutukna watu wote tuliosoma kwa kupiga umande. Mimi naona umetuvunjia heshima watu wote tulio kwenda JKT na kusota mwaka mzima, ili wale wote waliokacha kwa sababu baba zao wana sauti serikalini waendelee kupeta.

Unachokionyesha hapa ni Utamaduni wa kifisadi ambao nadhani ndiyo ulio kulea.Walikuwepo maelfu ya watoto Mahillsiders waliokacha kwenda JKT siyo kwa sababu ya ujanja ila ni kwa sababu za kifisadi. Leo hii unatuonyesha kwamba kuto kwenda JKT ulikuwa ujanja?
Utetezi ulioutoa juu ya Masha hauna msingi na zaidi umejaa dharau na zaidi hoja yako inaunga mkono umoja na mshikamano wa uovu ndani ya CCM.

Kuhusu hilo la Mafisadi kugeuziana vibao wenyewe kwa wenyewe hilo siingilii kwa sababu ni sehemu ya utamaduni wao kulana mikia ndani ya CCM.
Kama anayeliwa mkia sasa hivi ni Masha kisha atafuata Nchimbi hilo ni tatizo ndani ya CCM.

Wee Madela, utafungiwa BURE. Wacha matusi. Kwangu mie wala sijali sana maana kwenye Zege na Saidia wangu, ni lugha ya kawaida. Ukianzia ile mashine ya kufanyia compaction kwenye zege ili kuondoa hewa. Siku nyingine chagua matusi ya maana na siyo hayo matusi ya watoto wa chekechea.
Hivi unafikiri huku Sikonge kuna barabara ya Lami? Kama JKT niliripoti hapo Msange JKT, na kuhangaika na Mzee wa Morogoro (Kepten Mrimba) aliyetupiga kwata la Porini hadi ikawa tukahudhurie mazoezi ya Mirambo Division - JWTZ). Wewe hilo uliye tu maana hukuhudhuria. Hivyo kama Mwanajeshi nina tizi kubwa kukuzidi. Na huko niliimba "Magwega Wa Chiguru". Ulishamsikia Kibaka Magwega wa Chiguru? Alikuwa anatoka Majita B.
 
1-Ninavyofahamu Waziri Masha ni mwanasheria mahiri na kijana msomi pamoja na kuwa na kasoro zake za kibinadamu kama tulivyo binadamu wote kwa hiyo je, kisheria alikuwa sahihi kutoa majibu aliyoyatoa kwa waandishi wa habari?

2-Kwa ninavyofahamu Masha ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, wizara ambayo chini yake kuna Jeshi la Polisi, Magereza na Uhamiaj kwa hiyo ninajiulizai, je, hoja ya Mengi ilikuwa inahusu maeneo yaliyo chini ya wizara yake? Kwa kuanzia polisi wanashughulikia makosa ya jinai ina maana kauli ya Mengi ina jinai?

3-Kama kuna jinai inaangukia katika sheria gani? maana kasema kuna waziri kijana amependekeza abambikiwe kesi na hajasema serikali imeamua/imekubaliana/imepokea ushauri kwa hiyo hata huo ushauri haifahamiki kama umekubaliwa ama ulikataliwa.

4-Waziri Masha kasema kwamba asipotoa ushahidi baada ya siku saba sheria itachukua mkondo wake, sheria ipi? Sheria ya Uhaini? Uchochezi? Kashfa? kusema uongo?

- Mkuu Halisi, kama kawaida yako kwa kweli ninakubaliana na wewe kwa 100%, ni maswali sawa na valid, ndio maana mimi ninatka hii ishu iende kwenye sheria maana ndiko tu haya maswali yanaweza kujibiwa na mwenye makosa kuwajibishwa,

Hivi siku saba zinaisha lini wakuu maana I can't wait kuona kitakachofuata na ni sala zangu kwa Mungu kwamba this ishu itattatuliwa kwenye sheria na sio pembeni, maswali mazito sana haya mkuu.
 
....huo wivu ni wa waziwazi. Wanashindwa kuamini kuwa mwenzao, kasoma USA, akaja UDSM akaitwa Mmarekani mweusi. Akarudi USA na kufanya Master. Akawa aajiriwe World Bank ila akaghaili. Kaja kafanya kazi mbili tatu na mara huyoooo, kawa waziri akiwa na miaka 38 tu.

.... Mnaona WIVU kuwa mwenzenu kafanikiwa akiwa kijana namna hiyo, ana kampuni ya Uwakili, mbunge na katembea sana tu dunia hii. Nyie mmesoma kwa mbinde, km 10 kwenda shule (kupiga umande) na jioni kumi kurudi nyumbani. Mkaenda Secondary, JKT (kuruta nyie) na baadaye ndiyo Chuo kikuu. Mkimuona Masha DONGE hiloo hadi mnashindwa kuhema. Muone AIBU. Watu wazima kumfanyia mwenzenu huo mchezo. WIVUUU Mbaya!!!!

Kuna kitu nimejifunza hapa jamvini nilikuwa sikijui, na hiyo post yako Sikonge ni exhibit A ya swala hilo.

Kumbe maishani ukiwa na issues na mtu mwenye mafanikio, cheo, elimu, hela, na kadhakika, ukimkosoa tu, utaonekana una wivu. Hilo kwa kweli nilikuwa silijui kabisa.

Kwa mfano, wengine tumeambiwa tuna wivu dhidi ya mafanikio ya Masha. Wakina Fundi Mchundo na wengine wengi humu wameambiwa hayo hayo. The thing is, though, hujui huyo Fundi Mchundo ana mafanikio au failures gani za kumfanya amuonee wivu Masha. Hivi unapomsoma mtu kama Mchundo hapa unaona kweli ni failure maishani ? Kwamba ni jinga moja halikwenda shule lilikimbia umande kweli, kama anavyosema ? Unaona anaandika kama mtu ambae hana elimu kweli? Please!! Anaweza kuwa anaendesha baikeli kama anavyosema lakini ni kwa sababu anataka tu. Mtu mwenye kichwa ka Fundi akitaka kigari hawezi kushindwa. Na inawezekana analo au anayo mengi tu, ila tunazugwa tu hapa, ni mtu mwenye humility na modesty ya kutotaja mashangingi yake hapa. Humility comes before honor, wanasema, na ndio ninachokiona kwa huyu na wengi wa hapa. Huyu hawezi kutishwa na "mafanikio" ya Masha!!! Na ndio maana sio lazima asema anamjua Masha, sijui kamwendesha kwenda mitihanini na Airport kama Field Masha na Lau Masha, and all that obsequious gibberish! (Fundi nisamehe nimechukua liberty kukutumia kama mfano maana na wewe, kama mimi na baadhi ya wengine, umeambiwa una wivu.)

Halafu sio kila mtu anataka kuwa Waziri kama Masha. Waziri katika serikali ya mafisadi is not a very cushy job, I don't think.

Kingine, Masha sio wakili mwenye mafanikio peke yake, au kiongozi mwenye degree mbili. Cha ajabu cha kuonewa Masha wivu ni nini hasa? Kusoma na kuishi Marekani ? Kusoma kasoma sana, lakini jamani ni nini alichosomea Masha kuonea wivu, Masters ya Georgetown ? Hata Sumaye ana Masters ya Harvard, nini Georgetown. Au kuishi huko US ? Marekani hata khalagabaho kaa mimi naishi. And, believe you me, it ain't no seventh heaven, it's a nightmare, as Malcom X used to say. We huoni Masha mwenyewe aliingia mitini kurudi UDSM ? Wanasema alipokuwa UDSM alikuwa anaitwa Mmarekani, well, kama kukaa Marekani kunapandisha chati mbona alinyuti ? Ngoma yake ilikuwa ngumu nini ? Sioni cha kumuonea wivu Masha mimi.

Na hatuwezi kumuonea wivu Masha eti kwa sababu tuna uchungu yeye hakwenda JKT . No, yeye ali dodge National Service!! National Service ile ni badge of honor! Huyo Masha mwenyewe naamini anajuta saa hizi ndani ya moyo wake kwa kutoonyesha uzalendo. Hana cha kuonewa wivu hapo Masha kwa ku dogde JKT.

Na hata huo uwaziri, kusema tunamwonea wivu waziri kijana, uwaziri sio achievement ya kujivunia saaaana kwa sababu ni cheo cha kupewa tu. Sio bootstrap achievement, sio jasho lako linalokupa uwaziri necessarily, sio umaridadi wako kikazi. Hata mimi nisiyejua kitu ningekuwa najuana na Kikwete toka kwenye mizunguko yake ya usiku vilabuni toka wakati Kikwete yuko Naibu Waziri labda na mimi leo hii ningeukwaa uwaziri.

Masha hana cha kuonewa wivu. At least mimi sikioni.
 
tunasema hivi kiongozi yoyote ashambuliwe kwa shutuma zilizo na ukweli, kuna wakati alishambuliwa Mwenyekiti wa Chadema kwa maneno ya uongo wa kupindishwa kwa makusudi kuhusu shule yake UK, kwamba anafanyiwa mitihani na Balile, tulisema kuwa ule ni wivu wa binafsi,

- Kuna wakati ameshambuliwa Zitto hapa kwa makusudi kwa kupindishwa ukweli, tulisema kuwa ni wivu wa binafsi, na kuna wakati zililetwa article za kumchafua Dr. Slaa na Mbowe tena kwa makusudi mazima, tuliomba ziondolewe hapa JF haraka sana, kwa sababu zilikuwa ni uzushi na uongo uliochongwa kwa makusudi na at best ni wivu tu wa binafsi,

- Tuliyasema haya against wananchi wengi hapa waliokuwa hawakubaliani na mawazo yetu hapa na haikuwa tatizo, sasa tunasema tena kwamba waziri wa ndani ashambuliwe kwa makosa aliyokwisha yafanya na yanakubalika kua ni ya kweli lakini kupindisha ukweli kwa makusudi ili kumchafua ndio tunaita kama vile kule nyuma kua ni wivu wa binafsi, na it has nothing to na wasiokubaliana na mawazo yetu on the ishu.

- Tunajaribu sana kupata ukweli wa ishu maana kuna habari nyingi sana, ingawa Halisi leo ametoa maneno mazito sana kuhusu the ishu ninayakubali as ukweli wa ishu, lakini ninatofautiana naye on one thing only, namna ya kuimaliza ishu, maana tungependa sheria ifuate mkondo na kama waziri amekosea basi ajiuzulu kama alivyoahidi na sheria iangaliwe kama imevunjwa na matendo yake katika ku-deal nayo, na kama Mengi amekosea sheria ichukue mkondo pia,

- Mind you tunazo dataz za kutosha kuhusu ushahidi alionao Mengi, yaani tepu yenye maneno ya waziri mmoja kama anavyodai hilo leo ninalithibitisha kua halina ubishi na jina la waziri tunalo tayari, na tepu nyingi nyingine mojawapo ikiwa ya Makamba, naye akijaribu kushauri uvunjwaji wa sheria, sasa tunazo dataz za kutosha kuhusu tepu zote alizonazo na zilivyopatikana.

- Habari iko wazi kwamba kama Mengi asinge-act kwanza huyu waziri angemmaliza, sasa ndio maana tunasema ishu iende kwenye sheria, ili sheria ichukue mkondo na sio siri tena waziri anayehusika is in big shit. Tumeonywa sana kutosema majina ya wahusika wa hii ishu, lakini ninasema hivi tumewafahamisha wahusika kuwa kama ukweli haukuwekwa hadharani when the times come, tutayaweka yote nje kama yalivyo!

Thanxs!
 
Kuna kitu nimejifunza hapa jamvini nilikuwa sikijui, na hiyo post yako Sikonge ni exhibit A ya swala hilo.
Waliokaa, wakasoma na wakatafakari aliyosema Sikonge bila shaka wamejifunza mengi tu.
Kumbe maishani ukiwa na issues na mtu mwenye mafanikio, cheo, elimu, hela, na kadhakika, ukimkosoa tu, utaonekana una wivu. Hilo kwa kweli nilikuwa silijui kabisa.
Wengi tunaopiga kelele kupinga ufisadi tunaambiwa tunasukumwa na wivu. Ghafla neno wivu imekuwa silaha wanayotumia wezi na walevi wa madaraka kujihami wakiungwa mkono na wapiga debe wao
Kwa mfano, wengine tumeambiwa tuna wivu dhidi ya mafanikio ya Masha. Wakina Fundi Mchundo na wengine wengi humu wameambiwa hayo hayo. The thing is, though, hujui huyo Fundi Mchundo ana mafanikio au failures gani za kumfanya amuonee wivu Masha. (Fundi nisamehe kukutumia kama mfano maana na wewe, kama mimi na baadhi ya wengine, umeambiwa una wivu.)
Hakika inachekesha eti umwonee wivu mtu ambaye humjui wala hakujui -kisa ? Naamini mtu anayevurunda kama anavyofanya Masha ni wa kuhurumiwa na kamwe si kuonewa wivu. Mbio za watu wa aina hiyo ni fupi na zinakuwa tishio tu kwa wanaoishi kwa kutegemea fadhila zao.
Halafu sio kila mtu anataka kuwa Waziri kama Masha. Waziri katika serikali ya mafisadi is not a very cushy job, I don't think.
Ushikaji saa nyingine ukitangulizwa sana unadumaza upeo wa mtu kufikiri na kupambanua mambo. Mtu zima unakuta unatetea hata kile kisichohitaji utetezi - self evident. Halafu wanaojaribu kukuweka sawa unasema wana wivu - how low can one get.
Kingine, Masha sio wakili mwenye mafanikio peke yake, au kiongozi mwenye degree mbili. Cha ajabu cha kuonewa Masha wivu ni nini hasa? Kusoma na kuishi Marekani ? Kusoma kasoma sana, lakini jamani ni nini alichosomea Masha kuonea wivu, Masters ya Georgetown ? Hata Sumaye and Masters ya Harvard, nini Georgetown. Au kuishi huko US ? Marekani hata khalagabaho kaa mimi naishi. And, believe you me, it ain't no seventh heaven, it's a nightmare, as Malcom X used to say. We huoni Masha mwenyewe aliingia mitini kurudi UDSM ?
Come easy, go easy. Degree mbili zinazomtuma mtu kuongea upupu kama anavyofanya Masha, katu hazitufai. Hivi sasa Tanzania tunaanza tabia ya ku'tolorate' tabia za ajabu kama za kuwaenzi wezi na wahujumu wa taifa. No, this has to stop.
Wanasema alipokuwa UDSM alikuwa anaitwa Mmarekani, well, kama kukaa Marekani kunapandisha chati mbona alinyuti ? Ngoma yake ilikuwa ngumu nini ? Sioni cha kumuonea wivu Masha mimi.
BWM mwenyewe aliwahi kuwa Marekani tena kwa wadhifa mzito tu - balozi. Aliporudi na kuchaguliwa kuwa Raisi alianza kufanya mambo ya ajabu ajabu. Tulipopiga kelele tukaambiwa tuna wivu wa kike na wana habari walipoanza kudadisi wakaambiwa ni wavivu wa kufikiri. Masikini BWM siku hizi anatafuta pa kuficha uso wake, lakini angalau aliuonja Uraisi. Sasa huyu Lau aonewe wivu kwa kitu gani - eti anaota Ikulu - thubutu !
Na tuwezi kumuonea wivu Masha eti kwa sababu tuna uchungu yeye hakwenda JKT . No, yeye ali dodge National Service!! National Service ile badge of honor! Huyo Masha mwenyewe naamini anajuta saa hizi ndani ya moyo wake kwa kutoonyesha uzalendo. Hana cha kuonewa wivu hapo Masha kwa ku dogde JKT.
Kwa ya ku'dodge' JKT hana sifa ya kuwa waziri kwa sababu alionyesha wazi hana uzalendo. Halafu hii inaonekana wazi kabisa kwa kuthubutu kusuka mpango wa kumhujumu mzalendo - kwenye vikao vya siri. Huyu si wa kuonewa wivu, ni wa kuzomewa.
Na hata huo uwaziri, kusema tunamwonea wivu waziri kijana, uwaziri sio achievement ya kujivunia saaaana kwa sababu ni cheo cha kupewa tu. Sio bootstrap achievement, sio jasho lako linalokupa uwaziri necessarily, sio umaridadi wako kikazi. Hata mimi nisiyejua kitu ningekuwa najuana na Kikwete toka kwenye mizunguko yake ya usiku vilabuni toka wakati Kikwete yuko Naibu Waziri labda na mimi leo hii ningeukwaa uwaziri.
Wapemba hujuana kwa vilemba. Masha ameshaingia kwenye 'hall of fame' ya viongozi wabovu Tanzania na tayari ananuka ufisadi na hata akisafishwa kwa 'perfumes of Arabia" hawezi kutakata.
Masha hana cha kuonewa wivu. At least mimi sikioni.
Ni wa kuzomewa kama walevi wa madaraka wenzake na tutazidi kumbana mpaka kieleweke na simwonei wivu - labda huruma.
 
1.
Waliokaa, wakasoma na wakatafakari aliyosema Sikonge bila shaka wamejifunza mengi tu. Wengi tunaopiga kelele kupinga ufisadi tunaambiwa tunasukumwa na wivu. Ghafla neno wivu imekuwa silaha wanayotumia wezi na walevi wa madaraka kujihami wakiungwa mkono na wapiga debe wao

- Kwanza ilikuwa udereva sasa imekua wivu, yes ni wivu ukweli unapopindishwa kwa makusudi, hakuna wapiga debe ila tupo wananchi wa Tanzania wenye uchgunu na taifa letu, ila cha muhimu ni kwamba tunafikiri kwa kutumia vichwa vyetu sio lazima tulazimishwe na wengine kufikiri kama wao, kama thta ni kupiga debe so be it. Wivu ni wivu na uklwei ni ukweli tusichangaye ishus sio wote hapa ni watoto wadogo wa kufuata bila kufikiri on our own!

2.
Hakika inachekesha eti umwonee wivu mtu ambaye humjui wala hakujui -kisa ? Naamini mtu anayevurunda kama anavyofanya Masha ni wa kuhurumiwa na kamwe si kuonewa wivu. Mbio za watu wa aina hiyo ni fupi na zinakuwa tishio tu kwa wanaoishi kwa kutegemea fadhila zao.Quote:

- Hapa kwenye forum hakuna anyeishi kwa kutegemea anything kutoka kwa vbiongozi wa bongo, ila tupo wananchi wenye mawazo huru sio lazima wote tufuate upepo na kuamuliwa na mtu mmoja hapa JF, huo haujawahi kuwa utamaduni wetu hapa, never huwa tunafikiri independent na hatusithwi na anybody na maneno mengi ya taarabu, ukweli utawekwa wazi kama waziri ana makosa ataondoka kwenye kazi ya wananchi na Mengi akiwa na makosa pia atachukuliwa hatua za kisheria lakini hatuwezi kulazimishwa kufikiri kama mtu flani au kikundi flani, hatukuenda shule for that yaani kufikiriwa na wengine! We think for our own! na we speak up bila kuogopa!

3.
Ushikaji saa nyingine ukitangulizwa sana unadumaza upeo wa mtu kufikiri na kupambanua mambo. Mtu zima unakuta unatetea hata kile kisichohitaji utetezi - self evident. Halafu wanaojaribu kukuweka sawa unasema wana wivu - how low can one get. Come easy, go easy. Degree mbili zinazomtuma mtu kuongea upupu kama anavyofanya Masha, katu hazitufai. Hivi sasa Tanzania tunaanza tabia ya ku'tolorate' tabia za ajabu kama za kuwaenzi wezi na wahujumu wa taifa. No, this has to stop.

- Ushikaji hauna tatizo kama kulazimishwa kufikiriwa na wengine kwa nguvu, tutaendelea ku-think for ourself wale wanaofikiria wingi wao hapa unaweza kubadili mawazo ya wananchi wengine wamepotea njia, maana sifa za JF ni kufikiri independently, uwezo wetu na uhuru wetu wa kufikiri unafahamika hata na serikali, maana ilipotaka kutuvuruga hapa JF swali la kwanza lililoulizwa lilikuwa ni "...Nani ni Mwanakijiji" na nani ni "FMES" huwa hatusemi lakini ukweli upo na usahidi upo wazi, kwamba hata serikali inajua kuhusu kuwepo wketu hapa na indpendent thinking huwa sio tabia yetu kuambiwa na wengine ambao hawana idea hata wanachokisema, mradi tu tukubalike nao, sio uhuru huo hata mkiwa wengi kiasi gani tutaendelea kusimama tulipo na vita vyetu na mafisadi vipo pale pale, maneno matupu hayavunji mfupa!

4.
BWM mwenyewe aliwahi kuwa Marekani tena kwa wadhifa mzito tu - balozi. Aliporudi na kuchaguliwa kuwa Raisi alianza kufanya mambo ya ajabu ajabu. Tulipopiga kelele tukaambiwa tuna wivu wa kike na wana habari walipoanza kudadisi wakaambiwa ni wavivu wa kufikiri. Masikini BWM siku hizi anatafuta pa kuficha uso wake, lakini angalau aliuonja Uraisi. Sasa huyu Lau aonewe wivu kwa kitu gani - eti anaota Ikulu - thubutu !

- Tuko hapa kusimamia ukweli sio majungu, BM habari zake ziko wazi kwamba ni mwizi na ushaidi wote upo wazi, sasa na wengine ushahidi uwekwe wazi lakini sio majungu na taarabu, again JF we are not kondoo tunafuata tu hapana tunataka ukweli, sifa yetu siku zote ni ukweli sio kulazimishana na taarabu maneno ya wengine! Kama lau ni mwizi ushaidi uwekwe wazi hakuna atakayemtetea, lakini sio majungu! BM ni mwizi period!

5.
Kwa ya ku'dodge' JKT hana sifa ya kuwa waziri kwa sababu alionyesha wazi hana uzalendo. Halafu hii inaonekana wazi kabisa kwa kuthubutu kusuka mpango wa kumhujumu mzalendo - kwenye vikao vya siri. Huyu si wa kuonewa wivu, ni wa kuzomewa. Wapemba hujuana kwa vilemba. Masha ameshaingia kwenye 'hall of fame' ya viongozi wabovu Tanzania na tayari ananuka ufisadi na hata akisafishwa kwa 'perfumes of Arabia" hawezi kutakata. Ni wa kuzomewa kama walevi wa madaraka wenzake na tutazidi kumbana mpaka kieleweke na simwonei wivu - labda huruma.

- tunachotaka ni ukweli, sio majungu na wivu, kamwe hatuwezi kualzimishwa kufikiriwa na wengine, tuna akili ya kutosha ya kufikiri on our own, kama kwa kukataa kufikiriwa na wengine tunakuwa waarabu wa pemba so be it, na wale manofikiriwa na wengine poleni sana, JF tuna utamaduni wa kufiki for our own hata siku moja hatutaruhusu kuamul;iwa na wengine what to say na waht to think, sasa tuogope mafisadi wa taifa halafu pia tuanze kuogopa na mafisadi wengine humu JF waliotuvamia majuzi ambao wantaka kutumia hoja za nguvu na ubabe kutulazmisha tufikiri kama wao that is pathetic, huu ni uwanja huru wa mawazo huru na tutasimaia hiyo tabia mpaka mwisho, wale msiotaka kuwa huru msituchanganye tunajua where we are na hivi vita tumeanza navyo siku nyingi leo hatuwezi kufundishwa na maneno ya taarabu, kama hamuwezi kupigana vita vya taifa kama mnavyonyesha basi tuacheni sisi tuendelee, lakini humu ndani mnaleta vita ambavyo hamuwezi kushinda maana hatuwezi kuwapa hata one inch kama hamuamini subirini muone, mnawasumbua sana wananchi hapa na hizi taarabu,

Tupeni nafasi turudi kwenye taifa, hatuogopi mtu hapa, tutaendelea kusema tuinachoamini hata kama sio popular hiyo imekua tabia yetu siku zote, hatujawahi kubadilkika inagwa tumetishwa sana hapa, uwingi wenu haututishi hata kidogo, it is about time sasa mkaelewa kua Tazanania ni yetu sote sio yenu tu kwa sababu sisi hatuwezi kufikiriwa na nyinyi, Jf huwa tunaheshimu sana uhuru wa mawazo na hatujawahi kulazimishana kufikiri na wengine.

Kwa wananchi wengine tunajua kua haya sasa yanachosha, lakini mtuvumilie hatuna choice ila kusimama imara tusije tukalazimishwa kuwa watumwa wa mawazo ya wengine, kwa visingizio vya ushikaj na taarabu zisizoisha, Tanzania tuko huru wale wanaofikiri wanaweza kutulazimisha kuwa na mawazo kama wao, wamepotea njia hapa JF!

Mungu Aibariki Tanzania!
 
tunasema hivi kiongozi yoyote ashambuliwe kwa shutuma zilizo na ukweli, kuna wakati alishambuliwa Mwenyekiti wa Chadema kwa maneno ya uongo wa kupindishwa kwa makusudi kuhusu shule yake UK, kwamba anafanyiwa mitihani na Balile, tulisema kuwa ule ni wivu wa binafsi,

- Kuna wakati ameshambuliwa Zitto hapa kwa makusudi kwa kupindishwa ukweli, tulisema kuwa ni wivu wa binafsi, na kuna wakati zililetwa article za kumchafua Dr. Slaa na Mbowe tena kwa makusudi mazima, tuliomba ziondolewe hapa JF haraka sana, kwa sababu zilikuwa ni uzushi na uongo uliochongwa kwa makusudi na at best ni wivu tu wa binafsi,

- Tuliyasema haya against wananchi wengi hapa waliokuwa hawakubaliani na mawazo yetu hapa na haikuwa tatizo, sasa tunasema tena kwamba waziri wa ndani ashambuliwe kwa makosa aliyokwisha yafanya na yanakubalika kua ni ya kweli lakini kupindisha ukweli kwa makusudi ili kumchafua ndio tunaita kama vile kule nyuma kua ni wivu wa binafsi, na it has nothing to na wasiokubaliana na mawazo yetu on the ishu.

- Tunajaribu sana kupata ukweli wa ishu maana kuna habari nyingi sana, ingawa Halisi leo ametoa maneno mazito sana kuhusu the ishu ninayakubali as ukweli wa ishu, lakini ninatofautiana naye on one thing only, namna ya kuimaliza ishu, maana tungependa sheria ifuate mkondo na kama waziri amekosea basi ajiuzulu kama alivyoahidi na sheria iangaliwe kama imevunjwa na matendo yake katika ku-deal nayo, na kama Mengi amekosea sheria ichukue mkondo pia,

- Mind you tunazo dataz za kutosha kuhusu ushahidi alionao Mengi, yaani tepu yenye maneno ya waziri mmoja kama anavyodai hilo leo ninalithibitisha kua halina ubishi na jina la waziri tunalo tayari, na tepu nyingi nyingine mojawapo ikiwa ya Makamba, naye akijaribu kushauri uvunjwaji wa sheria, sasa tunazo dataz za kutosha kuhusu tepu zote alizonazo na zilivyopatikana.

- Habari iko wazi kwamba kama Mengi asinge-act kwanza huyu waziri angemmaliza, sasa ndio maana tunasema ishu iende kwenye sheria, ili sheria ichukue mkondo na sio siri tena waziri anayehusika is in big shit. Tumeonywa sana kutosema majina ya wahusika wa hii ishu, lakini ninasema hivi tumewafahamisha wahusika kuwa kama ukweli haukuwekwa hadharani when the times come, tutayaweka yote nje kama yalivyo!

Thanxs!

je ni masha umteteaye?? kama tape umeisikia..........
 
je ni masha umteteaye?? kama tape umeisikia..........

Bado ni ROMOURS, kama amreact si apeleke hizo TAPE mahakamani? sisi masuala ya waziri mmpoja kijana yanatusuhu nini? mawaziri vijana ni wengi. watu tuna mambo mengi ya kufuatilia SIO MNATUWEKA KWENYE PUZZLE.
KAma mmamua kukaa na SIRI basi IWE SIRI YENU.
 
Mimi naona hii saga ni fundisho kwetu na inaonyesha wa kufanya mabadiliko katika utendaji wetu wa kazi. Napendekeza yafuatayo:

1) Tuondoe neno ".....nyeti za serikali" katika msamiati wetu. Mikutano na vikao vyote vya serikali (katika ngazi zote) viwe na "minutes". Minute hizo zihifadhiwe na iwe ni haki ya raia yeyote kuweza kuzipitia. Maombi haya yanaweza kukataliwa pale tu itakapoonekana kuwa masuala yaliyodaliwa yanahusu usalama wa taifa. Hii itabidi ielezwe bayana na tafsiri ya "usalama wa taifa" uwekwe wazi. Kumbukumbu hizo ziwe zinapitiwa kila baada ya miaka kumi kuangalia kama kweli bado zinastahili kufichwa kutokana na sual a la usalama wa taifa.

2) Uteuzi wa mawaziri na viongozi wote wa juu wa serikali upate baraka za bunge. Naamini kwa wakina Kuhani hiki kinaitwa confirmation hearing. Mtu aliyeteuliwa kwanza ahojiwe na kamati ya bunge inayohusiana na uteuzi huo ambapo utendaji wake mpaka wakati huo ( kama ni mfanya biashara, potential conflict of interest, mafanikio yake n.k), qualifications zake ( shule na shahada alizokuwa nazo. Hii hasa ni kuangalia uhalali wake na si vinginevyo), masuala yake ya binafsi ambayo yanahusu utendaji wake ( mlevi, ufuska n.k.) vitajadiliwa na akionekana anafaa ndiyo apelekwe kwenye bunge kamili.

3) Bunge liwe na mamlaka ya kumuita na kumhoji waziri au mtendaji mkuu yeyote kuhusu utendaji wake wakati wowote itakapobidi.

4) Mawaziri wasiwe wabunge waliochaguliwa aidha jimboni au sehemu fulani ya jamii ( wakina mama na walemavu). Hii itapunguza uwezekano wa waziri kupendelea constituency yake katika utendaji wake. Waziri akumbuke kuwa anawajibika kwa nchi nzima na si jimbo lake tu au chama chake.

4) Kwa kufanya hivi, mawaziri wetu watakuwa ndiyo watendaji wakuu wa wizara wanazoongoza. hii itaondoa mkanganyano uliopo sasa juu ya mipaka ya waziri na Katibu Mkuu.

Mfumo tulionao ambao ni nchi nyingi tu unautumia unahitaji upinzani na public media iliyopevuka ili i-provide checks and balances kwa utawala. Kwa bahati mbaya nchi yetu bado hatujafika hapo. Pengine huu wa wamarekani unaweza kutufaa zaidi. Pengine itawakumbusha pia viongozi wetu kuwa wao wanatakiwa kuwatumikia wananchi wa nchi yetu na si vice versa.

Amandla.......
 
Last edited:
Mimi naona hii saga ni fundisho kwetu na inaonyesha wa kufanya mabadiliko katika utendaji wetu wa kazi. Napendekeza yafuatayo:

1) Tuondoe neno nyeti za serikali katika msamiati wetu. Mikutano na vikao vyote vya serikali (katika ngazi zote) viwe na "minutes". Minute hizo zihifadhiwe na iwe ni haki ya raia yeyote kuweza kuzipitia. Maombi haya yanaweza kukataliwa pale tu itakapoonekana kuwa masuala yaliyodaliwa yanahusu usalama wa taifa. Hii itabidi ielezwe bayana na tafsiri ya "usalama wa taifa" uwekwe wazi. Kumbukumbu hizo ziwe zinapitiwa kila baada ya miaka kumi kuangalia kama kweli bado zinastahili kufichwa kutokana na sual a la usalama wa taifa.

2) Uteuzi wa mawaziri na viongozi wote wa juu wa serikali upate baraka za bunge. Naamini kwa wakina Kuhani hiki kinaitwa confirmation hearing. Mtu aliyeteuliwa kwanza ahojiwe na kamati ya bunge inayohusiana na uteuzi huo ambapo utendaji wake mpaka wakati huo ( kama ni mfanya biashara, potential conflict of interest, mafanikio yake n.k), qualifications zake ( shule na shahada alizokuwa nazo. Hii hasa ni kuangalia uhalali wake na si vinginevyo), masuala yake ya binafsi ambayo yanahusu utendaji wake ( mlevi, ufuska n.k.) vitajadiliwa na akionekana anafaa ndiyo apelekwe kwenye bunge kamili.

3) Bunge liwe na mamlaka ya kumuita na kumhoji waziri au mtenda mkuu yeyote kuhusu utendaji wake wakati wowote itakapobidi.

4) Mawaziri wasiwe wabunge waliochaguliwa aidha jimboni au sehemu fulani ya jamii ( wakina mama na walemavu). Hii itapunguza uwezekano wa waziri kupendelea constituency yake katika utendaji wake. Waziri akumbuke kuwa anawajibika kwa nchi nzima na si jimbo lake tu au chama chake.

4) Kwa kufanya hivi, mawaziri wetu watakuwa ndiyo watendaji wakuu wa wizara wanazoongoza. hii itaondoa mkanganyano uliopo sasa juu ya mipaka ya waziri na Katibu Mkuu.

Mfumo tulionao ambao ni nchi nyingi tu unautumia unahitaji upinzani na public media iliyopevuka ili i-provide checks and balances kwa utawala. Kwa bahati mbaya nchi yetu bado hatujafika hapo. Pengine huu wa wamarekani unaweza kutufaa zaidi.

Amandla.......

Hapo mkuu umenena! Hiki ni kitu nakipigia debe siku zote kwani itasaidia Tanzania kuwa na checks and balances. Uwaziri utokane na qualifications za uongozi ambazo itabidi tujiwekee na kujiamulia kama Taifa. Pia Rais adhibitiwe katika uundaji wa wizara...Bunge liamue tuwe na wizara ngapi na kila Rais ateue baraza kwa mfumo huo.

Mkuu umesema cha maana sana na ningependa kuona thread mpya ianze itakayozungumzia utawala bora na tuchangie zaidi. Naona hii thread imepoteza mwelekeo wa suala zima la Masha na Mengi.
 
ES unatumia nguvu kweli kumtetea Lau...lakini angalia mwishoni usije ukaficha kichwa chako kwenye mchanga kama mbuni.
Hutaki kabisa kukubaliana na ukweli licha ya wazee wa data kukumwagia lakini hutaki kabisa unapiga bla bla bora uingie mitini uache twendelee kumgalagaza boss wako mpaka JK ampige chini.Kesha chafuka yule hasafishiki hata kwa maneno ya aina gani hawezi kutakata labda amwombe Makamba amsaidie kumsafisha.
 
Nipo ukurasa mmoja na Mkuu FMES,Atakayeangukia Pua ni Mzee Mwanakijiji.Makala yake ya jana Tanzania Daima(iko mtandaanoni sasa) kaeleza mambo mengi sana ambayo hayana uhusiano wowote na hoja ya masha.Ni sawa sawa ugombane na mke wako na uanze kukumbusha makosa yote aliyowahi kufanya huko nyuma.

Je tukianza kutumia makosa ya watu waliyofanya nyuma watu wnenye historia mbaya kama Mwenyekiti wa Chama kimoja cha siasa watabaki?I have already said mie siko kwa Mzee wa IPP hata siku mmoja
na inaniekera sana tabia yake ya kuanza kulia lia anapoona mambo yanamwenea vibaya
 
mmh.. chuki yako hiyo ya mengi imekuwa kama pazia usoni pako. Well, siongozwi na chuki (wengi wamejaribu kunibambikiza chuki zao wenyewe). Ukisoma makala yangu ya jana utaona kuwa sikugusa kitu hata kimoja ambacho hakihusiani na utumishi wake (Masha) wa umma! NONE! do you want to know why? rudi kwenye misimamo yangu yanapokuja mambo ya binafsi.

Ningetaka kumuandika vibaya kwa mambo ya binafsi, indiscretions za ujana n.k ningeweza, lakini nikifanya hivyo nitavunja kanuni yangu mwenyewe. Mambo ya binafsi ambayo hayahusiani na public service or public money.. is a no no kwangu.

Huwezi kujua hilo, kwa sababu wewe umeshaapa kuwa "mie siko kwa Mzee wa IPP hata siku mmoja"

Why is that? kwa sababu unamchukia na chuki ni ganzi mbaya sana!
 
Nipo ukurasa mmoja na Mkuu FMES,Atakayeangukia Pua ni Mzee Mwanakijiji.Makala yake ya jana Tanzania Daima(iko mtandaanoni sasa) kaeleza mambo mengi sana ambayo hayana uhusiano wowote na hoja ya masha.Ni sawa sawa ugombane na mke wako na uanze kukumbusha makosa yote aliyowahi kufanya huko nyuma.

Je tukianza kutumia makosa ya watu waliyofanya nyuma watu wnenye historia mbaya kama Mwenyekiti wa Chama kimoja cha siasa watabaki?I have already said mie siko kwa Mzee wa IPP hata siku mmoja
na inaniekera sana tabia yake ya kuanza kulia lia anapoona mambo yanamwenea vibaya

Duh umeshindwa hata kuficha hisia zako ahaaaaaaaaaaaa.Ila umefanya vizuri umekuwa si Mnafiki Umeonyesha rangi yako halisi kwa hiyo watu hatuta pata tabu kusikia yatokanavyo na utakayokuwa unasema.

Sisi news tulizokuwa tunazingojea ndio hizo za ushahidi na tunaomba tusambaziwe.No matter analialia mara ngapi hapa hoja ni halali anachololia kwa sasa ,ni kweli na kama kweli ni sahihi kwa watuhumiwa walichofanya.Ndio vikao vya serikali vya siri maana yake.?

Wewe unaungana na mtu ambaye anau hubiri udugu na ushwahiba na Masha,aliyejikanyaga kuanzia mwazo wa thread mpaka sasa. Ila kutokana na mabandiko yako mengine naona kama kambi yako ndani ya SISIMU imeshikwa pabaya ugali unataka kumwagika,kwa hiyo ungana na mwezako Press secretary wa Masha,swahiba,dereva ktk vita hii ya kumsafisha,kwa kweli akiona Masha mjumbe wake hapa alivyomtetea kama hana akili nzuri atakuwa na imaninae sana .
 
Kuna kitu nimejifunza hapa jamvini nilikuwa sikijui, na hiyo post yako Sikonge ni exhibit A ya swala hilo.

Kumbe maishani ukiwa na issues na mtu mwenye mafanikio, cheo, elimu, hela, na kadhakika, ukimkosoa tu, utaonekana una wivu. Hilo kwa kweli nilikuwa silijui kabisa.

Kwa mfano, wengine tumeambiwa tuna wivu dhidi ya mafanikio ya Masha. Wakina Fundi Mchundo na wengine wengi humu wameambiwa hayo hayo. The thing is, though, hujui huyo Fundi Mchundo ana mafanikio au failures gani za kumfanya amuonee wivu Masha. Hivi unapomsoma mtu kama Mchundo hapa unaona kweli ni failure maishani ? Kwamba ni jinga moja halikwenda shule lilikimbia umande kweli, kama anavyosema ? Unaona anaandika kama mtu ambae hana elimu kweli? Please!! Anaweza kuwa anaendesha baikeli kama anavyosema lakini ni kwa sababu anataka tu. Mtu mwenye kichwa ka Fundi akitaka kigari hawezi kushindwa. Na inawezekana analo au anayo mengi tu, ila tunazugwa tu hapa, ni mtu mwenye humility na modesty ya kutotaja mashangingi yake hapa. Humility comes before honor, wanasema, na ndio ninachokiona kwa huyu na wengi wa hapa. Huyu hawezi kutishwa na "mafanikio" ya Masha!!! Na ndio maana sio lazima asema anamjua Masha, sijui kamwendesha kwenda mitihanini na Airport kama Field Masha anavyomfanyia Lau Masha, and all that obsequious gibberish! (Fundi nisamehe nimechukua liberty kukutumia kama mfano maana na wewe, kama mimi na baadhi ya wengine, umeambiwa una wivu.)

Halafu sio kila mtu anataka kuwa Waziri kama Masha. Waziri katika serikali ya mafisadi is not a very cushy job, I don't think.

Kingine, Masha sio wakili mwenye mafanikio peke yake, au kiongozi mwenye degree mbili. Cha ajabu cha kuonewa Masha wivu ni nini hasa? Kusoma na kuishi Marekani ? Kusoma kasoma sana, lakini jamani ni nini alichosomea Masha kuonea wivu, Masters ya Georgetown ? Hata Sumaye ana Masters ya Harvard, nini Georgetown. Au kuishi huko US ? Marekani hata khalagabaho kaa mimi naishi. And, believe you me, it ain't no seventh heaven, it's a nightmare, as Malcom X used to say. We huoni Masha mwenyewe aliingia mitini kurudi UDSM ? Wanasema alipokuwa UDSM alikuwa anaitwa Mmarekani, well, kama kukaa Marekani kunapandisha chati mbona alinyuti ? Ngoma yake ilikuwa ngumu nini ? Sioni cha kumuonea wivu Masha mimi.

Na hatuwezi kumuonea wivu Masha eti kwa sababu tuna uchungu yeye hakwenda JKT . No, yeye ali dodge National Service!! National Service ile ni badge of honor! Huyo Masha mwenyewe naamini anajuta saa hizi ndani ya moyo wake kwa kutoonyesha uzalendo. Hana cha kuonewa wivu hapo Masha kwa ku dogde JKT.

Na hata huo uwaziri, kusema tunamwonea wivu waziri kijana, uwaziri sio achievement ya kujivunia saaaana kwa sababu ni cheo cha kupewa tu. Sio bootstrap achievement, sio jasho lako linalokupa uwaziri necessarily, sio umaridadi wako kikazi. Hata mimi nisiyejua kitu ningekuwa najuana na Kikwete toka kwenye mizunguko yake ya usiku vilabuni toka wakati Kikwete yuko Naibu Waziri labda na mimi leo hii ningeukwaa uwaziri.

Masha hana cha kuonewa wivu. At least mimi sikioni.

Hey Prophet, you said it all.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom