Mengi Vs Masha tuhuma, vitisho na matokeo!

Mengi Vs Masha tuhuma, vitisho na matokeo!

Status
Not open for further replies.
ES unatumia nguvu kweli kumtetea Lau...lakini angalia mwishoni usije ukaficha kichwa chako kwenye mchanga kama mbuni.
Hutaki kabisa kukubaliana na ukweli licha ya wazee wa data kukumwagia lakini hutaki kabisa unapiga bla bla bora uingie mitini uache twendelee kumgalagaza boss wako mpaka JK ampige chini.Kesha chafuka yule hasafishiki hata kwa maneno ya aina gani hawezi kutakata labda amwombe Makamba amsaidie kumsafisha.
Asante Fidel80
 
1.
ES unatumia nguvu kweli kumtetea Lau...lakini angalia mwishoni usije ukaficha kichwa chako kwenye mchanga kama mbuni.

- Haya yameshakukuta wewe maana toka jana tayari umeangukia puani, toka jana unajaribu kila njia kuharibu jina langu kwa niaba ya ndugu yako lakini wapi unapoteza muda wako bure.

2.
Hutaki kabisa kukubaliana na ukweli licha ya wazee wa data kukumwagia lakini hutaki kabisa unapiga bla bla bora uingie mitini uache twendelee kumgalagaza boss wako mpaka JK ampige chini.Kesha chafuka yule hasafishiki hata kwa maneno ya aina gani hawezi kutakata labda amwombe Makamba amsaidie kumsafisha.

- Sina bosi kama wewe unayempigania hapa na rangi zako mbali mbali, wewe umenikuta hapa nikipigana sikuanza leo, msimamo wangu ni imara hauwezi yumbishwa na wewe wala wenzako, siku zote ninasimama kwenye uwkeli sio uongo na ujinga ujinga, niliwoanya hii forum, siko hapa kumsafisha Masha niko hapa kusimamia sheria, msimamo wangu uko wazi kama Masha ana maksoa aondoke kama alivyoahidi mwenyewe,

- Ya huko ndani huyajui ila ninaweza kukupa idea ya kinachoendelea, lakini only ukiniuliza kwa adabu, JK hujui how he operates ninaweza kukusaidia on hilo, makelel mangapi amepigiwa Makamba mbona yupo? Acha hizi cheap shots, hakuna anyemsafisha anybody hapa, tunataka sheria itumike wka faida ya taifa la kesho na sio anything else,

Pole sana na kazi ya kumpigania ndugu yako toka jana, lakini ni yeye ndioye aliyenichokoza, dataz ninazo tena nyingi sana maana toka juzi hapa nipo na viongozi wengi wakuu wapiganaji wa taifa na nitakua nao for the next week and a half, kwa hiyo mkuu huwezi niharibu hata uafnye nini unahangaika sana najua nimekubana mbavu kwenye hall of fame lakini ndio maana demokrasia huwa hatukiriwi na wengine huwa tunafikiri on our own.

thanks bro!
 
Originally Posted by Mutu
Duh umeshindwa hata kuficha hisia zako ahaaaaaaaaaaaa.Ila umefanya vizuri umekuwa si Mnafiki Umeonyesha rangi yako halisi kwa hiyo watu hatuta pata tabu kusikia yatokanavyo na utakayokuwa unasema.

Sisi news tulizokuwa tunazingojea ndio hizo za ushahidi na tunaomba tusambaziwe.No matter analialia mara ngapi hapa hoja ni halali anachololia kwa sasa ,ni kweli na kama kweli ni sahihi kwa watuhumiwa walichofanya.Ndio vikao vya serikali vya siri maana yake.?

Wewe unaungana na mtu ambaye anau hubiri udugu na ushwahiba na Masha,aliyejikanyaga kuanzia mwazo wa thread mpaka sasa. Ila kutokana na mabandiko yako mengine naona kama kambi yako ndani ya SISIMU imeshikwa pabaya ugali unataka kumwagika,kwa hiyo ungana na mwezako Press secretary wa Masha,swahiba,dereva ktk vita hii ya kumsafisha,kwa kweli akiona Masha mjumbe wake hapa alivyomtetea kama hana akili nzuri atakuwa na imaninae sana .

- Irrelevant najua una uchungu sana na ndugu yako na jana, lakin huwezi fanya anything, na tarehe 27 nitakua intown ninakuja kwenye ile shughuli kama mna ubavu nisubirini pale tukutane maana sasa tunawachosha watu hapa JF, kama mna ubavu tukutane pale nitakuwepo.

FMES!
 
mmh.. chuki yako hiyo ya mengi imekuwa kama pazia usoni pako. Well, siongozwi na chuki (wengi wamejaribu kunibambikiza chuki zao wenyewe). Ukisoma makala yangu ya jana utaona kuwa sikugusa kitu hata kimoja ambacho hakihusiani na utumishi wake (Masha) wa umma! NONE! do you want to know why? rudi kwenye misimamo yangu yanapokuja mambo ya binafsi.

Ningetaka kumuandika vibaya kwa mambo ya binafsi, indiscretions za ujana n.k ningeweza, lakini nikifanya hivyo nitavunja kanuni yangu mwenyewe. Mambo ya binafsi ambayo hayahusiani na public service or public money.. is a no no kwangu.

Huwezi kujua hilo, kwa sababu wewe umeshaapa kuwa "mie siko kwa Mzee wa IPP hata siku mmoja"

Why is that? kwa sababu unamchukia na chuki ni ganzi mbaya sana!

Mwanakijiji ngoja nianze kukujibu hoja zako kama ulivyozianisha jana mnaaake nimeshakueleza ila hautaki kulelewa Mkuu Mwenzagu

Hata hivyo lazima nikiri na kuelemea upande wa kuhoji kama Masha ana uwezo wa kuongoza wizara nyeti kama ya Mambo ya Ndani. Kuna mambo ambayo ameyafanya siku hizi za karibuni, ukichangia na hili la Mengi sina budi kuhoji hekima ya yeye kuendelea na wadhifa huo ambao ushahidi wote uliopo unaonyesha kuwa umemzidi kimo mara nyingi sana

.
1.Mauaji ya Albino

Mkuu Mwanakijiji ulimaanisha atoe siku saba kwa akina nani? Waganga wa jadi au mapolisi? Mapolisi ambao hawana hata ushahidi ni waganga wangapi wanahusika na mauaji haya (in contrast na suala la mengi ambaye ana ushahidi kuwa kuna waziri flani alisema so anaweza kutoa ushahidi). Suala la siku saba hapa umeliingiza la nini?

Mkuu Mwanakijiji, suala la Maalbino kama alivyosema Mhe. Masha siyo watanzania wote wanohusika na suala la mauaji haya (rejea kipindi kile suala la Mapanki wewe ulisimama wapi?).


2.Vifo vya watoto 19 Tabora
Suala la vifo lilishaundiwa kamati na mawazo yalishatolewa na kinachoendelea ni suala la DPP kuangalia ushahidi aliopelekewa kama unatosheleza kufungua mashtaka juu ya waliohusika.

Hapa tena umemuingiza Masha kwa suala lisiloshabihiana na suala la Vifo vya Tabora. (Mengi ana ushahidi wa kutosha kuhusiana na anachokisema). Hapa Masha asingekurupuka kusema natoa siku saba watu flani waweke ndani sababu wanahusika bila kuanya uchunguzi (Kumbuka Masha aliomba Mengi awasilishe ushahidi within 7 days kw yale anayoyasema).

3.Madai ya Rostam Aziz
Hapa Tena.Madai ya Rostam yalikuwa ni ya kwake Binafsi na wafanyabiashara tusiowaju kama vile wewe na yule mnavyoweza kudai mnatishwa na hili linaweza kushughulikiwa na Mkuu wa kituo tu. Ila Mengi alikuwa akimtuhumu kiongozi wa serikali mwenye Dhamana na serikali na pia ukumbuke kuwa alisema walizungumza hayo katika kikao cha siri cha serikali. Hivyo serikali inahusika kwa kumtishia Mengi (unaweza kujiuliza kwanini walikuwa wakimjadili Mengi?). Haiwezekani mtu akazungumza siri za vikao vya juu vya serikali na asichunguzwe!.

Rostam hakuituhumu serikali ila Mengi alituhumu serikali, hivyo Masha Was Right?!


Hoja ni nyingi sana ulizojenga ,lengo ni kuchochea masha ang'oke tu ili iwe furaha yako kwamba umeweza kufanya flani atolewe.Binafsi siipendi tabia binafsi ya Masha ila utendaji wake ni thabiti na ninaweza kukuthibitishia hilo.

Mie nachoona ni kosa ni suala la Mengi kuzungumza mambo ya vikao vya seri vya serikali.

Pili.Nani alkimwambi Mzee huyu wa IPP kuhusia na viako vya siri vya serikali na ningependa mzeehuyu awajibike kwa kutoa siri za serikali.(sheria Ipo).

Jana Mzee Mwanakijiji ulichemka, na sababu ya wewe kuandika ni kukurupuka na inaonesha ulishirikishwa jambo usilolijua vyema. Kumbuka wewe ndiyo ulikuwa wa kwanza hapa kusema Waziri aliyehusika ni Masha kabla haujaedit mwenyewe
 
Mkuu ES umesema tusubili sheria zifuatwe mkondo wake.Ok ngoja twendelee kusubili lakini tukichambua hoja moja baada ya ingine...Lakini nashangaa umekuwa tofauti kabisa kwa Lau tofauti na wakulu wengine unavyo wachambua huyu naona unasisitiza tu maswala ya sheria au kwa vile yeye amesoma sheria ndio ataweza kuzipangua?
Lakini kuna deal nyingi chafu huyu mkulu kazicheza na wewe unazijua lakini hutaka hata kucoment hata kidogo licha kusema tusubili sheria.Naona hii picha kwako imekuwa chungu sana kuhusu Lau kila mmoja anaelewa wewe na Gembe mmebeba dhamana ya kumlinda Lau na kumtetea kwa misingi ya sheria.
 
Angalia ES baadae usije ukarusha ngumi maana tunako elekea na uwazi ukiwekwa bayana sielewi kama utaendelea kusema tusubili hukumu au???Najua kitakacho fuata hapo tusubili hukumu.
 
Ikawa usiku ikawa mchana, siku ya saba imefika, what next?!
 
Kuhani,

Post yako ya hapo nyuma imenifanya nifunguye kamusi nijikumbushe tena maana ya neno 'kuhani'! Umetoa elimu, wenye kuchota wamechota, wenye kukasirika acha wakasirike.

Yes, kuna tatizo kubwa katika nchi yetu na pengine katika bara letu. Tunafikiri kuwa mwanasiasa kama vile waziri ndiyo climax ya mafanikio, na mtu yeyote ambaye hayupo kwenye siasa anaonekana hajafanikiwa. Mwanzoni nilifikiri hii ni thinking ya watu wa vijijini pekee, maana kila nilipokuwa narudi nyumbani nilikuwa naulizwa wewe lini utakuwa waziri au angalau mbunge maana umesoma sana! Nikiwaambia mbona mimi ni mwalimu, tena wa chuo kikuu kwa nini mnataka niwe waziri au mbunge-maana kuna watu wengi wanaweza kuwa wabunge na mawaziri lakini ni wachache sana wanaoweza kuwa walimu wa chuo kikuu- hawanielewi mpaka leo!!!

Sasa, kupitia michango yetu hapa JF, nimegundua hii thinking ipo wide spread. Sasa wote tunaojaribu kumshangaa, binafsi simkosoi, namshangaa tu, Masha tunaonekana tuna wivu. Kama ulivyouliza, hao wanaosema tuna wivu ni kama vile wanajua watu wote humu JF wanavyoishi na kazi wanazozifanya.

Sasa tuendelee kuelimishana. Wengi tulikuwa na matumaini makubwa sana na Masha, na mimi binafsi nilishangilia sana Masha kuwa waziri na kuacha makada wazoefu kama vile rafiki yangu Nchimbi. Yote hii ni kwa sababu ilikuwa ni mara ya kwanza kwa kijana kuteuliwa kushika madaraka makubwa, sio kwa sababu ya ukada kama tulivyozoea, bali kwa sababu ya elimu yake nzuri, exposure yake kubwa, uelewa wake mzuri wa mambo local na international, na mafanikio yake ya kiutendaji katika sekta zingine nje ya siasa.

Lakini sasa matendo na utendaji wa Masha tangu awe mbunge, na hasa tangu awe waziri umetukatisha tamaa wengi. Kwanza, ni mzembe kwa kauli. Anaropokaropoka ovyo, tena wakati mwingine hata kwenye bar! Pili, na muhimu zaidi, utendaji wake kama waziri ni dhaifu. Tangu akamate hiyo wizara ujambazi umeibuka upya tena. Huyu ni waziri ambaye tulitegemea utendaji wake uwe kama au uzidi kidogo ule wa Augustine Lyatonga Mrema. Lakini badala yake utendaji wake umekuwa chini hata kuliko wa Omar Ramadhani Mapuri. Sasa hili la kujaribu kushiriki, kwa kujua au kutokujua, kumuangusha mfanyabiashara mzalendo, ambaye mafanikio yake yamepatikana bila wizi wa hela za EPA, ndiyo limetia mafuta ya taa kwenye moto, na kwa kweli yatamtokea puani, angalau kisiasa. Kwa kweli matendo na utendaji wa Masha umetoa faraja kubwa sana kwa watu wanaotegemea ukada pekee kufanya siasa. Akina Makamba watakuwa wanafurahia sana maana huwezi tena kujenga hoja ya usomi na ujana kama vigezo vya mtu kuteuliwa kushika wadhifa mkubwa serikalini na katika siasa kwa ujumla.

So guys, hatuna wivu, we are just concerned with the blunders and failures of our colleague whom we had so much expectations. He has just let us so much down, and wanting us to keep quite will be doing huge injustice not only to him but also to all people who are trying to bring change in the way we run our politics. So instead of telling us to shut up, you should indeed shut up. The most you can do is to print the pages in this thread and give them to your beloved Lau before it is too late!
 
Kuhani,

So guys, hatuna wivu, we are just concerned with the blunders and failures of our colleague whom we had so much expectations. He has just let us so much down, and wanting us to keep quite will be doing huge injustice not only to him but also to all people who are trying to bring change in the way we run our politics. So instead of telling us to shut up, you should indeed shut up. The most you can do is to print the pages in this thread and give them to your beloved Lau before it is too late!

Umegonga kwenyewe!
 
- Mkuu Fidel ni jana tu ndio nimepata all the information kuhusu the ishu, lakini with one condition kwamba nisitoe wakati zinafanyika juhudi za kulitatua tatizo, lakini na mimi condition yangu ni kwamba kama habari hazikusema wazi nitatoa zote nilizonazo,

- Masha sasa yuko Geneva, na Mengi yuko Arusha na muungwana I know that, sasa tunawasubiri kujua what is next, yes ninasikitishwa san all I know sasa kuhusu this ishu, lakini bado ninaheshimu the conditions under which nimepewa hizi dataz, kwa hiyo in the meantime sina tatizo kushambulwia na anything ndio maana ya demokrasia, lakini when the time is right then nitasema wazi, lakini kwa sasa ninaheshimu makubaliano niliyoyaweka, urafiki wangu na Lau sio bigger than my nation hapana, taifa kwangu siku zote linakuja mbele kwanza!

- Na wka kuheshimu hilo ndio maana nilikuwa njiani kuondoka lakini wapiganaji wa kweli wa taifa laetu wakaniambia nirudi hadi baada ya uchaguzi, nikakubali ama sivyo nilikuwa nimeamua kupeleka vita vyange mbele zaidi.

Lakini ashante wka concern.
 
Ahsante Kitila, post yako hii naona inashabihiana na sehemu ya sahihi ".....deciding collectively", ni kwamba ume-eleza vyema kwa nini baadhi yetu tunapiga kelele juu ya Lau na sio alichosema peke yake!
Kimsingi nakubaliana na FEMS, japo namuomba asiwe na jazba wakati anajibu hoja zake, akumbuke jamvi hili ni la wote , wa Tz wema, mafisadi, makuwadi nk. Asije akajikuta anatumia muda mwingi kujibu mambo amabyo watu wanamchokoza makusudi halafu wana mcheka. FMES , MM Kazi zenu tunazikubali, sio wote watakaozikubali-la msing fuateni misingi yenu mnayoamini mardi mna data za kutosha, mungu ibariki Tz, JF
 
Mkuu kitila,

Heshima mbele mkuu, wewe ninakuheshimu sana siwezi kukuweka kwenye makundi flani, ninaamini kuwa maneno yako unayaelekeza kwangu, si kweli kwamba nimesema watu wa shut up, hapana nimesema watu waseme ukweli na tusilazimishane kuamini ya wengine kwa nguvu, tupewe nafasi ya kufikiri for our own!

Otherwise, ninakubalaiana na maneno yako mengi kwamba viongozi vijana wametuangusha na hili nililisema toka siku nyingi sana, lakini dawa ni sisi kuingia huko wenyewe, ninakuaminia sana siku moja kushika usukani wa Chadema, na sisi tukiwa CCM, ninaamini tutaleta mabadiliko ya kweli kwa faida ya taifa,

Respect maaan siku you have my outmost respect!
 
Nashukuru mkuu ES kwa ufafanuzi wako mzuri hapo sasa tunakuelewa lakini ulivyo kuwa unaongea huko nyuma watu tulikuwa tunajiuliza kulikoni mpiganaji anaamua kushiriakiana na mtu jamii ina mhisi kuwa ni adui?Ok hapo endelea kuwepo msimamo wako wazi namna hii tunakuelewa kiunaga ubaga.Nakushukuru.
 
Mkuu Edo,

Msimamo wangu siku zote hapa ni kuhabarishana, sasa hivi nimemaliza kuongea na mkulu mmoja anyeifuatilia sana hii JF, amenipa faraja sana kwamba "...endeleeni kuhabarisha umma vijana hamjui jinsi mnavyoamsha wananchi wengine...",

Mkuu mimi ni mwanasiasa, ninategema kuingia kwenye ulingo in the future, can you imagine bila mimi kuwepo kwenye huu mjadala ungekuwaje? Ungefika huku uliko? Kwamba nina jazba hapana ninajibu tu kama ninavyorushiwa na mimi pia ni binadam kama wewe, ukweli ni ukweli tu hata ubadilishwe namna gani, mimi siku zote ninaamini in ukweli tu na sio anything else otherwise nimekusikia sana na infact kwa sababu ninajijua kuwa sina ufisadi wala sipati anyhting kutoka kwenye ufisadi wa yoyote yule, nido maana sina wasi wasi hata kidogo na maneno mengi ya kuatafutab umaarufu hapa JF, nimewahi kupewa nafasi kwenye taifa lakini nikazikataa wka sababu nilitaka wkanza kutafuta mali zangu maana siwezi kwua kiongozi masikini nitatamani, sasa hivi ninatafuta mali ili nikiingia kusiwe na harufu yoyote ya ufisad na niweze kuwashufghulikia wote waovu bila huruma, kama huamini subiri siku itakapokuja.

Mkuu fidel,

ukienda nyuma ya hii topic utaona nimeanza kushambuliwa hata kabla sijaingia kusema anything, kwenye siasa lazima uwe na nidhamu ya ku-stick to your point hata kama ni unpopular, as long as unaamini kua ni ukweli ila tatizo ni kama uansema uongo au kwa niia ya kuwahadaa wananchi wengine,

Msimamo wangu siku zote uko imara na wazi, kabla ya kutaka kuivuruyga hii forum serikali wkanza ilimuarifu mzazi wangu kwamba inajua nipo hapa aniambie nitoke haraka, nikamwambia over my dead body, sasa kwa yoyote anyetaka kunishambulia wka msiammo wangu ni sawa ndio demokrasia na ninaikubali, lakini msimamo wangu ni strong na solid na sina wasi wasi na hilo,

Niajua kua kwenye hii topic tumepitia mengi lakini sasa tunakaribia kufika mwisho wa hii ishu ukweli utajitokeza na utasemwa maana tunao na wanaohusika watawajibishwa ingawa kuna juhudi kubwa za kutaka kulimaliza hili suala pembeni, lakini ninaamini kuwa litamalizwa kwenye sheria kama tunavyoomba sana, ili kuweka muongoz kwa taifa la kesho.

Samahani sana kwa kukuwaza na msimamo wangu kwenye hii topic lakini tuvumiliane, wazazi wangu waliponipeleika shule kwa mara ya kwanza ilikuwa ni shule ya Kifungiro, kule Tanga enzi hizo ikiwa ni shule pekee ya kizungu kwa watoto chekechea na boarding, kabla ya kunikabidhi kwa mkuu wa shule waliniambia maneno mawili,

(1). tunakuacha hapa ili ujifunze kufikiri for yourself, na (2). ujifunze kuisema yes au no at the right time.

mpaka leo yamo kichwani wmangu na ndio hasa muongozo wangu, lakini nimekusikia. (Samahani kwa makosa ya herufi zangu maana nimo safarini)

Respect!
 
Nimekupata mkuu ES naona wote wanao fuatilia dot hizi saizi watakuwa wanajua nini unamaanisha hapa kuhusu hii ishu na mtu akidandia kwa mbele itakuwa vigumu kukuelewa inabidi arudi mwanzo aone ni nini kilikuwa kinaendelea.
Ok safari njema mkuu Wende bwinoo!.
 
FMES: Post yangu ni ya jumla, hailengi specific post maana sijaweza kuzisoma posts zote, na unajua mimi siwezi kukurushia mawe, maana mimi nipo kwenye nyumba ya kioo...ukirudisha itakuwa balaa.

respect mkuu, tuendelee kukata mbuga, tutafika tu...

Ila mwambie Lau aache hizo. Apambane na hao majambazi ambao sasa wameanza kutesa kama vile hatuna serikali, hiyo ndiyo itakayompa legacy na respect.
 
Business as usual at JF, kuchambuana kama mchicha badala ya hali halisi na mada! Poleni mnaopigwa makonzi na kutuhumiwa kuwa vibaraka au washiriki wa pande zote iwe ya Masha au Mengi! phew!
 
na unajua mimi siwezi kukurushia mawe, maana mimi nipo kwenye nyumba ya kioo...ukirudisha itakuwa balaa.
quote]


Ndio yale yale, hata mtu akiwa nje ya mstari anashindwa kuambiwa kisa ataonekana anarusha mawe. Kama mwanasiasa na academician, that one is your ...... Hii kauli nitakukumbusha siku moja, nitakwambia hufai kuwa kiongozi kwa sababu hauna clearly depicted principles. Viongozi wababaishaji ambao wako vuguvugu hawafai. Amua kuwa moto ama baridi. Hizi ni zama za mabadiliko vijana.

Endelea kudumisha amani na utulivu huku mafisadi wakikata mawingu.
 
Baada ya kuwatukana kiungwana na kisiasa, ngoja nitoe hii nukuu kama hamjaiongelea au kuiona, tujiulize kulikoni Tanzania?

Je Mengi kuwa mshika bango kuhusu uwajibikaji anaundiwa mkakati na Serikali wa kunyanyaswa na kudhulumiwa? Je tuna Serikali ya namna gani?

Wanasiasa kadhaa wa CCM na wale wa upinzani waliozungumza na gazeti hili wanasema, lengo moja la mzozo huu wa sasa ni hatua ya baadhi ya viongozi serikalini kujaribu kumdhibiti Mengi ambaye katika miaka ya hivi karibuni vyombo vyake vya habari vimeonekana kuwa mstari wa mbele katika kuhujumu kile wanachokielezea kuwa masilahi yao na ya taifa.
‘‘Wakubwa kadhaa serikalini kwa kauli moja wamefikia hatua ya kuanza kumuona Mengi kuwa ni tatizo. Huyu jamaa haeleweki ana malengo gani kisiasa, kwani amekuwa nyuma ya kila jambo kubwa hapa nchini. Ameshiriki kutukifisha mahali pagumu sana, hata kusababisha serikali ishindwe kufanya kazi yake sawasawa, kwa kweli ni lazima ashughulikiwe ipasavyo,” alisema mbunge mmoja wa CCM anayeunga mkono hatua ya Masha kumpa Mengi siku saba.
Ofisa mmoja wa juu serikalini aliyezungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa jina gazetini alisema, pendekezo la kutaka serikali ichukue hatua ya kumbana Mengi lilitolewa kwanza katika kikao kimoja cha juu cha kiserikali kinachoshughulikia masuala ya usalama nchini kabla ya jambo hilo hilo kujadiliwa tena katika Baraza la Kazi linalojumuisha mawaziri kadhaa. ‘‘Kilichoishtua serikali ni kumsikia Mengi akizungumza kuhusu mambo yaliyojadiliwa katika kikao kimoja nyeti cha kitaifa kinachohusisha watu wazito. Sasa jamaa walichofanya wanataka kumlazimisha Mengi amtaje mtu aliyempa taarifa hizo ili hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi yake,” kilisema chanzo kimoja cha habari.

Hii pekee ni kithibitisho kuwa Serikali yetu bado inafanya mambo si kwa ajili ya Taifa, bali ni kwa ajili ya kikundi au genge fulani. Inapofikia hatua madai ya kusema "Ameshiriki kutukifisha mahali pagumu sana, hata kusababisha serikali ishindwe kufanya kazi yake sawasawa" kutolewa na Serikali na hata kuonekana kuwa ni sawa kutoka baadhi ya wanasiasa na watendaji wa Serikali, huku kunaashiria kukosa nindhamu ndani ya Serikali na kunanipa mashaka kama kweli kwa Serikali na Wanasiasa tulionao leo hii, Tanzania inaweza kupata maendeleo na haswa zaidi kuishi katika demokrasia.

Kauli kama hizi zinaonyesha kuwa Serikali yetu na viongozi wake au kadhaa ni sawa na kundi la kihalifu la Mafia!

Ningependa sana kupata ufafanusi kutoka kwa huyo mbunge aliyedai kuwa Mengi kaifikisha Serikali mahali pagumu. Ni kivipi Serikali imefikishwa pahali pagunmu? na nyongeza anapodai kuwa Mengi anasababisha Serikali ishindwe kufanya kazi yake sawasawa, ni kwa minajili gani?

Ikiwa Mkaguzi mkuu wa Mahesabu anaonyesha ufujaji wa hali ya juu ndani ya Serikali na matumizi mabaya ya fedha, je hilo ni kosa la Mengi?

Ikiwa ujambazi unaongezeka, uhujumu, uhalifu, magonjwa, njaa, rushwa, migomo na maudhi mengine yanayokera jamii yanaongezeka kila siku, je ni Mengi aliyetuletea haya?

Iweje Serikali leo imlaumu mtu au kundi la watu wanaoikosoa kuwa kulaumu Serikali au kuishupalia ifanye kazi zake kwa umakini ni kuwa kikwazo kwa Serikali kufany akazi zake sawasawa?

Tanzania tumeshereheka miaka 47 ya uhuru juzi, je ni Uhuru gani tuliokuwa tukishehekea ikiwa Uhuru wa maoni, mawazo na kukosoa unawekewa nta, gundi na kupigiliwa misumari?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom