MAONI: Pamoja na maswali yangu hapo juu, kwanza kabisa kuna udhaifu mkubwa katika uelewa, uchambuzi, utafiti na uandishi wa waandishi wetu wa Tanzania tena hata wale wa vyombo vikubwa vya habari na hivyo mara nyingi naona baadhi ya migogoro na matatizo yanasababishwa na upotofu wa taarifa zinazotolewa katika vyombo vyetu vya Bongo. Waandishi wetu wanakosea na mara nyingi kupotosha sana mambo.
Katika upotoshaji ambao mara nyingi unatokana na uvivu, nakumbuka wakati Mkurugenzi wa TAKUKURU, Edward Hosea, aliposema kuna vigogo watafikishwa mahakamani kwa ufisadi, waandishi wakaandika "Vigogo wa EPA kufikishwa mahakamani" wakati Hosea hakusema ni wa EPA na alijua kabisa si wa EPA na waandishi walikuwa wavivu hata kufikiri kwamba Hosea hajawahi kutoa tamko kuhusiana na watuhumiwa wa EPA na hata Press Conf ya kina Mwanyika na IGP, Dk. Hosea hakuwapo. Hosea alikuwa akimaanisha Mramba na Yona na baadhi ya waandishi wakataja kuna mawaziri wawili na wakaendelea kusema ni tuhuma za wizi wa fedha za EPA bila hata kufanya marejeo katika magazeti ya THISDAY, KULIKONI na hata RAIA MWEMA waliowahi kuandika kuhusu kina Mramba kabla hata ya kushitakiwa kwao.
Mifano ni mingi lakini suala la Mengi na Masha pamoja na udhaifu wa hoja zilizoibuka waandishi wetu wanachangia kuchochea mgogoro huo.
Nakubaliana kabisa na maoni yako mkuu.
Mimi nadhani tatozi si la hawa wanahabari tu. Hawa wanahabari wanatoka katika jamii yetu, na wengi katika jamii hizi zetu ndivyo tulivyo. Kuna tatizo kubwa sana la kutofautisha ukweli (mambo yaliyothibitika) na na mambo ambayo hayajathibika (imani, speculations, maoni). Unasikia kitu, unatafsiri jinsi unavyoelewa, halafu unaichukulia tafsiri yako kama ndio ukweli, halafu unai-present kama ndio ukweli, na saa nyingine watu wakikuuliza umelitoa wapi unakuwa mkali kweli.
Ni rahisi sana kwa muandishi kuepuka kupotosha kwa kufanya mawili:
1. Kumnukuhu mtu kama alivyosema, na kuepuka kuongezea interpretation yake.
2. Kabla ya kuingiza intepretation yake, kumuuliza msemaji kama ndicho alichomaanisha.
Pia, waandishi wetu wengi ni waoga wa kuuliza maswali. Na saa nyingine wakiuliza unaweza kupata shida sana kujizuia kucheka, lakini insikitisha.
Kwa mfano kitu mwandishi wa ile habari ya "Barrick kujitoa tanzania" angefanya ni kumuuliza yule jamaa "je, unamaanisha mnataka kujitoa Tanzania?". Sasa yeye akasikia jamaa analalama, yeye akatengeneza hisia kwamba huwa jamaa wanataka kuondoka (yaani nashindwa hata kupata picha hii hisia ilitoka wapi), halafu akaamu kuandika hiyo intepretation yake kama vile ndio ukweli.
Ukitaka kujua hili ni tatizo kubwa, ona kwamba hiyo article ilipita kwa watu kadhaa, including mhariri, na hakuna aliyestuka. Hakuna aliyejiuliza hivi kuna ukweli hapa? Hakuna aliyejaribu hata kudadisi zaidi, au hata kumuuliza muandishi "e bwana huyu jamaa amekwambia wanataka kuondoka hapa?".
Ndio maana huku kwetu majungu yanaenea kwa urahisi sana, maana wapo wenzetu wengi wakotayari kuyatetea kwa nguvu zote hata kama hawawezi kuthibitisha wanayoyatetea.
Kuna rafiki yangu mwandishi wa shirika flani la habari la kimataifa, ukimkuta anaifanyia kazi story utaona raha yaani jinsi anavyohangaika kuutafuta ukweli. Kwa sababu anajua akiipeleka article yenye majungu yasiyo na uthibitisho uliosimama lazima article itarudi tu. Kama ni kitu kimesemwa na mtu na yeye hakuwepo, basi ni lazima apate kumhoji yeye mwenyewe au msemaji wake kuthibitisha, la sivyo hiyo story ndiyo imekufa. Very thorough and detailed.
Na nimmooja wa waandishi wawili ninaowafahamu ambao hawapokei vijibahasha baada ya press-conferences kamwe. Kama ulikuwa hujui, ni siri iliyowazi kwamba kwenye press-conference nyingi (za serikali na makampuni binafsi), waandishi huwa wanapewa vijibahasha waende navyo. Wewe nenda kwenye press conference nyingi utakuta waandishi wanasainishwa. Halafu waulize hayo majina na hizo signature ni za nini uone unavyopigwa siasa.
*Jambo lingine muhimu ni kwamba kwa kuwa Masha amezungumzia "serikali itachukua hatua" kwa hiyo yeye ndiye msemaji wa serikali? kwa hiyo Wizara ya habari kupitia Maelezo wana kazi gani? Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu ina kazi gani?
Hoja yangu ya mwisho ni kwamba yaliyotokea kwa Masha sitaki kuamini aliyoniambia mtu mmoja kwamba Waziri huyo kijana, alishitukizwa maswali na waandishi wa TBC1 waliomhoji katika kipindi cha jambo na hakuwa amejiandaa kwani alikwenda kuzungumzia suala la Albino. Pamoja na kwenda kuzungumzia Albino, tayari alikwishapokea simu nyingi kuambiwa kwamba Mengi kamtaja, na yeye (Masha) bila kujipa muda (kama walivyo wakongwe wengi wa siasa) alitoa majibu ya haraka kwa TBC1 na sehemu kubw aya majibu yaliegemea zaidi kwa taarifa za simu alizopata na si kwa kusoma taarifa HALISI ya Mengi au hata angetumia muda kuwasiliana na Mengi. Masha alijiamini na akaonyesha kiburi na jeuri ya utawala kwamba polisi wote wa Tanzania wako chini yake na anaweza kuwaamuru, kwa kusema, "kamata Mike wa JF, kamata Mac wa JF, kamata Kubenea" na wakakamata kabla ya kujikuta wamechemsha. Amesahau cheo ni dhamana. Hivi kwa mfano angekuwa ni Kingunge, Kagasheki, Wasira, Nagu au hata Dk. Husein Mwinyi, wangetoa majibu sawa na Masha?
Uko sawa kabisa mkuu. Mimi nadhani wengi, tukieka ushabiki pembeni, wanakubali (hata kama ni kwa kimoyomoyo tu) kwamba mshakaji alichemka angalau kidogo.
Kuhusu kama alishtukizwa na maswali TBC1, mimi hiyo ndiyo imebaki kama kitu pekee cha kunaelezea kwa nini alipitiliza vile. Nahisi tu kwamba kama angepewa maswali kabla, pengine angepata mda wa kujituliza, na hata kupata ushauri wa jinsi ya kuwakilisha, na pengine asingerauka namna ile. Imenifanya nijiuliza kama huyu jamaa ni smart kama wengi wanvyomuelezea? au pengine tatizo alilonalo mbele yake ni kubwa kiasi cha kuweza kumpanikisha kiasi kile?
Sasa hivi nalalia upande wa la pili ... kwamba tatizo aliloliona ni kubwa kuliko tunavyoliona sisi. He was in panic mode kwa sababu he didn't see what was comming, na hakuwa amefikiria vizuri nini cha kufanya.