Mengi vs Manji: Ukweli ni upi?

Hii ni ajabu ya Mgema eti kuangusha kisu akiwa mnazini anagema kweli ataeleweka? Mengi kuachia ngoma kwenda mbele anajua anacho kifanya .Warioba asije akawa amekosea hesabau? Ama wanalete mchezo wa mtu na shemeji yake maana Warioba kaoa mchaga kama sijakosea.
 
Zanaki,

Kachanganyia na Uzaramu, sio mzaramo, cheki source zako na ka kulia Uchagani.

Hapa hakuna cha Dully Sykes wala nini. mahakama ndio itatoa haki. Mzee Warioba ni mpenda haki!

FD
 
Mke wa waroiba ni MCHAGA NA WALA SI MZARAMO.

WARIOBA AK\JINGA MOSHI NA ALIKUWA NAENDA LIKIZO MOSHI. HAKUWA NA NYUMBA IKIZU HADI ALIPOTEULIWA KUWA WAZIRI MKUU!!
AKAJENGEWA KWA HARAKA HARAKA! WAZEE WA IKIZU WALIMUONYA!

LAKINI UKISHA OA MCHAGGA JIANDAE! SAMAHANI KWA WACHAGA LAKINI NDIYO UKWELI WENYEWE.

MADHAMBI YOTE YA MKPA KUNUANUA NUYMBA sa, NYUMBA ZA SERKALI KUUZWA, KUGAWA VIWANJA VYA TANAPA VYA PWANI NI KWA AJILI YA MAMA ANNA!

MKE WA WARIONA ALIWAHI KUTAKA KUMCHAFULIA JINA MZEE KWA KUWA LIK\HUSKIA NA MCHEZO WA UPATU AMBAPO AKINA MAMA WASIONA NA MAJINA WALILIZWA!

ANYWAY MKE WA WARIOBA NI MCHAGGA KWA HIYO MENGI NI SHEMEJI YAKE.
 
Mkuyuga,

Nitasema tena polepole kwa mara ya mwisho. KAKULIA UCHAGANI. SIYO MCHAGA, siyo Mzaramo.. nawaachia mtafute kabila.

FD
 
Aljazeera said:
Ukweli wa mambo ni kwamba hamna cha Warioba wala Mengi.

Hii kesi itazimika kama mvua ya vuli. Wanaweza wasimpende Mengi na magazeti yake lakini ukweli utabakia pale pale siku zote.

Halafu kitu wanachosahau ni kwamba This Day na Kulikoni hayamilikiwi asilimia 100 na Mengi, ndiyo maana hayachapishwi na Guardian Printers kama Nipashe na mengineyo. Pia ndiyo maana hutaona habari za jinsi ya Kulikoni na This Day kwenye magazeti yake.

Kwa wale wenye kumbukumbu zuri mtakumbuka kuwa Africa Media, kampuni inayochapisha This Day na Kulikoni ilitangaza Bodi ya Wadhamini na Wakurugenzi mwezi wa tano, na mengi ni mmojawapo wa wadhamini.

Tukirudi kwenye Kesi ya Warioba au ile ya Manji, nadhani wahusika wanasahau kuwa This day na Kulikoni walitumia makaratasi waliyopata kutoka BRELA (Business Registration and Licensing Agency). Makaratasi hayo ni pamoja na MEMART (Memorandum of Understanding and Articles of Association). Kwenye MEMART kuna kila kitu kuanzia number of shares, capital, directors and ownership, na Mwanasheria aliyetumika kusajili Kampuni.
Wewe binafsi pia unaweza kwenda kwenye ofisi zao na kutoa TZS 1000 na utapata access ya kupitia Registrar Directory.

Hapa hamna cha kusema eti kisa Warioba na Mwanasheria, jaji mkongwe basi apate free ticket ya kutokuandikwa. Mimi nakuakishieni yeye mwenyewe kimya kimya ataondoa hiyo kesi au utasikia ikitajwa mwaka 2008.

Tatizo watu wengi wanafikiri Mengi naye anaingia kichwa kichwa au hana wanasheria wanaomshauri. This guy has been there and he know what he is doing and the consequences. Ana timu ya mawakili wazawa na wasio wazawa.

tusubiri tuone, siyo ajabu hata hamna kesi iliyofunguliwa bali ni maneno ya magazeti tu, kwani tunafahamu tabia ya magazeti yetu, yanashindwa kutofautisha nia na dhamira ya kushita au kufungua kesi na kitendo cha kufungua kesi yenyewe.

Mzee,nakuunga mkono asilimia 101.Kuna watu wanam-underestimate Mengi.Kuhusu utendaji kazi wa Kulikoni na ThisDay,mie wala sina wasiwasi nao.Rafiki yangu mmoja yuko pale Guardian Ltd anilinifahamisha kuhusu kuanzishwa kwa magazeti hayo mwaka mzima kabla hayajaanzishwa,and in fact waandishi wake waiajiriwa almost a year before,na walikuwa wanalipwa mshahara na marupurupu mengine kwa muda wote huo kabla magazeti hayo hayajaanza kutoka rasmi.Pia jamaa alinijulisha kuwa selection ya waandishi ilifanywa kwa umakini sana,na Mengi pamoja na uzoefu wake wa kumiliki vyombo vya habari aliwatumia sana jamaa flani Waingereza katika kuhakikisha kuwa pindi magazeti hayo yatapoanza kutoka yatakuwa really serious newspapers.Kwa kifupi,hakukurupuka kuyaanzisha.Wanaodhani magazeti hayo ni ya kupita,wasubiri tu wagundue kuwa wanajidanganya.

Kulikoni na Thisday sio wajinga wanapoingia kwenye utaratibu tuliouzowea huku nje ambapo pindi gazeti linapochapisha skandali na kutaja jina la mtuhumiwa linakuwa na uhakika wa linachokiandika,pamoja na kuangalia legal implications za habari husika.Kwa maana nyingine,wanapoibua skendo wanakuwa wanafahamu wazi kuwa mhusika atakanusha na possibility kubwa ni kukimbilia mahakamani kudai fidia.Nadhani tatizo la Watanzania wengi ni yale mazowea ya gazeti kusema "kigogo mmoja (jina linahifadhiwa) anatuhumiwa kushirikiana na mfanyabiashara flani (jina limehifadhiwa) kuiba mamimlioni ya shilingi..."Matokeo yake,wewe msomaji unapata mtihani wa kutafsiri habari hiyo kwa njia ya guesswork kwa vile majina ya wahusika yamehifadhiwa.Jamani,haya ndio maendeleo.Nakumbuka marehemu Jaji Nyalali.Jaji Mark Bomani na Profesa Mmari kwa nyakati tofauti waliwahi kuwataka waandishi wa habari kuachana na uoga wa kutaja majina ya watuhumiwa hasa pale wanapokuwa na uthibitisho unaoweza kukubalika hata mahakamani kuhusu habari wanazotoa.Pia waliwashauri waandishi wa habari kujiendeleza kwenye profession ya sheria (hata kwa level ya certificates tu) ili watambue haki zao kama waandishi na kupambana na uoga wa kutaja majina ya watuhumiwa kwa hofu ya kufunguliwa kesi za madai ya fidia.

Mnao-doubt kuhusu utendaji wa magazeti hayo ni wale ambao hamtaki kubadilika na mmezowea kusoma habari zenye kuficha majina ya wahusika.Hatuwezi kuwalaumu sana kwa vile mbuzi yake kamba,mmezowea kukwatua ardhi,kupalilia,kupika kwa shida na kula kwa kusimama,mkiletewa ready-to-serve food mnaona kama kuna walakini.
 
nawasikiliza wazee wa data kama kuna mtu anajua lolote kuhusiana na pesa zilizopotea. zile zililetwa kwa ajili ya ukimwi nadhani kama bilion 40. maana zile pesa zililetwa kwa maslahi ya Taifa na hadi sasa sijapata ripoti ya polisi juu ya jambo hili. mada hii nimeiona sehemu ila sina hakika kama kuna wakata issue kama kwenye forum hii!! nakusikiliza mzee Fikiraduni.
 
Hakika kwa kweli Nungwi hii habari ya haya mabilioni kilichonichangaza ni kutokuwepo na kauli yeyote toka kwa wenye mamlaka kuwa uchunguzi unaendelea au kama watafuatilia kuhusu ''wizi'' huu?!!

Kinachoshangaza kingine ni pia kutokuwepo na kauli yeyote kutoka ofisi za umoja wa mataifa kuhusu watu hao.

Kimsingi mambo yafuatayo yananishangaza:

Hivi inawezekana kweli kwa benki yenye uzoefu wa ku-operate miaka mingi namna ya NBC kuweza kuruhusu watu kufungua akaunti bila mtu husika kujulikana?nijuavyo miongoni mwa taratibu ni kupeleka picha nk sasa haya hayakufanyika?

Hata kama inaweza kuwa argued kuwa ilikuwa ni jumuiya hivyo wadhamini tu wangetosha?hivi ule utoaji fedha wa kiasi cha bilioni 39 haukuwashtua wenye benki hizi kiasi cha kuweza kufuatilia japo kuulizia kwa Mengi mwenyewe ambae taarifa ilisuggest kuwa anazo akaunti zingine benki hiyo hiyo?

Ina maanda shirika la USAID nalo pia ni la kibabaishaji au kuna mpango ulisukwa?

Taarifa zote za kukanushwa kwa mambo 'anayosingiziwa' bwana Mengi ni kubwa mno kiasi unashangaa hivi vyombo vya sheria vipo wapi?

Mbona Mengi malalamiko anayoyatoa yote yanaonekana kama ni ku-attract media coverage tu manake hatuoni suggestion ya kuwa ameripoti kituo cha polisi au kuomba msaada wa dola 'kukabiliana na uhalifu dhidi yake'

Ujambazi upo namna nyingi, katika nchi nyingi 'Fraud' licha ya kuwa ni kosa la madai 'civil offence' bali pia ni kosa la jinai na ndio tanzania anti fraud squad wapo chini ya jeshi la polisi,sasa nadhani mheshimiwa IGP Mwema nae angelivalia njuga hili, lakini kwa hali ilivyo nae akianza kulizungumzia hili la wajanja waliokula 41 bilioni itabidi Mengi 'aisaidie' polisi oops!


Sasa binafsi yangu nina tatizo kidogo na overall conduct ya Bwana Reginald Mengi, sasa hivi kuna kesi inaendelea katika kamati ya maadili ya bunge kujadili madai ya Mbunge Adam Malima kwamba televisheni ya ITV na vyombo vya habari ambavyo vinamilikiwa na reginald mengi vimekuwa vikionyesha sana habari kwa maslahi yake tu, hili nitalizungumzia kwa kirefu kesi ikishatolewa hukumu lakini kwa sasa nasikia mengi anaelekea kubaya katika kesi kwani mbunge adam malima ana concrete evidence.

Habari za ndani kabisa kutoka kwa walio karibu na huyu bwana ni kwamba amepatwa na depression mbaya sana tangu kifo cha mtoto wake Mutie na madaktari wamemshauri apumzike kwa sasa kwani amekuwa na haphazard memory lapses na imekuwa inaathiri sana decision making yake na hii ndio inapelekea kuwa na ugomvi na kila mtu kwa sasa, kuna kesi kibao mahakamani ninazozikumbuka kwa sasa ni:

1. Warioba na wenzake wawili wanadai milioni 900 kwa kukashifiwa.

2. Managing Editor wa DAILY NEWS Mkumbwa Ally anadai 1 billion

3. Yusuph Manji anadai bilioni 50 kwa kukashifiwa

4. Katika press release yao wakiclarify habari za IPPMEDIA NSSF nao wamesema wanaconsider hatua za kisheria.

Sasa hii inakupa picha kwamba sasa enzi za ubabaishaji wa Reginald Mengi zinaelekea ukingoni hususan kutokana na ukweli kuwa hivi sasa anadaiwa VAT na TRA zenye thamani ya bilioni 6 na hivi sasa mamlaka ya mapato bandarini inachunguza malalamiko ya chama cha walemavu kuwa Reginald Mengi mwaka jana kaingiza BENZ fully automatic [kila kitu kipo kwenye usukani] kwa ajili ya disable. Documents ZOTE zinaonyesha gari ni ya Chama cha walemavu. Hivyo basi kapewa excemption ushuru. Kwenye usajili kaandika jina lake!!!!! Kawazika walemavu!!!

niliyoyasikia ni mengi na yote mtayapata hapa, sasa hivi inabidi Mengi aungame manake kishawaibia sana watanzania na kuwafinika kiinimacho, sasa hivi ni ari mpya inabidi acleane his act na akapumzike kama alivyoshauriwa na madaktari...
 
Wazee wangu hatimaye niliongea na "Mzee", mmoja wa nchi kuhusu hii issue na akaniambia kwamba hii issue kwa kifupi ni kwamba,

Manji aliuziwa jengo na NSSF, kwa shillingi billioni moja na baada ya muda mfupi tu NSSF tena wakaja na kununua majengo yale yale kwa shillingi billioni NNE toka kwa yule yule Manji,

Gazeti la This Day likaipata hiyo issue toka kwa mbunge mmoja, lakini Manji akagundua kuwa hiyo issue tayari imefika bungeni, akam-tip director wa NSSF, ambaye naye akawahi bungeni Dodoma na kuongea na "VIGOGO" wa CCM ambao wakamtuma mbunge Malima kuianzisha issue hiyo in favor of Manji,

Na Manji naye akaanzisha kampeni ya kumharibia jina Mengi kuwa hapendi Waisilamu, na huku akimpeleka mahakamani. For some reasons, Mengi na Manji, wakaelewana na ku-settle issue nje ya mahakama, na baraka za hakimu. Lakini ghafla Manji akaendelea kumpaka Mengi kuwa hapendi Waisilamu, nasikia Mengi from no where akaanza kujihusisha na kwenda misikitini na issues zinazowahusu Waisilamu, na Manji naye akaendelea kumpaka mpaka issue ilipofikia leo,

The issue nimeambiwa kuwa ni NSSF kuuza jengo kwa billioni moja, halafu kulinunua tena kwa bei mara nne ya walioiuzia kwa mtu yule yule, issue ambayo hata wa-Tanzania tungekuwa vipofu vipi na hata tuwe viziwi vipi ni clear kuwa ni wizi wa kitoto, na cha ajabu ni kuwa kuna "Vigogo" wakiongozwa na Kingunge wakimsaidia Manji,

it is a shame beyond any human imagination, na bado siamini kuwa hii hadithi ni kweli na nimeamua kuifuatilia kwa undani,

na Mzee wangu Mwanakijiji tayari nimeaanza kupata data za yule Mzungu anaeitwa Nolan uliyeniuliza kule nyuma, nikizipata zote nitaziweka hapa hapa!
 
Mzee ES,

Nashauri umuulize tena huyo 'Mzee', maana either haijui hiyo issue vizuri au kadanganya kwa makusudi. Ilivyoripotiwa na This Day/Kulikoni katika 'episodes' zao, na pia ilivyoripotiwa na NSSF in their 'rebuttal' ni kuwa: Manji/Qality Plaza walikopa bilioni 9 kutoka NSSF ili kukarabati Ubungo Godowns (Manji hakuuziwa haya ma-Godown na NSSF). Baada ya ukararabati huu Manji akawauzia NSSF kwa Bilioni 47.5 Sasa ikiwa huyo 'Mzee' hajafahamu hata hizi fact ambazo kwa sasa ziko public domain, from both parties, napata shida kidogo kuchukua the rest of his story.

By the way, Nlidhani topic hii ni kuhusu Mabilioni yaliyopotea around Mengi's name, na sio NSSF/Manji/Mengi Saga, which has/had a thread of its own. Anyway, labda vinahusiana.
 
Kulikoni
nakubaliana nawe kwa asilimia zote aidha hapa Mzee Es anataka tuamini kitu kingine ama kadanganywa lakini pia Mzee Es umechanganya mada hii haina uhusiano na Manji bali tunaongelea mapesa ya UN kuyeyuka Banki ya TZ kwa jina la Mengi .
 
Hii ni taarifa ya NSSF kwa vyombo vya habari ambayo Mengi na magazeti waliamua kui-blow out of proportion:

SHIRIKA LA TAIFA LA HIFADHI YA JAMII

MAELEZO KUHUSU UNUNUZI WA QUALITY INDUSTRIAL PARK


UTANGULIZI

1 Hivi karibuni, kumekuwepo na habari zilizochapishwa na baadhi ya magazeti ya Kiswahili na Kiingereza kuhusu ununuzi wa Quality Industrial Park uliofanywa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii [NSSF].

2 Katika habari hizo, yapo mambo makubwa matatu ambayo yamesisitizwa. Mambo hayo ni:

a] thamani ya majengo hayo ni kubwa mno;

b] ununuzi wa Quality Industrial Park haukufuata taratibu za Shirika za uwekezaji; na

c] mradi huu hauna faida kwa NSSF na wanachama wake.

3 Kabla hatujatoa taarifa kuhusu madai ya hapo juu, ni vyema wanachama wetu pamoja na wananchi kwa ujumla wakafahamu utaratibu unaotumiwa na NSSF katika kuwekeza katika miradi mbalimbali.

UTARATIBU WA UWEKEZAJI

4 Kwa mujibu wa Kanuni za Fedha [Financial Regulations] na Sera ya Uwekezaji [Investment Policy] ya NSSF, maamuzi kuhusu uwekezaji huanzia kwenye Kamati ya Uwekezaji ya Menejimenti [Management Investment Committee]. Kamati hii hufanya uchambuzi wa miradi yote inayowekezwa na Shirika na iwapo itaridhika kuwa miradi hiyo ina faida kwa Shirika, Kamati huwasilisha mapendekezo yake kwenye Kamati ya Bodi ya Wadhamini inayoshughulikia masuala ya Fedha na Uwekezaji.

5 Kamati ya Bodi nayo hufanya uchambuzi na kujadili hoja zinazowasilishwa na Menejimenti. Kamati ya Bodi ikiridhika na hoja hizo, huwasilisha mapendekezo kwenye Bodi ya Wadhamini ya NSSF [NSSF Board of Trustees] kwa maamuzi ya mwisho.

UKWELI KUHUSU SUALA HILI

Thamani ya majengo

6 Mnamo tarehe 13 Februari 2004, NSSF ilipokea mapendekezo kutoka kwa kampuni ya Quality Group Ltd kununua majengo ya “Quality Industrial Park” yaliyopo kwenye Kitalu namba 16 eneo la Ubungo kwa bei ya Shs. 50 bilioni. Ununuzi wa majengo hayo yenye hati namba 196551 ni kwa ajili ya kuanzisha “Export Processing Zones”, yaani EPZ.

7 Kabla ya kukamilisha taratibu za ununuzi, majengo hayo yalifanyiwa tathmini na Chuo Kikuu Kishiriki cha Ardhi [UCLAS] na Mthamini Mkuu [Chief Government Valuer] wa Serikali. Kwa mujibu wa taarifa ya tathmini ya majengo hayo iliyotolewa na UCLAS, thamani ya masoko [market value] ya majengo hayo ilionyeshwa kuwa ni Shs. 48.9 bilioni. Kwa upande mwingine, taarifa ya Mthamini Mkuu wa Serikali ilionyesha
kuwa thamani ya majengo hayo ni Shs. 46 bilioni. Ni vyema ikazingatiwa kuwa UCLAS na Mthamini Mkuu wa Serikali ni taasisi/idara ambazo zina wataalamu wa hali ya juu na zina heshima kubwa katika nchi yetu na hata kimataifa.

8 Baada ya kupata thamani kutoka kwa UCLAS na Mthamini Mkuu wa Serikali, NSSF na kampuni ya Quality Group zilifanya majadiliano [negotiations] na hatimaye kukubaliana bei ya majengo hayo ni Shs. 47.5 bilioni.

Utaratibu

9 Baada ya kukubaliana bei, mnamo tarehe 20 Aprili 2004, Kamati ya Uwekezaji ya Menejimenti ilikutana kujadili pamoja na mambo mengine pendekezo la ununuzi wa “Quality Industrial Park” kwa ajili ya kuanzisha miradi ya EPZ. Kamati ilijadili mapendekezo hayo na hatimaye ilipendekeza kununua majengo haya kwa bei ya shs 47.5 bilioni na kushauri mapendekezo haya yapelekwe kwenye kikao cha Kamati ya Bodi ya Wadhamini inayoshughulika na masuala ya fedha na uwekezaji.

10 Mnamo tarehe 27 Aprili 2004, mapendekezo ya kununua “Quality Industrial Park” yalijadiliwa na Kamati ya Bodi ambayo baada ya kuridhika na hoja zilizotolewa, iliagiza kuwa mapendekezo yawasilishwe kwenye kikao cha Bodi ya Wadhamini kwa maamuzi ya miwsho.

11 Tarehe 29 Aprili 2004, Bodi ya Wadhamini ya NSSF ilijadili mapendekezo ya Kamati yake ya Fedha na Uwekezaji. Baada ya kutafakari mapendekezo ya Kamati, Bodi ya Wadhamini ya NSSF iliidhinisha ununuzi wa “Quality Industrial Park” kwa bei ya Shs. 47.5 bilioni.

12 Ni vyema ikaeleweka kuwa Bodi ya Wadhamini ya NSSF ni ya utatu. Bodi hii ina wajumbe watatu kutoka Vyama Huru vya Wafanyakazi, wajumbe watatu kutoka kwa Waajiri na wajumbe watatu kutoka Serikalini. Aidha Katibu Mkuu wa Wizara inayohusika na masuala ya wafanyakazi ni mjumbe katika Bodi ya Wadhamini ya NSSF.

13 Kwa mujibu wa taratibu za uwekezaji za NSSF, ni dhahiri kuwa ununuzi wa “Quality Industrial Park” umefuata taratibu ZOTE zilizopo. Aidha ni dhahiri kuwa wadau WOTE wa NSSF, yaani wafanyakazi, waajiri na serikali walihusishwa kikamilifu katika kufikia maamuzi haya.

Hali halisi ya uchumi wa mradi huu

14 Yapo madai kwamba mradi huu hauna faida kwa NSSF kwani fedha zilizowekezwa zitarejeshwa baada ya miaka 73 kwa sababu ni 25% tu ya majengo ndiyo imepangishwa na kuwa eti kodi ya pango ni Dola za Marekani 1.5 kwa mita moja ya mraba (USD 1.5 per square metre).

Ukweli ni kuwa upangishaji wa maghala na ofisi kwa sasa umefikia 63%. Matarajio ya NSSF ni kuwa ifikapo mwezi Juni 2006 upangishaji utafikia 80%.

15 Kwa upande wa kodi ya pango, kodi inayotozwa ni kati ya Dola za Marekani 3 hadi 3.5 kwa mita moja ya mraba [USD 3 to USD 3.5 per sq. mt] kwa upande wa maghala na Dola za Kimarekani 10 kwa mita moja ya mraba [USD 10 per sq. mt] kwa upande wa ofisi.

16 Kwa kuzingatia hali ya upangishaji na kiwango cha kodi ya pango, muda unaohitajika ili kurejesha fedha yaani “payback period”, unakadiriwa kuwa ni miaka 10 [kumi].

17 Tunapenda kuwahakikishia wanachama wetu na wananchi wote kwa ujumla kuwa uwekezaji katika miradi mbali mbali inayofanywa na NSSF ikiwa ni pamoja na ununuzi wa “Quality Industrial Park”, unafanywa kwa umakini sana na unazingatia taratibu zilizopo na maslahi ya wanachama. Aidha tunawaomba wanachama wetu walielewe hilo na tunawahakikishia kuwa fedha zao zipo salama na watapata mafao yao kama yalivyoainishwa katika sheria.


HITIMISHO

18 Kutokana na maelezo hapo juu, ni dhahiri kuwa taarifa zilizochapishwa kwenye magazeti sio za kweli na zilikuwa na nia ya kuchafua jina zuri la NSSF, Bodi ya Wadhamini, Menejimenti na Wafanyakazi wake.

19 Kwa hali hiyo, NSSF inatafakari kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wote waliohusika katika kutoa taarifa potofu.



MKURUGENZI MKUU

SHIRIKA LA TAIFA LA HIFADHI YA JAMII

DAR ES SALAAM
 
Wazee wangu kama nilivyosema kuwa mimibinafsi sielewi lolote kuhusu hii issue, jana mchana niliongea na kigogo mmoja wa nchi ndye aliyeniambia hiii hadithi ambayo being nje ya nchi siwezi so far kuithibitisha kuwa ukweli uko wapi,

ingawaje toka jana mpaka leo tayari nimeanza kupata habaro tofauti kuhusu hiyo issue na nimeahidi kuwa I will get to the bottom ya hii issue, sasa kama huyu kigogo alinidanganya sijui kama alisema ukweli sijui isipokuwa hiyo posting yangu ni exactly alivyoniambia sasa wa kualumiwa hapa ni mimi kwa kutoijua na kutoifuatilia kwa makini hii issue,

lakini I promise kuwa nitakaporudi bongo nitaipata kwa karibu na ukweli, sasa kwa wale mnaoifahamu je si kweli kwamba Malima anamsaidia Manji?, Tena pia niombe radhi kwamba hii posting haihusiani na kichwa cha habari!
 
tafiti then jadili,

tunashukuru kwa hiyo taarifa kutoka NSSF.

kwa mtizamo wangu wa harak haraka nasema iko "too vague", nitarudi baadaye kuijadili zaidi, hawa jamaa wanawafanya watanzania wanavyotaka wakidhani wote ni wajinga
 
Lililo muhimu katika mijadala ni kuwa makini na unachokisema au unachoandika sasa ikiwa mtu unasikia kisha unaweka tu basi ujue kuna walakini katika negotioation skills.

I know this MZEE ES, I have been there manake story ya Ubalozi wa Holland mambo yalikuwa ni hivi as nilichukua mambo katika face value yake na kuyaweka hapa lakini niliomba radhi na nakupongeza na wewe kuendeleza spirit hii kwa kuomba radhi wanajamii hapa.

Hawea vigogo mimi naona kama ni gea tu manake hamna ukweli katika mengi unayosema, unadai hujui kwa vile upo nje ya nchi wakati hii habari ipo online tangu mwezi wa tatu! Tena IPPMEDIA wamekuwa wakiifanya kama ni episode kila wiki kwenye THIS DAY wanaweka kastori ka uongo kuhusu NSSF na kupachika hii habari,

Tafiti then jadili, that is the way to go!!
 
Naomba wachangiaji tutafute data za hizo pesa toka UN zilivyopotea kwani si busara kumvalia njuga Kasusura kwa wizi wa dola milioni 2 huku mabilioni ya Taifa yakipotea bila jibu la maana.

naona mada imekwenda kwa manji.

Pia Mzee ES nimepunguza credibility yangu kwako mfano umesema kuwa umeongea na mzee wa nchi halafu huyo mzee wa nchi hajui hata idadi ya pesa ambazo zipo kwenye issue sensitive kama ya NSSF? Ina maana kukalia madaraka makubwa ya nchi huku hajui suala la Mengi/Manji na NSSF huyo si mzee wa nchi na wala hastahili kupewa au kuendelea kukalia nafasi hiyo.pia usitegemee data zake kabisa na hao ndio wagomvi wetu tumewapa nchi watuongoze kumbe mbumbu mzungu wa reli.

Suala hili ni kama drama kila siku lipo hata kama mtu uko nje ya nchi. mimi nimeanza kuliona toka toleo la pili la magazeti ya this Day/Kulikoni back to march this year. Na hakuna nakala inayoka kwenye magazeti haya bila issue hii tena yapo on-line www.ippmedia.com.

Pia Mengi na Manji hawaja-settle nje ya mahakama kama ulivyodai mzee Es kwani suala linasubiri tarehe ya kupangwa kusikilizwa na Manji amedai Billion mia moja.

Mbunge Adam malima yeye hakuhusishwa na Manji kilichotea alikuwa anachangia hoja ya waziri Mohamed Seif khatibu yaani wizara ya habari wakati wa bajeti nadhani ilikuwa mwishoni mwa july. ambapo akasema Mengi amekuwa akijipiga debe kuliko Rais kwenye vyombo vyake vya habari suala hilo ndio likapelekwa kamati ya maadili ya bunge ambapo for the past 3 weeks kikao kinaendelea Dodoma.

Sasa utaona This Day walianza nalo toka machi tena ni second issue. Hapo utaona Mkurugenzi wa NSSF na MALIMA hakuna uhusiano ktk issue hizi mbili.

Binafsi nimeamua kuwa mshiriki humu kwa kushawishiwa na wakata issue kama rafiki yangu Fikiraduni na mada yetu ya Mzumbe, wewe mzee ES nimeona unafagiliwa sana na Tafiti then Jadili. Ila tunapoingia humu tusiweke habari tusiokuwa na uhakika nayo kwani tutakuwa hatuna tofauti na magazeti ya Kasheshe, komesha na akina kaboka mchizi.

Ni bora mtu unyamaze lakini ukija humu uje na dozi kamili na kama unapata habari hizo source ziwe za uhakika. sio lazima mtu achangie tu humu kila siku hata kama habari zenyewe ni nyepesi nyepesi.

Nimelazimika kusema haya kwa heshima niliyompa ES na hata alipoanza kuandika akasema 'WAZEE WANGU HATIMAYE NILIONGEA NA MZEE MMOJA WA NCHI' ikimaanisha utafiti wako umezaa matunda.

Pia kama kuna mtu anadai anatetea maslahi ya nchi na akawa hata hajui kama kuna mabilioni karibu 40 yamepotea kwa jina la Mengi au haijui issue ya NSSF sidhani kama mtu huyo kweli anatetea maslahi ya nchi.
ndio maana nilipoanzisha topic hii nikasema hapa nategemea watu watanifungua macho bado namshukuru Tafiti ingawa naye ame divert mada ila faida tumepata kama kuona Press release ila amesahau naye kuna kesi ya DR. mahalu na Mengi(This day).

ADMINISTRATOR- kuna issue mbili tofauti (1) kesi ya Manji na mengi kuhusiana na This day na kulikoni. na (2) wizi wa mabilioni ya UN kwa ajili ya Watanzania wenye ukimwi pesa hizo zimepotea kiajabu na zilitiwa kupitia jina la Mengi hapa Manji hahusiki hata kidogo mimi nauliza issue hii, kwani mengi hakuletewa pesa kama yeye bali kaletewa kwa ajili ya Taifa hapa ndio naomba tusaidiane wenye data za uhakika.

Mwisho mzee Es inabidi ukiwa na mchango ufanyie utafiti maana tunakutegemea sana humu,kuna mawili matatu ulinitia mashaka nyuma. mfano kwenye mada ya Mkurugenzi wa usalama wa Taifa ulisema kuwa kuna nyumba ilinunuliwa mwaka 1960 kama nyumba ya ubalozi. ukipiga hesabu fupi tu. utagundua mwaka 1960 hata uhuru hatujapata.

Pia kuna mada ya Mbowe na CCM ukasema wewe unamjua sana Mbowe na watu wengine wawili uliwataja lakini ukaja kusema gazeti la Tanzania Daima linamilikiwa na Mtandao! wakati mtu haitaji kumjua Mbowe ili kujua kama ni mkurugenzi wa gazeti la Tanzania Daima.

Naomba sana msamaha kama nimuvuruga lakini lengo forum iwe inajadili vitu kwa kina, hatutaki kuja kuitwa Wazee wa NYEPESI NYEPESI mliopo nje ya nchi akina Firaduni ulizeni kwa jamaa zenu waliopo hapa kwa bimkubwa(bongo) nini maana ya nyepesi nyepesi
 

Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom