Mimi ningependa kuungana na wale wanaosema kuwa editors wa haya magazeti ndio accountable na sio owners,when it comes to what has been printed.Mfano,mwaka jana wakati wa vuguvugu la kutafuta mgombea wa CCM gazeti la Mwananchi lilitoa picha ya Salim Ahmed Salim amepose na Sultan wa Zanzibar in the 60's.Ile picha lengo lake lilikuwa ni kuonyesha Salim ni Hizbu,hivyo asingefaa kuwa rais wa Tanzania.Hayo magazeti yanamilikiwa na gazeti la Nation la Kenya,ambalo linamilikiwa na Aga Khan.Huko nyuma,Salim alishalishtaki Nation la Kenya,na alilipwa kitu kama dola laki nane hivi.Picha yake na Sultan ilikuja kugundulika kuwa ni computer generated,matokeo yake Nation walimfukuza yule editor wa Mwananchi,na kuomba msamaha kwa Salim.
Sasa labda nae Mengi badala ya kuingia gharama kutoa matangazo kwenye magazeti kuwa hana ugomvi na Manji na kuwa yeye ni mmiliki tu wa magazeti,lakini ni msomaji kama wengine, angejiweka sawa na kuchukua hatua kama hizo za Nation pale inapoonekana kuwa ukweli ulipotoshwa ili kuondoa hio dhana kuwa habari hizo zinaandikwa kwa kumnufaisha yeye binafsi na biashara zake.
Lakini kwa mwendo huo,kinachonishangaza mimi ni hichi,kama hii forum ingekuwa gazeti,na watu tungeweza kuandika tunavyoandika humu,tungewacha? Mbona watu humu wanalalamika kuhusu rushwa za viongozi,lakini pale inapoandikwa kwenye magazeti haohao ndio wanakuwa wa kwanza kusema kuwa huyo aliyeandika ana sababu zake binafsi,sisi humu sababu zetu ni nini? Uchungu wa taifa letu au envy kwa sababu hao viongozi wanajipatia njia rahisi za kutajirika,na kama hata sisi tungekuwa kwenye nafasi tungefanya hivyohivyo? Kama Warioba na Manji wanamshtaki Mengi kwa sababu walizozitoa,si wana-exercise rights zao kama hayo magazeti yalivyojaribu ku-exercise rights zake kwa kuandika habari ambazo mhariri aliona zinafaa kuchapishwa,mahakama itaamua ni nani mwenye makosa.