Mengi vs Manji: Ukweli ni upi?

tafiti then jadili

hiyo Press Release ya NSSF ilikuwa danganya toto ili kuzima issue.

Baada ya hii Press UCLAS walikuja juu sana na kukataa katu kuwa hawajawahi kufanya tathimini au kushiriki kwenye tenda ya kufanya tathimini. ALiyefanya hiyo kazi ni mtu binafsi ambaye ni mfanyakazi wa UCLAS na hakufanya tathimini hiyo kwa niaba ya UCLAS bali aliifanya kama kazi binafsi na haina uhusiano wo wote na UCLAS

Pili kuhusu tathimini ya Serikali kupitia Mtathimini Mkuu, Wizara husika ilikataa katu kufanya kazi hiyo. Kumbuka hata mpaka juzi Katibu kuu kwenye wizara husika alikuja juu kupinga hiyo kauli.

Hili swala ni lizito sana labda tulianzishie mada yake pekee.
 
Hii imewahi kujadiliwa hata huko lakini kwa kusua sua!

Leo nimesikia Manji amemwaga milioni 40 kwa wana Yanga! Anajifanya kuwa MJANJA SANA??!
 
Aljazeera said:
Hili swala ni lizito sana labda tulianzishie mada yake pekee.

Yeah,kuepuka kuchanganya mada kulikotokea... naona hii taarifa ya NSSF (+ associated comments) either ifunguliwe mjadala tofauti au ihamishiwe kule kwenye topic ya Nssf,quality Garage,mengi & Ippmedia iliyoanzishwa na Dr.Who
 
Aljazeera,

Uliyosema ni kweli kabisa na hata kulikuwa na mjadara mkubwa saana ndani ya wahadhiri wa UCLAS kuhusu swala hili, na ninaweza kuushusha kama itahitajika.

Kuhusu Manji kuifadhili Yanga, ukweli huyu jamaa ameona ili kujikinga na haya lazima ajibanze Yanga ambapo anajua hata JK ni mpenzi mkubwa mno ili apate wa kumtetea, na anajua fika Gulamali alivyoitumia Yanga kujipatia umaarufu, the same Dewji ameitumia Simba pamoja kuwa naye alifanya mambo ya ajabu saana katika kuua shirika moja enzi za ruksa.
 
tafiti then jadili said:
Hakika kwa kweli Nungwi hii habari ya haya mabilioni kilichonichangaza ni kutokuwepo na kauli yeyote toka kwa wenye mamlaka kuwa uchunguzi unaendelea au kama watafuatilia kuhusu ''wizi'' huu?!!

Kinachoshangaza kingine ni pia kutokuwepo na kauli yeyote kutoka ofisi za umoja wa mataifa kuhusu watu hao.

Kimsingi mambo yafuatayo yananishangaza:

Hivi inawezekana kweli kwa benki yenye uzoefu wa ku-operate miaka mingi namna ya NBC kuweza kuruhusu watu kufungua akaunti bila mtu husika kujulikana?nijuavyo miongoni mwa taratibu ni kupeleka picha nk sasa haya hayakufanyika?

Hata kama inaweza kuwa argued kuwa ilikuwa ni jumuiya hivyo wadhamini tu wangetosha?hivi ule utoaji fedha wa kiasi cha bilioni 39 haukuwashtua wenye benki hizi kiasi cha kuweza kufuatilia japo kuulizia kwa Mengi mwenyewe ambae taarifa ilisuggest kuwa anazo akaunti zingine benki hiyo hiyo?

Ina maanda shirika la USAID nalo pia ni la kibabaishaji au kuna mpango ulisukwa?

Taarifa zote za kukanushwa kwa mambo 'anayosingiziwa' bwana Mengi ni kubwa mno kiasi unashangaa hivi vyombo vya sheria vipo wapi?

Mbona Mengi malalamiko anayoyatoa yote yanaonekana kama ni ku-attract media coverage tu manake hatuoni suggestion ya kuwa ameripoti kituo cha polisi au kuomba msaada wa dola 'kukabiliana na uhalifu dhidi yake'

Ujambazi upo namna nyingi, katika nchi nyingi 'Fraud' licha ya kuwa ni kosa la madai 'civil offence' bali pia ni kosa la jinai na ndio tanzania anti fraud squad wapo chini ya jeshi la polisi,sasa nadhani mheshimiwa IGP Mwema nae angelivalia njuga hili, lakini kwa hali ilivyo nae akianza kulizungumzia hili la wajanja waliokula 41 bilioni itabidi Mengi 'aisaidie' polisi oops!


Sasa binafsi yangu nina tatizo kidogo na overall conduct ya Bwana Reginald Mengi, sasa hivi kuna kesi inaendelea katika kamati ya maadili ya bunge kujadili madai ya Mbunge Adam Malima kwamba televisheni ya ITV na vyombo vya habari ambavyo vinamilikiwa na reginald mengi vimekuwa vikionyesha sana habari kwa maslahi yake tu, hili nitalizungumzia kwa kirefu kesi ikishatolewa hukumu lakini kwa sasa nasikia mengi anaelekea kubaya katika kesi kwani mbunge adam malima ana concrete evidence.

Habari za ndani kabisa kutoka kwa walio karibu na huyu bwana ni kwamba amepatwa na depression mbaya sana tangu kifo cha mtoto wake Mutie na madaktari wamemshauri apumzike kwa sasa kwani amekuwa na haphazard memory lapses na imekuwa inaathiri sana decision making yake na hii ndio inapelekea kuwa na ugomvi na kila mtu kwa sasa, kuna kesi kibao mahakamani ninazozikumbuka kwa sasa ni:

1. Warioba na wenzake wawili wanadai milioni 900 kwa kukashifiwa.

2. Managing Editor wa DAILY NEWS Mkumbwa Ally anadai 1 billion

3. Yusuph Manji anadai bilioni 50 kwa kukashifiwa

4. Katika press release yao wakiclarify habari za IPPMEDIA NSSF nao wamesema wanaconsider hatua za kisheria.

Sasa hii inakupa picha kwamba sasa enzi za ubabaishaji wa Reginald Mengi zinaelekea ukingoni hususan kutokana na ukweli kuwa hivi sasa anadaiwa VAT na TRA zenye thamani ya bilioni 6 na hivi sasa mamlaka ya mapato bandarini inachunguza malalamiko ya chama cha walemavu kuwa Reginald Mengi mwaka jana kaingiza BENZ fully automatic [kila kitu kipo kwenye usukani] kwa ajili ya disable. Documents ZOTE zinaonyesha gari ni ya Chama cha walemavu. Hivyo basi kapewa excemption ushuru. Kwenye usajili kaandika jina lake!!!!! Kawazika walemavu!!!

niliyoyasikia ni mengi na yote mtayapata hapa, sasa hivi inabidi Mengi aungame manake kishawaibia sana watanzania na kuwafinika kiinimacho, sasa hivi ni ari mpya inabidi acleane his act na akapumzike kama alivyoshauriwa na madaktari...

Posting ifuatayo nimeikutauta Darhotwire forums.Ni kuhusu Mengi lakini aliyeiposti huko anaonekana dhahiri kuwa Mujahidina flani jast like huyu "Tafiti Then Jadili"

Re: REGINALD MENGI MSANII?
« Reply #2 on: Today at 4:26pm » Quote Quote Modify Modify


mtu ameuliza kwa nia inayoonekana njema kabisa kuwa yale mamilioni ya Mengi Community Services yaliyoripotiwa kuwa kuna watu wanatumia jina lake yapo wapi, na akaonya kuwa isijekuwa mzee Mengi kuna watu wanataka kumchafua jina lake wewe umevamia unadai eti ni kuelekea kwenye udini na ukabila hapa nadhani mkuu Kakoza unataka kutuzuga au nyote na Kilala ni shirika moja hivyo mnaona raha kuchezea akili zetu.

To be fair kuhusu Mengi nadhani anahitaji sasa kupumzika kama alivyoshauriwa na madaktari manake nimepata habari kwa kweli kila business yake inafall into pieces kutokana na poor management ya bwana Mengi manake habari toka katika kiini hasa cha familia ni kuwa kwa muda mrefu Mengi amekuwa akikabiliwa na madeni na uchunguzi toka kila mahala na imekuwa ikimchanganya sana na huko nyuma mbinu ilikuwa ni kama idara ya serikali wanamdai pesa basi atamchafua vibaya mkurugenzi wa idara hiyo ili aogopwe na truce ipatikane sasa uongozi huu vijana wameingia na ari mpya hapendwi mtu ni maadili na uongozi bora tu basi mzee anahaha sana.

To add salt to injury, kifo cha mtoto wake Mutie miaka takriban miwili baada ya mzee kuachana na mkewe na kuamua kuishi kimada na mwanamke wake yule anaekaa pale Haidary Plaza imempa mzee huyu depression kubwa sana manake nasikia amekuwa na haphazard memory lapses ambazo zinaffect decision making kiasi saa nyingine anakuwa kama amedata hivi na hivi nasikia madaktari wanataka lazima apumzike manake the next stage ya ugonjwa wake ni wazimu!

hizi nimezitoa katika kiini kabisa kama mna access na walio karibu na mengi chekini nao...

Naam na katika upande wa magazeti yake napo hali ni mbaya sana manake kutokana na years ya poor management ambapo sasa uongozi kampa mwanawe REGINA ambae ni reknowned lesbian in town basi amekuwa na roho mbaya sana kwa staff kiasi wengi wanaondoka mmoja mmoja kutafuta uluwa kivyao manake sasa hivi mzee anaingilia mpaka editorial policies kiasi kuna makundi matatu pale ippmedia:

1. Manji
Kila shabiki wa Yanga basi wanamuona yeye anamsupport Manji hadi kufikia kuwa hii ni sababu unaweza ukaondolewa!

Mfano mzuri ni kijana wa watu maskini anaitwa Maulidi Juma ambae kwa mapenzi yake tu kwa Yanga ambayo mfadhili ni Yusuph Manji basi ameonekana ni supporter wa Manji kiasi sasa wamemtoa!

2. Mengi
Hawa ni waandishi uchwara ambao wapo radhi kubend rules na maadili ya uandishi kumridhisha mzee na wapo wengi wamejazwa THIS DAY ambapo kwa kweli wanajua kabisa wakitoka pale hawawezi kufanya kazi mashirika mengine kwa vile shule yenyewe feki!!

3. Waoga
Hawa ni wale ambao hawajatake sides na huwa hawapewi kabisa promotion kwa vile mzee hajajua wanaelemea upande upi!

Yaani ni uoza mtupu ippmedia mtu ukiwa hapo huna hamu.

Halafu mzee sasa anakabiliwa na madeni kibao, TRA wanajiandaa kumfikisha mahakamani kwa lengo la kuseize goods zake kwa vile wanamdai kodi bilioni sita!

Naam wasifu ni huu kwa sasa tutafyatua kadiri vyanzo vyetu vinavyotupasha, habari kwa kirefu punde tu!

stay tuned, mengi aungame loh kumbe jibaba mwizi hana lolote kujidai kusaidia walemavu ilhali kaingiza gari BENZ fully automatic kila kitu kipo kwenye usukani akadeclare ni gari ya walemavu ili aisilipe ushuru then kwenye registration kaandika jina lake...inachefua!!
:confused:

JIHADIST AGENDA?
 
tafiti then jadili said:
Hii ni taarifa ya NSSF kwa vyombo vya habari ambayo Mengi na magazeti waliamua kuiblow out of proportion:

When it comes to allegations about corruptions they (the accused) can always rely on your staunch support and defence.
 
tafiti then jadili said:
Lililo muhimu katika mijadala ni kuwa makini na unachokisema au unachoandika sasa ikiwa mtu unasikia kisha unaweka tu basi ujue kuna walakini katika negotioation skills.

I know this MZEE ES, I have been there manake story ya Ubalozi wa Holland mambo yalikuwa ni hivi as nilichukua mambo katika face value yake na kuyaweka hapa lakini niliomba radhi na nakupongeza na wewe kuendeleza spirit hii kwa kuomba radhi wanajamii hapa.

Hawea vigogo mimi naona kama ni gea tu manake hamna ukweli katika mengi unayosema, unadai hujui kwa vile upo nje ya nchi wakati hii habari ipo online tangu mwezi wa tatu! Tena IPPMEDIA wamekuwa wakiifanya kama ni episode kila wiki kwenye THIS DAY wanaweka kastori ka uongo kuhusu NSSF na kupachika hii habari,

Tafiti then jadili, that is the way to go!!

HIVI WEWE UMEFANYA UTAFITI KWA KIASI GANI KABLA YA KUJA KUTOA UTETEZI WAKO KWA WATUHUMIWA WA UHUJUMU WA UCHUMI WETU?UNALALAMIKA KUHUSU "EPISODE YA THISDAY/KULIKONI vs MANJI" WAKATI KUNA "EPISODE" NYINGINE ZIMEKUWA ZINAENDELEA MIAKA KADHAA eg IPTL SCANDAL,NA SASA HIZI POROJO ZA UTATUZI WA TATIZO LA UMEME.YOU HAVE GOT SERIOUS ISSUES AND I JUST CANT UNDERSTAND WHY DO YOU ALWAYS SIDE WITH THE UNSCRUPULOUS CHARACTERS (THE CORRUPT,BANDITS,THOSE MILKING OUR ECONOMY,ETC)

THE WAY TO GO IS NOT TO TAFITI AND THEN JADILI (THAT'S ALREADY PROVED USELESS.AND YOU ARE A LIVING EXAMPLE) BUT TO THINK OF TANZANIANS AS PEOPLE WHO DESERVE EVEN BETTER SERVICES FROM THE RULERS.
 
Mlalahoi said:
Posting ifuatayo nimeikutauta Darhotwire forums.Ni kuhusu Mengi lakini aliyeiposti huko anaonekana dhahiri kuwa Mujahidina flani jast like huyu "Tafiti Then Jadili"

JIHADIST AGENDA?

Mlalahoi, kwa jinsi hizo points na lugha zilivyofanana, inawezekana kabisa zikawa zimeandikwa na the same person au wanaofahamiana.

Uliponiacha tu ni hapo ulipoilink na ujahidina, maana so far sikuona kutajwa masuala ya dini katika hizo posts mbili.

Regardless of the "agenda' kama ipo, Vipi hizo points zina ukweli?
 
Mzee Tafiti,

Nimesema hivi hii habari siijui, sasa usinilazimishea tuuu ili upate kujiosha upuuzi wako, director wa NSSF nimemuona kwa macho yangu bungeni akiwa na Kingunge, na Malima, saaa za jioni, the next thing I know ni Malima kulivalia njuga hili suala, namba zilizohisuka na hayo majengo sizijui, halafu sio kwamba habari zikiandikwa kwenye magazeti ya bongo lazima kila mtu asome, tena huko bongo tuliacha kuyasoma siku nyingi huwa tunaingia huku na kupata data,

Sasa hivi niko NY, na nikaamua kuongea na mzito mmoja wa nchi kuhusu hiyo issue, sikusema kama wewe kuwa "NINAJUA", kama wewe ulivyosema kwenye hoja ya ubalozi wa UHOLANZI, ambako ulikamatwa kuwa hujui, mimi nimesema sina uhakika na hiyo issue na nimesema kuwa nikirudi bongo nitaifuatilia kwa makini, na nikaomba radhi kuwa hii issue haifanani na posting yangu ilipaswa kuwa kwenye Manji/Mengi, kwa hiyo posting yangu ni
tofauti na ya kwako ya kudai unajua wakati ulikuwa unajua dhahiri kuwa hujui, upokamatwa badala ya kuomba radhi ukaanza uabunuwasi kuwa ooh mimi nimekosa lakini wengine huwa hawakubali, NONESENSE!



sasa ninakuona unataka kunivuta kwenye hoja zako za kudai balozi ana-sexual relations na mama wa ki-sirilanka, ulipoambiwa kutoa ushahidi ili balozi arudishwe ukakaa kimya, ukasema Dr. Kitine ni form six, ukaambiwa hatujawahi kusikia form six akiwa lecture wa university Canada!, ukasema Mzee marehemu Mzena ni darasa la nne-nane, kumbe mzee amesoma na Lusinde na mzee Chiume, kule Makerere, hakukuwa na wanafunzi wa darasa la nne?

Niliposema kuwa habari za Sozigwa nimepata kwa kigogo mmoja, mbona usiseme kuwa ni za uongo? Mzee wangu nafikiri ulishagundua kuwa wazee wengi humu walishakuweka sehemu fulani na habari zako, ukalia sana kuwa Es akisema basi, wakakupinga kuwa huna ukweli zaidi tu ya kutetea viongozi wezi, sasa kama kawaida yako huwezi kuandika humu bila ya kulitaja jina langu, mzee wangu at this point wewe ni mjumbe tu kama wengine huna lolote special kama ulivyotaka kujifanya mwanzoni kwa kutumia jina langu, huwezi kuwa UK ukajua mambo ya bongo, yaani data hizo tuachie sisi wa kunyumba, au kukaye huku Ruvuma mpaka Maputo, au Matimila!

Na mzee wangu Nungwi,

kama hapa ndipo mahali pako pa kutafuta heshima, samahani sio wote tunaokuja hapa kutafuta heshima, mambo ya Freeman nilikwambia kuwa wewe unamjua sana, lakini CCM ndiyo iliyoshinda, uchaguzi tena ni 2010,

na kwa taarifa yako sasa ni kwamba Freeman ameamua kutogombea tena urais na atagombea ubunge tena Hai, sasa ameamua kuyasikiliza tuliyomwambia kwa siku nyingi ya kuimarisha Chadema toka ngazi za chini, kama CCM, ninayasema haya kwa sababu ninamfahamu bro, sasa kama hutaki itabadilisha nini?

Issue ya Manji pamoja na kutoijua kwangu, tayari ninajua kuwa analindwa na vigogo wengi wa serikali yangu ya CCM, kama ni billioni moja au 20, haibadilishi kitu! Kama hamna data za kujadili hii issue kubalini kushindwa lakini sio kutafuta mchawi ambaye hayupo!

Na Mzee wangu Mwanakijiji,

Ninajua kuwa ulikuwa unaitafuta namba ya simu ya PM, ili umhoji ni hii hapa cell yake # 0744-800-000, usipompata mpigie Akukweti kwenye cell# 0745-555-555, na ukitaka namba ya kigogo yoyote yule nitakupatia, au ukitaka kumhoji JM, cell yake ni # 784-544-544!, Kingunge ni # 0744-310-064,

kazi njema ndugu yangu!
 
Jaribu # 744-777-777, kama hupati nifahamishe nitakupa nyingine!, au msaidizi wake wa karibu sana # 748-783-996, ambaye atakupatia au kukuwekea appointment naye!

Kama haziendi nifahamishe nitakupa nyingine!
 
Mimi huwa sibishani na tafiti maana nilisha jua ni mbabaishaji wa makusudi ama kutokujua . Alipewa maonyo mengi lakini akawa haelewi naona wakati anaambiwa kuja hapa hakukaa chini nakutafiti kabla hajaingia hapa .Mwangalieni huyu maana anaweza kubishana hata na jiwe wakati halisema ama kibao ambacho kinaweza kukuonyesha toilet ni kule kwa mshale lakini chenyewe hakijawahi kufika huko chooni .
 
Duh,

Maskini topic ya nungwi imebadilishwa mpaka imevurugika sasa, imeenda NSSF na sasa imekuwa ni kumjadili/kumshambulia tafiti.

Nlikuwa na hamu ya kujua ukweli kuhusu hayo mabilioni yaliyopotea... maana to me the news was fishy.. na kulikuwa na 'rumours' kuwa ni kweli Mengi ameattempt hilo dili na likakaribia kushtukiwa. Sasa akafanya preemptive defence ya kutangaza kuwa kuna watu wametumia jina lake kuattempt wizi. Sasa nlitarajia wazee wenye data humu watazimwaga.

Inanshangaza sasa kuwa badala ya kudiscuss issues tunamdiscuss mchangiaji. Regardless of whether data kaleta tafiti au mtu mwingine, the issue is whether aliyoyaleta hapa yana ukweli au la, the message rather than the messenger.

Kwa mfano, ikiwa ni kweli kuwa Mengi kawaibia walemavu ... I don't see atashindwa vipi kutapeli hayo mabilioni. Ikiwa ni kweli kuwa anakwepa kulipa VAT na kodi nyinginezo, nae pia ni mhujumu wa uchumi ... no better than the other BANDTIS and CORRUPTS.

Kwa maoni yangu hii ripoti ya NSSF imekuja hapa kimakosa, hata hivyo .. badala ya kumshambulia mletaji ... ilikuwa tudiscuss ukweli/uongo/mapungufu ya ripoti hiyo.


My attempt to get us back to the topic.
 
Kulikoni

Ni kweli Mengi hana tofauti na wezi wengine kama akina Manji etc . Lakini hawa ndiyo wanao sikika kwamba ni wazawa . Issue hii ya Mengi iko polisi kwa upelelezi hakuna mwandishi wa habari anaweza kudiriki kwenda kwa DCI kuuliza mwisho wa upelelezi inapelekea kufa kifo cha kawaida kama ilivyo kwene kuwachunguza walio tuhumiwa kugushi vyeti na kuitwa ma Dr. kazi kubwa sana TZ media imelala na wanachi ndiyo kabisaaaaaaaaaaa
 
Kwa kuheshimu taratibu zetu za kidemokrasia nayapokea yote yanayosemwa dhidi yangu binafsi badala ya kujadili yale ninayopost some people have decide to go for the softer option in a discussion yaani kumjadili mjumbe badala ya ujumbe.

Inashangaza mambo yoooote ninayochangia humu ndani kama mwanachama mwingine yeyote mimi naitwa mtetezi wa wala rushwa!! yaani hii ni kali, nimeitwa mbishi kama jiwe yaani mzee mugishagwe licha ya kuamua kuwithdraw my comments kwenye ile topic uliyoweka na kukuomba radhi bado unaona kwamba mimi ni mbishi....katika kanuni za busara ni kujifunza wakati gani you have to move on...


Naam in the spirit of our mjadala kuhusu mabilioni yaliyopotea ambayo ndio mada halisi mshukiwa ni mengi au at least alitakiwa kuwa ni yeye manake haingii akilini kwamba pesa zote zile zipotee halafu kusiwe na japo mengi kuitwa katika kituo cha polisi kuhojiwa!

Jambo kuu ni kuwa taarifa aliyotoa yeye ni kuwa kuna watu wametumia jina lake kuanzisha charity na wamepokea misaada kutoka shirika la umoja wa mataifa ambapo jamaa wamepokea bilioni arobaini na moja na kutoa bilioni thelathini na tisa!

Taarifa hiyo ilisema vile vile kuwa Mengi ana account katika benki hiyo sasa maswali yangu ni haya kwa wachangiaji na mamlaka husika:

-Hizi ni fedha ambazo zilikusudiwa kutolewa kwa jamii nchini tanzania for good causes imekuwaje licha ya taarifa hiyo kutoka kwa NGUMA ambae ni company secretary wa IPPGROUP bado kusiwe na kauli yoyote kutoka POLISI,UN,NBC au serikali kwa ujumla katika taasisi zake za kuzuia ufisadi?

Tukumbuke hapa tunazungumzia takriban robo ya mapato ya serikali kwa mwezi!

- Mengi baada ya kuona kuwa kuna watu wametumia jina lake kuiibia UN and in other ways kuwaibia wananchi wa tanzania ambao kikhalisi hasa walistahili kuwa ndio beneficiaries wa hizi pesa kwa nini asitoe taarifa kituo cha polisi au relevant authority yeyote badala yake kukanusha tu.

Nimemjua Mengi for a long time kuamini kuwa anapenda kuonekana kama ni mtu wa watu mwenye kujali utu na maadili mema, kama raia mwema wa tanzania kwanini hakutoa taarifa kunakohusika au tu kuomba wahusika matapeli washughulikiwe?

- Benki ya NBC nayo inalake swali kwanini baada ya kuona jina la mmoja wa account holder wao [ripoti ilieleza kuwa mengi ni account holder hapo] wasijaribu kuhoji iwapo anataarifa na fedha au taasisi hii?

Ni basics gani zimetumika kufungua akaunti hii?

Nimeshawahi kuwa mwanachama, mwanzilishi na kiongozi katika taasisi kadhaa za hiari Tanzania na najua utaratibu ni kwamba unapofungua akaunti ya taasisi basi unahitaji kuwa na zaidi ya mtu mmoja kuweka sahihi zao na hao ndio wanakuwa authorised officials katika masuala ya fedha mara nyingi huwa ni mweka hazina na mwenyekiti au katibu na hawa majina yao yanafahamika wazi, sasa tuseme benki haiwajui hawa watu au vipi?

-Ili taasisi iweze kuqualify na misaada mizito kama mabilioni haya inabidi iwe na usajili katika ofisi ya msajili wa vyama vya hiari tanzania ambayo inaoperate chini ya wizara ya mambo ya ndani, nao wamekaa kimya!

-Naam kuna walakini mkubwa kwa waandishi wa habari tanzania kama asemavyo Mugishaghwe manake haya ni maswali nyeti yenye kuhitaji majibu, sifikirii kama watu wenye uchungu na nchi yao wataweza kuona kiwango hiki na kuturn another page bila kujiuliza maswali kadhaa....

Hivi hapa kuna nini, wananchi tunahitaji kujua pesa hizi....
 
Nungwi,

Kwanza samahani kwa kutokujibu mapema, jamaa walikuwa wananisumbua, ikabidi nipoe kidogo ili wanisahau.

Ninahaidi kuwasiliana na NMB kuulizia. Suala ni tata sana.

Kuhusu kujadili watu mi naona imekuwa kawaida humu, sijui kwanini!! Ila pia wakemewe waliokuwa wanapindisha topic kwa maksudi kabisa.

Ngoja nijaribu ndugu yangu, lakini mbele yangu naona harufu sio nzuri, nilitegemea magazeti ya this day na kulikoni yendeleze "episodes" za huo ujanja walifanyiwa bosi wao!!.

Imenishangaza kidogo.

FD
 
tafiti then jadili said:
Hakika kwa kweli Nungwi hii habari ya haya mabilioni kilichonichangaza ni kutokuwepo na kauli yeyote toka kwa wenye mamlaka kuwa uchunguzi unaendelea au kama watafuatilia kuhusu ''wizi'' huu?!!

Kinachoshangaza kingine ni pia kutokuwepo na kauli yeyote kutoka ofisi za umoja wa mataifa kuhusu watu hao.

Kimsingi mambo yafuatayo yananishangaza:

Hivi inawezekana kweli kwa benki yenye uzoefu wa ku-operate miaka mingi namna ya NBC kuweza kuruhusu watu kufungua akaunti bila mtu husika kujulikana?nijuavyo miongoni mwa taratibu ni kupeleka picha nk sasa haya hayakufanyika?

Hata kama inaweza kuwa argued kuwa ilikuwa ni jumuiya hivyo wadhamini tu wangetosha?hivi ule utoaji fedha wa kiasi cha bilioni 39 haukuwashtua wenye benki hizi kiasi cha kuweza kufuatilia japo kuulizia kwa Mengi mwenyewe ambae taarifa ilisuggest kuwa anazo akaunti zingine benki hiyo hiyo?

Ina maanda shirika la USAID nalo pia ni la kibabaishaji au kuna mpango ulisukwa?

Taarifa zote za kukanushwa kwa mambo 'anayosingiziwa' bwana Mengi ni kubwa mno kiasi unashangaa hivi vyombo vya sheria vipo wapi?

Mbona Mengi malalamiko anayoyatoa yote yanaonekana kama ni ku-attract media coverage tu manake hatuoni suggestion ya kuwa ameripoti kituo cha polisi au kuomba msaada wa dola 'kukabiliana na uhalifu dhidi yake'

Ujambazi upo namna nyingi, katika nchi nyingi 'Fraud' licha ya kuwa ni kosa la madai 'civil offence' bali pia ni kosa la jinai na ndio tanzania anti fraud squad wapo chini ya jeshi la polisi,sasa nadhani mheshimiwa IGP Mwema nae angelivalia njuga hili, lakini kwa hali ilivyo nae akianza kulizungumzia hili la wajanja waliokula 41 bilioni itabidi Mengi 'aisaidie' polisi oops!


Sasa binafsi yangu nina tatizo kidogo na overall conduct ya Bwana Reginald Mengi, sasa hivi kuna kesi inaendelea katika kamati ya maadili ya bunge kujadili madai ya Mbunge Adam Malima kwamba televisheni ya ITV na vyombo vya habari ambavyo vinamilikiwa na reginald mengi vimekuwa vikionyesha sana habari kwa maslahi yake tu, hili nitalizungumzia kwa kirefu kesi ikishatolewa hukumu lakini kwa sasa nasikia mengi anaelekea kubaya katika kesi kwani mbunge adam malima ana concrete evidence.

Habari za ndani kabisa kutoka kwa walio karibu na huyu bwana ni kwamba amepatwa na depression mbaya sana tangu kifo cha mtoto wake Mutie na madaktari wamemshauri apumzike kwa sasa kwani amekuwa na haphazard memory lapses na imekuwa inaathiri sana decision making yake na hii ndio inapelekea kuwa na ugomvi na kila mtu kwa sasa, kuna kesi kibao mahakamani ninazozikumbuka kwa sasa ni:

1. Warioba na wenzake wawili wanadai milioni 900 kwa kukashifiwa.

2. Managing Editor wa DAILY NEWS Mkumbwa Ally anadai 1 billion

3. Yusuph Manji anadai bilioni 50 kwa kukashifiwa

4. Katika press release yao wakiclarify habari za IPPMEDIA NSSF nao wamesema wanaconsider hatua za kisheria.

Sasa hii inakupa picha kwamba sasa enzi za ubabaishaji wa Reginald Mengi zinaelekea ukingoni hususan kutokana na ukweli kuwa hivi sasa anadaiwa VAT na TRA zenye thamani ya bilioni 6 na hivi sasa mamlaka ya mapato bandarini inachunguza malalamiko ya chama cha walemavu kuwa Reginald Mengi mwaka jana kaingiza BENZ fully automatic [kila kitu kipo kwenye usukani] kwa ajili ya disable. Documents ZOTE zinaonyesha gari ni ya Chama cha walemavu. Hivyo basi kapewa excemption ushuru. Kwenye usajili kaandika jina lake!!!!! Kawazika walemavu!!!

niliyoyasikia ni mengi na yote mtayapata hapa, sasa hivi inabidi Mengi aungame manake kishawaibia sana watanzania na kuwafinika kiinimacho, sasa hivi ni ari mpya inabidi acleane his act na akapumzike kama alivyoshauriwa na madaktari...

Yaani you just nailed it na natumai kutakuwa na majibu mapana na marefu na ya kina ambayo wana FORUM hii wanayo...kwani humu ni kama kisima cha ma PROFESA wa kufanya analysis bila ushabiki unaopendelea upande wowote
 
Hizi billioni 40 wamevuta wajanja wachache wa hapa mjini.Hizo pesa zilitoka UNAIDS. Na hio NGO yenye jina la Mengi ilianzishwa kwa ajili ya kuwajali watoto waathirika wa Ukimwi majumbani kwao,yaani watahudumiwa hukohuko makwao badala ya kuwa wanakwenda kwenye centers au zahanati.

Inasemekana kilichotokea mpaka IPP kushtukia ni query iliyotokana na hio account yenye hizo pesa.Mengi alipiga kelele sana,lakini baadae akawa kimyaaa,na habari zilizopo ni kuwa hao vijana walimkatia dola milioni 3.
Hao vijana sasa ndio matajiri wa kiafrika waoongoza hapa Dar,wamenunua majumba Masaki,Oysterbay...wana magari ya kifahari aina karibia zote,na magari yao huwa yanaletwa na ndege,sio meli!

Hili bomu sio rahisi kulipuka,kwa sababu;
-kwanza kwenye nchi ya kimaskini kama hii yetu kuwa na dola millioni 40,ambazo hazijaibiwa bongo hata hao wanaotakiwa kuku-prosecute watakutafuta urafiki.Uko mfano wa Franco Tromontano,ambaye ni mkurugenzi wa DTV,yeye hawezi kwenda ulaya,kuna arrest warrant kule Belgium,na walishaomba kuja kumtafuta hapa(sijui liliishia wapi).Yeye alipewa pesa kule kama mkopo sijui wa nini,akaja nazo huku,ndio wakaanzisha station ya TV na kiwanda cha kutengezea mafuta ya break na spring.Cha kushangaza baada ya habari hizo kutoka kwenye magazeti, kama mwezi baadae, akaonekana kwenye vyombo vya habari akilisakata rumba na Anna Mkapa,(wakati huo 1st lady)Ameji-embed kwenye TELEFOOD,hii sijui ni NGO au nini,lakini wadhamini wake ni yeye mwenyewe,Anna Mkapa,Jenerali Ulimwengu nk. Na mpaka leo anaonekana kwenye sherehe za viongozi na anaendelea na maisha yake kama kawaida,lakini ni mwizi!

-Pili,hii ni scandal kubwa kwa UNAIDS,kwa hio wao ni lazima watajaribu kulizima hili.Hizo pesa ni kutoka nchi hisani na kama bomu kama hilo linalipuka,they will be put under a microscope,na shady deals within the UN organisations ni mambo ya kawaida tu,(sio zamani sana kulikuwa na ile ya Oil for Food Programme ya Iraq...)kwa hio kazi za watu wengi zitakuwa at risk,kwa hio hatutasikia UNAIDS wametaka hao watu washikwe,wao watajaribu kwa kadri wanavyoweza kuonyesha kuwa hizo pesa zilitumika kama ilivyopangwa,ila ndio unakuwa ni mwisho wake hapo,hawatatoa pesa zaidi.Haya mambo yanafanyika sana within these organisations,ndio maana ikawa ni moja sababu ya Marekani kusitisha kutoa mchango wake UN,huko nyuma,lakini walielewana baadae.

Kwa hio uwezekano upo kuwa Mengi nae alifaidika,kwa sababu kelele zake zilizimika ghafla,na yule ni mfanya biashara Mchagga,kweli dola milioni 40 zipitie kwenye mgongo wake hivihivi tu,asione hata chenji!Lazima kavuta,lakini deal haikuwa ni yake.

-
 

Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom