Mengi vs Manji: Ukweli ni upi?

Mengi vs Manji: Ukweli ni upi?

Kwa mtu anayemfahamu Mengi na biashara zake ukweli uko wazi kwamba kwa kipindi cha 1995 mpaka 2005 amekuwa kinyume kabisa na upinzani nchini. Vyombo vya habari vya Mengi particularly ITV vina nguvu sana-kama angeunga mkono CHADEMA mambo yangekuwa tofauti sana. Lakini ilikuwa kinyume chake.

CHADEMA bado haijaamua mgombea urais wake, kusema kwamba Mengi ni mgombea wa CHADEMA wakati hata sio mwanachama ni kutokututendea haki.

Baadhi mmeunganisha msimamo wa CHADEMA kuhusu pesa za NSSF ama shutuma za ndesamburo na Mengi na uchaga. Huku nako ni kutukosea haki na kuhamisha mjadala wa msingi. CHADEMA tumesimamia mambo mengi ya kitaifa na tunaendelea kuyasimamia. Wakati tunapinga ununuzi wa ndege ya rais sikusikia mtu akisema anayepingwa ni Mramba Mchaga. Wakati tunapinga ununuzi wa RADA haya hayajitokeza. Wakati tunamshambulia Lowasa kuhusu Richmond sijasikia yoyote hapa akisema kwamba huo ni UKASKAZINI.

Bottomline, hapa kuna watu wanataka kututoa kwenye kujadili masuala ya vyanzo(source issues)- kwenye suala la NSSF/PSPF-suala la msingi ni je, bilioni 83 za michango ya walipakodi ziliwekezwa vizuri au zilizochotwa kutokana na ufisadi? NSSF/PSPF/Manji nk wanawajibu wa kujibu?

Ndesamburo ameweka bayana madai ya rushwa na amesema chanzo ni nini, Mengi na Lowasa. Lowasa ni kiongozi wa umma, hajajitokeza kujibu. Rais amesema serikali haitajibu. Kuna nini hapa kinafichwa? Hili ni suala hapa! Tulijadili na kuhoji

Ya Mengi na Manji tuwaachie wenyewe wameshapelekana mahakamani kwa tuhuma za kukashifiana. Tusiingilie uhuru wa mahakama.

Lakini haya matumizi ya pesa za walipa kodi na tuhuma za rushwa; ni ya kwetu haya, tuyajadili kweli kweli...

CHADEMA si chama cha wachaga: rejea tamko rasmi la chama kuhusu suala hili http://www.chadema.net/tamko/2007/mwanri.php

Kwa hiyo mtanzania yoyote ana haki ya kuwa ndoto ya kugombea urais kupitia CHADEMA 2010: awe msukuma, awe mhaya, awe mchaga, awe mjita:wote karibuni ili mradi tu uendani na misingi ya falsafa ya nguvu ya umma http://www.chadema.net/nyaraka/falsafa.php na itikadi ya mrengo wa kati http://www.chadema.net/nyaraka/itikadi.php

JJ

OK, bado hii ipo hai jamani mengine haya tena
 
Umenikumbusha Shujaa Mwamwidi.
Hapa kuna tatizo kubwa.Tukiambiwa ukweli tunabisha.
Tumelala usingizi.Ukisikia huu ndio Uzube au Ufala.
Mtu fala ndio unaweza kumnunua kwa hela.Waache wahidi na wageni wengine wajinafasi.Sasa wafanyeje wakuu?
Hawa jamaa hata wakiburizwa mahamani haitoshi, hizo hela wanazoiba ni nyingi mno! Think of 83 billion shs, in other words, USD 83 million sasa jamani hata tunaweza kuwaburuza. Hizo hela labda ziko ulaya tayari. Is real painful. Muhindi anakuja tanzania na dollar 2000 anachonga misheni anatoka na dollar million 80!! Mie sometimes huwa naona hata akina mwamwindi hawakuwa na makosa!! Samahani lakini! Mie siona kama na sisi ni nchi yetu hii! Tuna rais, tuna mawaziri, tuna polisi, na hiki chombo chao PCB (Protection of Corrupt Bureau!) better go to hell!!
 
Nakubaliana Na Mr Choveki Ila Nina Nyongeza,

Suala La Muhimu Ni Kuwapa Wananchi Elimu Ili iwape maarifa ambayo yatawawezesha kufanya kazi ama kupewa Mikopo yenye masharti nafuu, Amabayo Kwa Kutumia Elimu Yao Watanufaika Kwa Kujikwamua Kiuchumi Na Kuboresha Maisha Yao Na ya Jamii Kwa Ujumla.

Na sio hilo tu!ila pia watapata uwezo wa kufanya uchambuzi yakinifu pale inapokuja kwenye issue nyeti ambazo zinaigusa jamii moja kwa moja!tujiulize Swali Moja!je Wahindi Walikuwa Wana asset gani kama Colateral Wakati Wa Kuchukua Mikopo Huko Kwenye Mabenki pindi walipowasili hapa nchini?inawezekana cash kwenye akaunti ama uwekezaji ndio vielelezo vinavyotumika.

Ninavofahamu Mimi Wahindi bado hawajaonyesha kwamba ni Waendelezaji Wa Nchi Yetu Na bado kwa maoni yangu binafsi Hawaja "PROVE" KAMA WANA NIA NZURI NA MAENDELEO YA WANANCHI WENZAO!Kwanini wasi invest kwa namna ambayo itainufaisha sio tu jamii inayowazunguka bali pia wao wenyewe!Kwa kujirundika eneo moja kwenye nyumba zenye mfumo wa apartment complex karibu na biashara zao hakuinufaishi jamii husika kwa namna yoote ile!ingekuwa vyema kama wangewekeza pia vijijini!kwasababu ndiko kwenye asilimia karibia 90 ya watanzania wote na pia kwenda kujenga kwenye maeneo ya wazi ili kuiendeleza nchi na kuongeza ajira na kuiletea jamii maendeleo!

Najua wanahaki ya kuwa na hofu kwani wanakumbuka yaliyowakumba wakati wa utawala wa Idi Amin wa Uganda pale alipowapa masaa kadhaa ya kutimka nje ya nchi!lakini hapa Tanzania hatuna na hatujawahi kuwa na uongozu mithili ya ule wa Amin,Wahindi kama raia wengine wa Tanzania wanalindwa na sheria zote husika,kwanini wasionyeshe upendo wa kweli kwa maslahi ya nchi iliyowakaribisha bila kujali tofauti zetu?

Ni Kwanini Wasiende Kujenga Ili Kwanza Watoe Ajira Pili Iwe Ni Investment Yenye Kuonyesha Ishara Ya fadhila, Uadilifu Na Nia Njema Dhidi Ya Waliokukaribisha?viongozi Wetu Kwa Kujali Maslahi Binafsi Hawataki Wananchi Wengi Waelimike Na Pia Wanafanya Maamuzi Ambayo Hayazingatii Maslahi Ya Wazawa!tunawapenda Wahindi kama watanzania wenzetu Na Ndio Maana Nao Bado Wapo Nchini Kwetu!tulizingatia Busara Za Mwalimu Za Kutokubaguana!

Lakini Wahindi Na Wageni Wengineo Kwa Ujumla Ni Lazima Watuhakikishie Kwamba Na Wao Wamekuja Nchini Kwetu Kwa Nia Nzuri Na Ni Lazima Waprove Hilo Suala Pale Inapotakikana!Na pia vile vile kwa vitendo!

Sio kwa kuwapa viongozi wachache rushwa ili watetee maslahi yenu,bali kuwekeza kwa wnanchi ili kujenga uhusiano mwema na taifa jema lenye maendeleo mema!Wazungu walitumia "devide and rule"hiyo ni mbinu ambayo ni wazi bado iko appilcable kwenye levo karibia zote za kijamii kwenye kizazi hiki!mzungu anagundua kuwa itamgharimu zaidi kama akifanya biashara na nchi flani kwa maslahi ya nchi nzima,ili kuepuka hilo wanatumia hio rule ya devide and rule kwa kuwalinda na kuwanufaisha watu wachache ambao in return watalinda maslahi yao badala ya maslahi ya wale waliowaweka madarakani!

Na wahindi nao kwa kupenda kutoa rushwa ama takrima kama ilivyobatizwa wakati wa uhalalishaji wanakwepa kuwekeza kwa wanachi kwani itagharimu zaidi,so devide and rule inakuwa applicable pale ambapo serikali na wananchi wanakwaruzana kwa sababu ya rushwa inayosababisha upendeleo,ubaguzi na umasikini uliokithiri wakati ambapo kodi inayolipwa na wavuja jasho ndiyo inayowalipa mishahara viongozi ili wasimamie maslahi yao.

Nasema inabidi waonyeshe mabadilko kwasababu kama Unahamisha Fedha Zote Ulizozichuma Nchini Kwenye Akaunti Za Kigeni Halafu Unahamia Huko Ukishazeeka ama kustaafu!kweli Utakuwa Umekuja Kwa Nia Nzuri?

Kuna Mashamba Mangapi Na Maeneo Mangapi Mazuri Ambayo Wangeweza Kujenga Na Kwenda Kuishi Huko Wakati Wamezeeka Ama Wamestaafu ama wamechuma vya kutosha?KWA NINI MSIWE KAMA ZIMWI LIKUJUALO AMBALO HALIKULI LIKAKWISHA?

Ni wazi sheria nyingi zimewekwa sasa hivi ambazo mara nyingi zinamlinda mwekezaji zaidi ya maslahi ya nchi husika,huo ni mwendelezo wa mabadiliko kutokana mageuzi ya kiuchumi,lakini issue ya wahindi ni tofauti kwasababu wao ni wananchi wa hapa kabla hata ya mageuzi ya kiuchumi,so hawaangukii kwenye cateogory ya foreign investor,sasa kama Umepewa Haki Zote Za Kiraia Kwa Nini Uact Kama Sio Raia Mwenye Uchungu Na Nchi iliyoamuakukulinda kisheria, Inayokutambua,kukuheshimu Na Kukuhudumia Kama Raia?

Umefikia Wakati Ambao Wahindi Inabidi Wabadili Mienendo Kama Hiyo si tu Ili kurudisha imani kwa raia wenzao,bali pia Kujenga mazingira mazuri ya kuwakwamua walalahoi na wavuja jasho kwa ujumla sio tu kiuchumi bali pia kijamii ili kudumisha amani,utulivu na upendo wa kitaifa!
 
Bora sasa hii mada ianze upya kujadiliwa,, kwani kesi ya MAnji na PCB imefia wapi? Kesi ya Manji na Import Support imefia wapi? Au ndio amesamehewa? Nasema hii ni hatari sana. Watanzania wanatafuta fedha za kujenga madarasa wakati kuna Sh bilioni 83 zimechukuliwa na kijana mdogo sana ambaye wanasema tabia zake si za "kimaadili"
 
Mjukuu umekumbusha mambo, Hivi kwanza THISDAY "wamemalizana" na MANJI manaa naona kama siku hizi hawamgusi kabisa mtoto wa kihindi... Hahaaaa... hebu tuelezeni siri ya urembo, kijana siku hizi anaendelea kutanua na tena sasa anaendelea kutanua na "vijana" wenzake... Vipi kuhusu Lotto Kitita? Mbona kimyaaaaa? Au ndio Tarimba naye amelamba? Hivi kweli polisi, PCCB, TRA, Hazina, TIB wmeshapata fedha za Import Support? Hebu tujikumbushe tunaambiw watanzania wepesi kusahau mambo
 
Mtihani huo kwa Mzee Mwanakijiji ulianzisha mada ikafa kifo cha mende sasa imefufuka, huo ni mzimu ulizikwa sasa umefufuka, watu wanataka kujua, KULIKONI? mahela yetu kama anavyoyaita JOTI yako wapi? Yamerudishwa? Hebu nenda pale Millenium Bussiness Park ambako liko gazeti la Raia Mwema, viwanda na ofisi kibao lakini bei yao ilikua Biliono 16 tu lakini magofu yale MAnji hawauzia NSSF kwa Bilioni 46, jamani JK kama unapitia mikataba na huu pia wa NSSF na Quality upitie uangaliwe upya, wataalamu wafanya usamini upya, watupe bei... tulisahau ndio maana wengine wakaanza kuuza viwanja katikati ya jiji.
 
Kesi ya Mengi na Manji yatua Mahakama ya Rufani

na Happiness Katabazi
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

MFANYABISHARA maarufu jijini Dar es Salaam, Yusuf Manji, amewasilisha katika Mahakama ya Rufaa Tanzania ombi la kuitaka mahakama hiyo iitishe jalada la kesi ya madai ya kashfa Na. 91/2006 iliyopo Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ili iweze kupitia amri iliyotolewa na mahakama hiyo mwaka jana.
Katika kesi hiyo, Mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi, anamshitaki Yusuf Manji kwa kumkashfu kwa kutumia matangazo mbalimbali yaliyochapishwa kwenye baadhi ya magazeti hapa nchini.

Ombi hilo la Manji ambalo limepewa Na. 30/2008, lilipokewa katika Mahakama ya Rufaa Machi 7, mwaka huu, likitokea Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Kutokana na ombi hilo, kesi ya msingi iliyopangwa kuendelea kusilizwa mbele ya Jaji Amir Mruma jana na leo, haikusikilizwa kwa sababu faili la kesi ya msingi limeshapekwa katika mahakama hiyo ya juu.

Katika hati iliyopo Mahakama ya Rufaa, Manji anaiomba Mahakama ya Rufaa ipitie amri ya Jaji Mruma aliyoitoa Julai 18 mwaka jana kwa nia ya kujiridhisha usahihi na uhalali wa amri ya jaji huyo kwamba wazee wa baraza ambao ni wanahabari; Ndimara Tegambwage, Theodatus Mchunguzi na Mkurugenzi wa MISA Tan, Rose Haji, kwamba walikuwa na sifa za kuisaidia mahakama katika muda wote wa usikilizaji wa kesi ya msingi.

Manji anadai tangu ilipoanza kusikilizwa kesi ya msingi, aliwasilisha ombi la kuwapinga kina Ndimara na wenzake kwa madai kuwa wana uhusiano wa karibu na Mengi na wanajihusisha na biashara ya vyombo vya habari ambayo ina uhusiano wa karibu na Kampuni ya mlalamikaji ya The Guardian Ltd, na kuongeza kuwa kutokana na ukaribu huo anaamini hatatendewa haki.

Pingamizi ambalo lilitupiliwa mbali na Jaji Mruma kwa maelezo kwamba wasaidizi hao wa mahakama wana sifa zote za kuisaidia mahakama katika kesi hiyo inayomkabili.
 
Huyu Manji anajifanya kujua kila kitu ethics za sheria hazijui. Wazee wa baraza wanaplay role yao chini ya maelekezo ya kimahakama kwa kufuata haki. Alitaka kujiridhisha tu katika maana kwamba alidhani hukumu iliyotolewa haikuwa ya haki. Uliye tu Manji.
 
Kosa Afanye Kabila Nyingine Lakini Akifanya Mchagga Itakomaliwa Mpaka Basi, Punguzeni Wivu Fanyeni Kazi,
 
Manji hajaachwa, kwanza katika EPA pamoja na kuwa anawabeba kina RA, alihusika kwa kiasi kikubwa na amekubali kulipa wizi wa KAGODA na amekwisha kulipa kiasi cha Sh bilioni 12 na kuahidi kulipa Bilioni 20, ifikapo Juni, 2008 kabla ya Timu ya Mwanyika kukabidhi ripoti yake kwa Rais. Anasemekana analipa fedha hizo kwa "kushirikiana na wenzake" ambao hakika hawatajwi. Yeye anajiona/anaonekana kijogoo wa ufisadi na HAKUNA WA KUMFANYA KITU na HANA CHA KUPOTEZA mambo yanayompa KIBURI cha kujitokeza. Eti anasema analipa kwa kuwa yeye ni sawa na mnunuzi wa gari ambalo kumbe liliibwa na kupita mikono mingi, lakini hivi jamani FEDHA unaweza kuzifananisha na gari ama mifugo. Maneno hayo ndiyo yaliyosemwa na IGP katika mkutano wake na waandishi. Mwizi wa gari anaenda kuuza, mwizi wa fedha anatumia, sasa fedha jamani ndizo ameuziwa MANJI? Mbona haieleweki?
 
Posting ifuatayo nimeikutauta Darhotwire forums.Ni kuhusu Mengi lakini aliyeiposti huko anaonekana dhahiri kuwa Mujahidina flani jast like huyu "Tafiti Then Jadili"


😕

JIHADIST AGENDA?
WANAJF MIMI NASHANGAA SANA KUONA KUWA WATU KAMA DR. DAU BADO WAKO MADARAKANI:
1. ANAHUSIKA KUHAKIKISHA MANJI ANAKOPESHWA BILA MASHARTI 9B
2. ANAHAKIKISHA MANJI ANAUZA MRADI WA 9B KWA 39B KWA NSSF
3. ANAHAKIKISHA MADARAKA NDANI YA NSSF YANAENDA KWA UDINI
4. ANAWAPUMBAZA WAANDISHI WA MAGAZETI YA TANZANIA KWA KUWAANDALIA MASHINDANO YASIYO NA TIJA KILA MWAKA ILI WASAHAU KUANDIKA HABARI ZA NSSF
5. NI MUHUBIRI MZURI WA DINI NSSF
6. ANAJARIBU KUINGIZA MAMBO YA CHAMA KTK NSSF KWA KUMUUNDIA MBOWE DENI LISILOLIPIKA
7. ANA UKABILA WA DHAHIRI
8. HASHAURIKI NA HILI LIMEKUWA TATIZO NSSF KWA MUDA WOTE WA MADARAKA YAKE
9. ANAHUSIKA KTK KUIMPLEMENT SYSTEM ISIYOISHA YA ORACLE
10. BAYA ZAIDI NI LAST WEEK TU AMEHAMISHA OFISI ZA NSSF KUTOKA BI. TITI ROAD (CHEAPER AREA) KWENDA JENGO JIPYA (AZIKIWE) ILI TU AWE ANAKAA FLOOR YA 17 NA KUWA CEO ANAYEKAA OFISI ZA JUU ZAIDI TZ. JENGO HILO LA AZIKIWE LINGEWEZA KUIINGIZI NSSF HELA NYINGI ZAIDI YA JENGO LA BI. TITI-NADHANI HAFAI
NAWAKILISHA
 
Kifo, mbona hata tuliiambiwa na kuimbiwa kuwa Dr. Dau is the best next thing to happen in Tanzania na wengine walipiga kampeni kuwa ndiyo anapaswa kuwa Gavana Mpya Benki Kuu? Ina maana tulikuwa tunaghilibiwa?
 
Yeye anajiona/anaonekana kijogoo wa ufisadi na HAKUNA WA KUMFANYA KITU na HANA CHA KUPOTEZA mambo yanayompa KIBURI cha kujitokeza. Eti anasema analipa kwa kuwa yeye ni sawa na mnunuzi wa gari ambalo kumbe liliibwa na kupita mikono mingi, lakini hivi jamani FEDHA unaweza kuzifananisha na gari ama mifugo. Maneno hayo ndiyo yaliyosemwa na IGP katika mkutano wake na waandishi. Mwizi wa gari anaenda kuuza, mwizi wa fedha anatumia, sasa fedha jamani ndizo ameuziwa MANJI? Mbona haieleweki?
Hata mimi haijaniingia vema kichwani. Kazi ipo!
 
Kifo, mbona hata tuliiambiwa na kuimbiwa kuwa Dr. Dau is the best next thing to happen in Tanzania na wengine walipiga kampeni kuwa ndiyo anapaswa kuwa Gavana Mpya Benki Kuu? Ina maana tulikuwa tunaghilibiwa?

Mwanakjj kwani haya mapya? ...Mwanakjj hukutakiwa kukubali weak points kama hizo!!!

Kifo atajifia kama wengine...
Hoja alizozitoa hazina kichwa wala Miguu na hawezi kuzithibitisha

Labda nimuombe ndugu kifo atuletee Ushahidi au maelezo kuwa Dau Mdini na Mkabila. Lete nafasi zote za NSSF na tuone!!! Mwenzako mmoja alisema Ifakara kumejaa udini kisa BOSI mwislam!!! zilipoletwa posts zote, wakristo ndo walikuwa wengi...
 

Labda nimuombe ndugu kifo atuletee Ushahidi au maelezo kuwa Dau Mdini na Mkabila. Lete nafasi zote za NSSF na tuone!!! Mwenzako mmoja alisema Ifakara kumejaa udini kisa BOSI mwislam!!! zilipoletwa posts zote, wakristo ndo walikuwa wengi...

Tatizo ni kuwa kuna watu wameshajiwekea vichwani mwao kuwa katika Tanzania watu wa jamii fulani ndio wenye haki na uwezo wa kuongoza na wengine nafasi yao ni kusaidia kuongoza. Ndio maana wenye akili waliweza ng'amua propaganda ya Mama Clinton kuwa rais na Obama kuwa msaidizi wake, yaani mzungu ndio anapaswa kuwa rais na mweusi anapaswa kushika majukumu ya usaidizi. Hapa kwetu kina mama Clinton ni wengi. Wapo wanaosupport fikira za aina hii kwa kujitambua kuwa na ajenda za kibaguzi na wapo wasiojitambua.

Wanaodai DAU ama Dr Hassan wa Ifakara Centre ni wadini na ni udini, yaani upendeleo kwa waislamu ndio unaowawezesha wenye majina ya Huseni na Rajabu kupata nafasi hawana tofauti na yule mshauri wa Clinton aliyedai OBAMA anaghara kisiasa kwa kuwa ni mweusi na hivyo anaonyesha uwezo tofauti na ule wanaodhani ndio kiwango cha weusi.

Tatizo zaidi ni kuwa wenye kuendesha propaganda kama hizi za kuwatuhumu kina DAU ndio haohao ambao ukisimama kusema Tanzania kuna tatizo la udini wanakuambia kuwa wewe ndio mdini na unakosa uzalendo.

Tanzania kuna udini na sio kwa Ramadhani DAU na wengine wa "aina yake" kuwa Mkurugenzi bali ni pale ambapo wale waliogubikwa katika fikira mgando zilizogubikwa dharau na chuki za kidini wanaporipuka na tuhuma za udini mara tu Hussein na Rajabu anapoteuliwa katika nafasi ambazo kwa fikira mgando zao wanaamini ni kwa ajili ya watanzania wa kundi fulani pekee.

Tanzanianjema
 
hapo pazuri tunahitaji data za udini NSSF, data muhimu jamani tufunguke masikio nami nahofia isije kuwa udini kwa kuwa tu wa juu ni miongoni mwa wale ambao hawajazoea kusikika au kushika nafasi hizo.

Ni vipi utendaji wake wa kazi kwa wenye kufahamu maana niliwahi sikia kuwa huyu jamaa ni mchapa kazi na si fisadi, kutajwa hapa imenishtua inabidi nianze kumtafuta undani



Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni
 
WANAJF MIMI NASHANGAA SANA KUONA KUWA WATU KAMA DR. DAU BADO WAKO MADARAKANI:
1. ANAHUSIKA KUHAKIKISHA MANJI ANAKOPESHWA BILA MASHARTI 9B
2. ANAHAKIKISHA MANJI ANAUZA MRADI WA 9B KWA 39B KWA NSSF
3. ANAHAKIKISHA MADARAKA NDANI YA NSSF YANAENDA KWA UDINI
4. ANAWAPUMBAZA WAANDISHI WA MAGAZETI YA TANZANIA KWA KUWAANDALIA MASHINDANO YASIYO NA TIJA KILA MWAKA ILI WASAHAU KUANDIKA HABARI ZA NSSF
5. NI MUHUBIRI MZURI WA DINI NSSF
6. ANAJARIBU KUINGIZA MAMBO YA CHAMA KTK NSSF KWA KUMUUNDIA MBOWE DENI LISILOLIPIKA
7. ANA UKABILA WA DHAHIRI
8. HASHAURIKI NA HILI LIMEKUWA TATIZO NSSF KWA MUDA WOTE WA MADARAKA YAKE
9. ANAHUSIKA KTK KUIMPLEMENT SYSTEM ISIYOISHA YA ORACLE
10. BAYA ZAIDI NI LAST WEEK TU AMEHAMISHA OFISI ZA NSSF KUTOKA BI. TITI ROAD (CHEAPER AREA) KWENDA JENGO JIPYA (AZIKIWE) ILI TU AWE ANAKAA FLOOR YA 17 NA KUWA CEO ANAYEKAA OFISI ZA JUU ZAIDI TZ. JENGO HILO LA AZIKIWE LINGEWEZA KUIINGIZI NSSF HELA NYINGI ZAIDI YA JENGO LA BI. TITI-NADHANI HAFAI
NAWAKILISHA


Hoja nzuri. Zinahitaji vidhibitisho tu.
 
JF

Jamani naomba nisaidiwe ili nami nichangie mjadala wa Udini na Ukabila wa Dr Dau.


Hivi Dr Dau ni dini gani? Kabila yake ni ipi?

Nimekwenda kwenye web site ya NSSF haikunisaidia sana. Wamesema tu kuwa jina lake ni Ramadhani lakini wapo Ramadhani Wakristo kama vile Jaji Mkuu wetu.

Please help
 
Jamani Mwacheni Dkt.dau Afanye Kazi. Haiwezekani Kila Binadamu Afanane Na Kambarage,jesus,mohamed Is Too Much Jamani

Siyo Wote Wanaomiliki Magazeti Na Tv Ni Wasafi,kuna Maeneo Ni Wasafi Lakini Upande Mwingine Nao Ni Wachawi . Tuombe Mungu Kuwa Tuko Salama
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom