Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,036
Jana, Mkurugenzi wa Makampuni ya IPP na mwanamazingira Bw. Reginald Mengi amepewa tuzo ya Martin Luther King Jr. Katika Hafla fupi iliyofanyika kwenye Ubalozi wa Marekani.
Tuzo hiyo inayotolewa kila mwaka na Ubalozi huo kwa Mtanzania ambaye ameonesha mchango mkubwa katika masuala ya haki za binadamu, mazingira, na mambo kadhaa mwaka huu nafasi hiyo imemuangukia Bw. Mengi.
Akizungumza wakati wa kumkabidhi Bw. Mengi tuzo hiyo, Balozi wa Marekani Bw. Mark Green alisema kuwa mchango wa Bw. Mengi katika eneo zima la uandishi wa habari hususan ule wa uchunguzi ni mkubwa na ambao unastahili kutambuliwa na kuthaminiwa. Bw. Green alisema kuwa utawala wa demokrasia unaenda sambamba na uhuru wa vyombo vya habari jambo ambalo Bw. Mengi amekuwa akilisimamia.
Pia mchango wa Bw. Mengi katika mazingira, kusaidia wasiojiweza na masuala mengine ulitambuliwa. Watanzania wengine ambao wamekwishapata tuzo hiyo kabla ya Bw. Mengi ni pamoja na Baba wa Taifa, mzee Kawawa, Dr. Salim, na Jaji Warioba.