Mbowe na Lissu na kisa cha Martin Luther King Jr. na Malcolm X

Kinjekitile Jr

JF-Expert Member
Dec 12, 2021
422
1,156
Asalaam ndugu wana jukwaa.

Ukitazama kwa makini siasa zinazo endeshwa ndani ya CHADEMA kwa sasa, unaona kutokuelewana fulani hivi kati ya Mwenyekiti Freeman Aikaeli Mbowe na Makamu wake,nguli wa sheria wa nchi hii Mheshimiwa Tundu Anthipas Lissu.

Miaka ya nyuma,huko Marekani kuliibuka na Wanaharakati wawili nguli kweli kweli na wenye wafuasi wengi ndani ya jamii ya watu weusi (Malcolm X na Mwenzake King Jr). Hawa watu walikuwa na lengo moja la kumkomboa mtu mweusi kutoka kwenye mikono ya kinyonyaji ya Wazungu ILA walitofautiana kwenye mbinu gani watumie ili kufanikisha matarajio na mipango yao

Malcolm ni mtu aliyeamini kabisa kuwa Mweusi marekani au sehemu yoyote Ile duniani hawezi kupata kutoka kwenye minyororo ya Mzungu bila kutumia Fujo,ghasia,maandamano na kujitenga kabisa na mambo yote ya kizungu. Lakini King Jr aliamini Mtu Mweusi anaweza akapata uhuru wake Kamili kwa kuendelea kuwa pamoja na wazungu,kutofanya furugu yoyote na pia kuwa mnyenyekevu kwa utawala. Hawa Jamaa hawakuwahi kuelewana ata mara moja na Malcolm X alikuwa anamdharau,anamkebehi na kumuona Martin Luther King Jr kama kibaraka wa wazungu

Tundu anaamini dhahiri shairi kuwa nchi hii kumtoa CCM madarakani,haiwezekani kwa kufanya maridhiano,vikao na mazungumzo yasio kuwa na Faida yoyote. Mwamba anataka mambo yawe moto moto,wakimwaga ugali na yeye anamwaga mboga. Jamaa alifaaa azaliwe Uarabuni maana uwa hanaga unafiki nahisi angekuwa na mambo kama ya Osama,Gamal Abdel Nassar au Saddam Hussein

Kwa upande mwingine,Freeman Mbowe yeye ana historia ya kupenda sana maridhiano toka enzi za Jakaya Kikwete, ni mtu wa taratibu,hataki kufuata mihemko na wala haendeshi mambo yake kwa kufuata nini wanachama wanataka bali anaona ni faida gani ataipata au Chama kitapata iwapo atafanya jambo fulani na kwa wakati fulani,jamaa ni Opportunist(Mchaga wa Machame😂😂).

Hii mbinu ya kuendesha Chama imekuwa ikionekana kama Jamaa anataka kuwaingiza mkenge Wanaharakati kama Mdude Nyangali,Dk Slaa na Mwamba wao Tundu Lissu na Kuna baadhi ya Wanachama na wapenzi wa siasa za upinzani wanaamini kabisa kuwa huyu Mmachame ni Kachero wa TISS (CIA ya Bongo) na kazi yake kubwa ni kuhakikisha kuwa nchi haiingii kwenye machafuko. Vijana wanaamini kabisa kuwa jamaa anapewa bahasha kila mwezi ili kutuliza mihemko chamani kwake,kwani kila hatua ya kutaka KUINGIA BARABARANI jamaa hataki kuisikia...

Wengine wanaenda mbali sana wanasema ata Prof Lipumba wa CUF ni kachero ndio maana hayati Maalim Seif aliondoka kwenye Chama na kujiunga na ACT Wazalendo,na hapo akafahamu tena kuwa ZITTO nae ni mtu wa kitengo, ikambidi amwambie Chama wakigawe kwa Bara na visiwani,yaani asijaribu kuingilia mambo ya Zanzibar ata kidogo

NOTE;Hakuna Chama chenye nguvu ya kuiondoa CCM kama CHADEMA kwenye nchi,Hawa wengine ni observers tu,ukiona CCM wanawafuata wale wa vijana wa Kanda ya Ziwa kama Makonda na Biteko Jua wameogopa sana shughuli ya hiki Chama ni moto sana

My Take;Ili kuiondoa CCM madarakani ambao wapinzani wanaamini ndio kizuizi cha Maendeleo ya Nchi hii,basi hawana budi kuunganisha nguvu zao pamoja ili kufikia kule wanapotaka kwenda,vinginevyo watakuwa wanaisindikiza CCM kwenye kila chaguzi
 
Back
Top Bottom