Halisi
JF-Expert Member
- Jan 16, 2007
- 2,802
- 614
Tuna matatizo makubwa sana humu ndani ya JF, kwanza naamini na nitaendelea kuamini kwamba kazi kubwa ya JF ni kuleta mabadiliko ya kweli katika jamii yetu na humu mara kadhaa tumekua tukitumia magazeti ya THISDAY kama refference za taarifa zilizoibua mambo yote tunayoyaona sasa ndani ya serikali ikiwamo BoT na kadhalika. Wakati THISDAY walipokua wakiandika kuhusu BoT, baadhi waliona kama "wana chuki" na hata kuhusu Mkapa wako waliosema Mengi ana chuki. Leo hii watu wameamini na kukubali BoT kuna tatizo. THISDAY waliandika mfululizo kuhusu Kagoda na hiyo ni baada ya gazeti la Serikali la Daily News kuanza kuandika na kuiachia njiani. Leo hii Kagoda na EPA imekua ajenda hata katika vikao vya juu vya CCM (Kamati KUU) na hotuba ya Rais ya Mwisho wa mwezi. Sasa THISDAY limeanzishwa na nani (Mengi) na wanalipwa kiasi gani hata wakashindwa kunuliwa na watu wanaoonja joto ya jiwe akina VITHLANI, Jeetu Patel na wengine. Sasa alieanzisha na kugharamia THISDAY munasema "anatafuta sifa na hastahili TUZO. Mulitaka tuzo apewa RA aliyeua RAI na Mtanzania? Munataka apewe MANJI kwa kusaidia YANGA? Munataka apewe Severe kwa kuuza vitalu vyetu vya mbuga kwa wageni? Munataka apewe nani? Hamuoni mabadiliko ya sasa katika mwamko wa Watanzania kutambua PUMBA na MChele yametokana na juhudi za magazeti? Hamuoni Mkapa kazidiwa na Chisano sababu ya THISDAY? Hamuoni jinsi wabunge na mawaziri wa CCM walivyozomewa majimboni na sasa wameshituka wameamua kuisema serikali? KAMA MUMEKEREKA AMA NI WAATHIRIKA WA HATUA ZA THISDAY POLENI SANA. HAMTAFANIKIWA KWANI WATANZANIA WAKO MACHO SANA