Raia wa Taifa
Member
- Jan 28, 2024
- 79
- 112
Benki ya NMB imetunukiwa Tuzo ya Benki Bora ya Biashara Ndogo na za Kati Tanzania kutoka Jarida la Kimataifa la Global Finance katika hafla iliyofanyika jijini London, Uingereza.
Mchakato wa kupata washindi wa Tuzo hizo za Benki Bora za Biashara kwa mwaka 2024 ulihusisha tathmini ya kina ya mawasilisho na tafiti huru, pamoja na maoni kutoka kwa wataalamu wa kisekta na wabobezi wa masuala ya biashara na teknolojia duniani.
Pamoja na mambo mengine, tuzo hii imetambua mchango wa NMB katika kuwawezesha wajasiriamali Tanzania kukuza biashara zao.
The Finance wanaitaja Benki ya NMB toka Tanzania kama Benki yenye kuwapa mikopo ya riba nafuu na kwa wakati wateja wake.
NMB wamekuwa wakimtoa Mikopo mbalimbali ikiwemo mikopo kwa biashara zinazomilikiwa na wanawake au ambazo huduma zake zinamgusa mwanamke, kupitia Hati Fungani ya Jasiri.
Wameitaja NMB kuwa ndio Benki inayowapa elimu ya fedha kuhusu ukuzaji wa biashara zao kupitia majukwaa ya Business Clubs, Business Executive Network na mengine mengi.
NMB imetajwa pia kuwa ndio Benki inadhamini sana Uwekezaji katika mifumo ya teknolojia inayowawezesha wateja kupata huduma za kifedha kwa urahisi na haraka kwa njia za kidijitali ikiwemo NMB Mkononi, NMB Direct, mikopo ya kidijitali isiyokua na dhamana (Mshiko Fasta), na huduma nyingine nyingi.
Tuzo hii imetolewa na Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Uhariri wa Jarida la Global Finance - Bw. Joseph Giarraputo na kupokelewa na Mkuu wetu wa Idara ya Biashara - Bw. Alex Mgeni, alieambatana na Maafisa Waandamizi kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza.
Itakumbukwa kuwa Benki hii kwa Sasa iko chini ya mwanamama wa Kitanzania Ms Ruth Zaipuna hivyo hatuwezi kushangilia ushindi huu wa kidunia bila kumtaja kiongozi huyu mchapakazi.
#GlobalFinanceAwards