Rais Samia anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Jukwaa la Kodi kitaifa lililoandaliwa na Wizara ya Fedha na Ofisi ya Rais Mipango

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Na. Saidina Msangi, WF, Arusha.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Jukwaa la Kodi kitaifa lililoandaliwa na Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji pamoja na Sekta Binafsi linalotarajiwa kukutanisha wadau mbalimbali wa kodi.

Hayo yameeelezwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bw. Elijah Mwandumbya, alipokutana na kuzungumza na waandishi wa Habari jijini Arusha, katika ukumbi wa Hazina Ndogo, kuhusu Jukwaa la Kodi na Uwekezaji Kitaifa 2024 linalotarajiwa kufanyika tarehe 27 - 28 Februari, 2024, katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

‘’Serikali imeshirikisha Sekta Binafsi katika hatua zote za maandalizi ikijumuisha ziara za Kikanda ambazo zilifanyika kuanzia tarehe 20 Novemba, 2023 hadi tarehe 07 Desemba, 2023 katika Kanda za Kaskazini (Arusha), Kanda ya ziwa (Mwanza na Shinyanga), Kanda ya Magharibi (Kigoma), Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (Mbeya), na Kanda ya Kusini (Mtwara)’’, alisema Bw. Mwandumbya.

Alisema kuwa Wizara ya Fedha ina jukumu la kuratibu upatikanaji wa maoni ya wadau, kuchakata maoni hayo na hatimaye kuwasilisha kwenye Kamati ya Ushauri wa Kodi mapendekezo mbalimbali ya sera za kodi yanayotarajiwa kufanyika katika mwaka wa fedha unaofuata.

‘’Kila mwaka Kamati hii imekuwa ikipokea maoni ya wadau, kufanya uchambuzi, na kufanikisha majadiliano ya masuala mbalimbali yanayohusiana na sera za kodi na usimamizi wake ambayo yamekuwa na mchango mkubwa kwetu waandaa sera na yamesaidia katika kuunda mfumo wa kodi ambao umewezesha utatuzi wa masuala mbalimbali ya kodi kwa ufanisi na uwazi’’, alifafanua Bw. Mwandumbya.

Bw. Mwandumbya aliongeza kuwa katika kupanua wigo wa kupata maoni ya wadau, Wizara ya Fedha ilianzisha Jukwaa la Kodi Kitaifa (National Tax Forum) mwaka 2023, ambalo kwa mara ya kwanza lilifanyika tarehe 11 Januari 2023, Jijini Dar es salaam, ambalo maoni yaliyopokelewa yalitumika katika maandalizi ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2023/24 inayotekelezwa hivi sasa.

Alifafanua kuwa Jukwaa hilo limeongeza ushirikishwaji wa sekta binafsi katika maandalizi ya Bajeti Kuu ya Serikali ambapo maoni yaliyotolewa yalilenga kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara na uwekezaji, kulinda viwanda vya ndani, kuvutia uwekezaji nchini na kuongeza ushindani wa viwanda vya ndani.

‘‘Baadhi ya maeneo yaliyofanyiwa kazi ni pamoja na kuongeza kima cha usajili wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kutoka shilingi milioni 100 hadi milioni 200; kuanzisha utaratibu wa kufanya marekebisho kwenye viwango vya ushuru wa bidhaa kila baada ya miaka mitatu kwa ajili ya utulivu wa kisera; kuondoa VAT kwenye malighafi zinazotumika kutengeneza vifungashio vya dawa pamoja na kuondoa ada ya ukaguzi kwenye madini yanayouzwa kwenye vituo vya kusafishia madini nchini’’, alifafanua Bw. Mwandumbya.

Aidha, Bw. Mwandumbya alitoa rai kwa wananchi kutumia fursa iliyotolewa na Serikali kwa kila mmoja kutoa maoni na kuwasilisha mapendekezo yake ya kuboresha sera za kodi na uwekezaji kupitia dirisha la kidigitali kwa ku-scan QR code iliyoambatishwa kwenye tangazo ambalo tayari linasambazwa kupitia mitandao ya kijamii.

Kauli Mbiu ya Jukwaa la Kodi na Uwekezaji Kitaifa mwaka huu ni " Mageuzi ya Sera za Uwekezaji, Ukusanyaji wa Mapato ya Ndani na Ukuaji wa Uchumi Jumuishi’’.
PIX-1b.jpg

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha bw. Elijah Mwandumbya, akizungumza na waaandishi wa habari katika Ukumbi wa Hazina Ndogo, jijini Arusha, kuhusu Jukwaa la Kodi na Uwekezaji Kitaifa 2024 linalotarajiwa kufanyika siku ya tarehe 27 - 28 Februari, 2024, katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, ambalo limeandaliwa na Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji pamoja na Sekta Binafsi.
PIX-2.jpg

Baadhi ya waandishi wa habari wakichukua matukio wakati wa mkutano na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bw. Elijah Mwandumbya, alipokutana na kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu Jukwaa la Kodi na Uwekezaji Kitaifa 2024 linalotarajiwa kufanyika siku ya tarehe 27 - 28 Februari, 2024, katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, katika ukumbi wa Hazina ndogo Jijini Arusha.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Arusha)
 
View attachment 2911202

View attachment 2911203

Mkumbushe kupaka mikorogo ili haonekane muarabu muarabu
 
Halafu TRA ondoeni ile kodi yenu ya wizi ya 10% mnayowakata wafanyabiashara kutegemeana na kodi yake ya pango anayolipa kwa mwenye nyumba.

Kwa mtazamo wangu, hii kodi ni wizi wa mchana! Sioni mantiki kwa mfanyabiashara kulipia 10% ya kodi ya pango anayolipa na wakati hiyo nyumba ya biashara aliyopanga, kila mwezi inatozwa 1500 ya kodi kupitia mita ya LUKU!

Acheni kuwaonea wafanyabiashara. Haiwezekani mumfanyie makadirio ya kodi na kulipa! Halafu mnamuongezea na 10% ya kodi anayolipia fremu/ofisi/jengo alilopanga!! Huu ni wizi, na pia ni kiashiria tosha cha kukosa ubunifu kwenye kutafuta vyanzo vipya na rafiki vya kodi.
 
Na. Saidina Msangi, WF, Arusha.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Jukwaa la Kodi kitaifa lililoandaliwa na Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji pamoja na Sekta Binafsi linalotarajiwa kukutanisha wadau mbalimbali wa kodi.

Hayo yameeelezwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bw. Elijah Mwandumbya, alipokutana na kuzungumza na waandishi wa Habari jijini Arusha, katika ukumbi wa Hazina Ndogo, kuhusu Jukwaa la Kodi na Uwekezaji Kitaifa 2024 linalotarajiwa kufanyika tarehe 27 - 28 Februari, 2024, katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

‘’Serikali imeshirikisha Sekta Binafsi katika hatua zote za maandalizi ikijumuisha ziara za Kikanda ambazo zilifanyika kuanzia tarehe 20 Novemba, 2023 hadi tarehe 07 Desemba, 2023 katika Kanda za Kaskazini (Arusha), Kanda ya ziwa (Mwanza na Shinyanga), Kanda ya Magharibi (Kigoma), Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (Mbeya), na Kanda ya Kusini (Mtwara)’’, alisema Bw. Mwandumbya.

Alisema kuwa Wizara ya Fedha ina jukumu la kuratibu upatikanaji wa maoni ya wadau, kuchakata maoni hayo na hatimaye kuwasilisha kwenye Kamati ya Ushauri wa Kodi mapendekezo mbalimbali ya sera za kodi yanayotarajiwa kufanyika katika mwaka wa fedha unaofuata.

‘’Kila mwaka Kamati hii imekuwa ikipokea maoni ya wadau, kufanya uchambuzi, na kufanikisha majadiliano ya masuala mbalimbali yanayohusiana na sera za kodi na usimamizi wake ambayo yamekuwa na mchango mkubwa kwetu waandaa sera na yamesaidia katika kuunda mfumo wa kodi ambao umewezesha utatuzi wa masuala mbalimbali ya kodi kwa ufanisi na uwazi’’, alifafanua Bw. Mwandumbya.

Bw. Mwandumbya aliongeza kuwa katika kupanua wigo wa kupata maoni ya wadau, Wizara ya Fedha ilianzisha Jukwaa la Kodi Kitaifa (National Tax Forum) mwaka 2023, ambalo kwa mara ya kwanza lilifanyika tarehe 11 Januari 2023, Jijini Dar es salaam, ambalo maoni yaliyopokelewa yalitumika katika maandalizi ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2023/24 inayotekelezwa hivi sasa.

Alifafanua kuwa Jukwaa hilo limeongeza ushirikishwaji wa sekta binafsi katika maandalizi ya Bajeti Kuu ya Serikali ambapo maoni yaliyotolewa yalilenga kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara na uwekezaji, kulinda viwanda vya ndani, kuvutia uwekezaji nchini na kuongeza ushindani wa viwanda vya ndani.

‘‘Baadhi ya maeneo yaliyofanyiwa kazi ni pamoja na kuongeza kima cha usajili wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kutoka shilingi milioni 100 hadi milioni 200; kuanzisha utaratibu wa kufanya marekebisho kwenye viwango vya ushuru wa bidhaa kila baada ya miaka mitatu kwa ajili ya utulivu wa kisera; kuondoa VAT kwenye malighafi zinazotumika kutengeneza vifungashio vya dawa pamoja na kuondoa ada ya ukaguzi kwenye madini yanayouzwa kwenye vituo vya kusafishia madini nchini’’, alifafanua Bw. Mwandumbya.

Aidha, Bw. Mwandumbya alitoa rai kwa wananchi kutumia fursa iliyotolewa na Serikali kwa kila mmoja kutoa maoni na kuwasilisha mapendekezo yake ya kuboresha sera za kodi na uwekezaji kupitia dirisha la kidigitali kwa ku-scan QR code iliyoambatishwa kwenye tangazo ambalo tayari linasambazwa kupitia mitandao ya kijamii.

Kauli Mbiu ya Jukwaa la Kodi na Uwekezaji Kitaifa mwaka huu ni " Mageuzi ya Sera za Uwekezaji, Ukusanyaji wa Mapato ya Ndani na Ukuaji wa Uchumi Jumuishi’’.
View attachment 2911202
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha bw. Elijah Mwandumbya, akizungumza na waaandishi wa habari katika Ukumbi wa Hazina Ndogo, jijini Arusha, kuhusu Jukwaa la Kodi na Uwekezaji Kitaifa 2024 linalotarajiwa kufanyika siku ya tarehe 27 - 28 Februari, 2024, katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, ambalo limeandaliwa na Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji pamoja na Sekta Binafsi.
View attachment 2911203
Baadhi ya waandishi wa habari wakichukua matukio wakati wa mkutano na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bw. Elijah Mwandumbya, alipokutana na kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu Jukwaa la Kodi na Uwekezaji Kitaifa 2024 linalotarajiwa kufanyika siku ya tarehe 27 - 28 Februari, 2024, katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, katika ukumbi wa Hazina ndogo Jijini Arusha.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Arusha)
Alete eme
 
Back
Top Bottom