Mchungaji Gwajima: Daudi Albert Bashite alipata division Zero

Mchungaji Gwajima: Daudi Albert Bashite alipata division Zero

Hivi hatuwezi kupata link ama source yoyote yenye kuwa matokeo kipindi ambacho mh. anamaliza kidato cha nne ili tuione, naamini jamii forum kuna watu wengi na waina mbali mbali, yeyote ambaye analink ama source ya matokeo ya kidato cha nne ya pamba sec aiweke , maana katika hili nakumbuka kale kamsemo maalufu cha mh. Raisi Mstahafu JK... wapili...


ili kumaliza mzizi wa fitna mwenye source ama matokeo hata kwa picha ayapige tuyaone na tumtafute huyo daudi Bashite kama kweli alikuwapo na aliscore zeo.

Ni vema kuweka matokeo ya Pamba secondari hapa kama walivyoweka ya mhe Ole Sendeka ya kitado cha sita(form six) kumbuka mwanafunzi hawezi kwenda form five kama hana minimum ya credit tatu at least C tatu at the same time lazima kuwa na at least pass tatu/tano level ya D ili kuruhusiwa kwenda for certiface course ya aina yeyote na certicate ni lazima kupata wastani wa B ili kuendelea na Diploma course then Degree course, kwa hiyo kama alienda degree course kwa kutumia form four results za F masomo yote ni lazima kunyanganywa shahada yaani kufutwa na chuo husika na apelekwe mahakamani sheria ifuate mkondo wake!!hapa kazi tu!!!!
 
Sijawah kuona kiongozi wa kiroho asiyejitambua Kama gwajima. Ulimwengu unazid kuchafuka yeye Kama kiongozi wa kiroho badala ya kuhubiri watu waache maovu(dhambi) zao wampokee na kumkiri kirsto katuma maisha yao ili yesu akirudi waokolewe. Yeye amekomaa na mambo ya kipuuzi kabisa

Wewe ni kundi la wanaotumia vyeti feki au vyeti vya wengine possibly!! However ninashangaa kwa nini waliofanya vetting ya Makonda kwanini walimficha Rais madhambi hayo? Possibly kuchafua jina na utawala wa Rais Magufuli.
 
~~~>>>>Hayo ni maneno ya kujifariji tu... Uwe umesoma kwa kuunga unga ama lah... hata ikiwa hujasoma mwisho wa siku tunaangalia "Una nini".

Una vyeti vyenye A lkn ukisikia Makonda anakuja ofisini kwako unaanza kujijambia jambia....

Una vyeti vyenye A kibao lkn unapanga foleni dukani kwa Mangi aliyeishia darasa la 7 ili umkope ulipe mwisho wa mwezi...


Bado kwangu naona Makonda nimpambanaji... Kuwa jambo alikutana na changamoto za Shule ila alitambua kuwa maisha hayahitaji vyeti... Jamaa akapambana na ametoboa kweli.


Hongera sana Makonda...
 
Wanabodi!

Nawasilisha kwenu baadhi ya misemo ambayo itakusaidia maishani mwako baada ya hili sakata la bashite.

1. Chokochoko mchokoe pweza mwanadanu huto muweza.

2. Ukiweka ugoko sisi tunaweka jiwe
3. Mdomo aulimponza kichwa
4. Hakuna lenye mwanzo lisilo na mwisho
5. Asiefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu


Weka misemo mingine jamii ipate kujua kwamba wahenga waliona mbali.

Karibu.
 
We we na aliemteua nani anamfahamu vizuri?!

Hata Mungu alikuwa/ana upendeleo ndo maana kamtukuza mwanaye Yesu! Ila kwa Rais Dr Magufuli, jamaa kapotea step, sheria itachukua mkondo wake na sasa kama wale wa kuhakiki vyeti hawajafanya kazi wamepigwa ganzi, Rais ataanza nao then Daudi afuate!
 
Ili upate uongozi Tanzania unatakiwa ujue kusoma na kuandika tu,Msimchoshe Makonda,elimu yake inamtosha

Iddi Amin Dada alimaliza darasa la nne(std IV) yaani grade four lakini kawa Rais wa Uganda kwa zaidi ya miaka nane and notably he was ruthless kama Makonda alivyo ruthless kwa wafanyakazi na waziri mkuu mfaafu Warioba na kusema akisimama mahali ni Mungu kasimama! Sikiliza audio yake kwenye mitandao!
 
Hili nalo ni kosa tu, hamna cha form four au drs la saba wote wamewadhulumu maskini hao wenye majina
Mwigulu hakutumia cheti cha mtu. jina unaeza badili hata kesho ni kias cha kwenda kuapa mahakaman au kwa mwanasheria.

ila kutumia cheti cha mtu? yaan mwenye cheti aende form 5 wewe ukitumie kwenda soma diploma/certificate hili ni kosa tena la Jinai
 
Kila mtu anaona jinsi RC wa Dar es Salaam anavyotapatapa kwa Viongozi wa Dini. Jambo hili Manji alilisema kwenye press conference yake kwamba Makonda alipaswa kutafuta Viongozi wa Dini wamsaidie kabla hajakurupuka.

Matokeo yake ameona umuhimu huo baada ya kuwa aneshaharibu. Binafsi naona Manji ana afadhali kukaa mahabusu kuliko unaetangatanga kwenye makanisa, misikiti, mabaraza ya viongozi wa dini na mabudha wa kihindi.

Maana yake ni kwamba, miungu imeshamkataa hivyo anakimbia huku na huko. Kiuhalisia, ulimwengu wa roho haufungamani...yani maombi ya waislamu, mapdri na mashehe wa kibudha eti yajumuishwe kizaliwe kitu chema k.v. ulinzi, amani ya nafsi n.k.

Makonda ameharibu maisha yake mwenyewe.


OVA.
 
Back
Top Bottom