Mchungaji Gwajima: Daudi Albert Bashite alipata division Zero

Wakubwa poleni sana na kazi,

Napenda niwakumbushe jambo moja lililowahi kutokea hapa Tanzania na kuvuta hisia za watu wengi ndani na nje ya nchi. Mchungaji Mwasapile Almaarufu babu wa Samunge aligundua dawa ya miti shamba iliyodhaniwa kuwa inatibu magonjwa mengi ukiwemo UKIMWI.

Watu wengi walikwenda kupata tiba hiyo iliyokuwa ikihusisha unywaji wa dawa kwenye Kikombe. Kimsingi watu wengi waliamini na baadhi yao walikatisha dozi zao za madawa waliyopewa mahospitalini.

Wengi walikufa kutokana na kukatisha dozi. Swala la mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar bwana Makonda na kazi anayofanya kwa manufaa ya wananchi itadumu katika mioyo ya wenye kuhitaji ila wenye kubeza kwa ajili ya kuguswa na kazi hizo watavuma kwa muda mfupi na kisha kusahaulika.

Uteuzi ulipofanyika kwamba Makonda awe RC wabaya wake kwanini hawakuyasema haya ya Bashite? Kwanini sasa?

Nawaomba wananchi wote wenye dhamira ya dhati kuweza kumaliza janga hili la madawa ya kulevya tushikamane na Mkuu wetu wa nchi na viongozi wengine wenye kulitakia mema taifa hili. Muda si mrefu huu upepo wa madai yasiyo na vielelezo utazimika kama Mzee wa Kikombe, a.k.a Mwasapile.
Hili lishaisha ndugu we unadhani bado lipo..
 
Hili la Daud Bashite ni funzo,ni elimu,ni darasa tosha kwetu sisi na hata watoto tunaowalea na kuwatunza.Sasa hata mtoto anayelegalega au anayegoma kusoma shule anatishiwa,kwamba "We zembea tu yakukute ya Daudi Bashite",

Tuchukue tukio hili kama funzo na shukrani kwa Mungu,kwetu sisi au kwa watoto wetu waliosoma na kujaliwa kufuata mtiririko sahihi wa elimu bila "bashitelism".Sisi tulio watu wazima,tuwashukuru sana wazazi na walezi wetu.

Tuwashukuru wale wote ambao kwa majitoleo yao na nguvu zao,mali zao na hali zao walituwezesha kusoma na kufikia malengo yetu.Kuna tuliosomeshwa na wamama wauza gongo,tulisomeshwa na wamama wauza vitumbua,wamama waosha samaki mwaloni na hata mama lishe.Kuna akina Mama walioamua kufanya vibarua vya kuvuna ktk viwanda vya kahawa na chai,ili watoto waende shule.

Sio kwamba walikuwa wasomi sana,lkn kwa ukubwa wa umri na ung'amuzi wao juu ya changamoto za maisha,walibaini shule ndio njia pekee ya urithi usio na dhihaka.Wengi hawakutoka ktk familia za wafanyabiashara,wala za wakulima wakubwa(Peti bujwazii),wala zile za wafanyakazi wa kati na juu,bali familia za kipato cha "kilimo cha mkono kwenda mdomoni"

Hakika shule sio njia ya moja kwa moja kufikia mafanikio ya kiuchumi,lakini ni mtaji na silaha ya kijana wa familia duni kuanzia hatua ya kwanza kwenda ya pili.Tuwahimize watoto wetu kuwa na elimu dunia ambayo ni msingi wa ziada kufikia uhuru wa kifikra na kuepuka unyanyasaji wa kitaaluma.

Tuwakumbuke wale wote waliojitolea kwa ajili yetu,waliotutia moyo wakati ule wa "foolish age" ambapo hatukujua umuhimu wa elimu.Tuwaombe radhi wale wote tuliowachukia sbb walitaka tutimize wajibu wetu darasani na nje ya darasa.Walimu tuliowaona wakuda na wanoko,walezi tuliowaona wambea kwa kufuatilia maendeleo yatu ya shule.Hawa wote wanastahili shukrani.

"Bashitelism" isikie tu kwa jirani.Inafifisha kujiamini,inadidimiza heshima kwa wote wanaokuzunguka,inaondoa furaha na kupoteza moyo wa ujasiri kukemea makosa yanayohusiana na taaluma au uweledi.Bashistelism inazima moyo wa kiuongozi na kiutawala ndani ya nafsi ya mtu.

Tuwashukuru pia hata "vipanga" waliojitolea kutufundisha au kudesa wakati wa majaribio na mitihani.Wale walioshindwa kwenda "tuition" miaka hiyo,kuna walituletea madesa toka Mzumbe,Tabora Boys,Kibaha na Ilboru,Kilakala,Msalato na Weruweru.Hawa wote walituokoa na "Bashitelism".

Tunaweza tusiwalipe pesa au mali zisizohamishika wale wote waliotuokoa.Lakini moyo wa shukrani na kuwaenzi ktk kipindi hiki cha sakasaka la Basheti ni malipo tosha juu ya mchango wao.Shule haiongopi,isipokushuhudia leo,itakuokoa kesho.

Tujitahidi kuwaepusha watoto wetu na njia za mkato,hii inaweza kulipuka wakati sisi tukiwa mavumbini na kuwaachia simanzi,maana maamuzi mengi yanayoakisi "kesho" ya watoto wetu hufanyika wakiwa chini ya umri wa utu uzima wa miaka 18.Wasije wakajuta....

Hata kwa kuuza mbuzi na kuku,tuwekeze kwa vijana wetu.Tuepuke njia za mkatomkato.
 
Mtu anafeli kuanzia mtihani wa darasa la nne,lazima alikuwa mtoro wa shule au laaa, kwa kuwa alizaliwa mtoto pekee kwao basi akawa yai, kudekadeka,akiguswa na walimu/watoto wenzie wazazi wanakuja juu,akiamua kulala tu asiende shule,hachapwi.

Watoto wanaozaliwa peke yao pia wana tabia za kusingizia wenzao sana na kutokana na shida alizopata katika kutafuta elimu,wanachukia sana waliokuwa vipanga
 
Wakubwa poleni sana na kazi,

Napenda niwakumbushe jambo moja lililowahi kutokea hapa Tanzania na kuvuta hisia za watu wengi ndani na nje ya nchi. Mchungaji Mwasapile Almaarufu babu wa Samunge aligundua dawa ya miti shamba iliyodhaniwa kuwa inatibu magonjwa mengi ukiwemo UKIMWI.

Watu wengi walikwenda kupata tiba hiyo iliyokuwa ikihusisha unywaji wa dawa kwenye Kikombe. Kimsingi watu wengi waliamini na baadhi yao walikatisha dozi zao za madawa waliyopewa mahospitalini.

Wengi walikufa kutokana na kukatisha dozi. Swala la mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar bwana Makonda na kazi anayofanya kwa manufaa ya wananchi itadumu katika mioyo ya wenye kuhitaji ila wenye kubeza kwa ajili ya kuguswa na kazi hizo watavuma kwa muda mfupi na kisha kusahaulika.

Uteuzi ulipofanyika kwamba Makonda awe RC wabaya wake kwanini hawakuyasema haya ya Bashite? Kwanini sasa?

Nawaomba wananchi wote wenye dhamira ya dhati kuweza kumaliza janga hili la madawa ya kulevya tushikamane na Mkuu wetu wa nchi na viongozi wengine wenye kulitakia mema taifa hili. Muda si mrefu huu upepo wa madai yasiyo na vielelezo utazimika kama Mzee wa Kikombe, a.k.a Mwasapile.

Kama Bashite na Makonda ni mtu mmoja wembe ni ule ule. Bashite/Makonda anafanya kazi kwa niaba ya watanzania na anaonyesha uchungu alionao kwa nchi yake. Wauza unga si watu wa kuwabeza, ni wauwaji na waangamizi wa jamii popote pale duniani....si wa kuwachekea kabisa. Wanafanya maovu kwa faida yao na familia zao si kwa watanzania, hivyo ni lazima wampinge yeyote yule atakayekemea vita dhidi ya madawa ya kulevya awe Bashite/Makonda au hata wewe. Tumuunge mkono mkuu wetu wa mkoa kwa vita hivi.
 
Hao watu wawili sijawai wapenda

Naona unga ulikusaidia kuendesha maisha yako ya kila siku hapa mjini. Na bado sana, mtakamatwa mpaka mrudi vijijini mnakotoka. Tunataka Tanzania safi si ya wababaishaji, unataka ubabaishaji nenda Chadema wakunadi.
 
Mtu anafeli kuanzia mtihani wa darasa la nne,lazima alikuwa mtoro wa shule au laaa, kwa kuwa alizaliwa mtoto pekee kwao basi akawa yai, kudekadeka,akiguswa na walimu/watoto wenzie wazazi wanakuja juu,akiamua kulala tu asiende shule,hachapwi.

Watoto wanaozaliwa peke yao pia wana tabia za kusingizia wenzao sana na kutokana na shida alizopata katika kutafuta elimu,wanachukia sana waliokuwa vipanga
Duuuh!!!Mkuu unaua band
 
Wakubwa poleni sana na kazi,

Napenda niwakumbushe jambo moja lililowahi kutokea hapa Tanzania na kuvuta hisia za watu wengi ndani na nje ya nchi. Mchungaji Mwasapile Almaarufu babu wa Samunge aligundua dawa ya miti shamba iliyodhaniwa kuwa inatibu magonjwa mengi ukiwemo UKIMWI.

Watu wengi walikwenda kupata tiba hiyo iliyokuwa ikihusisha unywaji wa dawa kwenye Kikombe. Kimsingi watu wengi waliamini na baadhi yao walikatisha dozi zao za madawa waliyopewa mahospitalini.

Wengi walikufa kutokana na kukatisha dozi. Swala la mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar bwana Makonda na kazi anayofanya kwa manufaa ya wananchi itadumu katika mioyo ya wenye kuhitaji ila wenye kubeza kwa ajili ya kuguswa na kazi hizo watavuma kwa muda mfupi na kisha kusahaulika.

Uteuzi ulipofanyika kwamba Makonda awe RC wabaya wake kwanini hawakuyasema haya ya Bashite? Kwanini sasa?

Nawaomba wananchi wote wenye dhamira ya dhati kuweza kumaliza janga hili la madawa ya kulevya tushikamane na Mkuu wetu wa nchi na viongozi wengine wenye kulitakia mema taifa hili. Muda si mrefu huu upepo wa madai yasiyo na vielelezo utazimika kama Mzee wa Kikombe, a.k.a Mwasapile.
Wapiiii safari hii watashaaa yani ... mwanzo mwisho siku litakapokwisha ni siku Bashite atakapo tuachia kiti pale ilala Boma ...
 
Naona unga ulikusaidia kuendesha maisha yako ya kila siku hapa mjini. Na bado sana, mtakamatwa mpaka mrudi vijijini mnakotoka. Tunataka Tanzania safi si ya wababaishaji, unataka ubabaishaji nenda Chadema wakunadi.
Hivi ushasikia zmekamatwa kilo ngapi..??
 
Mchungaji Gwajima wewe ni Mtumishi baba unahubiri upendo mara kwa mara na ndiyo kazi yako kuu.

Mimi nakuomba MSAMEHE MH. MAKONDA Saba Mara Sabini ( 7*70 = 490). Naamini umekutana na mengi katika maisha yako na bado mengi utakutana nayo. Kwa heshima ya nafasi yako naona haipendezi kumnanga mtu jukwaani hivyo kama wewe ni wanasiasa vile. Acha yapite Mungu wako atakulia kwa maana "Haki ya mtu haipotei" ila inacheleweshwa tu.

Samehe kwa heshima ya kazi yako ya Utumishi itakuwa ni baraka kubwa kwako na kwa Mungu wako unayemuamini. Ahsante.
 
Back
Top Bottom