Mchungaji Gwajima: Daudi Albert Bashite alipata division Zero

Mchungaji Gwajima: Daudi Albert Bashite alipata division Zero

Mkuu, Mwigulu alisoma Ilboru form one to four na akaibuka na div three akaendelea na advanced level (EGM) pale Mazengo sec. enzi hizo. Mwigulu kosa lake ni kutumia jina la mwenzake pale alipotaka kuendelea darasa la sita baada ya kutoroka shule.

Ila huyu Makonda alilaghai cheti cha mtu cha form four akakitumia kama ngazi kuendelea na chuo. Kimsingi Makonda anatakiwa awe amekamatwa mpaka sasa (Makonda halisi na Daudi wote wawili wakamatwe ili wajibu tuhuma)
 
Lakini huyu kijana aliekua machachari ghafla amekua mkimya sana siku za sasa
Screenshot_20161221-100955.png
 
*CV YA PAUL MAKONDA*

1. Alizaliwa tar.15/02/1981 katika kijiji cha Koromije, wilaya ya Misungwi, mkoa wa Mwanza.

2. Majina yake halisi ni *Daudi Albert Bushite*

3. Alianza darasa la kwanza mwaka 1988 katika shule ya msingi Koromije akitumia majina ya *Daudi Albert Bushite*. Mwaka 1991 alifeli darasa la 4, akarudia.

4. Mwaka 1992 alifeli tena na hivyo akahamishiwa Mwanza mjini, ili aweze kusoma na kupata masomo ya jioni (tuition).

5. Mwaka 1996 alihitimu darasa la 7 lakini hakuchaguliwa kuendelea na elimu ya sekondari katika shule ya serikali.

6. Mwaka 1997 akajiunga na kidato cha kwanza shule ya sekondari ya Pamba.

7. Mwaka 2000 akahitimu kidato cha 4 na kupata daraja sifuri (division zero).

8. Mwaka 2001 akatumia cheti cha Ndg.Paul Christian Muyenge (chenye div.3 ya points 25) kujiunga na chuo cha uvuvi Nyegezi (Nyegezi Fisheries Training Institute) kwa masomo ya Certificate akahitimu mwaka 2002.

9. Mwaka huohuo 2002 akitumia cheti cha *Ndg.Paul Christian Muyenge*, alijiunga na Chuo cha uvuvi Mbegani Bagamoyo kwa masomo ya Diploma ya uvuvi (ORDINARY DIPLOMA IN MASTER FISHERMAN, NTA LEV.6), na kuhitimu mwaka 2005.

10. Mwaka 2003 alikutana na Ndg.Benjamin Sitta (mtoto wa Marehemu Samwel Sitta, ambaye ni Mayor Kinondoni kwa sasa). Wakawa marafiki.

11. Mwaka 2005 baada ya kuhitimu Stashahada yake ya uvuvi, aliomba admission Chuo cha Kilimo Sokoine kusoma shahada lakini akakosa nafasi.

12. Baada ya kukosa nafasi alienda kuishi nyumbani kwa Marehemu Sitta akiwa kama rafiki wa Ben (mtoto wa Sitta). Kwakuwa alitoka familia duni, Sitta aliahidi kumsomesha elimu ya juu.

13. Mwaka 2006, alipata udahili Chuo cha ushirika na biashara Moshi (wakati huo kikiwa chuo kikuu kishiriki cha SUA), kwa kutumia vyeti vyake vya certificate (ya Nyegezi) na diploma (ya Mbegani).

14. Alidahiliwa kwa course ya BA in Cooperate Management &Accounting. Mwaka 2007 alimaliza first year lakini akashindwa kuendelea na 2nd year baada ya kupata Suplementary 6 kati ya Course 8 alizokua akisoma (akawa discontinued).

15. Mwaka huohuo 2007 akaomba Admission upya. Akamaliza first year akiwa na _carries 3_ ambazo alienda nazo 2nd year. Mwaka 2008 akiwa 2nd year akapata supplementary 4 kati ya course 8 alizokua akisoma. Akawa na mzigo wa _carry over_ na _supplementary_. Akaamua kuacha chuo.

16. Mwaka 2008 akaenda kujaribu kuomba udahili chuo kikuu SUA kwa mara nyingine lakini akakosa.

17. Mwaka 2009 akarudi tena MUCcoBS kwa udahili mpya. Akaachana na CMA akachagua Community &Economic Development (CED).

18. Mwaka 20012 akahitimu shahada ya kwanza ya Community &Economic Development kwa jina la *_Paul C Makonda_* badala ya majina yake halisi ya *_Daudi A Bushite_*

19. Jina *_Makonda_* analitumia baada ya kula kiapo mahakamani kubadili jina. Cheti cha Form four kinasomeka *_Paul C Muyenge_* lakini vyeti vya elimu ya juu vinasomeka *_Paul C Makonda_* baada ya kuapa mahakamani.

20. Ndugu Daudi Albert Bushite ameoa (tangu mwaka 2009) lakini hajabahatika kupata mtoto. Na ndiye mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kwa sasa.
*********Nawasilisha********
Ova
 
Sijui huyu mtuhumiwa ana nini ambacho ni spesheli!!!
Hermaphrodite labda? Kwa hiyo anaweza kuwa Kimada wa Mtu na asistukiwe? May be sababu ni hivyo, vinginevyo kuna faida gani ya kumkigia Kifua Buffoon kama huyu?
 
ziro wanapewaga vyeti?
miaka ya zaman walikuwa wanapewa, baada ya ndalichako kuanza kuwa Katibu Mtendaji wa baraza, huku mwenyekiti wake akiwa Prof Mkandala, ndio wakasitisha hyo huduma...

fuatilia kwenye familia yako huko nyuma utakuta kuna ndugu anacho, kama hakuna kabisa
 
Clouds walikuwa bize na Kili Marathon. Naamini muda si mrefu watatoa fursa kwa mkuu kuweka kumbukumbu sawa na wauza madawa watatulia...raha!
 
Cheti cha zero hakipatikani Ndio sababu hata CCM wakisema Mbowe Ana zero ya form six huwa hawa semi cheti wanacho. Ukiwa Miongo uwe na Kumbukumbu.


Wekeni hadharani hayo Matokeo halisi ya Makonda na ya kughushi!

Mtu Mwenye akili akisikiliza vizuri hiyo audio utasikia namna ya usanii wa Gwajima kwa mfano anajiepusha kwa kutumia Maneno Kama vile a Wana Yule au Kiumbe Yule au kujifanya kasahau Jina la Makonda then Waumini ndio wanataja kwa Sauti then yeye anaendelea kutoa Maelezo. Huu ni aina ya Uongo ambao unausambaza kwa Njia za Ujanja ujanja ili usiingie kwny Mikono ya Vyombo vya sheriay
Naona imwaeingia!

Tulieni itakatikia
 
Mkuu, Mwigulu alisoma Ilboru form one to four na akaibuka na div three akaendelea na advanced level (EGM) pale Mazengo sec. enzi hizo. Mwigulu kosa lake ni kutumia jina la mwenzake pale alipotaka kuendelea darasa la sita baada ya kutoroka shule.

Ila huyu Makonda alilaghai cheti cha mtu cha form four akakitumia kama ngazi kuendelea na chuo. Kimsingi Makonda anatakiwa awe amekamatwa mpaka sasa (Makonda halisi na Daudi wote wawili wakamatwe ili wajibu tuhuma)
Mwigulu hakutoroka shule, alifeli darasa la saba kisha akanunua jina la mwanafunzi darasa la...... Ili apate nafasi tena ya kufanya mtihani wa darasa la saba.

Hili ni kosa kikanuni.
Kama vipi atupishe tu na yeye.
 
Mwigulu mitihan yote kuanzia la saba mpaka chuo alifanya mwenyewe. tatizo kipind ambacho aliacha shule darasa la tano na kurudi ndo chenye utata
 
Mwigulu mitihan yote kuanzia la saba mpaka chuo alifanya mwenyewe. tatizo kipind ambacho aliacha shule darasa la tano na kurudi ndo chenye utata
Hili nalo ni kosa tu, hamna cha form four au drs la saba wote wamewadhulumu maskini hao wenye majina
 
Audio ya Askofu Gwajima hii
Hatimaye katuni ya Gado inaanza kupata maneno taratiibu.

Hapa namnukuu Askofu Gwajima mwisho mwishoni
"..... Sijui anaitwa Paul Christian Mananiliii....
..... hapa iko ishuuu....... nitashangaa shangaaaa, nitasema Mbona JIPUU kubwa namna hii, tena liko usoni HAPA KAMA TOCHIII, kwanini halitumbuliwi???"
1cdf6b1612444ce5c2086e63e2a44483.jpg
 
Back
Top Bottom