Mchezo: 'Niongezee Sentensi' – Hadithi Hai ya Mtaa na Taifa

Mchezo: 'Niongezee Sentensi' – Hadithi Hai ya Mtaa na Taifa

Emmy na Zara wakaingia kwa kasi ndani ya Club kumfuata Tjedi na kumkuta akiwa amesimama peke yake ndani ya ofisi ya Mukheef anashangaa akiangaza huku na kule kuashiria anamtafuta Mukheef.

"Yule dada... wa Crown nyeupe aliyetupa lift... yupo nje!" Emmy aliongea kwa sauti yenye hofu na woga.

"Haiwezekani..." Tjedi alitoka haraka na kwenda kwenye chumba chenye mitambo ya CCTV kuhakikisha, akamwona yule mwanamke akiwa amesimama nje ya gari yake huku akivuta sigara na pia akiwa ameweka simu kwenye masikio.

"Nifuateni" Tjedi aliwaambia Emmy na Zara kisha akaelekea kwenye mlango wa dharura, kitendo cha kufungua mlango wakashtuka.Kila mtu alipigwa na bumbuazi baada ya kuona Toyota ALPHARD mbili na majambazi zaidi ya nane wamejipanga na bunduki zao, tayari kwa kuachia risasi.

“Tulieni hivyo hivyo pigeni magoti” mmoja wa majambazi akasema.
Hiyo ilifanya Zara, Emmy pamoja na Tjedi wote wapige magoti kusalimu amri.Hakukua na chaguo lingine zaidi ya hilo kwani majambazi waliwazingira kila pembe wakiwa na bunduki zilizojaa risasi za kutosha. Majambazi watatu wakasogea karibu na kuwainua kisha kuwafunga kamba kwa nyuma,haraka wakakokotwa mpaka kwenye ALPHARD. Hakukua na maongezi zaidi ya majambazi kuingia ndani kisha zile ALPHARD zikatoka kwa kasi ya ajabu na crown ya yule mwanamke aliyekuwa nje ya Club nayo ikaunga nyuma. Ulikua ni ushindi mkubwa kwa majambazi na walijisifu kwa hilo. Wakiwa njiani kiongozi wa wale majambazi akatoa simu akapiga kwa boss wake kutoa taarifa ya kuwakamata Tjedi, Zara pamoja na Emmy.

"Mkuu kazi imekamilika, mtoto wa bwana aesh, mlinzi wake pamoja na mwanamke mwingine ambaye hatujajua ni nani wapo chini ya himaya yetu na tupo njiani tunaelekea kambini".Aliongea yule jambazi kwa sauti iliyodhihirisha furaha na ushindi.
"Wanaotakiwa ni wawili tu binti yake na mlinzi huyo mwingine hatuhusu, mpotezeni" ilisikika sauti nzito ya kuamuru kwenye simu
"Sawa Mkuu" alijibu kiongozi wa majambazi

Ghafla bila kufikiria mara mbili mlango ulifunguliwa huku gari likiwa kwenye mwendo kasi kisha jambazi mmoja akamshika Emmy kwa nguvu akamtupa nje, mwili wake ukabilingita mpaka kando ya barabara ukatulia, haikujulikana kama bado yupo hai.

Tjedi hakuamini alichokiona, hasira zilimjaa alijilaumu sana, aliangaza na hakukua na upenyo wowote wa kutoroka. Mawazo mengi yalipita, alijisikia uchungu sana juu ya Emmy hakujua kama atakuwa bado yupo hai au Lah. Akiwa katika mawazo mazito, wakiwa wamekaribia pori la madale ghafla, kikasikika kishindo kikubwa cha mlipuko. ALPHARD ya mbele ilirushwa hewani lilikua ni kombora aina ya RPG. Ni tukio lililofanya Majambazi na bunduki zao washushe vioo vya gari na waanze kurusha risasi hovyo, hawakukaa sawa.Likapigwa kombora lingine CROWN lililokuwa nyuma likasambaratishwa. Upande wa kushoto likatokea gari aina ya Toyota HIACE, mlangoni wamesimama wanaume warefu waliojazia na mkononi wameshika silaha hatari aina ya AK47,kitendo cha kuachia risasi Majambazi wote waliobaki walikua wanatupwa mbali na kudondoka kama kuku wenye mdondo. Hali ilivyokua shwari kidogo wanaume sita wakashuka wakiwa na vitambaa usoni kuziba sura zao.Wakaingia mpaka ndani ya gari alilokuwepo Tjedi na Zara, wakafunikwa vitambaa vyeusi na kuanza kuwaburuza mpaka kwenye HIACE.Jinsi gari ilivyogeuzwa ilitishia amani,ilitimua vumbi na kutoka kwa kasi ya kimondo.

Sio Tjedi wala Zara kila mtu alikua katika hali ya sintofahamu,hofu iliwatanda na kujua tayari wanaenda kufa kwani watu hao walikua hatari sana zaidi ya majambazi wa mwanzo.Hakuna mtu yoyote aliyezungumza isipokua gari ilitembea zaidi ya masaa matatu barabarani waliamini kabisa kwa masaa waliyotembea ni lazima wangekua nje ya mji tu!Lisaa limoja lingine ndipo taratibu gari likaanza kusimama na kupaki kando.Mlango wa TOYOTA HIACE ukafunguliwa.

“Wafungueni kamba na vitambaa usoni”

Sauti hiyo ikasikika jamaa huyo akasema akiwa na kitambaa cheusi,Tjedi na Zara wakafunguliwa kamba na vitambaa vyeusi usoni vilivyokua maalum ili wasione ni wapi wanaenda.Mbele yao kulikua na wanaume wanne waliopanda hewani na kujazia miili yao.Walivyoangalia nje,wakaona gari aina ya Subaru legacy inakuja kwa kasi kisha kupiga breki mbele ya Toyota HIACE, mtu waliyemuona anashuka aliwashangaza sana.Sio Tjedi wala Zara kila mtu alipigwa na bumbuazi.

“Mukheef” Thedi,akaita kwa sauti ya mshangao!

“Tjedi hatuna muda wa kupoteza,nimetumwa na Bwana Aesh”

“Umetumwa nini?”

“Anataka muende London,passpoti zenu hizi hapa.Helkopta itawachukua na kuwapeleka mpaka nchini kenya huko mtachukua Ndege”

Mukheef alizungumza akiwa makini huku akiwa na hati mbili feki za kusafiria,akamkabidhi Zara na Tjedi.

“Na vipi kuhusu Emmy ambaye sijui kama yupo hai na vipi familia yangu?” Tjedi aliuliza maswali mfululizo kwa mshangao na hasira.

“Tjedi Emmy yupo hai na salama amepata majereha madogo na sasa yupo hospitali anaendelea vizuri, kwa sasa hivi,inabidi uondoke mengine baadaye mambo yakitulia.Haitakiwi mtu yoyote kujua mlipo kwa usalama wa emmy na wako, vita uliyoingia ni kubwa.”

“Mukheef,asante sana.Hakikisha Emmy anakua salama” alijibu Tjedi

“I promise you…Ongea na Bwana Aesh”

Simu ikapigwa hapohapo,Bwana Aesh akapokea simu na kuzungumza na Tjedi pamoja na Zara.!

“Tjedi,nakutakia kila la kheri mlinde mwanangu kwa uwezo wako wote”

“Ukifika London mtafute mtu mmoja anaitwa Nikolai Vostrikov,atakupokea kuna baasha amekupa Mukheef itakuelekeza mji utakaofikia.Maagizo mengine nishampa Nikolai Vostrikov”

"Sawa" Tjedi alijibu kisha akampa simu Zara ambaye alishindwa kuongea zaidi ya kububujikwa na machozi.

Simu ikakatwa.Dakika tano baadaye,mlio wa helkopta ukasikika. Taratibu Helkopta ikaanza kutua mpaka ardhini huku vumbi kali likitimka. Zara na Tjedi wakapanda. Taratibu ikaanza kuinuka juu huku Tjedi akiangalia chini na kumpungia Mukheef kwa ishara ya kumuaga,Mukheef akabaki chini mpaka alivyohakikisha Helkopta imepotea kwenye upeo wa macho yake!

----------------------
--DAR ES SALAAM, USIKU WA JANA--
Baada ya gari aina ya Toyota HIACE kuwavamia majamba kwa RPG kisha kuwachukua Tjedi na Ziara na kutokomea nao kusikojulikana, Gari aina ya Subaru LEGACY ilifunga breki eneo la tukio, akashuka Mukheef na alionekana kuwa makini kuamgaza na kuchukua mabaki ya vitu kadhaa yaliyoonekana kama mabaki ya makombora na kuyaweka kwenye buti la gari yake kisha akaanza kuzipanga maiti za majambazi kwenye magari yao ambapo alihamisha maiti ya kike iliyokuwa ndani ya CROWN nyeupe na kuiweka kwenye ALPHARD iliyokuwa katikati kisha akaongeza maiti zingine nne za kiume, Alionekana kuwa makini sana Japo kazi ilimchosha lakini alijitahidi, ilikua ni lazima aikamilishe na iaminike kua Tjedi na Zara wakiwa na majambazi kwenye ALPHARD ya katikati waliuwawa tayari kwaajili mbaya iliyopelekea gari zote kuungua moto. Baada ya zoezi hilo kukamilika,akachukua dumu kwenye buti la gari yake lililokua na mafuta ya petroli ndani na kuanza kumiminia gari zote za majambazi kila pande, alivyomaliza akaliweka dumu ndani ya gari la katikati kisha akarudi nyuma hatua kumi.Akaingiza mkono mfukoni na kutoa kibiriti cha gesi,akakiwasha na kutupa juu ya gari.la katikati, Mlipuko uliotokea ulikua wa aina yake,alivyohakikisha zoezi hilo limekamilika akarudi barabarani na kutokomea kwa kasi.
-------------------------

Baada ya Helikopta iliyowabeba Tjedi na Zara kutokomea kwenye macho ya Mukheef, alipokea simu kwa mara nyingine kutoka kwa bwana Aesh

“Kila kitu kipo sawa?” Aliuliza bwana Aesh
“Ndio Mkuu,nimefanya kama ulivyotaka” alijibu Mukheef

Bwana Aesh alikua ndani ya ofisi yake kubwa,amesimama nyuma ya kiti chake,sikio la kushoto ameweka simu anazungumza na Mukheef upande wa pili wa simu. Hakuwa tayari kuona mwanae na kipekee Zara akipoteza maisha, na aliamini Tjedi ndie mtu pekee anaeweza kumlinda mwanae na tayari alikwisha kumuingiza kwenye hii vita kubwa ndiyo maana alisuka mipango na Mukheef, ambapo aliamini kivyovyote vile kusingekua na namna ya mtu kutoboa uwepo wa Tjedi na Zara kuwepo hai.Kitendo cha kukata simu alishusha pumzi ndefu ya kuchoka.

Mukheef alichokifanya baada ya hapo ni kurudi dar es salaam ili aelekee hospitalini kuangalia afya ya Emmy inaendeleaje.Alijisikia uchungu sana na kujaribu kuvaa viatu vya Emmy juu ya kifo cha kugushi cha Tjedi, alielewa ni kwa jinsi gani angezipokea habari hizo kwa mshtuko lakini hakua na jinsi ilikua ni lazima ayaweke maisha ya Tjedi, Zara na Emmy salama, vingenevyo wote wangekua hatarini.

Baada ya kuwasili dar es salaam, alielekea hospitali ...usiku wa siku hiyo Mukheef, alikua na mawazo mengi sana aliwaza juu ya Tjedi na Zara, alimuangalia Emmy na kuhisi uchungu wa hali ya juu sana, akamsogelea kwa karibu na kumuangalia.
“Pole sana shemeji”
“Ahsante”
Kutokana na kurushwa nje ya gari wakati likiwa kwenye mwendo kasi Emmy alikuwa amechubuka sama mwilini, hiyo ilifanya apatiwe matibabu na maangalizi makubwa sana.
“Mmefanikiwa kumpata Tjedi?” Emmy aliuliza kwa sauti iliyokata tamaa kabisa.Kwa jinsi mambo yalivyotokea hakua ana uhakika kama Tjedi angetoka salama hata hivyo alijipa matumaini na kuupiga moyo konde.
“Atapatikana tu, tayari polisi wanafanya kazi yao.
“Ahsante sana Mukheef”
“Usijali shemeji”
Mukheef,alijikausha na alitamani kumwambia Emmy kila kitu kilivyosukwa na mpaka wakati huo Tjedi na Zara wapo kwenye ndege na pengine tayari wameshafika nchini London,hata hivyo alimezea na kuacha mambo kama yalivyo.
....Mukheef hakutaka kusema lolote kwa Emmy, huku nae Emmy alikuwa kwenye maumivu makali huku uso wake ukiwa umevimba kutokana na majeraha ya kusukumwa toka kwenye gari na kubiringika barabarani.

Madaktari na manesi wa hospitali kuu ya jeshi Lugalo wakiongozwa na Dr. B. Haji walijitahidi kumuhudumia mgonjwa Emmy kwa hali na mali ili afya yake iweze kuimarika vyema.
---------------------------------

----MBWENI, NYUMBANI KWA ZARA----
Ile milio miwili ya risasi iliyopigwa na yule jambazi aliyeuliwa iliwashtua wenzake waliokuwa ghorofani, ilibidi wakimbilie chini jikoni haraka ili kujua kuna nini.
"Aisee Bey, njoo uone...jamaa kauliwa bwana" alisema jambazi Henry

"Hawa washenzi wamemuua kiongozi wetu, lazima tuwasake popote walipo na nadhani bado watakuwa humuhumu ndani, hawajatoka nje"

"Henry, hebu sogeza friji hapo pembeni kidogo, mbona kama kuna michirizi ya damu?"

"Pumbavuuu!!!....hawa washenzi watakuwa wamepitia hapa, kuna njia ya chini huku aisee, Henry lete tochi!" Aling'aka Bey kwa gadhabu.

Tochi ilipoletwa, walishuhudia tobo la wastani likiwa mbele yao na likiwa limepita kwa chini na walipojaribu kulifuatilia, walijikuta wanatokea nje, tena nyuma ya ukuta wa nyumba hiyo...wote wakapigwa na butwaa na kujua sasa wale waliokuwa wanawasaka wameshawatoroka!!.

"Washenzi sana hawa, sasa tunafanyaje?" Aliuliza Bey.
"Hakuna cha kupoteza hapa, ni kumchukua mwenzetu na kumtia kwenye gari kisha tuondoke kabla hakujakucha na watu kuwa 'shazi', mambo mengine tutajua mbele kwa mbele!"

Gari ilisogezwa mbele ya mlango mdogo wa jikoni na wakaanza kupakia ile maiti ya mwenzao, kisha wakachukua vitu vyao ambavyo wanahisi vitaacha ushahidi, wakavitia ndani ya gari kisha wakatoa gari kwa mwendo wa kasi sana.
-------------------------------

----BUNJU NYUMBANI KWA BABY----
"Niambie mwari wangu, hujaalikwa kwenye sherehe za Xmass na yeyote leo, kweli huna bahati!!" maneno hayo aliongea dada mmoja rafiki yake Baby aliyeitwa Naomi

"Mimi na boyfriend wangu tumealikwa Mbweni kwenye sherehe za Xmass na lazima tuende" alizidi kusema Naomi

"Mbweni kwa nani tena?"
"Kwa mtoto wa boss wa boyfriend wangu"
"Huyu hapa ona.....ni muhindi"
Alizidi kusema Naomi huku akimuonesha Baby picha za Zara.

"Huyu dada, ni mtoto wa mmiliki wa Club AB anakofanyia kazi shemeji yako...alikuwa anasoma Ulaya, kwa sasa amemaliza masomo na amerudi Tanzania na anakula tu pesa za baba yake..."

"Watu wana pesa bwana, baba yake nasikia kamnunulia nyumba kubwa ya kifahari tena ya ghorofa na walinzi juu huko Mbweni ambako kutafanyika hizi sherehe leo..."

"Mhhh!!!"aliguna Baby
"Ngoja nikajiandae, nitapiga picha na kukutumia nikiwa ndani ya sherehe" alisema Naomi.

"Ukifika upige picha na huyo dada mwenye mjengo ili nimuone jinsi alivyopendeza"
"Sawa, mie tena..lazima nikutumie picha na video" aliongeza Naomi

Naomi aliongea kwa furaha huku akimsimulia rafiki yake Baby jinsi atakavyoenda kwenye sherehe hiyo, huku akiwa hajui ni kwa jinsi gani Baby alikuwa na historia mbaya na hiyo Club AB.

"Sasa naona muda wa kulipiza kisasi umewadia, haiwezekani mali za baba yangu anakula mtu mwingine na kufanya starehe zao......."
"Puu!! Puuh!! Puuh!!!...." alipiga mkono mezani Baby kwa jazba na hasira kali.
Ghafla akaukumbuka mwili wa marehemu baba yake uliookotwa ufukweni mwa bahari ya Hindi ukiwa mfu! hapo machozi ya uchungu na hasira vilimtoka na kuapiza kufanya jambo.

"Shenzi,....niko tayari kufa ili kukomboa mali za baba"

Aliinuka na kuingia ndani kisha kutoka na simu na kuanza kuongea na upande wa pili......

"Sawa...nimewaelewa"
"Gari, kila kitu kipo sawa na uzuri ni kwamba kuna mtu anaenda kwenye hiyo sherehe hivyo nitawaambia jinsi ratiba itakavyoenda"
"Hakikisheni mnamleta akiwa hai au na majeraha...sawa!!"
Aliongea Baby huku akiinuka kitini kufuata funguo ya gari lake aina ya TOYOTA CROWN nyeupe tayari kwa lolote.

Aliingia ndani ya gari na kushika usukani tayari kwa safari yake nzito ya kutafuta haki ya marehemu baba yake......
Screenshot_20250411_002536_Chrome.jpg
 
View attachment 3299588
Nimeipenda hii umetupa info za character yule ambaye aliwapa lift katika crown na kupata picha kwanini alitega pale na kwenda kuwachomesha kule town

Kumbe mchongo mzima aliupata toka kwa Naomi

Imekaa poa kwasababu kwa kila character /mhusika ambaye mtamuongeza inabidi kwa namna moja au nyingine alink na story
 
Ndio,Naomi ndio kama alimpa mchongo, japo Naomi mwenyewe hakuwa analifahamu hilo.

Karibu na nyie muweze kutia aya zenu wakuu Etugrul Bey, Daisy Leaf, muendelezo wenu ni muhimu.
Al-mukheef mbona uko kimya kaka?....una like tu na sioni tena aya zako.
Tjedi Hongera kaka, stori inazidi kuwa tamu, nakutegemea.
HenrysoN Kimya?
 
Endeleeni nitakuja baadae baadae
 
Waandishi naona kimya haya ngoja niamshe fikra zenu kisha mchukue peni muanze kuandika
 
Wakiwa kwenye helikopta Tdjei na Zara wakashuka nchini kenya tayar kuunganisha safari kwenda nchini Uingereza kufuatia maagizo ya bwana Aesh

Kwanza ilibidi wafanye shopping ndogo walau wabadilishe nguo maana nguo zao hazikuwa nadhifu tena kutokana na sekeseke ambalo wamekutana nalo

Ni saa moja usiku saa za Afrika Mashariki Tdjei na Zara ndani ya Shirika la ndege la KLM tayar kwa safar ya kuelekea Uingereza

Wakiwa ndani ya KLM hakuna ambaye alikuwa na hamu ya kumsemesha mwenzake,kila mtu alionekana ana mawazo sana kwa yale mambo yaliyotokea,lkn ni Zara alienza kuvunja ukimya kwa kumwambia Tdjei

"Hivi kule Uingereza ndio baba amesema tutakutana na mwenyeji wetu anaitwa nani vile"?
Tdjei akajibu "Anaitwa Nikolai Vostrikov"

Mda si mrefu mhudumu wa ndege akafika na kuwauliza wangependa kunywa vinywaji gani,baada ya kutoa oda yao,walitewa na kuanza kunywa taratibu huku kila mmoja akionekana yupo kwenye dimbwi la mawazo mazito sana

Tdjei pamoja na mambo mengine alikuwa na mawazo mazito sana juu ya mpenzi wake Emmy,je anaendeleaje kwasasa? Na wakati huo huo dhamira yake ikimshtaki kwa kumuingiza binti wa watu katika shida kubwa sana

Baada ya safar ya masaa kadhaa angani,mara akasikika mhudumu wa ndege akisema " sasa tunakaribia kushuka katika uwanja wa ndege wa Heathrow,tafadhali naomba mfunge mikanda yenu"

Huu ni uwanja mkubwa sana wa ndege nchini Uingereza na mamia ya abiria wanasafiri duniani kote kupitia uwanja huu

Wakiwa na hamu kubwa sana ya kukutana na Mwenyeji wao bwana Nikolai Vostrikov,wakashuka kuelekea sehemu ambayo utaratibu hufuatwa kwa wageni waiingiao nchini na kisha baada ya taratibu kukamilika walielekea nje tayar kukutana mwenyeji wao

Mwenyeji wao alikuwa na kibao kimeandikwa jina lake kwa herufi kubwa "NIKOLAI VOSTRIKOV" ikawa rahisi kutambuna na baada ya salamu za hapa na pale,aliwachukua kwenye gari ndogo aina ya volkswagen gold na kuelekea mji mdogo wa Wells ambao ndio mji mdogo sana nchini Uingereza una wakazi takribani 10,000

Na waliamua kwenda mji huu ili kuondoa uwezekano wa taarifa zao kupatikana kirahisi,maana hii vita ilikuwa ya kufa na kupona
 
KAnuni namba moja inasema uandike sentensi moja tuu.
Watu mnaandika insha.

Fuateni kanuni bana.
 
KAnuni namba moja inasema uandike sentensi moja tuu.
Watu mnaandika insha.

Fuateni kanuni bana.
Kanuni hubadilishwa,inategemea story ilianzaje,sasa story imekuwa kubwa utaandikaje sentesi moja?

Hapa ilipofikia sio mchezo tena ni story,ndio maana umeona waandishi wamepiga kimya wanatafakari
 
Ushauri kwa waandishi,wakati tunaandika,ebu tupate kiini cha ugomvi kati ya Aesh na majambazi,kwasababu mpaka sasa hatujui ilikuwaje mpaka imefikia timbwili timbwili la kutafutana
 
Back
Top Bottom