realMamy
JF-Expert Member
- Apr 28, 2024
- 7,307
- 18,240
Kamwe usiamini hadithi ya upande mmoja. Daima huwa na kurasa zilizokosekana.
Watu wengi wamekuwa wakihukumu watu kwa kutumia upande mmoja wa hadithi, bila kujali ni kwa namna gani wanaumiza wengine.
Kusikia upande mmoja tu wa story ni hatari. Mara nyingi mtu anakwambia sehemu inayomfaa yeye na kuacha zile zinazomtoa kwenye lawama.
Hadithi yoyote ya upande mmoja inakosa ukamilifu. Ni kama kitabu kilichoraruliwa kurasa kadhaa - huwezi kuelewa mwisho wake vizuri.
Hii inatufundisha kuwa wavumilivu na kutafuta ukweli wa pande zote kabla ya kuhukumu watu Katika urafiki, kazi, na hata kwenye mitandao.
Na uvumi mwingi unatokea kwa sababu watu wanasikiliza upande mmoja tu wa hadithi.
Kwa hiyo unapoletewa story au hadithi yoyote kuhusu mke,mfanyakazi wako,mwanao,rafiki Yako na wengine tumia muda kufuatilia, kuuliza, kusikiliza, na kuelewa kwanza ndipo utapata ukweli kamili utakaokusaidia kuhukumu.