Mbunge wa Muheza, Hamisi Mwinjuma apata ajali Morogoro

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,666
218,168
Ni Mbunge wa Muheza, Hamisi Mwinjuma ambaye ni mkazi wa Upanga Dar es Salaam.

Inasemekana yuko katika hali nzuri

=====

MBUNGE wa Muheza, Hamis Mwijuma maarufu kwa jina la Mwana FA (CCM) amepata ajali usiku huu Agosti 30 katika eneo la Mkambarani mkoani Morogoro baada ya gari alilokuwa akitumia kugongana na gari ndogo aina ya Toyota Crown.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro amethibitisha kuwa ajali hiyo imetokea maeneo ya Mkambarani Mkoani Morogoro ikihusisha gari la Mbunge na gari ndogo iliyokuwa na imebeba watu wanne.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Fortunatues Musilim, Mbunge huyo yuko salama na kwamba abiria wawili katika gari ndogo iliyokuwa ikitaka kuipita gari ya Mbunge wamejeruhiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Mkoa-Morogoro.

"Ni kweli Mh. Mbunge amepata ajali majira ya saa mbili usiku. Yeye yuko salama kabisa. Kilichotokea ni ajali ambayo imesababishwa na gari ndogo aina ya Toyota Crown iliyokuwa ikijaribu kulipita gari la Mbunge nahivyo kusababisha ajali," amesema.

Hata hivyo Musilim alisema, Baada ya ajali hiyo watu wengine wawili waliokuwa katika gari hiyo ndogo walipata michubuko midogo. Musilim amesema, Mbunge huyo alitumia gari lake kuwakimbiza majeruhi hao katika hospitali ya Mkoa Morogoro na wanaendelea vizuri.

Chanzo: Habari leo

 
Pole zake nimemsikia akizungumza mwenyewe ajali hii na yuko vyema maumivu kidogo.
Mbunge wa Handeni lakini mkazi wa upanga!? Ni shida ndio maana hatubadiliki wananchi hawamwoni mbunge hadi kampeni!! TZ pekee!!?
😆😆😆
 
Hivi mnafikiria nyie hamfi hadi mnachulia wenzenu vifo, sote tutakufa, kuanzia Mtei, Gaidi Mbowe na Lissu, na wote tutakejeli maiti zao kama mnavyokejeli za wapendwa wetu.
Uzuri ni kuwa ninyi mnao taka kuua wenzenu ndio mtatangulia kwanza.Kuna mwenzako alianzisha fyoko fyoko za kuteka, kuua na kutesa RAIA wema. Akatamani amuue Lissu kwa risasi mchana kweupee. Laki habari njema ni kuwa amedhibitiwa na yupo mikono salama huko kuzimu.
 
Uzuri ni kuwa ninyi mnao taka kuua wenzenu ndio mtatangulia kwanza.Kuna mwenzako alianzisha fyoko fyoko za kuteka, kuua na kutesa RAIA wema. Akatamani amuue Lissu kwa risasi mchana kweupee. Laki habari njema ni kuwa amedhibitiwa na yupo mikono salama huko kuzimu.
😆😆😆
 
Back
Top Bottom