Morogoro | Ajali ya basi la Abood yawaua wawili , Wengine wajeruhiwa

Mwl.RCT

JF-Expert Member
Jul 23, 2013
13,580
18,615
WATU wawili wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha basi la Kampuni ya Abood na Noah zilizogongana uso kwa uso asubuhi ya leo Septemba 11, 2023 eneo la Kitungu Manispaa ya Morogoro.

Ajali hiyo imehusisha basi lenye namba za usajili T904 DKY mali ya Kampuni ya Abood iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kuelekea Morogoro na gari ndogo aina ya Noah yenye namba za usajili T828 DNB iliyokuwa ikitokea Morogoro kuelekea Dar es Salaam.

Uongozi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro umethibitisha kupokea miili ya watu wawili pamoja na majeruhi wawili.

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, ACP Alex Mkama amezungumzia kutokea kwa ajali hiyo huku chanzo kikitajwa kuwa uzembe wa dereva wa basi la Abood.

 
1101978067_univ_lsr_lg.jpg
 
Upo sahihi ila nadhani tatizo la mwenye noah hakutaka kumpisha abood, haya mabasi makubwa wanapenda kuonea magari madogo wanakuletea tu kazi ni kwako umpishe ukapambane na vicheche porini au ukaze fuvu ubutuliwe
Tatizo haliwezi kuwa mwenye noah, kuna vipande vya barabara havikupi nafasi ya kutoka, pamebana.. mm nimekoswa design hiyohiyo miezi hata miwili haijatimia
 
Back
Top Bottom