Watu watatu wa Familia moja wafariki katika ajali ya gari Pwani

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,416
5,778
Ajalii.jpeg
Watu watatu wamefariki na wengine kujeruhiwa kwenye ajali ya gari iliyohusisha lori na gari ndogo aina ya Toyota Alphard iliyotokea katika Kijiji cha Mbwembwe, wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.

Kamanda wa Polisi mkoani humo Pius Lutumo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa amepata taarifa ya tukio hilo na kwa wakati huo alikuwa njiani kuelekea eneo la tukio, hivyo kuahidi kutoa taarifa zaidi wakati unaofuata.

"Nimesikia hivyo nipo njiani naelekea huko kwenye tukio,”- Kamanda Lutumo.

Diwani wa kata ya Mbwewe Omary Msonde amesema kuwa ajali hiyo imetokea saa kumi na mbili alfajiri ya leo, Alhamisi Desemba 28.2023.

Katika hatua nyingine, Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mkoani Tanga, Albert Msando kupitia mitandao yake binafsi ya kijamii amesema kuwa waliofariki ni familia ya Diwani wa Kata ya Kabuku, Halmashauri ya Wilaya Handeni mkoani Tanga, Nurudin Semnangwa ambapo amepoteza mke, mtoto na dada wa kazi.

Chanzo: JamboTV
 
Duh!

Tarehe za watu kufariki kwa ajali sababu ya kusafiri, si vyema sana kukusanyana familia...

waliofariki ni familia ya Diwani wa Kata ya Kabuku, Halmashauri ya Wilaya Handeni mkoani Tanga, Nurudin Semnangwa ambapo amepoteza mke, mtoto na dada wa kazi.
 
Back
Top Bottom