Mbunge wa Arusha Mjini kupitia CCM,Mrisho Gambo aanza kazi kwa kishindo kwa kununua nondo zenye thamani ya milioni 25 kwa ajili ya ujenzi wa sekondari

CCM haipo Arusha, hayo maigizo yenu endeleeni nayo tu, but siku baba yenu akiondoka mkamkosa wa kuwabeba mgongoni, ndio mtaifahamu vizuri Arusha Mjini.
I'm afraid that will be a little bit too late! Wanasema "in politics, every minute counts"
 
Amenunua Nondo za 25m kutoka fungu gani? Maana nijuavyo serikali ina taratibu zake, au siku hizi mtu anaamua kutoa fedha zake mfukoni ili kufanya show? Kama ni hela yake toka mfukoni hakupaswa kusubiri kuwa mbunge, bali alipaswa kufanya hivyo bila hata ubunge. Ukiona hivyo ujue atakuwa amelazimisha matajiri watoe pesa ili akajichukulie ujiko, dakika za mwisho utakuta hao matajiri anaoenda kuwalazimisha watoe hela, wakiwa na matatizo ya kikodi anaanza kwenda kuzitisha mamlaka ziache kuwadai.
Kwa hiyo unapinga?
 
N
Nakubaliana na wewe Mheshimiwa ! Arusha mjini ccm haipo !!!
Kipindi cha nyuma tulikuwa tunaambiwa watu wa arusha mjini na Mbeya mjini ni moto wa kuotea mbali na kwamba hata polisi wanaweza kuchezea vitasa wakijaribu kuwabughudhi wabunge wao.

Matokeo yake:
Lema alipigwa ndani hakuna hata sisimizi akisogea.
Sugu alipigwa ndani hakuna hata sisimizi alisogea.

Hitimisho:
Wakazi wa Arusha na Mbeya ambao ni wafuasi wa chadema hawana tofauti yeyote na wafuasi kutoka sehemu nyingine za nchi. Yani wote ni mdebwedo kama tulivyoona juzi wote wakijificha uvunguni Lisu alipoitisha maandamano.
 
Hiyo sio kazi ya mbunge kutumia hela zake huo ni upumbavu kazi yake nikushawishi serikali itoe hela
Kwa hiyo akina Lema walitafuna mamilioni yote bila kurudisha fadhila kwa wapiga kura ? Aisee Afadhali Lema alipigwa chini na Chadema wenzao wamezidi uchoyo
 
Hiyo sio kazi ya mbunge kutumia hela zake huo ni upumbavu kazi yake nikushawishi serikali itoe hela
Kwa hiyo kazi ya mbunge Ni kuchonga mdomo tu bungeni ? Chadema ndio maana mumepigwa chini mkiambiwa na wananchi onyesheni mlichowafanyia wanamchi mnabaki Ohhh sisi Chadema kazi yetu sio kuleta maendeleo ya vitu Kama hivyo vya shule nk sisi kazi yetu Ni maendeleo ya watu sio vitu

Haya mkiulizwa hayo maendeleo ya watu kwenye majimbo yenu mlipokuwa wabunge Ni yepi mliyaleta Majimboni mwenu kipindi chote Cha ubunge wenu mnabaki kutoa mimacho utafikiri mjusi aliyefiwa na mkwewe hamna Cha kuonyesha

Hongereni Sana Wana Arusha na watanzania kuwapiga chini wabunge matapeli wa Chadema

Hongera Sana Mrisho Gambo una Cha kuwaonyesha wananchi
 
Back
Top Bottom