Mrisho Gambo: Kuongeza Tsh. 100 ya Mafuta na Tsh. 200 ya Saruji ni kuongeza mzigo kwa Mwananchi

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Akichangia mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2023/24, Mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo amepinga pendekezo la Serikali kuongeza Tsh. 100 kwenye kila Lita ya Dizeli na Petroli kwa maelezo tayari Mafuta yana Kodi 22.

Akifafanua zaidi amesema tayari baadhi ya Kodi zinazotozwa kwenye Mafuta zinakwenda kwenye Ujenzi wa Barabara hivyo ongezeko hilo litasababisha nauli za Mabasi na Daladala zipande pamoja na gharama nyingine za maisha.

Kuhusu ongezeko la Tsh. 200 kwenye kila Kilo ya Saruji, Gambo amesema Kodi hiyo itamnyima Mtanzania uwezo wa kununua Sauruji kwaajili ya ujenzi wa Nyumba nzuri na hivyo Serikali itafute chanzo kingine cha mapato na sio kumbebesha kodi Mwananchi.
 
Saruji iliyoongezwa bei ni ya Nje Sasa Kuna shida gani?

Harafu ukipinga jambo toa alternative sio unaropoka tuu.Tumenunua mafuta Kwa sh.3500 Mkoani Sasa yameshuka hata mia ikiwekwa Wala haifiki hata elfu 3 Sasa shida Iko wapi?
 
Ni upuuzi kutoza kodi kubwa saruji kwa sababu eti inatoka nje.saruji inauhitaji mkubwa na uzalishaji wa ndani hautoshelezi.ruhusu saruji iingie ili bei ishuke wananchi wanunue hata mfuko kwa elfukumi. watu watu wanaopakana na kenya huwa wananunua kenya sababu ni ya bei chee
 
Kuhusu ongezeko la Tsh. 200 kwenye kila Kilo ya Saruji, Gambo amesema Kodi hiyo itamnyima Mtanzania uwezo wa kununua Sauruji kwaajili ya ujenzi wa Nyumba nzuri na hivyo Serikali itafute chanzo kingine cha mapato na sio kumbebesha kodi Mwananchi.
Mbona wanakwepa kuongeza kwenye kila lita ya vinywaji
 
mwigulu nchemba ni mmoja wa mawaziri wa hovyo sana kuwahi kutokea nchini. Na jambo hili nilishawahi kulisema hata pale alipoteuliwa kwenye hii Wizara nyeti. Bora hata ya Dr. Phillipo Mpango alikuwa ni mbunifu.

Hajawahi kumiliki ubunifu wowote ule wa kuongeza mapato nje ya kukopa, na kuongeza kodi/tozo kwa wananchi. Huyu jamaa ana roho ya kikatili sana.
 
Sasa viwanda Vya ndani vitaongeza Bei mara dufu kwakuwa havina mpinzani
Siku zote havikuongeza viongeze saizi Kwa sababu zipi za msingi Wakati uzalishaji wa ndani ni mkubwa kuliko mahitaji?

Wizara ya Fedha Ina wapumbavu ambao wanakula dili na wafanyabiashara uchwara na pia inaonekana Bajeti Huwa inaandaliwa bila kushirikiana na Wizara za kisekta.
 
Kinachokera ni kua mbunge wa CCM akishatamka jambo ujue wamejadili huko kwenye kikao chao (party caucus) wanatuchora tu mwisho wote wanaafiki hoja.

Inasikitisha sana tunafanywa mazuzu wanajiamulia tu, kama mtu amesahau kumbuka ile issue ya tozo kwenye miamala ya simu.
 
Akichangia mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2023/24, Mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo amepinga pendekezo la Serikali kuongeza Tsh. 100 kwenye kila Lita ya Dizeli na Petroli kwa maelezo tayari Mafuta yana Kodi 22.

Akifafanua zaidi amesema tayari baadhi ya Kodi zinazotozwa kwenye Mafuta zinakwenda kwenye Ujenzi wa Barabara hivyo ongezeko hilo litasababisha nauli za Mabasi na Daladala zipande pamoja na gharama nyingine za maisha.

Kuhusu ongezeko la Tsh. 200 kwenye kila Kilo ya Saruji, Gambo amesema Kodi hiyo itamnyima Mtanzania uwezo wa kununua Sauruji kwaajili ya ujenzi wa Nyumba nzuri na hivyo Serikali itafute chanzo kingine cha mapato na sio kumbebesha kodi Mwananchi.
Hakuna binadamu mnafiki km Gambo, kila akichangia sijawahi kumwelewa, Sasa anataka hilo li-stand la Bondeni city litajengwa na nini km siyo kodi. Kuongezwa nauli kuna mamlaka inayosimamia mambo hayo ya nauli. Ni wake wakwamishaji wa maendeleo ya nchi kwa mgongo wa kutetea wananchi. Ili tupate maendeleo lazima tulipe kodi.
 
Back
Top Bottom