WanaCCM Arusha wamtaka Mrisho Gambo naye aitishe mkutano wa hadhara kujibu mapigo ya Lema

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
10,129
35,152
Hayawi hayawi sasa yamekuwa, Arusha kumekucha upya baada ya Godbless Lema kutua nchini na kulitikisa jiji lolote la Arusha kwa kishindo cha mapokezi, shamrashara mitaani na mkutano mkubwa wa hadhara.

Sasa makundi mbalimbali ya wanaCCM yameamua kupiga kelele kwa mbunge wa Jimbo la Arusha mjini, Mrisho Gambo ili atoke mafichoni na kuitisha mkutano wa hadhara ili kujibu kishindo na mapigo na hoja za Lema. Mpaka sasa CCM Arusha hawajatoa tamko lolote rasmi, huku wakingojea huenda labda Kinana atakuja kufanya ziara ili kufufua mwamko wa wanaCCM wa Arusha ambao wamepoa sana. Weekend hii (Jumamosi ya leo?) Mama Samia alitarajiwa kuwa jijini Arusha kiserikali na hatakuwa na ratiba yoyote ya kufanya vikao vya ndani vya CCM wala kuonana na wananchi moja kwa moja.

Kwa miaka kadhaa uhusiano wa uongozi wa CCM Arusha na Mrisho Gambo umekuwa mbaya kiasi cha kila upande kufanyiana fitina kila mara.
 
Hana mda mchafu, kampeni hazijaanza
 
Gambo anajua siasa, huwa hakurupuki, anamsubiri Lema amalize dukuduku lake ajibu mapigo, utafurahi mwenyewe
Gambo hajui kitu wala hakubaliki. Hata huo ubunge alilazimishwa tu na mwendakuzimu.

Arusha tunamkubali Lema na hata hao ccm waitishe mkutano labda wakasombe watoto wa shule kwenye mafuso.

Gambo anajua hana uwezo wa kupambana na Lema kabisa. Bila "chafuzi" wa Magufuli bunge lingekuwa 90% upinzani.

Hiyo ipo wazi kama uchi.
 
Mfufueni Magufuli ndipo anaweza kuongea kitu.....na kukamata walimu walete wanafunzi waje kuhudhuria
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom