Arusha. Mkuu wa wilaya ya Arusha, Felisian Mtehengerwa amemtaka Mbunge wa jimbo lake Mrisho Gambo kutekeleza wajibu wake ndani ya halmashauri kuliko kubeba ajenda za ubadhilifu ili kujitafutia umaarufu wa kisiasa.
Mtahengerwa amesema hayo leo April 19,2023 wakati akizungumza na waandishi wahabari juu ya msimamo wake kuhusiana na tuhuma zilizotolewa na Gambo bungeni hivi karibuni akielezea ubadhilifu wa fedha za umma katika halmashauri ya jiji la Arusha na serikali.
"Gambo ifikie mahali aache siasa za maji taka maana kutuhumu viongozi kwa ufisadi wakati yeye ni sehemu ya viongozi wanaosimamia utekelezaji wa mipango ya jiji la Arusha ni kutafuta pa kutokea na huruma ya wananchi wakati yeye mwenyewe ni mmojawapo," amesema Mtahengerwa.
"Gambo anaonyesha wazi hajui wajibu wake maana anasahau kuwa halmashauri inaundwa na madiwani na mbunge hivyo anapoona mambo hayaendi vizuri wangekuwa wakwanza kuzuia na kuchukua hatua za awali lakini matokeo yake anakubali utekelezaji ufanyike halafu baadae anaenda kuukosoa, awajibike ndani kwanza kwa kukataa isifanyike," ameongeza.
Pia, amesema wakati mambo hayo yanatokea miaka ya nyuma ambayo pia yeye (Gambo) ni mmoja wa wajumbe wakuu hivyo anafaa kuwajibika maana ni sehemu ya mpango huo.
"Sisi kama wilaya tunawajibu wa kuingilia pale tunapoona akili za halmashauri zimefikia ukomo, mambo hayaendi, nilipoingia madarakani nilizungukia miradi yote na kuwaita madiwani wote na kutoa maelekezo yangu, ninachoshangaa yale yaliyowahi kuchukuliwa hatua bado anabeba Kama ajenda mpya na kuimba kila kukicha badala ya kuwajibika hivyo nimtake arudi jimboni tuchape kazi aache utoto wa mashtaka,”amesema.
Hivi karibuni Gambo akiwa bungeni dodoma alieleza mambo mengi ya ufisadi katika jiji la Arusha huku akidai changamoto kubwa ya ubadhilifu na usimamizi mbovu wa fedha za halmashauri.
Alitolea mfano baadhi ya tuhuma ukiwemo ujenzi wa jengo la utawala lenye urefu wa gorofa sita, na kusema halmashauri imetafuta fundi mjenzi akidai ni rafiki yao bila kutangaza tenda, taratibu za manunuzi hazijafuatwa na kumpatia kiasi cha fedha Tsh. 199.7 milioni na kununua vifaa vya Tsh. 132 milioni ambavyo havijafika eneo la mradi.
"Ziada ya nondo kiasi cha tani 6.48 zenye thamani ya Sh17 milioni pia waliongeza malipo ya sh21 milioni kwa fundi yanayotokana na uzembe wa wataalamu wetu, pia kumekuwepo na risiti feki za EFD zenye thamani ya Tsh. 699.9 milioni,” alituhumu Gambo.
Aidha sio mara ya kwanza Gambo kutoa tuhuma za ubadhirifu wa fedha katika halmashauri hiyo kwani mapema Mei, 2022 alitoa tuhuma hizo mbele ya waziri mkuu Kasim Majaliwa hali iliyopelekea kusimamishwa kazi watumishi sita wa jiji la Arusha akiwemo aliyekuwa mkurugenzi Dk John Pima.
MWANANCHI