Mbunge wa Arusha Mjini kupitia CCM,Mrisho Gambo aanza kazi kwa kishindo kwa kununua nondo zenye thamani ya milioni 25 kwa ajili ya ujenzi wa sekondari

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,156
4,510
Mrisho Gambo amekabidhi Nondo hizo zitakazotumika kujenga Sekondari ya Ghorofa maeneo ya Unga Limitedi Jijini Arusha

FB_IMG_16053665893996312.jpg
FB_IMG_16053665852214030.jpg


Tuliahidi
Tunatekeleza
 
Mrisho Gambo amekabidhi Nondo hizo zitakazotumika kujenga Sekondari ya Ghorofa maeneo ya Unga Limitedi Jijini Arusha

View attachment 1626445View attachment 1626446

Tuliahidi
Tunatekeleza
Kumbe wabunge wana mihela hivi? Aliyemaliza muda wake kwetu Ukonga, walau Viwege, Zavala, Kigezi etc mvua zikianza wenye magari wanapaki na unakuwa mwendo wa kuvuka madimbwi ya maji na sijawahi kusikia kama kuna hela yoyote aliyoweka au wekeza kuondokana na hizo kero.
 
Mbona umeandika kama unawahi mahali?, hapo ni Ungalimitedi wapi au upande gani maana Ungalimited ni kubwa?
 
Mrisho Gambo amekabidhi Nondo hizo zitakazotumika kujenga Sekondari ya Ghorofa maeneo ya Unga Limitedi Jijini Arusha

View attachment 1626445View attachment 1626446

Tuliahidi
Tunatekeleza

Amenunua Nondo za 25m kutoka fungu gani? Maana nijuavyo serikali ina taratibu zake, au siku hizi mtu anaamua kutoa fedha zake mfukoni ili kufanya show? Kama ni hela yake toka mfukoni hakupaswa kusubiri kuwa mbunge, bali alipaswa kufanya hivyo bila hata ubunge. Ukiona hivyo ujue atakuwa amelazimisha matajiri watoe pesa ili akajichukulie ujiko, dakika za mwisho utakuta hao matajiri anaoenda kuwalazimisha watoe hela, wakiwa na matatizo ya kikodi anaanza kwenda kuzitisha mamlaka ziache kuwadai.
 
Hiyo kampuni hawajitambui; kwanini wasikabidhi misaada yao kwa jamii wenyewe badala ya kuwatumia wanasiasa? Anyway labda atafanya namna wasamehewe au wakwepe Kodi!
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom