Mbunge Norah Mzeru awataka wanawake kumuunga mkono Rais Samia

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
942

MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro, Mhe. Norah Mzeru, amewataka wanawake katika maeneo mbalimbali hapa nchini kuwa mstari wa mbele kumuunga Mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na Serikali yake kwa kazi kubwa anayoifanya kuleta maendeleo kwenye jamii na kuboresha upatikanaji wa huduma.

Kauli hiyo ameitoa Machi 10/2024 katika hafla ya pamoja ya wanawake iliyoandaliwa na Kituo cha habari cha Planet FM chini ya Mkurugenzi wa Vipindi, Bi. Warda Makogwa kwenye Ukumbi wa Mount Uluguru Manispaa ya Morogoro.

Akizungumza na wanawake waliojitokeza katika hafla hiyo, Mhe. Mzeru, amesema kuwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, amekuwa akianzisha harakati nyingi zenye lengo la kumkomboa mwanamke kiuchumi.

"Rais wetu anapambana kuhakikisha wanawake wananyanyuka kiuchumi lakini hata hizi program ambazo nchi yetu imekuwa ikizifanya juu ya wanawake ni program zenye tija ukiziangatia Tanzania ipo katika jitihada za kumkomboa na kumuinua mwanamke kiuchumi" Amesema Mhe. Mzeru.

Mhe. Mzeru, amesema Tanzania ni mojawapo ya Mataifa yanayotekeleza malengo ya Jukwaa la Kimataifa ya Kukuza usawa wa Kijinsia ambapo katika hilo Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kinara wa utekelezaji wa Jukwaa hili hususan kuhusu Haki na Usawa wa Kiuchumi.

Aidha, amewataka wanawake kuendelea kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufanya kazi kwa bidi na kuwa na biashara zenye tija na zenye ushindani kimasoko.

" Nimevutiwa na kauli mbiu ya mwaka huu 2024 “ WEKEZA KWA WANAWAKE KUHARAKISHA MAENDELEO YA TAIFA NA USTAWI WA JAMII” niwaombe wanawake wenzangu wale ambao ni wajasiriamali basi tuhakikishe tunapowekeza basi bidhaa zetu ziendanane na ubora wa uwekezaji ili kuleta ushindani wa masoko hapo tutakuwa tunafanya uharakishaji wa kuuza bidhaa na tutaleta maendeleo chanya kwa Taif ana Ustawi wa Jamii" Ameongeza Mhe. Mzeru.

Mbali na yote aliyozungumza, amesema kuna wimbi la unyanyasaji wa kijinsia na ubakwaji kwa Watoto, huku akisisitiza hayo mambo siyo ya kuyafumbia macho na kuwataka wazazi/ walezi kuwa karibu na watoto wao mara kwa mara na sio kuwaachia waalimu kwani wazazi ni sehemu ya msaada ya kumlinda mtoto ili atimize malengo yake.

Mwisho, amewashukuru sana Planet FM kituo bora kabisa cha habari nchini kwa kuandaa tukio hilo la kuwakutanisha wanawake shupavu, huku akiiomba Planet FM waanze kuwafikiria wajasiriamali wa chini angalau kuwapatia vipindi mara moja bure hata cha dakika 5 ili wajitangaze na baadae waje kuona Fahari ya kuwa na meneja mwanamke wa kituo cha Habari.

Naye Mkurugenzi wa vipindi Planet FM, Bi. Warda Makongwa, amempongeza Mhe. Mzeru kwa kufika katika sherehe yao huku akimuomba kuangalia namna ya kuwainua wajasariamali wa chini ili wanyanyuke kiuchumi.

Makongwa, amesema wameandaa hafla hiyo kwa wanawake wasioendeshwa na mfumo dume ili wazidi kupeana fursa mbalimbali kwa ustawi wa Jamii na kuharakisha maendeleo ya Taifa kama kauli mbiu ya siku ya wanawake inavyosema.
 
FURAHI SANA BINTI SAYUNI MFALME WAKO ANAKUJA AMEPANDA PUNDA AMEBEBA WOKOVU WAKO

ZEKARIA 9:9
 
Sijawahi kuona wala kusikia mchango wake Bungeni.

Enewei. Huwa wanaibukiaga miwshoni kutetea ugali
 
Huwa hufuatilii wabunge wote wakiwa wanauliza maswali na kichangia hoja na mijadala. Mbona sisi tunamjua sana na kazi zake tunaziona
 
Hicho ndio wanachoweza, maana hatujawahi kumsikia kabisa kwenye ajenda za maana kama bandari, katiba na sukari.
Imagine mbunge hatujawahi kumsikia hata kupiga chafya tu
 
Nina uhakika kwa post hii tayari watoto wana uhakika wa kwenda maliwato wiki nzima...

Hivi mkuu, nikae nakesha hapa kwenye siasa kisha niwe mzembe kufuatilia siasa za nchi yangu kweli? Unadhani hoja tunazoziibua hapa tunazitoa wapi kama siyo utendaji wa viongozi, serikali na wanasiasa wetu?
 
majuzi nilikua wilayani basi katika pitapita salimia watu nikawa na neno la kichokozi nauliza vipi hali mambo mnayaonaje mwingi tunaupiga sio siri hata wanawake wenyewe hawaelewi nn kinafanyika mbaya zaidi wamebugi kutumia jinsia kutaka kuungwa mkono tukumbuke..
ni mwanamke huyo huyo ndie anajua machungu ya kulea familia ni mwanamke huyo huyo hana fursa na anaona watu wanakula ni mwanamke huyo huyo hali yake inazidi kuwa ngumu alafu mnakuja kusema wamuunge mkono.

wale washona sare wengi wao wamelazimishwa kulingana na maeneo ya kazi ila sio siri mbali na uchawa hakuna mtu anaelewa nn kinaendelea na mashaka ni hapo 2025 usaliti utakuwa mwingi
 
Hicho ndio wanachoweza, maana hatujawahi kumsikia kabisa kwenye ajenda za maana kama bandari, katiba na sukari.
Imagine mbunge hatujawahi kumsikia hata kupiga chafya tu
Ni kawaida kwa binadamu yeyote huwezi kuwa competent kwa kila kitu. Kuna wabunge kama Mpina amejaliwa kipawa cha kujua vitu vingi, ila kuna mwingine ana deal na mambo ya kupinga ukatili wa kijinsia. Mbunge mwingine haongei sana Bungeni ila kwa wananchi anatatua changamoto. Naamini hata wewe hapo kuna sehemu uko vizuri ila kuna sehemu uko shallow. Tusiwabeze wabunge kwa kuwataka wa deal na kila kitu wakati hata sisi ukitupeleka huko hatuwezi kuchangia kila kitu.

Fuatilia kipindi cha kupitisha Sheria mpya, utaona hata Spika anataka kumsikia Mpina, Mdee na wengine wachache, wengine waliosalia wote wanabaki kupiga tu makofi
 
Nina uhakika kwa post hii tayari watoto wana uhakika wa kwenda maliwato wiki nzima...

Hivi mkuu, nikae nakesha hapa kwenye siasa kisha niwe mzembe kufuatilia siasa za nchi yangu kweli? Unadhani hoja tunazoziibua hapa tunazitoa wapi kama siyo utendaji wa viongozi, serikali na wanasiasa wetu?
Afadhali nipost nilipwe kuliko kuiba. Kikubwa tunatunza familia maisha yanaenda kama kawaida
 
Back
Top Bottom