Mbunge Norah Mzeru Akabidhi Mashuka Yaliyotoka kwa Rais Samia Hospitali ya Gairo na Mafiga Morogoro

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

MBUNGE NORAH MZERU AKABIDHI MASHUKA YALIYOTOKA KWA RAIS SAMIA HOSPITALI YA GAIRO NA MAFIGA MKOANI MOROGORO

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro, Mhe. Norah Waziri Mzeru tarehe 17 Februari, 2024 baada ya Bunge kuhitimishwa amefika Hospitali ya Wilaya ya Gairo na Mafiga zilizopo Mkoa wa Morogoro na kukabidhi mashuka yaliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa wabunge wote wanawake ili yafike kwenye vituo vya afya na Zahanati

Katika ziara yake, Mhe. Norah Waziri Mzeru ameambatana na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali wakiwemo viongozi wa UWT Wilaya ya Morogoro Mjini, UWT Wilaya ya Gairo, Diwani na kukabidhi vifaa hivyo kwa Kaimu Mganga Mfawidhi wa kituo cha Afya cha Mafiga

"Tumekutana mahali hapa kituo cha Afya cha Mafiga ili kuleta Mashuka kutoka kwa Mheshimiwa Rais. Namshukuru na kumpongeza Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kukuza huduma za kijamii kwa kasi kubwa nchini" - Mhe. Norah Waziri Mzeru, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro

"Rais Samia ameboresha taasisi nyingi nchini ikiwemo taasisi za afya, ujenzi wa Zahanati pamoja na vituo vya afya, lakini bado anaendelea kuboresha huduma za kijamii. Mashuka mnayoyaona yametoka kwa Mheshimiwa Rais, hii yote ni kwamba Mheshimiwa Rais ana mapenzi mema na watu wake" - Mhe. Norah Waziri Mzeru, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro

"Tunapaswa kumuunga mkono Rais Samia kwa yote anayoyafanya na kuhakikisha mwaka 2025 anapita kwa kishindo. Nipo Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mitaji ya Umma, tuna safari lakini nikaona Mheshimiwa Rais ametoa Mashuka kwa watu wake kutokana na uhitaji uliopo nikaona niyalete haraka iwezekanavyo" - Mhe. Norah Waziri Mzeru, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro

"Nitatoa Mashuka katika Wilaya zote Nane za Mkoa wa Morogoro. Nampongeza Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu kwa kazi anayoifanya ya kumsaidia Mheshimiwa Rais katika kuboresha Afya ya Mama na Mtoto" - Mhe. Norah Waziri Mzeru, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-02-18 at 20.17.59(2).jpeg
    WhatsApp Image 2024-02-18 at 20.17.59(2).jpeg
    145.3 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2024-02-18 at 20.17.59.jpeg
    WhatsApp Image 2024-02-18 at 20.17.59.jpeg
    120.2 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2024-02-18 at 20.17.56.jpeg
    WhatsApp Image 2024-02-18 at 20.17.56.jpeg
    197.3 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2024-02-18 at 20.17.57.jpeg
    WhatsApp Image 2024-02-18 at 20.17.57.jpeg
    157.5 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-02-18 at 20.17.57(2).jpeg
    WhatsApp Image 2024-02-18 at 20.17.57(2).jpeg
    178.8 KB · Views: 4
"Tunapaswa kumuunga mkono Rais Samia kwa yote anayoyafanya na kuhakikisha mwaka 2025 anapita kwa kishindo. Nipo Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mitaji ya Umma, tuna safari lakini nikaona Mheshimiwa Rais ametoa Mashuka kwa watu wake kutokana na uhitaji uliopo nikaona niyalete haraka iwezekanavyo" - Mhe. Norah Waziri Mzeru, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro
KUmbe ni kampeni kwa kutumia kodi zao
 
Back
Top Bottom