Mbunge Norah Mzeru Aongoza Wanawake Kupanda Miti Mvomero Katika Maadhimisho ya Wiki ya Wanawake Duniani

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
942
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro, Mhe. Norah Waziri Mzeru ameshiriki maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kwa kupanda miti na kugawa mashuka katika Wilaya ya Mvomero.

Siku ya Wanawake duniani huadhimishwa Machi 08 ya kila mwaka. Malengo ya maadhimisho haya ya Siku ya Wanawake duniani yanalenga kuongeza chachu katika harakati za mapambano katika usawa wa kijinsia kwa Wanawake na wanaume katika jamii.

Siku hii pia huchochewa na vuguvugu la Wanawake la kupigania haki zao. Pia, lengo Kuu ni kutathimini utekelezaji wa Sera, Programu, Mikakati na Miongozo iliyoandaliwa kwa lengo la kuleta usawa wa kijinsia na uwezeshaji Wanawake kiuchumi.

"Nimpongeze Sana Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani katika kipindi chake cha Uongozi tumeshuhudia Mabadiliko makubwa Kwa upande wa Wanawake." - Mhe. Norah Waziri Mzeru, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro

"Ukiangalia Wakuu wa Mikoa, Wilaya, na Wakurugenzi kumekuwa na ongezeko kubwa la Wanawake katika Uongozi, hii ni hatua kubwa Sana na tunapaswa Sana kumpongeza RAIS wetu kwa kustawisha Wanawake." - Mhe. Norah Waziri Mzeru, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro

"Sisi kama Wanawake jukumu letu ni kuhakikisha tunamsemea mwanamke mwenzetu vizuri na kumuunga mkono kwa kazi kubwa anazozifanya." - Mhe. Norah Waziri Mzeru, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro

"Tuna Rais msikivu Sana, mwanamke mwezetu, ametuheshimisha Sana na tuna kila sababu ya kumpongeza na kuhakikisha tunampa ushirikiano mkubwa Sana na sisi twende nae Hadi 2030 ili aendelee kutuvusha zaidi sisi Wanawake." - Mhe. Norah Waziri Mzeru, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro

Mwisho, - Mhe. Norah Waziri Mzeru amewatakia maandalizi mema ya Siku ya Wanawake duniani na Kitaifa ambapo kwa Mkoa wa Morogoro maadhimisho yanafanyika Manispaa ya Morogoro.

KAULI MBIU: WEKEZA KWA WANAWAKE, KUHARAKISHA MAENDELEO YA TAIFA NA USTAWI WA JAMII.

WhatsApp Image 2024-03-07 at 09.52.33.jpeg
WhatsApp Image 2024-03-07 at 09.52.25.jpeg
WhatsApp Image 2024-03-07 at 09.52.23.jpeg
WhatsApp Image 2024-03-07 at 09.52.20.jpeg
WhatsApp Image 2024-03-07 at 09.52.19.jpeg
WhatsApp Image 2024-03-07 at 09.52.17.jpeg
WhatsApp Image 2024-03-07 at 09.52.14.jpeg
WhatsApp Image 2024-03-07 at 09.52.10.jpeg
WhatsApp Image 2024-03-07 at 09.51.59.jpeg
 
Back
Top Bottom