Mbowe vs Chifupa + CHADEMA vs Family Business

Status
Not open for further replies.
Tafiti: Pole ndugu yangu, mimi sitoki kaskazini ng'o. Nitafute vizuri hujanipata bado.

Naam, nilikuwa najua sana hayo mahusiano kati ya Philemon, Grace na Lucy. Hao watu wote nimefanya nao kampeni mwaka jana, nisingeacha kujua jambo lililo wazi kiasi hiki! Hii haijawahi kunipa shida hata kidogo. Nitafafanua baadaye, kwa sasa ngoja nimalizane na wewe kwanza katika utafiti wako.

Japokuwa unakimbia hii forum kwa kudai kuwa adm amekuuzi, kabla hujakimbia lazima nimalizie majibu yangu katika utafiti wako kama ifuatavyo.

Utafiti mzuri wa aina yako ungefanya pia comparative analysis. Kwa mfano hali ikoje katika vyama vingine angalau viwili vitatu kabla ya ku-draw such bold conclusions. Kwa mfano, kwa kutumia idadi ya watu uliotumia wewe hao viongozi sita. Tukifanya hivyo hivyo katika uongozi wa CCM wa sasa utakuta kwamba katika viongozi sita wa juu yaani Mwenyekiti, Makamu wawili, Katibu Mkuu na Manaibu Makatibu wakuu wawili (total six)-utakuta kwamba 4 kati ya hawa wote ni waislamu, hii ni sawa na 66.7%, Je hii inatosha kusema kuwa CCM ina mwelekeo wa kidini yaani kiislamu? Bila shaka jibu unalo. Tukiangalia uongozi uliopita chini ya Mkapa, utakuta kwamba katika viongozi wa juu wa CCM(6), wanne kati ya hawa walikuwa ni wakristo ambayo ni sawa na 66.7%. je tuseme kuwa hiki chama kila mwenyeketi anapokuwa dini fulani basi kinakuwa na mwelekeo wa dini hiyo? Nafikri jibu pia unalo.

Maoni yangu ni kuwa tuwe makini sana katika kutumia takwimu. Wakati mwingine takwimu zikitafsiriwa vibaya zinapotosha mno. Ukiwa na viongozi wawili na moja ni muislamu na mwingine mkristo, unaweza kabisa ukasema asilimia 50% katika hiki chama ni wakristu au waislamu kadri unavyotaka! Kimahesabu upo sawa kabisa, lakini kimantiki unaweza ukawa mbali kabisa na ukweli.

Huyo chinga mimi sioni cha ku-argue naye tena!
 
Mwanasiasa nakujua ulipo na najua hasa kazi yako, in my line of job it is very easy kukujua.

Nakutumia PM kukusalimu kwa jina lako halisi..... anyway let us not personalise this, niliposema mtu wa kaskazini kakerwa sikumean wewe nilimean Administrator anajijjua anatokea wapi! soma vizuri, ni vizuri sana kupotoka unaposoma kishabiki....

Naam will be back ngoja nifanye kazi za kujenga taifa letu.
 
Doesn't this become even sweeter? There are people who think they can continue to cheat, guys we want the truth only, otherwise you will burn your fingers.
 
Kulikoni Admin?

Are we going forward or backward - where is 'where we dare talk openly?'
 
Dua,
The displayed Motto is the shorter version. The complete one has some exceptions which so far include Mengi (nae ni wa kaskazini??), Chadema na ya tatu muulize Mwanakijiji. Kabla thread za Mengi kufutwa... zilianza kuvurugwa kwa mtindo kama huu. Kitakachofuatwa ni DrWHO, Tafiti, Wacha and the likes kupatiwa temporary ban... na Changa's account will be deleted. And his IP subnet will be banned.. hata kusoma mtandao huu hatoweza.

On the topic,
I think Chadema needs to work more on making the chama appear national, if at all it is. Maana inaonyesha Mtei alipokuwa akifungua matawi alikuwa akiangalia kuna Kimaro gani kule Tanga? Kuna Massawe gani Lindi n.k. (which was probably a quick move kupata usajili) Ila kwa sasa Pamoja na maelezo mazuri na theories za ki-Phd, the composition is still troubling. Kuwa na zaidi ya 25% ya wabunge kutoka familia moja .. tena yenye direct link na familia ya uongozi wa juu na waanzilishi... hasa kwa wabunge wa kuteuliwa.. kwa vyovyote vile ni questionable.

Lastly, nliwahi kumuuliza swali Mh. ndabita lakini naona shughuli zimemzidi hajawahi kujibu, nalitafuta swali langu silioni .. sijui ndio katika yaliyofutwa kama anavyodai DrWHO? Anyway ntasummarize hapa mwenye info atusaidie: What is the standard procedure in chadema katika kuwapata wabunge wa kuteuliwa? hupigwa kura au huwa inakuwaje? kama ni kura hupigwa na kitengo gani cha chama? Is that the procedure used in 2000, 2005 and to be used in 2010. Assuming hakuna mabadiliko ya katiba. I'm just curious kuwa ilitokea tokea vipi hawa wanafamilia ndio wakateuliwa.
 
washakula pesa za CHADEMA hao

sipendi kuongea ki simple namna hii lakini ndio conclusion yangu hiyo

Mwanakijiji UPDATE WEBSITE YAKO na ujifunze kutokana na makosa wanayoyafanya hawa jamaa
 
Chinga,

Kusema Freeman alipewa kazi benki kuu na Mtei hapo mshikaji umeteleza. Sii kweli na sisi tuliokuwa karibu naye enzi hizo tunajua Freeman alikuwa na nani.

chinga anateleza katika mengi. Ila nimeshangaa kidogo kwa nini Kichuguu ametumia muda mwingi kumjibu. Was it all that important kujibu udaku? chinga anafaa zaidi kuwa mhariri/mwandishi wa magazeti ya udaku kule bongo.

Nikipata mtaji wa kutosha nitamwomba awe mhariri wa gazeti langu la udaku. Najua nitatengeneza pesa nzuri, maana majority ya wabongo hushabikia sana mambo ya chooni.
 
washakula pesa za CHADEMA hao

sipendi kuongea ki simple namna hii lakini ndio conclusion yangu hiyo

Mwanakijiji UPDATE WEBSITE YAKO na ujifunze kutokana na makosa wanayoyafanya hawa jamaa

Dr WHO: Polepole mzee, CHADEMA watoe hela kwa lipi hasa? Is it really you saying this?
 
WANABODI.

inabidi tuwe makini na kila forum kujua ina malengo gani inawezekana tunatoa michango ambayo inakinzana na malengo ya forum,

nimekuwa nikiwambia rafiki zangu Mnyika na Mwanasiasa kuwa wako kwenye gari ambalo safari yake hawaijui ikawa na sisi hadithi hiyo inatugusa.

kulikuwa na mwanabodi aliyekuwa mstari wa mbele sana huko siku za nyuma lakini alipochangia mada Ya Mengi reginald alifungiwa moja kwa moja si mwingine ni Mswahili.

Na ikatokea tena mwanabodi mwingine sikumbuki jina lake lakini ziliwahi kuwekwa hadharani password za computer yake (IP address za computer) kitu ambacho ni kinyume na computer law, ni sawa na kuweka pin number ya kadi ya benki ya mtu au daktari kuweka hadharani siri za mgonjwa wake,lakini jambo forum waliweka hadharani.

hata kuchanganywa kwa mada hizi bado kunaacha maswali mengi zaidi ya majibu, Mbowe alianzisha thread ambayo katika huu mseto yake haijachanganywa, pia kuna Tamko la chadema liloandikwa na Mnyika nalo halijachanganywa ila mada aliyoanzisha Chinga, Dr.Who na Tafiti zimechanganywa na kuwa kama biriani.

jee kama zinachanganywa mada zinamuhusu Mbowe iweje aliyoanzisha mwenyewe ambayo ndio mzizi haijachangaywa? hapa kuna jambo si bure?

Chukulia niko Dar na nimeenda kulipa elfu moja internet cafe ili niingie Jamboforums unakuta mada zimechanganywa kiasi hicho hujui uanzie wapi au uishie wapi na kwa uslow wa computer unakuta nusu saa yako imekwisha huku hujaambua kitu mseto mtupu.

Kingine kinachonitia wasiwasi ni wengi wa wana chadema humu kwenye forum na watu kuwa na confidence za kulazimisha watu wajiunge kwenye chama chao, mambo haya sijayaona forum zingine,utakuta jiunge chadema kwa mabadiliko n.k, walipoona wamekuwa wengi, wakatokea wengine kuua soo kwa kuweka bendera ya vyama vingine mfano william King huku maudhui yake ni ya kichadema tu,

hata kitendo cha Mbowe kuja kujimwaga humu na asiende kwa mwanakijiji lazima alikuwa na yakini na anachokifanya(mcheza kwao hutunzwa),

Binasfi nimekuwa nikipata vitisho na matusi kwenye PM yangu kuwa natumika kuihujumu chadema, kutokana na hali hiyo nachelea yale yalimkuta mfanyakazi wa kinyakyusa aliyekwenda kufanya kazi Kilimanjaro tawi la TRA pale Holili,alipokuwa akiwajibika kisawasawa na kuwazuia watu kufanya mambo yao, walimwambia unatubana, yule bwana kwa kutokujua akaripoti kwa wakubwa wake makao makuu ili apate kinga na aifanye kazi inavyotakiwa, hakujua kama ni kesi ya Muhogo kumpelekea nguruwe, alikuwa hajui TRA ni Taasisi ya watu wa mahala fulani tu,
wale jamaa kuona anazidi kuleta ugumu ikaamuliwa jamaa auliwe kwa nyumba kuchomwa moto kwa bahati jamaa aliokolewa ila nyumba ilichomwa moto.

katika mijadala kama hii inategemewa ADMIN kuwa neutral lakini kama akiwa kaelemea sehemu moja, raha ya mjadala haipo na hata maana ya Forum kuwa serious kama tulivyofikiri mwanzo inakuwa haipo.
Pia haiwezi kuwa forum ambayo akiguswa mtu toka mkoa fulani basi mjadala unavurugwa hiyo si kuwatendea haki watu, chukulia JK anajadiliwa kila kona ingekuwa vyema naye ukakusanya mada zote na kuweka mseto kama huu.

Admin.

Kitu ambacho kinatunyima raha kwanini watu wa kilimanjaro wakiguzwa wewe unavuruga? na kinachotia shaka unatoka huko huko naomba tuweke sawa,

Mwanakijiji.

Nimekuwa nikikuzimia sana katika uendeshaji mambo wako kwani kila jambo linazungumzwa na watu wana uhuru wa kweli, ombi langu kama alivyosema DR.Who weka sawa ikiwezekana tuje huko, hapa hatujui malengo ya forum labda yanafanana na malengo ya NGO zingine, tusipoteze muda wetu tuwaachie wenyewe watangaze sera.

sina nguvu tena ya kujadili wazeee akina Es, Kulikoni, Dua,wacha na DR.Who,mwanasiasa, Lunyungu n.k nasubiri ushauri wenu.
 
Chinga,
Ningekushauri upitie tena sheria na kanuni za Jamboforums.
Labda itakusaidia kukata issue kwa ustaarabu zaidi bila kutumia heresay na innuendo.
 
jASUSI
asante kwa ushauri wako,ila sikujua gari nililopanda linalekea wapi? nimesoma hizo kanuni hakuna sehemu inasema una merge mada ya Chinga, DR.WHO na tafiti halafu ya Mbowe na Mnyika unaiacha inngawa ni same topic.

Mambo ya Kilimanjaro ni mazito, mie mmachinga nimetolewa knock-out.
waswahili wanasema kupotea njia ndio kujua njia.

asante sana.
kwaherini
 
Ndugu yangu Chinga,

Sasa unaposema kwa heri ndio umeamua kuwapa ushindi?
 
It wll never be the same humu ndani


at least kwa mtazamao wangu


unajua nilikuwa nafanya recritment ya nguvu over the weekend halafu jamaa wakija wakaona haya yanayotendeka huku sidhani kama nitakuwa na la kujibu


unajua within a month hii website ilipata hits kuliko TANZATL,TZUK,TANZANINOW NA ZINGINEZO?


mwanasiasa

hiyo ya CHADEMA ni possible kwa sababu opiki za RICHMOND na TANESCO mbona hazijawa merged?

FANYA HESABU HAPA:

CHADEMA & FAMILY BUSINESS ilikuwa na replies at around 70

CHADEMA CONSERVATIVES ilikuwa na replies zaidi ya 50

MBOWE vs CHIFUPA ilikuwa na replies zadi ya 300


baada ya threads kuwa merged JUMLA zimekuwa 210


HESABU gani hizi au ndio yale ya 70-30?
 
Admin,
Kusema kweli sote umetupiga goli vibaya vibaya...yaani tobo la nguvu!.

Kuchanganya mada imeharibu kabisa sura nzima.

Binafsi, naona sisi wenyewe ndio tunajigonga na huyu Chinga kwa sababu, Chinga alianzisha mada yake nje ya ile ya Chadema familily business na pia ndoa ya Chadema na Conservative.

Kama mngechunguza mngeweza kuona kwamba Chinga hakuchangia sana ktk mada zile ambazo sisi wengi wetu tulisubiri kupata mwanga kutoka viongozi wa Chadema.

Sasa hivi kuzichanganya hizi mada inanipa picha kuwa Freeman hawezi kabisa kuingia tena kuichangia hapa kwa sababu namjua Freeman hawezi kujiingiza ktk mambo ya Kihuni! hata mazoea yz vijiwe vya kihuni hana toka enzi. Kifupi kuchanganya mada hizi kumekifanya kijiwe kizima kiwe uhuni mtupu.

Please, Admin kuna wengi hapa ambao tunapenda sana kufahamu safari ya hiki chama cha Chadema kabla hatujalivamia bus!

Viongozi wa Chadema sii watoto wadogo wanaweza kuchambua mchele ktk pumba na kujibu yale yenye manufaa kwetu.

Hata CCM wangeweza kuingia hapa wangekutana na kila aina ya maswali, ni juu yao kuchagua yapi yajibike na yapi kumfukuza mwizi wa nguo zako ukiwa uchi.

Hadi kufikia sasa hivi nimewaona Chadema kuwa watu smart ile mbaya kwani hawavamii vitu ovyo, wako very organised pamoja na kwamba maswali ni mengi sana yanayopandana.

Rudisha mada kama zilivyokuwa ili tupate kusikia Chadema wakitupa Dawa. Dereva wa gari lao kesha wacha injini na sintapenda kubaki nyuma!.
 
Oops, kumbe zilikuwa merged kuja hapa... So sorry members!

Ni hivi: Once the topic is merged it can't be back. Hapo ndipo pabaya. Kama nilivyoomba radhi hapo awali ( Jibu langu ) ni kwamba si kwa dhamira mbaya lakini kwa maelezo ya aliyezi-merge hakuweza kutofautisha contents za threads zenyewe. Anaomba radhi nami kwa niaba yake naomba radhi.

Naomba tuvumiliane, we'll change. Soma Jibu langu

Regards,

Invisible
 
Imeeleweka Admin, sisi wote ni binadamu tunakosea, hata mitume walikuwa wanasisitiza tusamehane.

FD
 
Nashukuru kwa kueleweka. Kwa kueleweka kwa FD ambaye ni Senior Member kunamaanisha wengi mmenielewa. Am out now, nawatakia ufanisi katika mfanyayo.

Tanzania ni yetu sote!
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom