Mbowe vs Chifupa + CHADEMA vs Family Business

Status
Not open for further replies.

chinga

JF-Expert Member
Nov 17, 2006
312
9
Sawa nimeshauriwa kama nataka kumjadili Mbowe nifungue thread mpya, sasa hii kwa kuangalia hii NGO [au niseme SACCOS ya exclusive members?] CHADEMA nimegundua mgombea urais MBOWE ni bomu heri hata Chifupa.

Inaonyesha kuna baadhi yenu hamjashtukizia jinsi profile za Chifupa na Mbowe zinavyofanana. Kwa hiyo nimekaa chini leo nianze kukuonyesheni hapa.

1. Public CV
Mbowe:
BUNGE::
Chifupa:
BUNGE::
CV zinafanana mno kwa kutokuwa na kitu.. although ya
Chifupa imenonanona kiasi kuliko ya Mbowe.

2. Elimu
(a) Wote wawili ni form 6.
(b) Mbowe anajifua sasa hivi kupata shahada 2,
zilizoandaliwa maalum kwa ajili yake, within 3 years,
semi part time, kutoka vyuo vitatu tofauti, vilivyo
katika mabara matatu tofauti.
(Damn! doesn't this qualify as an entry in Guinness
book of record?)

By the way, mbona inatajwa Hull tu, hivyo vyuo vya marekani na japan mbona havitajwi majina? au ni mazabe?

Being about 20 years younger, Chifupa has better chances of advancing, she can go to school kwa raha zake .. as a normal student, bila kulazimisha syllabus maalum na mazabe mengineyo.

3. Siasa
(a) Mbowe kishakuwa Mbunge, Chifupa ni Mbunge hivi sasa.
(b) Hakuna loloote kubwa katika miaka mitano ya ubunge wa Mbowe.

Within one year ubunge wa Chifupa umewasha moto dhidi ya madawa ya kulevya ambao wengi wanaugwaya .. na 'wazungu' kadhaa wameanza kunaswa.

(c) Chifupa kaingia siasa kwa initiatives zake.
Mbowe kavutwa kurithi kiti cha Mkwewe.

(d) Mbowe kagombea urais na kukosa, lakini bado ndoto haijafutika.
Chifupa ame-hint kwa mbaaali kuwa nae ana ndoto hizo. Refer mahojiano yake na Radio Butiama.

4. Biashara
Wote ni wafanya biashara, mmoja anamiliki saloon aliyofungua mwenyewe, mwingine anamiliki night club na guest house, vya urithi!

5. u-DJ
Wote wawili wamekuwa ma-DJ. Mmoja wa Night club, mwingine redioni.
Kwa hiyo hapa ngoma draw, isipokuwa tu u-DJ wa Mbowe utakuwa umeleta Maambukizi zaidi ya ukimwi kuliko ule wa redioni.

6. Uwezo wa kujieleza
Mbowe anaonekana ana uwezo zaidi.

7. Kupenda Umaarufu
Chifupa amecapitalize kupata umaarufu through kuiguza jamii kwa kusaidi yatima, watoto n.k. kwa vipesa vyake na kwa kukabili matatizo yanayoogopwa.
Mbowe anacapitalize on ushamba wa wananchi vijijini kwa kuwaonyesha helikopta, spending millions!

Mbali na mamilioni ya wakati wa kampeni, kwa vile umaarufu umeanza kupungua Mbowe anataka kurenew tena kwa helikopta, eti kutoa shukuran kwa kutochaguliwa!
Ref:
http://www.darhotwire.com/dar/Habari/2006/11/25/26678.html

Tufanye hesabu kidogo: Kuikodi Helikopta hii kunawagharimu dola 1,200 kwa saa. Na watakuwa nayo kwa siku 23, kila siku ina masaa 24.

Kwa hiyo jumla ni 23 x 24 x 1,200 = USD 662,400.00
Exchange rate ni about TShs 1300, kwa hiyo hizi ni 662,400 x 1300 = Tshs 861,120,000 Yaani takriban Milioni mia tisa zinaunguzwa hivi hivi, na hapo hatujaangalia gharama za mafuta, per diem na gharama nyinginezo za mikutano! Hiki kweli ndio chama mbadala au ndio hiyo NGO flani.... and the guy wants to be a president. What a joke?!

Hii inaonyesha kana kwamba strategy ya Chifupa ya kujipatia umaarufu ni far more effecient, kwake binafsi kipesa na kwa jamii kufaidika.. kuliko hii ya Mbowe.

Point hizi za kuanzia zinatosha kuwapatieni mwangaza wa jinsi hawa 'wanasiasa' wawili wanavyoshabihiana, and it is clear nani mwenye potentials zaidi.
 
hili suala sasa linarun out of control na inabidi hao jamaa wa CHADEMA waliclarify ili liishe then turudi back to normal otherwise naamini kuwa by next week hali itatisha na hatutofika huko tunakotaka kwenda
 
Hi Chinga, you need a cellotape to shut that dirrehea coming out of your mouth!

Don't you see that one of the achievement of mbowe is for you wasting time on making unpopular arthmetics on his expenditure?
The best cat is that one who catches the mouse!
 
wewe chinga ni MPUUZI,MJINGA NA MPUMBAVU,
LETE CV YAKO WEWE TUIONE KWANZA HALAFU TUKUPE NAFASI YA KUZUNGUMZIA CV ZA WENGINE.
INFACT WEWE UMETUMWA NDIO MAANA UNA MUDA MWINGI WA KUANDIKA UJINGA WAKO.
 
Chinga I think you have gone too far . Unamkosea Mbowe heshima kabisa na sisi unatudhalilisha kama tutaendelea kukuvumilia . Unamlinganisha Mbowe na Chifupa ? Jana nimeuliza hao wasomi wako ndani ya CCM wameifikisha wapi Nchi na ma degree ya kuchonga kuanzia mawaziri hadi chini hujajibu.

I have met Mbowe several times akiwa Broad . Mojawapo kubwa ni last 2yrs ama na last year akipo kuwa amehudhuria mkutano wa Vyama vya Siasa .Tanzania alienda yeye na Jamaa mmoja wa CCM. Mbowe was a star kujieleza na kueleza issue hata watu walishangaa wakati mwana CCM huyo bwana Cosmas Hinju aliyekuwa Deputy Sec General wa Wazazi TZ bara akiwa na Degree moja ya UDSM alikuwa anajiuma na akabaki kumshambulia kwamba yeye anatumia magazeti yake na kusema tu Watanzania njoeni TZ maana Kikwete anatisha which was nonsense.

Lugha iliyo tumika ni Kiingereza . Uwezo wa Mbowe na Chifupa kweli tunaweza kuulinganisha ? I am tired .
 
Nilipoona kicha cha habari, nikaona huu upuuzi gani tena CHINGA analeta lakini nimeisoma naona kuna walakini katika siasa za CHADEMA kama anayoyasema Chinga yana ukweli.

I must admit kuwa naona hakuna upupu alioweka, ni ubunifu kaonyesha Chinga, wengine badala ya kutukana nadhani ni bora tukashambulia mawazo au kuyaunga mkono au kuentertain the thoughts without accepting them.

The motto here is ''where we dare talk openly'', na Chinga kama wengine humu anapomjadili mtu ambae ni public figure hahitaji kujitaja wala kuweka cv yake bali ijadiliwe ya public figure, ingekuwa kuweka cv ni sharti la kujadili mtu kusingekuwa na waandishi wa habari!!
 
Umaarufu kwa madai ya kuwa na orodha ya wauza unga, tena wale wa mtaani kwake bado kunigusa kabisa.

Iwapo Chifupa amepata ubunge kwa kupitia nafasi maalumu, ni vema atafute umaarufu kwa kuweza kuongelea kero na matatizo makubwa ya wanawake wa TZ, na jinsi gani ya kutatua.

Wanawake katika maisha ya Watz ndio wamekuwa na jukumu kubwa la kulea familia, kwa kuteka maji, kukata na kubeba kuni, kupika n.k Zaidi sasa ndio wafagiaji na wazoaji taka ngumu katika majiji ya Tanzania.

Mh. Chifupa hana budi kuangalia ni kwanini linapokuja suala la kuuza maji, wanaume huwa mbele ilhali kuchota maji kwa ajili ya mahitaji ya familia hukimbilia kijiweni kupiga domo.

x1pUKtwnwfCFuA54sJOA48IgGcdCr2MaVcL9ix5sjP-Y4BpAd8EU5b0Qx0_bia8xclPU4lR0p8a94ltV8j4BDY0Y7iNO5LKvPahwsU6Lu2T6_o


x1pUKtwnwfCFuA54sJOA48IgDahjRxi1DKbYMlluflAhpGrcHLY6ci6fso1YQLRzMv8bfWdxpst0RYXZNR99aKHlaTS3uq0r_POD9_G1V3rj0k

Mh. Chifupa kama anaguswa na kero ndani ya Watz, basi hana budi kuangalia akina mama hawa ambao wapo kwenye sekta ya usafishaji, jinsi gani wanavyofanya kazi katika mazingira magumu.
 
Kweli Amemkosea Heshima Mbowe Hawa Wanasiasa Sio Wa Kuwafananisha Kabisa Hata Kidogo Na Sioni Sababu Ya Kuendelea Zaidi Ila Mwenyewe Anajua
 
uliyeweka hizi picha umefanya jambo la maana sana,ili tunapoongea hali mbaya watu waone hali halisi,
maana kunawatoto wengine humu wanaandika wakiwa masaki ndio hawa akina chinga, matatizo yetu wenyewe tunashindwa kuyatatua mpaka waje watu weupe kutoka washington, newyork, london.

siku hizi kila siku kwenye vyombo vya habari utasikia serikali ya sweden inakerwa na huduma mbovu za afya au serikali ya finnland imeishauri serikali ya tanzania kushughulikia tatizo la rushwa, au superstar wa hollywood ametoa kiasi fulani kuchangia watoto yatima.

why?
kwasababu sisi wenyewe watanzania tunashindwa kuzungumzia matatizo yetu kwasababu watu kama chinga wakipewa shiling 700, anatumia 300 kwenye mtandao na 400 anaenda kula chips kavu siku imeisha na akili yake imeishia hapo.
 
#5 Today, 07:03 PM
quarz
Member Join Date: Sep 2006
Posts: 58
Rep Power: 1


wewe chinga ni MPUUZI,MJINGA NA MPUMBAVU,
LETE CV YAKO WEWE TUIONE KWANZA HALAFU TUKUPE NAFASI YA KUZUNGUMZIA CV ZA WENGINE.
INFACT WEWE UMETUMWA NDIO MAANA UNA MUDA MWINGI WA KUANDIKA UJINGA WAKO.

Chinga is not a public figure wala hajasema anataka kuwa mmoja wao hivyo hana haja ya kuweka CV yake. It is his constitutional right to question.

These Cv are already in public domain anyway (kule bungeni). Chinga ameleta hapa kwa sababu anajua wengi hawazioni.

I think CHADEMA themselves should come and explain rather than condemning Chinga.

This are the facts - Chadema want to rule 40 million people - they should explain.

Welldone Chinga


Wacha
 
Uwezi wetu na nguvu za michango tunaiweka ama kuchangia CCM ishinde na Lowasa na JK watasimamia ama maadhimisho ya Uhuru wa Tanzania ambao haupo ila tuna uhuru wa Tanganyika .
 
Aisee!

This Chinga kid is very entertaining. He has an interesting way of delivering his missiles.

Anyway, hoja hujibiwa na hoja. Wanachadema hapa kazi mnayo!

Tukiachana na approach na lugha iliyotumika .. hizo data hapo ni sawa au?
 
so what are you trying to tell us?
if someone is a public figure doesnt derserve respect?

yes if he (chinga) has the right to attack others,i also have the right to atack him,and i will...

we know that character assasination is your political game in ccm, please dont spread that shit to the emerging parties.
 
Nadhani Chinga huu ni muda wa kuisaidia CCM yako kuweka vyema maslahi ya Nchi kwa kuwa uongo wenu soon utakujulikana kwa uwazi zaidi na mtashindwa kuelezea umma uchaguzi ujao ila mtashinda kwa wizi wa kura , badala ya kuwatukana akina Mbowe hapa. Yaani unaweza kumlinganisha Mbowe na Chifupa ?
 
Bwana Chinga umefikia hata kumfananisha Freeman Mbowe na Amina Chifupa, ii inaonyesha jinsi gani upeo wako wa kuelewa mambo uko mbali mnooo. Mbowe aliingia bungeni kwa kupigiwa kula na sio kwa viti maalum.

Katika miaka mitano ya mbowe Bungeni aliweza kutufaamisha wananchi jinsi bunge letu linavyofanya kazi( kwa hili unaweza kupitia nakala alizoandika kipindi cha nyuma kwenye gazeti la RAI) Mbowe ni mwenyekiti wa Chadema, je unaweza kumchagua Amina kuongoza chama chochote cha siasa Tanzania?zaidi ya kuongoza Kitchen party?.

Kuhusu Amina kuongoza kasi ya madawa ya kulevywa- unafahamu kwamba anatumiwa tu na serikali na magazeti ya Home yakiongozwa na IPPMEDIA; kuwazuga wananchi wasahau kujadili matataizo halisi yanayokabili taifa letu kama vile issue za upungufu wa umeme,RICHMOND; Mikataba yA madini na hali ngumu ya life home.

Kama issue ya madawa ya kulevya ingekuwa ya kweli, niambie wangapi wametajwa, na wangapi wamekamatwa, zaidi ya JK kila kukicha kusema anayo majina ya wauza unga.na IPPMEDIA kuishia kuandika kasi ya kuwataja wauza unga pamefikia mahala patamu, au orodha inatisha.Je unajua sasa JK wameanzisha topic nyingine ya kutaifisha mali za wala rushwa.

Maana yake ni kwamba issue ya Amina na madawa ya kulevya ikishapoa, Topic ya kutaifisha mali za wala rushwa inachukua nafasi yake kwenye Tanzania Press,ikipoa anaanzisha topic nyingine, wananchi mkishtuka tayari JK kamaliza miaka yake kumi na sio hajabu nae akaenda kusoma USA. Kwa kifupi Amina chifupa na freeman Mbowe huwezi kuwafananisha hata kidogo labda uwe umetumwa na Secretariety ya Chama cha Mapinduzi.
 
Mimi sidhani kama kuna haja ya kumjibu Chinga , kwa sababu ni mjinga ! Adminstrator unafanya kazi gani ondo huu ujinga ulioandikwa na huyo kilaza PLEASE !
 
Ni sawa na kusema simba na fisi nani ana nguvu zaidi kwa vile wote ni wanyama wa porini, wanakula nyama na wanaweza kutoa makelele; halafu ukatumia kigezo cha kwamba kwa vile fisi anaweza kutoa makelele mengi inawezekana yeye akawa ni zaidi.................................

Pamoja na mimi kuwa ninavyo vidigrii kadhaa tena vya nguvu kweli kweli, huwa ninasema kuwa uongozi wa kisiasa siyo wa madigrii. Kinachotakiwa kwa kiongozi wa kisiasa ni kujua vizuri shida za jamii na jinsi ya kuzipatia ufumbuzi ili kuleta maisha mazuri kwa jamii hiyo. Kiongozi mzuri atafanya kazi ya kuwapanga wataalamu mablimbali ili kutatua matatizo ya jamii, siyo kwamba yeye ndiyo atakayetatua matatizo hayo kwa mkono wake.

Machifu wetu kama akina Mkwawa, Milambo na wengineo hawakuwa na digrii yoyote lakini tunajuwa jinsi walivyopigania wananchi wao.

Ninapoona wanasiasa wetu wanajipachika madigrii lukuki wakati wakiwa kwenye madaraka ya kisiasa na kutaka watambuliwa kwa madigrii hayo huwa ninakereka sana kwa sababu inaonyesha jinsi gani wasivyojiamini na wasivyojua wajibu wao kama wanasiasa. Ni kutokana na kutojua wajibu wao, huwa wanaishia kufanya kazi ambazo zilitakiwa zifanywe na wataalamu lakini wao wanasiasa wanajipachika utaalamu huo na matokeo yake ndiyo tunayoona hivi sasa. Tanzania sasa hivi inaweza kuwa inaongoza kwa kuwa na wansiasa wengi madokta wakiwa wamepta udokta wao madarakaini na wote wanataka watambulike kwa udakitari wao huo: Dr. Malecela, Dr. Mzindakaya, Dr. Nchimbi, Dr. Kamala, Dr. Mary Nagu, Dr. Masaburi, Dr. Makongoro Mahanga, Dr. George Nangale, Dr. Waryoba, na wengine wengi wenye masters lukuki zote zilizopatikana kimkatomkato. Mmoja wao ana masters 2 na bachelors 2 zote zikiwa zimepatikana kwa mpigo katika kipindi cha miaka mitatu tu wakati akiwa ni ofisa wa kibalozi.

Ukiangalia katika nchi za wenzetu, utashangaa kuwa viongozi kama John Major hakuwa msomi na wala hakujipachika madigrii baada ya kuwa madarakani. Vile vile madokta halisi kama akina Paul Wolfowitz, Condoleeza Rice, Madeline Albright, Gordon Brown, Newt Gingrich, na marehemu Paul Wellstone hawatumii title za udakitari wao katika shughuli za kisiasa ingawa wote wameingia kwenye siasa wakiwa na Ph.D. na wengi wao waliwahi kuwa maprofesa kwenye vyuo vikuu. Wanajali zaidi utendaji wa kisiasa kuliko sifa za kuwa wasomi.
 
Bwana Chinga tusaidie CV yako, ili tujue pa-kuanzia na hii mada yako
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom