Naam Mwanasiasa:
Hujajibu swali la msingi nililokuuliza mara mbili takriban:
Ulikuwa unajua kama Lucy Owenya na Grace Kihwelu wana mahusiano na Mzee Ndesamburo ya uzazi kabisa?
Kama ulijua kabla je huhisi kwamba hapa kuna walakini, hata kama wamechaguliwa kwa kura, is it fair kichama kinachotaka kuwa mbadala na CCM?
Kama ulikuwa hujui, nipe reaction yako sasa.
Naam leo naanza rasmi kudisect information nilizopewa na kujaribu kuanalyse kama CHADEMA ni biashara ya watu wa kaskazini au ni chama mbadala:
Data nilizopewa zipo biased i have to say manake zimechagua kipengele kimoja tu cha viongozi. Kwa mujibu wa tovuti ya CHADEMA, Viongozi wa kitaifa ni hawa wafuatao:
Freeman Aikaeli Mbowe [KILIMANJARO]
Mzee Saidi Mzee [visiwani]
Wilbroad Slaa [Karatu- Arusha]
Shaibu Akwilombe [masasi lindi]
Himid Yusph-Pemba
Victoria Kimesera [KIteto manyara]
Hawa ndio viongozi wa kitaifa, you can see kuna viongozi sita, watatu wanatoka kaskazini:
Mbowe, Slaa, Kimesera [50% ya top team!!]
Kumbuka tanzania ina mikoa ishirini na sita, lakini viongozi watatu wakubwa wametoka tanzania north!!
WABUNGE:
Chadema imefanikiwa kupata viti kadhaa vya wabunge waliochaguliwa na wananchi kwenye uchaguzi mkuu na hivyo kufanikiwa kupata viti maalum, wafuatao ndio wabunge wa chadema:
SLAA[KARATU]
Maulidah Anna Komu -VITI MAALUM
SAID AMOUR ARFI [MPANDA]
CHACHA WANGWE [TARIME]
SUSAN LYIMO [VITI MAALUM]
NDESAMBURO [MOSHI MJINI]
HALIMA JAMES [VITI MAALUM]
MHONGA SAID [VITI MAALUM]
LUCY OWENYA [VITI MAALUM
ZITO KABWE [KIGOMA VIJIJINI]
GRACE KIHWELU [VITI MAALUM]
Unaweza kuona kuwa CHADEMA ingawa kimepata wabunge katika several locations in the country lakini wabunge wa kuteuliwa Owenya,Lyimo,Grace, wote ni kaskazini!!! Ukichanganya na Mzee Ndesamburo na Slaa ina maana wabunge watano kati ya kumi na moja wametoka kaskazini!! Hapo hatujamchanganya Mama Komu ambae anajidai mzanzibari mwenye asili ya uchaga na Mwanasiasa nisaidie Halima anatoka wapi.
Ukiwatoa Anna Komu na Halima James, unakuta kwamba wamebaki wabunge tisa na watano kati yao ni kaskazini, 55%!! ukiwachanganya na hao wawili unaona kwamba ni 45% wanatoka kaskazini!!
What is interesting to note here ni kuwa viti vya ubunge wamepata sehemu tofauti za nchi lakini kwa vile kuna maslahi ya mishahara minono nk basi wabunge wawili ukimchanganya na mzee Ndesamburo mwenyewe ni familia moja! Hivi ni viti vya kuteua, hivyo wangeweza kuvibalance lakini ndio hivyo kwa chama chenye domination na kaskazini....
Ukija kwenye Sekretarieti ya CHADEMA ambayo ina wajumbe 30 utakuta kumi na moja kati hao wanatoka kaskazini. Check for yourself:
http://www.chadema.net/uongozi/sekreta.php
hii ni about 36% of the total members of the secratariet
Katika mikoa ishirini na sita kuona wajumbe wakiwa mostly kutoka mikoa miwili mitatu wakishikilia nafasi nyeti na nyingi zenye ulaji inakupa shida kukiona hiki kama chama mbadala.
The analysis will continue.....