Kichuguu.
Unachekesha sana mbona unaleta Udikteta wa chadema humu? unasema nisikuulize chochote wala nisikujibu huku ukijenga hoja, hapa hatupo Chadema kusiko na uhuru wa kuhoji.katika haki ndogo kabisa za binadamu ni kumpa nafasi ya kujibu au kuhoji ina maana Chadema wakiingia madarakani mtu akituhumiwa tu basi anawekwa ndani hana nafasi ya kujitetea?someni adminstrative law kuna kitu judicial review halafu tizama natural justice inasema nini?
Inaelekea una ushabiki wa kisiasa badala ya kuchambua issues. Sasa swala la Chadema na post yangu limekujaje hapa. Mimi si mwanachama wa chama chochote pale Tanzania; sishabikii wala kumchukia mwanasiasa yeyote ila ninasupport mambo mema au kukemea mambo mabaya wanyofanya wanasiasa wote bila kujali vyama, makabila, dini au elimu zao.
Nimekuambia usinijibu wala kuniuliza swali kusudi nisikutoe nje ya mada yako. Maoni yangu hayako kwenye mwelekeo wa mada yako, kwa hiyo kuendelea kujibizana nitakuwa ninayumbishwa mwelekea wa mada yako bure tu.
Kwa hiyo wewe unajidhani kuwa una akili pana ndiyo maana unakaa kujadili watu binafsi tena kwa kwa jazba hivyo? Watu wenye akili pana wanachambua mambo kwa jumla na kupokea mwazo ya upande mwingine. Wewe siyo mmja wao kwa vile unapigania kuwa usikilizwe na ajenda yako hata kama kuan uwongo
Watu wanaposema Bush kachukua kazi ya baba yake haina maana kuwa alipotoka baba yake aliingia yeye,kwa akili zako za kichadema utasema NO alichukua baada ya Clinton.
No, wacha upumbavu hapa. Hujui kuwa baba yake Bush alikuwa President na Bush mweyewe naye ni President; kwa hiyo kuna kosa gani kusema kuwa Bush alichukua kazi ya baba yake. Bush aliinga madarakani baada ya Clinton je unaona hiyo siyo kweli? Kama ungekuwa na akili pana usingeweka upupu kama huu.
kuna mifano mingi ya hilo nenda kwenye Taasisi mbalimbali hasa hizo za fedha hapa nyumbani utaona labda hazina kuna watu wengi wa kaskazini, jibu kuwa huko nyuma kulikuwa na mtu au watu toka maeneo hayo wameacha athari kwangu mimi ni athari mbaya, ukienda Bima, Nbc,jeshini na hata polisi ndio utakuta kuna misemo ya maeneo fulani ya kazi imeathiriwa na huo mfumo mbaya wa kupendeleana au kujaza watu wake mfano mtu anasema" harrow liafande" na huo msemo unakuta umetawala ktk kitengo fulani ni kuonyesha jinsi watu hao walivyomiliki eneo hilo. samahani Jasusi kama nimegusa,
Kichuguu.
Nimesema Mtei alimpa kazi Mbowe na yeye mwenyewe hajakanusha kwanini wewe uje kujibu wakati mwenyewe yupo hai na ametoa ahadi hiyo?, bahati ya mwenzio usi ilalie mlango wazi, unashangaa kupewa kazi na mke?, yote yanawezekana. hakuna principle yeyote inayosema mtu akikupa kazi hawezi kukupa mwanawe.
Kurundikana kwa makabila fulani katika taasisi fulani fulani kulitokana na ama makabila hayo kupenda kazi hizo sana (kwa mfano wakurya na jeshi) kiasi kuwa mamobi yao yalikuwa ni mengi kupita maombi ya makabila mengine, au kuwa na afisa utumishi mweye ukabila.
Mtei hakuwa ofisa utumishi wa benki kuu wakati huo, kwa hiyo asingefanya hivyo labda kwa kumwomba afisa utumishi ambayo sioni mantiki yake kama nitakavyoeleza huko mbele.
Mtei na Mbowe kutokanusha unayoandika haina maana kuwa wameyakubali. Nimeonyesha kuwa Mtei asingempa kazi kulingana na timeline ya Mtei alipokuwa madarakani na umri wa Mbowe. Mimi ninakupinga siyo kuwa ninawatetea ila ninapinga kwa vile taarifa unazotuletea siyo za kweli. Mengine uliyoandika ni upuuzi tu.
kukusaidia uelewa wako mdogo tizama suala la Mkapa kuwa rais wa Tanzania watu wengi wanasema na kuamini kuwa Marehemu mwalimu Nyerere alimsaidia kumpata hayo madaraka, na kuna wengi wanasema na kuamini kuwa Malecela na Lowassa walikosa nafasi za kuwa marais 1995 kwa mkono wa mwl. jee mwaka 1995 mwl Nyerere alikuwa rais wa Tanzania? au alikuwa Mwenyekiti wa chama? au alikuwa makamu mwenyekiti? au alikuwa katibu mkuu wa CCM?
na hakuna mahala kusikia watu wakisema aliyekuwa rais na mwenyekiti wa chama Alhaji Mwinyi alimsaidia Mkapa kupata nafasi ile, au kusikia Malecela ana kinyongo naye kwa kuikosa nafasi ile.
kwani hiyo ni siri? Wewe ndiye kipunga kweli kweli, hata hujui kuwa Nyerere alikuwa powerhouse wa Tanzania. Kwenye kamati kuu ya CCM hakuna aliyekuwa akimpinga. Umesahau kuwa ndoto ya Lowasa na Kikwete kwenye kinyang'anyiro hicho kilizimwa na Nyerere? Alilokuwa akisema lilikuwa linafuatwa? Halafu bado unajifanya kuwa na ulewa mpana wa mambo? Unataka kusema kuwa Mtei alikuwa powerhouse wa Benki kuu hata baada ya kuondoka kama Nyerere kiasi kuwa kila alichosema kilifanyika?
kumbuka hayo ni madaraka makubwa kabisa ktk nchi.
jee Mtei atashindwa kumpa kazi ya ukalani BOT bwana Mbowe?
Unachosema ni kuwa Mtei alimpa kazi Mbowe, na hilo ndilo sijakubaliana nalo. Ungekuwa unapanga mawazo yako kwa makini labda nigewezea kukuelewa lakini kwa vile unabwatuka bila mpangilio ndiyo maana labda sikuelewi. Kupata kazi ya ukarani kulikuwa hakuhitaji high level authority ya Mtei ambaye wakati huo alikuwa aidha World Bank au IMF. Kwanza kumbuka kuwa miaka hiyo ya 70na mwanzoni mwa miaka ya 80 vijana wote wa form six walikuwa wakipangiwa kazi na utumishi; ni watu wa utumishi ndio waliokuwa wakigawa post zile kiupendeleao. Kwa vile Mtei hakuwa serikalini tena, kama ilikuwa ni lazima amsaidie Mbowe kupata ukarani wa direct employment pale benki kuu, ni kwamba alitakiwa ama "amwombe" afisa utumishi wa Benki Kuu au "afanye mipango huko utumishi" ili post ya Mbowe iwe ni benki kuu, tena hilo lifanyike wakati angali JKT. Umuhimu wa Mbowe kwa Mtei wakati huo hadi Mtei afikie hatua ya kufanya mojawapo la hayo mawili siuoni na ndiyo maana jambo hilo haliingii kichwani mwangu. Kwa bahati mbaya umeshindwa kunionyesha hilo, badala yake unabwatuka tu.
Kichuguu sitakwenda mbali naona uoni wako mdogo sana.
Nimeshakuonyesha kuwa wewe ndiyo kipunga kabisa; kelele tupu, mantiki hamna. Mifano yako yote uliyoweka hapo kuhalalisha kuwa Mtei alimpa kazi Mbowe pale BOT haina mantiki yoyote. Kuna upupu mwingi sana ulioandika ambao hauna mantiki yoyote. katika yote uliyoandika nimefurahishwa na jambo moja tu la matumzi ya helikopta ingawa baadaye umeshindwa kulisupport vizuri, mengine yote unayoandika ni ya ki-KCC tu.