John Mnyika
JF-Expert Member
- Jun 16, 2006
- 713
- 1,249
Wapendwa,
Bwana Forum nimekuja kujibu nimekuta umechanganya mahindi, mchele, mtama nk kwa kuwa zote tu zi nafaka. Umenichanganya. Lakini nimeona radhi yako. Nashukuru. Hivyo nitachangia hapa hapa. Hivi hivi kwa kuwa sehemu kubwa ya hoja zilizoshwa nazikumbuka.
Chinga nashukuru kwa pole ya msiba wa kwanza. Ulikuwa ni wa kaka yake na Akwilombe kwa hiyo unastahili kumpa pole zaidi yeye. Jana nilitumia tena sehemu ya muda kwenye msiba mwingine. Katibu wa CHADEMA mburahati jimbo la Ubungo alifariki(Mungu amlaze mahali pema).
Sasa nanza kujibu rasmi hoja mbalimbali zilizoelekezwa kwangu. Michango imekuwa mingi sana kwa hiyo nitajibu kwa ujumla zile hoja ambazo hazijatolewa ufafanuzi. Na kama kuna zingine nitaziruka wahusika waniambie nizijibu.
Nianze na kukumbusha hoja zilizoleta maswali kuhusu elimu yangu: Moja ni mjadala ya kuwa Tanzania kuna udini na kwamba wakristu wanapendelewa zaidi na kwamba kutokana na kupendelewa huko mimi nilipendelewa kupata division 1.7 kidato cha nne nikiwa na A tisa na kwamba kidato cha sita kwa kuwa sikusoma shule ya kanisa nikapata division 3.17(tatu ya mwisho).
Pili, niliweka tamko la CHADEMA kuhusu uchaguzi wa EALA, mara ikaja hoja kuwa CHADEMA haiwezi kutoa tamko kuhusu suala la nasaba katika kushika nafasi za uongozi kwa kuwa na yenyewe ina utamaduni huo. Kabla hata jibu halijatoka mjadala ukabadilika Chinga akaingiza tena hoja ya kwamba nimepata division 3 ya mwisho kidato cha tatu pindi nilipofafanua hili akaendelea kusisitiza kuwa nina division 3 na akaingiza hoja nyingine kuhusu kuchelewa kwangu kumaliza shahada yangu chuo kikuu cha DSM. Huu ndio muktadha wa mjadala mzima kuhusu elimu yangu.
Maneno makali makali yalitumiwa katika mjadala mengi yanakaribia matusi kwangu lakini sioni busara kuyajibu hayo badala yake nitajadili masuala yaliyojitokeza.
Ila nirejee tena kauli yangu ya mara kwa maratujadili masuala sio masihara!.....kwa upande mwingine tunaotumia majina ya kalamu tuheshimu wajibu wetu.nia ya kutumia jina la kalamu ni kuweza kusema ukweli bila hofu ya kutambulika kutokana na sababu mbalimbali na si kutumia fursa hiyo kutukana. Ni suala la ubinadamu tu.
Baadhi wamesema kuzuka kwa hoja ya udini ni suala dogo. Mimi naamini ni suala kubwa sana. Na kuna suala kubwa zaidi ya hilo, UBAGUZI. Tanzania kuna ubaguzi unaochemka chini kwa chini. Its a volcano, and perhaps a time bomb.
Binafsi kabla ya kuingia kwenye uchaguzi mwaka jana nilipata nafasi ya kusoma kitabu cha Mauaji ya Mwembechai kilichopigwa marufuku. Na kumbuka Mwembechai kama eneo lina taathira kuwa katika siasa za Ubungo hususani Makurumla na Mburahati. Lakini niliacha kabisa kuizungumzia hii ajenda.
Kwa kuwa nilijua sensitivity yake hususani wakati wa uchaguzi. Lakini sasa ni wakati mwafaka wa kuyajadili haya. Mimi ni msomaji wa kila wiki wa magazeti yenye mrengo wa kidini ya kislamu the likes of Al Nour, Nasaha, Alhudaa. Na magezeti ya kikristu the likes of Msemakweli, Nyakati, Kiongozi, Tumaini letu na mengineyo.
There is a volcano boiling. Infact, it seems to be a global phenomenon-the conflict between western and eastern civilization that is fought through various fronts including religious. Nisingependa kulijadili hili hapa,nisije nikaendelea kutoka nje ya mstari!