chinga,
sijui kama utanielewa ila nitajaribu kukuelewesha, katika mawasiliano kuta kitu kinaitwa "protocals". ili watu au vitu viwili viweze kuwasiliana na kuelewena lazima kuwepo na protocals, protocals ni kanuni na sheria za kurahisisha mawasiliano,
mfano lugha tunayotumia humu ndani ni moja ya protocals, wote tunatumia lugha ya kiswahili na kunawakati tunatumia lugha ya kiingereza kwa asumptions kuwa wengi wanailewa,
kama kuna mtu angekuja hapa ndani na kuanza kuzungumza kichina au kihindi sidhani kama tungekuwa na mawasiliano.
sasa kanuni hizo za mawasiliano haziishi tu kwenye lugha, manaweza kuwa mnatumia lugha moja lakini bado mkawa hamuelewani kwasababu bado kuna kanuni nyingine hazijafuatwa,
mfano freeman mbowe ni mwenyekiti wa chama,kwa mtazamo wangu unapotaka kuwasiliana na mtu kama huyo lazima ujitahidi kufuata protocals hizo,mojawapo ikiwa ni kumheshimu yeye na wadhifa wake, siamini kama amekimbia maswali bali hajakuelewa kutokana na lugha unayoitumia, nafikiri ungekuwa makini katika kufuata hizo kanuni za mawasiliano angekuwa ameshatoa majibu.
mfano unao wewe unapotaka kwenda kuwasiliana na mzazi wako lazima utumie lugha ya heshima ili muweze kuelewana.
pili kwa wale wanaodai kuwa viongozi wa chadema wamekosea kutumia majina yao kwenye forum hii natofautiana nao,
kwa mtazamo wangu hii ilikuwa ni nafasi muhimu kujadili mambo mengi ya msingi ikiwa ni pamoja na hayo mnayo hoji kama ya uhusiano wa chadema na conservative na mambo ya hellocpter na sera ya majimbo.
tungepata majibu kutoka kwa mwenyekiti mwenyewe wa chadema ambaye ndie muhusika mkuu.
tatizo ninaloliona hapa ni hilo la immotional incompetence kama linavyojadiliwa kwenye ile topic ya waafrika ndivyo walivyo?
watu wengi wanafikiri hii forum inasomwa na watanzania pekee,hawajui kuwa kuna watu wa mataifa mengine wanasoma humu kama wakenya, waganda, warwanda...
mfano kunasiku nilikuta mke wa professor mbilinyi(mzungu) ameweka post yake mahali fualani.
sasa wageni hawa wanapokuja kusoma humu na kuona mitazamo ya watanzania na jinsi tunavyojenga hoja ni wazi kuwa tunajiabisha.
kuna sehemu zimetengwa kwa ajili ya mambo kama haya ya udaku, manaweza kwenda kule mkaweka hizi post zote na waopenda kujadili mambo haya watawafuata huko, ila kutuletea hapa ni wazi tunajionyesha jisni tusivyo serious na mambo muhimu katika nchi yetu.
naomba kutoa hoja.