Mbowe vs Chifupa + CHADEMA vs Family Business

Mbowe vs Chifupa + CHADEMA vs Family Business

Status
Not open for further replies.
Ndugu Chinga kama nilivyokuahidi kurudi na majibu yangu hoja kwa hoja, nafanya hivyo. Majibu yangu yatatumia marejeo yalipo kwenye Taasisi za Serikali ikiwemo, Tume ya Uchaguzi, Kitengo cha Nyaraka za Wafanyakazi wa Serikali (kipo nyuma ya UNICEF), nk. Bado nasubiri nyaraka za NECTA na

Hoja 1: Public CV

Website ya Bunge la Jamhuri ya Muungano, ni sehemu ya mwisho kabisa kutafuta wasifu wa wabunge kwani kuna historia ya siku nyingi kuhusu ukweli wa record zilizopo. Ukitaka kuona hili basi jaribu kuangalia CV ya Mbunge mwingine ye yote halafu ulinganishe na ukweli halisi. Kwa harakaharaka unaweza kuanzia na wabunge wenye majina makubwa hapa Bongo na hata viongozi wa vyama.

kama unataka kuona CV halisi na timilifu basi nenda tume ya Uchaguzi utapewa kama una sababu zitakazowaridhisha. Miaka ya nyuma niliwahi kuwasiliana na wanaosimamia hiyo website Datavision kuhusu info za aliyekuwa mbunge wangu kwani yeye binafsi alipinga kuwa na shahada ya Kilimo iliyokuwa imeonesha kwenye website infact alikuwa mafunzo ya miezi mitatu ya bwana shamba Uholanzi, lakini wakasema hizo habari walipewa na wafanyakazi wa bunge.

Mfano: hiyo CV uliyotuletea inasema High School bila kusema jina la Shule, ukiendelea kusoma nyingine utaona watu wamepewa Shahada kibao bila kusema wamepata wapi na mwaka gani.

Kwa hilo tu linatosha kusema, website ya Bunge letu siyo chanzo kizuri cha habari, na kuna makosa mengi mno kiasi kwamba tunaweza kusema ni vigumu kutumia cv za hawa wahusika kuwachambua.

Hoja 2: Elimu

(a)Si wote wana elimu ya kidato cha sita. Hapa siongelei mambo ya kufaulu au kushindwa. Kuendana na record kutoka source nilizotaja hapo mwanzo ni kwamba Freeman Mbowe ana Stashahada ya Elimu. Mpaka sasa hivi sijafanikiwa kupata majibu kamili kutoka NECTA kama Mbowe alisomea hiyo stashahada baada ya Form Four au Form six, kwani wale wa miaka ya nyuma mtakumbuka kwenda kusomea ualimu uliweza kufanya baada ya kidato cha nne au cha sita. Pia kwa sasa siwezi kutaja shule na chuo alichosomea kwani sijathibitisha kutoka kwa mamla husika au shule.
Nadhani Mbowe mwenyewe ndiye anaweza kuondoa utata huu wakati tunasubiri NECTA watumwagie vitu.

b) Huwezi kulinganisha uelewa wa Mbowe na Chifupa, hata mtu mwenye akili makini hawezi kumlinganisha mtu aliyewahi kuajiriwa na Bank na mtu ambaye hakuweza kuajiri na vyombo vya Uandishi wa habari pamoja na Diploma yake uandishi wa habari (sijui kutoka chuo gani). Ijapokuwa ni fani tofauti lakini ukijaribu kulinganisha sidhani kuna mlinganyo.

c) Kuhusu mbowe kusomea shahada mbili kutoka vyuo tofauti hilo siyo swala geni hata kidogo. Usilinganishe Tanzania ambako mtu huwezi kufanya shada mbili kutoka vyuo tofauti, mfano Open University na Mlimani. Binafsi nikiwa nafanya shahada yangu nje, nilikuwa nafanya vyuo viwili tofauti katika miji tofauti, kuna kitu kinaitwa "interdisciplinary studies". hapa vyuo vina makubaliano na vyuo vingine ili kusimamia program ambazo hazipo chuoni kwao, lakini ni sehemu ya degree ya mwanafunzi. mfano mimi nilipata degree kutoka UK na Canada wakati muda wote nilikuwa kwenye chuo kimoja isipokuwa mara chache kama kwenye defense ya thesis.

d) Pia kumbuka Mbowe hasomi program za kawaida ambazo mimi na wewe tunaweza kusoma, tumeambiwa program zimetengenzwa mahsusi kwa ajili yake. Kwa hiyo course load inaweza kuwa tofauti kabisa na course work ya wanafunzi wa kawaida.

d)Kuhusu kutajwa Hull tu nadhani, kwenye gazeti habari ilisema rpogram moja imetengenezwa kwa kushirikisha vyuo vya Uingereza, japani na Marekani, haikusema kuwa atasomea kwenye vyuo vitatu. Naomba mwenye hile habari kwenye archieve zake aiweke tena hapa.
>>Nadhani Mbowe pia anaweza kujitokeza kuclarify mambo zaidi

e)Ndugu yangu nani alikuambia elimu inategema umri. Nyerere (rip) aliwahi kusema elimu haina mwisho wakati anaanzisha Elimu ya Watu wazima. Kama watu wangefuata umri kwenda shule basi tusingekuwa na maprofesa kwani hamna mtu anayepata huo uprofesa kwa sababu ana umri mdogo bali wanazotea bila kujali alianza akiwa na mwaka mmoja au hamsini.
Pia mtu mwenye majukumu ya kisiasa kama mbowe au kiongozi mwingine hawezi kufuata syllabus ya kawaida, pita dunia nzima na utaona huu ukweli.

Yaani wewe badala ya kumshauri Chifupa hata angalau ajiunge na open University tena wamtengenezee program maalum kwa ajili yake (kuenddana na habari za kimtandao hana sifa za kujiunga na University kama kweli alipata Division 0 kidato cha sita).

3. Siasa
Umesema
(b) Hakuna loloote kubwa katika miaka mitano ya ubunge
wa Mbowe.

Ndugu yangu basi sasa unanipa wasiwasi hata kuamini kama unafahamu unachosema. Hebu jaribu tu kupitia hansard za bunge halafu urudie kusoma hoja yako hapo juu. Angalia maswali na hoja zake akiwa bungeni, kuanzia mgawanyo wa madaraka, pesa za Serikali, ujenzi na matumizi mabaya fedha.

Pili, nadhani upo bongo, naomba tu ufanye trip angalau ya siku moja tu kutembelea jimbo la hai halafu uone ndani ya miaka mitano alifanya nini kuanzia maswala ya maji, miundo mbinu, viwanja. jaribu kufikiria kwa nini Serikali iliamua kugawa jimbo la hai mara mbili, hii ilikuwa kudhoofisha upinzani kwani walidhani Mbowe angegombea lakini hakugombea. Watu wa hai walitokwa na machozi kwa kitendo chake cha kutokugombea tena.
Ndugu yangu hapa ni sawa na mtu kusema Wibroad Slaa hajaleta maendeleo Karatu.

(c) Chifupa kaingia siasa kwa initiatives zake. Mbowe kavutwa kurithi kiti cha Mkwewe.

Holy cow: inaoneka hujui historia ya siasi Tanzania au unakataa kukubali jambo usilolijua. kwa upande wa Chifupa sijui nianzie wapi. Lakini la Mbowe kwa kweli hufahamu historia yake. Mbowe siasa hakuanza leo, tizama historia kuanzia babake na ikiwezekana waulize wanaomfahamu wakuambie. Naomba nikuulize hivi Mtei kaachia uongozi wa Chadema lini na Mbowe kachukua lini, je enzi ya mtei kuna mtu alikuwa anamfahamu Mbowe. hata kwenye uchagzui wao mkuu hamna aliyetarajia angechukua uenyekiti wa chama kwani kulikuwepo na wagombea wengine na kama nakumbuka vizuri aliwapita wenzake kwa kura chache sana


Kuhusu Helikopta:
Pitia ripoti ya matumizi ya Uchaguzi wa chadema.

Tatizo lako kubwa na kwamba unatumia habari ya kwenye Guardian 08/12/2005 aliyotoa David Mgasi na Lucy Mdemu baada ya kuhama Chadema na kuhamia CCM. Walisema CHADEMA walipewa bilioni tatu na Conservative Party ya Uingereza lakini walipoambiwa watoe vielelezo walisema email haifanyi kazi.

Ijapokuwa sijui gharama halisi ya helikopta, ninachoweza kusema ni kwamba gharama kubwa zililipiwa na Mbowe mwenyewe kutoka kwenye michango aliyopewa na marafiki siyo kwa ajili ya chama bali kwa ajili yake binafsi, kama baadhi yetu tulivyomchangia Mnyika. Chadema tofauti na CCM kwenye Uchaguzi uliopita hatukuwa na ruzuku kubwa kama CCM, ndiyo maana uliona wagombea wakigharamia baadhi ya mambo peke yako kama kuweka mafuta kwenye magari yao baada ya kupewa magari na chama.

Hivi leo hii ni nani anaweza kutuambia zile dola milioni ishirini alizopewa kikwete na Iran (source BBC) zilitumikaje kuwasaidia wagombea wengine mnaweza kutuambia. Tutenganishe misaada au michango binafsi na ili ya chama.

naomba niishie hapa kwa leo.
 
Mimi sio mshabiki wa siasa, lakini naona mpaka sasa Chinga hajapata jibu. Yaaaaaaaaaaaaaaaaaaani nani zaidi ?
 
Jibu lake ni kwamba, swali lake halina mantinki. Huwezi kuwalinganisha hawa wawili,itakulazimu kuwa kichaa kuweza kuwalinganisha.
 
Jafar,

Unatakiwa uprint hardcopy ya maswali ya Chinga, kisha futa yale maswali yasiyo na maana halafu print hardcopy ya mada hii kuanzia ukurasa wa tano kisha utapata majibu. Kama huoni majibu basi ujue una matatizo.

FD
 
SUCKER PUNCH

Duh! Yaani Chinga amewapiga Chadema na washabiki wake sucker- punch. maana yake hata Mbowe na wasaidizi wake hawajatokea tena.
 
Mkuu Chifupa na Mh.Mbowe hawafanani nikiwa na maana kwamba Mbowe babkubwa kubali au kataa na vilevile angalia maneno yako unayoyatamka au umetumwa?
 
Kwako Chinga,

Simply enough: MBOWE'S CALIBRE AND INTEGRITY IS BETTER OFF A THOUSANDS TIMES OF THAN CHIFUPA'S

Waulize wanamtandao wake aliouanzisha "AL - QAIDA IN DAR"

Kaiba Wambandwa
 
Chinga,

Asante kwa changamoto yako. Kwa haraka tu, au kwa kiswahili 'your are comparing apples and oranges". Ki-utaalam kila mwanadamu ana "strenghes" zake na "weaknesses" zake. Kwangu mimi wote ni ba'bkubwa kama utatafiti "SWOT analysis" zao. Cha maana ni kuacha ile kasumba ya mimi-CCM au mimi-CHADEMA katika kujadili kitu kama hiki.

Tanzania ya sasa inawahitaji akina-Mbowe wengi na akina-AC wengi. Watu ambao "dares to speak openly"
 
Hayo mahesabu uliyopiga ni ya kitoto na vile vile ni makubwa hiyo Helikopta haitoweza kufanya kazi masaa 24 kwa siku na kwa siku zote hizo 23 wanazotaka kuzikodi inaonesha mambo ya ukodishaji wewe huyajui

Chadema watachajiwa masaa ambayo hiyo Helikopta itafanya kazi ni si masaa 24 kama unavyofikiria,kwa siku inaweza ikafanya kazi masaa 5 kwahiyo zidisha mara 1200 uliyosema na si 1200x24 hii si sahihi,sahihi ni kwamba 1200 x 5=kwa siku nafikiri utaendelea kufikiri vzuri kuhusu hili suala.
 
Eeeeh naam. Angalau angalau sasa akina Kakindomaster, Al-Jazeera na baadhi wengineo wamekuja vizuri kihoja hoja. Mkiendelea hivi ni poa sana.

Mkiweka CV ya Mbowe hapa mtakuwa mmetuweka pazuri zaidi, maana iliyoko bungeni hata mimi nadhani imekosewa, hata tarehe za ubunge inaonyesha alianza 15 Oct 2005 na kumaliza 30 August 2005!! Na information nyingi zinasema 'no item in the list'!

Kama Mbowe ana stashahada/diploma ya ualimu kama alivyosema mmoja wenu, ile CV ya Chifupa inaonyesha nae ana stashahada/diploma ya uandishi.. kwa hiyo bado inaashiria kwa sasa ngoma draw kielimu, ila in 3 yrs time mzee atakuwa na bachelor na masters, au sio?

washawasha anasema helikopta inalipiwa ikiwa angani tu. I find that a bit hard to believe. Maana hata tunapokodi magari huwa tunalipia kwa muda wote linapokuwa mikononi mwetu, na sio mda tunaoendesha tu. Na ile source ya habari aliyotoa chinga inaonyesha "Gharama kukodi ndege hiyo kutoka Kenya ni dola za Marekani 1,200 kwa kila saa moja itakapokuwa mikononi mwa CHADEMA ..", au ndio habari nayo ilikosewa?

Wambandwa, eti kuna mtandao wa Mbowe unaoitwa "AL - QAIDA IN DAR", hebu tumegee zaidi mzee ututoe wasiwasi, eti ni mtandao wa kuhusu nini?
 
Hayo mahesabu uliyopiga ni ya kitoto na vile vile ni makubwa hiyo Helikopta haitoweza kufanya kazi masaa 24 kwa siku na kwa siku zote hizo 23 wanazotaka kuzikodi inaonesha mambo ya ukodishaji wewe huyajui,Chadema watachajiwa masaa ambayo hiyo Helikopta itafanya kazi ni si masaa 24 kama unavyofikiria,kwa siku inaweza ikafanya kazi masaa 5 kwahiyo zidisha mara 1200 uliyosema na si 1200x24 hii si sahihi,sahihi ni kwamba 1200 x 5=kwa siku nafikiri utaendelea kufikiri vzuri kuhusu hili suala.

Nashindwa kuamini juu ya ukodishaji huu wa helikopta. Kwa hiyo Helikopta hii inapotua kijijini kwa masaa, let say 4, wakati Mbowe anahutubia inakuwa haijakodiwa na kwamba Lipumba akitokea hapo kijijini anaweza pia akakodisha akarukanayo kijiji kingine huku akimwacha Mbowe anadandia magari?

Je Mbowe akikodi Helikopta hii kutoka Arusha hadi Songea, na mara baada ya kufika Songea akaamua arudi Dar kwa basi, nani yuko responsible na gharama za kurudisha Helikopta?

Hesabu za Chinga zinakaribiana na ukweli kuliko hizi za Bw Washawasha.
 
AL- JAZEERA
Mbowe hakupa kazi BOT kwa juhudi zake alipewa ma mkwewe ambaye alikuwa gavana.na hata uenyekiti alipewa na mkwewe huyo huyo ambaye ndiye mwenye Ngo.Makani alishika kwa muda tu.

Kakindo master.

Inawezekana Chifupa alikwenda Masasi na Bongo fleva, lakini Mbowe ni maarufu sana ktk muziki kwani alikuwa dj na alikuwa na club yake Mbowe club, akaja kuibadilisha kuwa bilicannas,sasa Mbowe anajulikana zaidi kama Dj na alikuwa anachukua ten percent kwa kila malaya atakayepata mzungu pale kwenye club yake, yaani wale changudoa alikuwa akiwatosa pesa kama kodi ikafika mahala wale changudoa wakawa wanaona bora wakakae magoti, kuliko Mbowe club jinsi alivyokuwa anachukua kamisheni kubwa.

na pale club bilicannas dada zetu wanauzwa kwa wazungu na huo ni mradi wa huyu mnayedai mwenyekiti wa chama, lini ulisikia Mbowe kukemea biashara ya malaya? au Ukimwi sababu ana hisa kwenye hiyo business.
hivyo basi kujulikana kwa muziki, mbowe anajulikana zaidi ya Chifupa, na hadi anamiliki disko. kama wewe unapima na ziara ya amina huko masasi hakuna uwiano Mbowe zaidi.
Nyanza

Nasubiri vitisho vyenu sikujua kama Chadema hakuna demokrasia kiasi hiki? nilikuwa najiuliza Mtei aliweza vipi kumpitisha mkwewe na kuwa mwenyekiti? jibu umenipa Nyanza kwani huko hakuna kuhoji. ni ubabe tu
'MIMI EDWIN MTEI NAMPITISHA MKWE WANGU MBOWE AWE MWENYEKITI WA HII NGO' wajumbe wote kimya. wanaogopa kuuliza.

mie nitaendelea kuuliza tu na wala msinichagulie maswali ya kuuliza.
 
Chinga,
Sasa hapo unaleta uwongo. Mbowe alifanya kazi chini ya Gavana Charles Nyirabu. (RIP) Check your facts man, si kutumwagia hapa upupu.
 
Jasusi
wewe ndio muongo.timama tena hizo facts zako au makengeza?

najua unamtaja Nyirabu kwa vile ni home boy wako, tuliza boli Jasusi hii ngoma nzito mwenyewe alisema atajibu kila hoja ya maana mbona kimya? mtu mzima ukimuona JIIIII, UJUWE NGOMA NZITO. na kule Mnyika alisema tarehe 5 atajibu kaulaza jiiii. naona ndiyo sera ya chadema kuulaza tu.
 
When i heard that CHADEMA's leader Mr Freeman Mbowe was at Conservatives Convention last summer i though this will be interesting, and then when he came clean on the Marraige between CHADEMA and CONSERVATIVES i thoough what is so special about Conservatives to have them as allies.

But after going through CHADEMA's website i couldnt make out on their objective and they they have hidden this alliance.

Now i still think its not too late for CHADEMA to come clean about their alliance with REPUBLICANS in the United States and CONSERVATIVES in UK

From their website below there isnt anymention of Republicans or Conservatives

http://www.chadema.net/
 
tuliza boli Jasusi hii ngoma nzito mwenyewe alisema atajibu kila hoja ya maana mbona kimya? mtu mzima ukimuona JIIIII, UJUWE NGOMA NZITO. na kule Mnyika alisema tarehe 5 atajibu kaulaza jiiii. naona ndiyo sera ya chadema kuulaza tu.

This is interesting. Maswali ya maana? To whom?
 
Hiyo ni siri kubwa tunajua wachache kinachoendelea akina Mwanasiasa, Mnyika na Lunyungu ni washika mapembe tu, wakamua maziwa ni Mtei na Mkwewe Mbowe.
 
By the way kuna mtu anayefahamu kazi ambayo Mbowe alikuwa anafanya pale BOT? Was this after or before being a DJ?
 
Is the Conservative party policy (UK) similar to CHADEMA in Tanzania or in other words do they share the same goals in UK/Tanzania i.e. Immigration, Development, Education etc.

When will Chadema MP's start asking concrete questions in Parliament?

We are still waiting for answers to numerous questions asked to Mr. Mbowe.


Wacha
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom