Kitendo cha kumfananisha Mbowe na Chifupa sijakielewa mwandishi alitumia kigezo gani.
Mimi nadhani Mbowe mpinzani wake ni yule aliyefikia level yake yaani naye kagombea urais au anaongoza chama chake.Maana kumfananisha na Chifupa ambaye tunajua ni 'chakula' ya watu kibao CCM,na ndio maana mumewe kaoa mke mwingine bila yeye kujua, na waliomfikisha hapo kwenye ubunge ni wakina Nchimbi,yule mzee wa TOT-Capt Komba...kati ya wachache.
Mbowe ninavyojua mimi alianzia chini,akajipatia Ubunge na mpaka kuwa mwenyekiti wa chama chake kwa jitihada zake mwenyewe.Sasa labda mtu awe anajua zaidi na aseme kuwa Mbowe ni shoga ndio kweli tungeweza kumfananisha na Chifupa.Chifupa yuko kwenye kundi kubwa tu la ma-miss CCM ambao wengine wamepata u-DC n.k.
Mbowe ni kati ya wachache waliojitokeza kutumia haki yake ya kikatiba kutaka uongozi wa juu wa nchi hii,nani hapa kati yetu ambaye akihakikishiwa urais ataukataa? Lakini hapohapo ni wangapi wenye jeuri ya kuutafuta kwa juhudi zao wenyewe? Jibu,ni wachache sana,na mmoja wao ni Mbowe.Mimi sio shabiki wa chama chake wala siasa zake,lakini i do admire the bloke kuweka ukawaida.Kwamba hata urais mtu yeyote anaweza kuugombea,yaani ni kawaida tu.
Sawa katumia helikopta,lakini zile sio pesa za walipa kodi,kazitafuta mwenyewe...kwanza ile helicopter ilikuwa ni ya Nyachae(waziri Kenya) na taarifa nilizonazo ni kuwa hakuilipia ile helicopter,yeye aliambiwa ajaze mafuta na kumlipa pilot tu,huo ulikuwa ni mpango wa baba mkwe wake(inasemekana ana urafiki na Nyachae),ndio maana kulikuwa kuna shemeji yake ndani ya ile helicopter katika kila safari. Kwani ile helicopter si haikumaliza muda,maana ilikodiwa na watu wa mashindano ya magari,angekuwa na yeye kaikodi si ingebaki?
I also admire Mr Mbowe for becoming a member here.Maana wakati akifanya hivyo alijua kuwa atatukanwa na kukashifiwa kwa kila aina.Maana hili pia ni jukwaa,hatuonani wala kusikiana lakini tunawasiliana.Yanayoandika humu yanasomwa na watu wengi sana.Simpingi mtu yeyote kwa lile analosema maana haya ni mawazo yake binafsi na ana imani nayo,lakini pia nadhani kama tunataka kufaidika na hizo forum tungejitahidi kidogo kuwa constructive,ili tuelimike au tuelimishwe na wale wanaojua zaidi yetu.Mimi binafsi nimejifunza vitu vingi sana humu na nawashukuru wanabodi wenzangu kwa hio elimu,na nikiona anaingia mtu kama Mbowe humu natumaini kuwa atachangia ipasavyo na kutupa upeo wake alionao