Mzee Es:
Nimeamka!
Naona mnanichokoa kusema. Nimenyamaza kwa miezi mingi kuzungumzia watu!
Iliwahi kusemwa-watu wenye akili/hekima kidogo huzungumzia watu, watu wenye akili/hekima za kawaida huzungumzia matukio, lakini watu wenye akili/hekima nyingi huzungumzia masuala. Na ndio maana wakati wote naepa kuzungumzia watu.
Lakini wewe umekwenda mbali-umeibua hoja za kumhusu Mbowe(mtu) lakini umezihusisha na Masuala(Ukweli vz Uwongo, Uongozi Vs Kuwa safi/coming clean, Kuweka kumbukumbu sahihi vs Kuchafulia jina).
Mimi nawaombeni hapa niyajadili haya masuala. Nawaomba kabisa nisijadili watu wala mtu. Na najua naweza kupata lawama toka kwa chama changu kutokana na michango ninayoitoa humu. Lakini naamini hatma ya siku ukweli utatufanya huru.
Nitachangia kiasi kuhusu Swali Na. 1 mpaka 3. Swali namba 4 mpaka 7(imeandikwa 8), nitayaacha kwa sababu mbili-mosi mjadala wa family business nimesema nitachangia siku za baadae lakini pili- mtoa hoja na hata wachangiaji wengine bado hawajasema bayana nini ni nini kinachotakiwa kutolewa ufafanuzi. Kwa hiyo kama mnataka ufafanuzi sema ni masuala yapi hayo. Na kama nilivyosema nitazungumzia masuala! Sio mtu. Na kama mnataka nizungumzie mtu au watu,basi niambieni kabisa niache kuendelea kuchangia.
Suala la Elimu ya Mbowe lilisemwa humu sana kwenye thread nyingine. Sikuchangia wakati huo nikijua hoja zilizotolewa na watu mbalimbali zilijitokeza. Lakini naona linaendelea kuibuliwa tena na tena , kwenye mijadala tofauti tofauti. Sijui ni kwa nia gani. Kila tukijadili masuala nyeti ya kitaifa Mbowe anaingizwa katikati. Inaleta hisia kwamba ni mkakati wa kuhamisha mjadala.
Suala hili limeshika chati wiki hii kutokana na hoja za Kulikoni. Nadhani hata Mzee Es ameamua kulichukua kuanzia hapo.
Sasa kwa nia ya kuchagiza mjadala na kuweka kumbukumbu sahihi nirudie hoja za Kulikoni:
1. Kwamba Mbowe anasoma Shahada tatu
2. Kwamba Mbowe anasoma Shahada hizo zote kwa miezi 18
(kulikoni aliyasema maneno hayo katika thread hii
http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=2032&page=10)
Nikamwambia Kulikoni kuwa Mbowe anasoma shahada mbili: moja Hull na nyingine kwa distance Learning.
http://www.jamboforums.com/showthread.php?p=25927#post25927
Na nikamuomba Kulikoni alete ushahidi wa maneno yake kwamba Mbowe anasoma Shahada tatu kwa miezi 18 ama walau atuambie ni wapi Mbowe amesema meneno hayo:
Kulikoni akaleta ushahidi wa chanzo chake cha habari kuwa ni
http://www.habaritanzania.com/articles/1609/1/Mbowe-amua-kunoa-ubongo-Ulaya
Ukisoma chanzo cha Kulikoni chenyewe utaona amemua kudanganya(natumia neno hili badala ya neno kukosea kwasababu amerudia maneno haya mara kadhaa pamoja na kuona wazi kabisa kuwa chanzo kinasema tofauti na pamoja na kuelezwa ukweli):
Mosi: Chanzo kinasema Mbowe anasoma programu mbili. (kwa maana ya shahada mbili) ila kwa nchi tatu tofauti.) . Kwa hiyo kulikoni kusema Mbowe anasoma Shahada tatu amemua kwa dhati kabisa kupotosha. Hii inaleta hisia ya kwamba alilenga katika suala la kumchafulia Mbowe jina lake kwa kumfanya uonekane ni mdanganyifu. Sasa Kati ya Kulikoni na Mbowe nani ni mdanganyifu? Kwa bahati mbaya kwako Mbowe anasoma Hull, anasoma distance learning na kama sehemu ya digrii yake ya Hull atakwenda Japan-hii ni special arrangement ambayo amepanga kuifanya kwa ajili ya kupata exposure ya masuala ya middle East)
Pili: Chanzo kimesema Mbowe atasoma kwa miaka mitatu. Kulikoni amesema Mbowe atasoma kwa miezi 18. Kwa hiyo Kulikoni ameamua kudanganya. Kwa motive gani? Ama unataka ijengeke picha kuwa Mbowe anasoma digrii ya uzushi ama ya kununua kama zile za Udaktari wa Mawaziri kadhaa wa Serikali ya CCM ya awamu ya nne ya Kikwete? Kwa bahati mbaya kwako ukweli unajulikana wazi kuwa Mbowe yuko Hull ambacho ni moja ya vyuo vinavyoheshimika.
Nimeandika kwa kifupi. Nimeepuka kuandika kwa kina- na siwezi kuandika kwa kina kwa kuwa sipendi kujiingiza katika mjadala wa kujadili watu, sitaki kila sentensi niandike Mbowe, Mbowe, Mbowe, Mbowe. Nataka nipate wasaa wa kujadili masuala ya nchi.
Mimi nami ni kiongozi wa kisiasa. Na watu wanaamini maisha ya kiongozi wa kisiasa ni maisha ya umma. Kila kitu lazima kifahamike kwa umma. Lakini kumbuka hata mwanasiasa ni binadamu na anayo maisha yake binafsi. Yanakuwa tu yakujadiliwa kama yana uhusiano na masuala ya umma. Binafsi huwa naweka mambo wazi lakini si kila kitu. Uanike kila njia unayotaka kupita ili wapinzani wako wakuwekee vikwazo? Kama CCM waliweza kutuma mtu kwenda Kenya kufanya Booking ya Helikopta katika kampuni ambayo CHADEMA ilipanga kukodi Helikopta inashindwaje leo nikisema naenda kusoma chuo fulani mkaanza kuweka kauzibe? Ndio maana hata Mbowe alitangaza kuwa anakwenda Hull baada ya kufanikisha kila kitu ikiwemo visa ya kwenda masomoni. Kama Besigye anaminywa kutoka Uganda, kama Tvangirai ananyimwa kutoka Zimbabwe, wanasiasa wa upinzani waamini vipi hii Comrades Club ya CCM, ZANU PF, Movement nk? Kwa hiyo msitegee kuchokonoa tutoe kila taarifa hapa. Mambo mengine tutawaambie-UKWELI ni huu, kwa taarifa zaidi subirini miaka mitatu ijayo wakati mambo yote yamekamilika.
Kwa herini kwa leo
tutaonana panapo majaliwa
ngoja nielekee kwenye mkutano wa hadhara katika kata mojawapo Hapa Ubungo
..Hakuna Kulala, Mpaka Kieleweke.
JJ
(Mzaha)Ps: Mkimaliza kuuliza maswali haya kwa Mbowe muulize maswali kama hayo kwa Kikwete, Lowasa, Mwinyi etc
duh kwa kwa heli orodha ni ndefu na muulize maswali hayo-nani ana elimu gani, ana uhusiano gani na nani, anapata wapi pesa zake na anazitumiaje!. Lakini msiwajadili maisha yao binafsi mjadili masuala UKWELI VS UWONGO, UONGOZI Vs MASLAHI YA TAIFA etc teh teh teh, its like hide and seek(Joke)
Mabadiliko ya Kweli, hayawezi Kuletwa na Mafisadi wale wale, wa chama kile kile, chenye uoza ule ule, wakiendeleza yale yale, eti kwa Ari, Nguvu na Kasi mpya
kwa falsafa ya Chukua Chako Mapema
Tanzania yenye neema haiwezekani.